GE2025 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Lake Oil Group: Wanasiasa hawahusiki na umiliki wa vituo vyetu vya mafuta

GE2025 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Lake Oil Group: Wanasiasa hawahusiki na umiliki wa vituo vyetu vya mafuta

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
WAulizwe kama walikuwa wanapekeka michango ya wafanyakazi hao 300 kwenye mifuko ya pensheni!
Wapeleke wapi wahuni tu hao.

Wengi wanafanya kazi kwenye haya makampuni ya kifisadi kwa sababu ya umaskini tu lakini huko kuna unyanyasaji na kutokujali kwa viwangi vya juu sana.

Watu wanafanya kazi kama vibarua miaka na miaka kuwatajirisha wengine.
 
Shida hao maboss wakiwa wananyanyasa wafanyakazi hujimwambafai kuwa wao hawagusiki kamouni INA watu wazito serikalini.

BTW: Mlikuwa wapi kukanusha hizi tuhuma miaka ile zinahusishwa na mwana wa mfalme?
 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Lake Oil Group, Stephen Mtemi, ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha watu kuchoma vituo vya mafuta vya kampuni hiyo, akisema mbali na hasara kubwa iliyotokea, Watanzania zaidi ya 300 waliokuwa wakifanya kazi kwenye vituo hivyo sasa wako nyumbani bila kazi.

Amesema kampuni hiyo ina wafanyakazi takribani 8,000, huku asilimia kubwa wakiwa Watanzania. Katika vituo takribani 38 vilivyochomwa moto Tanzania nzima, Mtemi amesema vilikuwa na wafanyakazi zaidi ya 300 ambao kwa sasa wamepewa likizo bila malipo.

“Kwa habari tulizozisikia mitandaoni na mitaani, watu wengi wanahusisha Lake Oil na wanasiasa. Inaelezwa kuwa hilo ndilo lilisababisha washambuliaji kufanya vurugu na kuharibu mali kwa lengo la kuwafikia wanasiasa,” amesema.

Amefafanua kuwa kampuni ya Lake Oil ni mali ya Mtanzania mzawa anayeitwa Ally Adha Awadhi, na kwamba hana uhusiano wa aina yoyote na wanasiasa wanaotajwa, wala hawana umiliki wowote ndani ya kampuni hiyo.

Amesema si haki kwa wananchi kuharibu mali ya Lake Oil kwa kudhani inamilikiwa na wanasiasa, kwani hatua hiyo inaathiri maisha ya wafanyakazi pamoja na mmiliki wa kampuni.

Hata hivyo, Mtemi ametoa pole kwa wananchi wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na vurugu zilizoibuka kufuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

Aendelee kujichanganya akidhan mpaka vinachomwa, watu hawakua na taarifa.


Yajayo, vinaondoshwa tena
 
SAsa milikua mnahusishwa na wanasiasa alafu mkakausha si mngepinga ingewasaidia
 
Wengi watajifanya hawahusiki na wanasiasa ila tunaijua michezo yao😂
 
Back
Top Bottom