TANZIA Mkurugenzi wa Ulinzi, Usalama wa Vyombo vya Majini na Utunzaji wa Mazingira ya Bahari (TASAC ) Mhandisi Japhet Loisimaye afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Ulinzi, Usalama wa Vyombo vya Majini na Utunzaji wa Mazingira ya Bahari (TASAC ) Mhandisi Japhet Loisimaye afariki dunia

Bado mashemeji wa walinzi wa ofisi za wasiadizi wa wakurugenzi kuanza kuketewa Tanzia zao jukwaani
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Ulinzi, Usalama wa Vyombo vya Majini na Utunzaji wa Mazingira ya Bahari (DMSE) Mhandisi Japhet L.Loisimaye kilichotokea Jana Jumapili, tarehe 10 Mei, 2020 jioni jijini Dar es salaam.

Shirika linatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa marafiki na watu wote walioguswa na msiba huu. Taarifa ya mazishi itatolewa kwa wafanyakazi wa Shirika mara baada ya kujulishwa na familia.

Bwana ametoa,Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Imetolewa na Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania.

Naona Mgeni HATARI kutoka Jijini Wuhan bila Huruma anaendelea tu Kutudondoshea Watu kwa mfumo wa Top to the Bottom.
 
[emoji41][emoji41][emoji41]
20200511_084948.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom