TANZIA Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege Kilimanjaro, Mhandisi Christopher Mukoma afariki dunia

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Kaimu Mkurugenzi wa kampuni inayoshughulikia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO) Mhandisi Christopher Ande Mukoma amefariki dunia mapema asubuhi ya leo.

Taarifa kutoka kwa Uongozi wa uwanja wa ndege wa KIA zimeeleza Mhandisi Mukoma amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa nyumbani kwake mkoani Arusha.

RIP Eng uliupaisha uwanja wa ndege KIA uongozi wako utakumbukwa na kuenziwa

Mhandis Mukoma.JPG
 
Huyu mkoma alikuwa akiishi Kongwa mlali? au ni mwingine mkuu
 
Wakuu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu KIA Eng Mukoma kafariki leo asubuhi.

Eng Mukoma alitotokea Dodoma kwa I majukumu alisumbuliwa na homa ,kikohozi na mafuta ya hapa na pale

RIP Eng uliupaisha uwanja wa ndege KIA uongozi wako utakumbukwa na kuenziwa
Rip Eng. Mukoma. Pole sana kwa familia na jamii ya KIA kwa ujumla.
 
Huyu mkoma alikuwa akiishi Kongwa mlali? au ni mwingine mkuu
Makaazi yake rasmi ni Jijini Arusha.Wafanyakazi wa KADCO muda huu ni vilio,kuzimia hovyo,kutapika yaani ni shida juu ya shida.

Tangu arejee kutoka Dodoma kama siku nne au tano zilizopita hakuwa katika hali nzuri mafua na kikohozi vilimwandama sana.Fikiria kuanzia secretary,Wakurugenzi wenzake finance technical ... Wahasibu,maafisa ugavi security ........ Wote kwa nyakati tofauti tofauti walikaribiana na Mkuu 😷.
 
Hali ni tete!
 
Back
Top Bottom