Nimeishi na Wakurya, wakiwemo Wanzanaki na koo mbalimbali ambazo wakati mwingine hujitambulisha kama makabila tofauti, lakini ukiangalia kwa karibu utaona ni wale wale tu wote wanaitana MURA ! mambo mengi wanafanana kuanzia majina, mila, tohara na mambo mengine mengi. Kwa kifupi, wote ni kina Mura.
Lakini ukiachana na wale wa kuchovya chovya, Wakurya wanajulikana pia kwa msimamo. Ukishawahi kuishi nao, unaelewa kwamba wakisimamia jambo, ni vigumu sana kuyumbishwa. Wakishasimamia kitu, wamekisimamia kweli kweli. Na ukitaka kununua msimamo wao, ni kazi ngumu sana.
Na pengine hapa ndipo tunapopaswa kujifunza kutokana na yaliyowahi kumtokea Chacha Wangwe. Tukio lile lilituachia funzo kwamba kuwa na msimamo pekee wakati mwingine hakutoshi. Kuna aina ya watu wakiona huwezi kuyumbishwa, wanaweza kuamua kwenda mbali zaidi.
Na kwa yanayoendelea kwa huyu mwingine sasa, inaonekana naye anafuata njia yenye mfanano. Tuombeane uzima, yasije yakajirudia yaliyowahi kutokea kwa Chacha Wangwe.
Msimamo ni muhimu, lakini pia ni muhimu kutambua watu wanaokuzunguka wapo willing kwenda mbali kiasi gani, mazingira unayopambana nayo na gharama ambazo zinaweza kuja pamoja nao.