Kwa hekima tu, wazuiaji wa huo mkutano wasingejitokeza wao kutoa zuo, mkutano utakuwa una mwenyeji ambaye ndiye angetangaza kuwa hakuna mkutano utakaoendelea. Watu wasiohusika na mkutano huo kuvamia na kutoa katazo ni uhuni na ni fujo, bora polisi wangevamia na kuutawanya mkutano huo kwa yale mabomu ya machozi hata kama hawana maelezo ingeeleweka mkutano umevunjwa na polisi labda hauna kibali cha kukusanyika. Hekima na busara ni bora sana katika kuamua mambo kwa amani na upendo