Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Napata vishiari vya hali hii kutoka katika hotuba zake za hizi karibuni. Vyama vinavyofikiria kuweka wagombea vinaonyeshwa kuwa siyo vya kizalendo na ni vyenye matatizo, huku Mrema na Lipumba wakisifiwa!
Hana sifa ya kushinda kwa box la kura toka zamani. Na hilo la kuwa na fomu moja ya matokeo General Election ni agizo lake. Unaposikia atashinda kwa 90%+ ujue hayo ni maagizo yake. Na kuna misukumo mikubwa ya kutaka wapinzani wasishindane na yeye ili apite bila kupingwa. Na iwapo wapinzani watakaza kamba tutarajie damu kumwagika, na uchaguzi wa kishenzi kuwahi kutokea hapa nchini.