Mkutano nchi za Afrika na NORDIC: Rais Magufuli awakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini, kwa sababu kuna amani na ukuaji mzuri wa uchumi

Mkutano nchi za Afrika na NORDIC: Rais Magufuli awakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini, kwa sababu kuna amani na ukuaji mzuri wa uchumi

Chadema zile misele zenu kwenye barozi za nje bado mnakwenda au mnaonekana mnanuka mavi tu

State agent
 
Ni kweli Tanzania sio masikini.

Uchumi unakua kwa 27%.

Ajira za kumwaga, viwanda zaidi ya 4,000 vimejengwa(Tanzania ina viwanda vingi kuliko Ujerumani yenye viwanda 2,500)

Tanzania sasa ni industrial country, wafanyakazi wameongezewa mishahara 100%, barabara za juu kila kona, umeme wa uhakika, fyovers zaidi ya 37 zimejengwa, gesi imesambazwa kila nyumba, maji yamesambazwa kila nyumba, 80% ya watanzania wanakunywa maji ya kopo.

Watu wa ulaya wanakuja kujifunza kwetu Tanzania.

Mikaa 2 ijayo Tanzania itaanza kuzikopesha Marekani, China na nchi nyingine.

Mataga oyeeeeeeee.
 
Kabisa hii nchi tunajitekenya na kucheka wenyewe!
 
1573211049774.png

RAIS Dkt. John Magufuli amewataka Viongozi wa Bara la Afrika kubadili fikra na mtazamo wa kutegemea misaada na utegemezi wa kiuchumi kutoka nchi tajiri na badala yake kutumia diplomasia ya uchumi kuwa msingi wa ushirikiano katika kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za NORDIC na Bara la Afrika ulioufunguliwa leo Ijumaa (Novemba 8, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema uhuru wa kisiasa uliozipata Nchi za Bara la Afrika hautakuwa maana iwapo Nchi zake zitaendelea klwa wategemezi wa misaada kutoka Nchi tajiri.

Rais Magufuli alisema kuwa Bara la Afrika lina mambo mengi mazuri yanayopaswa kuwekewa kipaumbele katika kujikwamua kiuchumi kupitia ushirikiano wake na Nchi za NORDIC ikiwemo fursa za biashara na uwekezaji, hivyo kuliweka katika ajenda muhimu inayopaswa kuwekeza msisitizo.

‘Ushirkiano wetu na Nchi za NORDIC kwa miaka mingi umekuwa ni utegemezi wa kiuchumi, Viongozi wa Afrika tunapaswa kutambua kuwa mustakabali wa mataifa yetu upo mikononi mwetu, ni lazima tuondokane na aina hii ya ushirikiano’’ alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa raslimali na vivutio mbalimbali vya biashara na uwekezaji ukilinganisha na Nchi za NORDIC, lakini hata hivyo Mataifa hayo ya NORDIC yamekuwa yakipiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi ikilinganisha na Nchi za Bara la Afrika.

Akitoa mfano Rais Magufuli alisema katika Nchi tano za NORDIC zenye ukubwa wa kilometa za mraba Milioni 3.5 na mwaka 2018 zilikuwa na Pato la Taifa la Dola Trilioni 1.7 kwa mwaka huku idadi ya wananchi wake ikiwa ni Milioni 27 wakati Bara la Afrika lenye watu Bilioni 1.2 mwaka 2018 lilikuwa na Pato la taifa lenye thamani ya Dola trilioni 2.334, na kuongeza kuwa Nchi za Bara la Afrika lipo jambo linalopaswa kujifunza.

Aidha Rais Magufuli alisema ni wajibu wa Viongozi wa Bara la Afrika kuweka nguvu ya pamoja katika kusimamia rasilimali na maliasili ilizonazo kwa ajili ya kuleta ustawi wa maendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo, madini, misitu, mafuta, gesi, nishati na mifugo

‘Asilimia 30 ya ardhi bora ya kilimo duniani ipo Afrika, na kwa mujibu wa takwimu zilizopo Kati ya Nchi 10 bora zinazoongoza kwa kasi ya ukuaji uchumi duniani, Nchi 5 zinatoka Bara la Afrika, hii ni fursa ambayo haina budi kuitumia Afrika katika kuleta maendeleo kwa ustawi wa wananchi’’ alisema Rais Magufuli.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Tanzania kwa upande wake imepiga hatua kubwa za maendeleo katika Nchi za Bara la Afrika kwa kuwa imeimarisha sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafiri na kuweka mazingira bora ya uwekezaji.

Aidha aliwataka Viongozi wa NORDIC kutumia fursa zilizopo katika Bara la Afrika kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa viwanda vya malighafi, kwa kuwa bidhaa nyingi za Afrika zimekuwa zikisafirishwa kwenda kuuzwa nje ya Nchi, hivyo wawekezaji hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Bara la Afrika.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Prof. Palamagamba Kabudi alisema kwa miaka mingi sasa Nchi za NORDIC zimekuwa rafiki wa kweli kwa Nchi za Bara Afrika ikiwemo Tanzania ambapo tangu uhuru wa Tanzania Nchi hizo zimekuwa zikisaidia ujenzi wa miradi mbali ya maendeleo nchini.

Kwa mujibu wa Prof. Kabudi alisema katika Mkutano huo, Mawaziri wa Nchi za NORDIC na wale wa Bara la Afrika watapata fursa ya kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo diplomasia ya uchumi na masuala ya ulinzi na usalama na kuweka mkakati wa pamoja utakaowezesha nchi hizo kufikia malengo waliyojiwekea.

‘Suala la Mpango wa Maendeleo Endelevu wa mwaka 2030 pia ni moja ya maeneo yatakayojadiliwa na Mawaziri wa Nchi hizi, tutaliangalia kwa undani zaidi suala la mabadiliko ya tabia nchi katika namna bora ya kukabiliana na changamoto zake katika Mataifa yetu ya Bara la Afrika’’ alisema Prof. Kabudi.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Ine Eriksen Soreide alisema Nchi za NORDIC zitaendelea kushirkiana na Mataifa ya Bara la Afrika katika kuleta maendeleo ya wananchi pamoja na mipango ya pamoja ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya binadamu ikiwemo ugaidi na magonjwa ya milipuko.

Nchi za NORDIC zitaundwa na Nchi tano za Sweden, Norway, Finland, Iceland na Denmark pamoja ikiwa na ushirikiano wa Nchi 29 za Bara la Afrika.
 
Tanzania ni tajiri kweli,ilihali hata madarasa hayana sakafu,wanafunzi wanakaa chini,kila siku wanatafutwa wafadhili ili kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.bado tuna bajeti tegemezi.
Tuache kujimwabafai hata pale tusipostahili.
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania Endelea kuchapa kazi

Tanzania ni Nchi tajiri, inahitaji mipango tu ya kugeuza raslimali kuwa utajiri

Tunakuamini kipenzi cha watu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameshiriki Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa Nchi za Afrika na NORDIC unaofanyika akatika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es salaam.

________
HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWA UFUPI

Viongozi wa nchi za Afrika tumetambua muafaka wetu uko miongoni mwetu, uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na tija kama hatuna ukombozi wa kiuchumi, lazima tubadilishe muelekeo na tushirikiane na nchi zenye nia ya kushirikiana kiuchumi.

Ukilinganisha pato la nchi na Nordic na nchi Afrika ni tofauti sana, tofauti ni kubwa sana na sisi Waafrika lazima tijitafakari na tujifunze kwa nchi marafiki zetu wa Nordic.

Kwa miaka ya hivi karibuni nchi nyingi za Afrika zimepiga hatua kwenye uchumi, katika nchi zinazoongoza kwa ukuaji mzuri wa uchumi, tano zinatoka Afrika. Kuhusu amani, nchi nyingi Afrika zina amani licha ya kuwepo kwa changamoto kwa nchi chache.

Nchi yetu inashika nafasi ya pili kuwa na vivutio vingi vya utalii, tuna Mbuga za wanyama, Milima na miti mirefu Duniani iko kwetu.

Sisi pia tunapambana na rushwa, kwa sababu rushwa ni moja ya kansa ya uwekezaji barani Afrika.

Ili kuvutia biashara katika Bara letu la Afrika ni lazima tuweke mazingira mazuri na wezeshi kwa wafanyabiashara, lakini pia tuondoe urasimu.

Tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania, kwa sababu tuna amani, ukuaji mzuri wa uchumi (uchumi unaokua kwa asilimia 7) lakini pia Tanzania ni mwanachama wa SADC.

Magufuli azifagilia nchi za Nordic kusaidia ukombozi Afrika

Rais Dk. John Magufuli amezipongeza nchi za Nordic kutokana na msaada wake mkubwa katika kusaidia harakati za ukombozi kwenye nchi mbalimbali hususani kusini mwa Afrika.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa Novemba 8, katika ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje na nchi za Nordic ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji wa mkutano huo uliozikutanisha nchi 34 zikiwamo za Nordic.

“Kama mnavyofahamu Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa harakati za ukombozi ambapo kulikuwa na kambi nyingi za wakimbizi hivyo tunafahamu mchango mkubwa wa Nordic ikiwamo ujenzi wa Chuo cha Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini cha Solomon Malangu Freedom College (Somapco), kilichojengwa mwaka 1975 mkoani Morogoro.

“Ikumbukwe kuwa nyakati hizo haikuwa rahisi kwa mataifa ya Ulaya kuja kuunga mkono jitihada za ukombozi kwa nchi za Afrika, lakini marafiki zetu wa nchi za Nordic walikuja, na huu ndiyo upekee wa nchi za Nordic ahsanteni sana,” amesema Rais Magufuli.

Amesema hata baada ya kusimamia harakati za kupigania uhuru nchi za Nordic zimeendelea kuwa washirika wa maendeleo wa nchi za Afrika, ambapo wameshirikiana katika nyanja nyingi ikiwamo afya, elimu, kilimo, sayansi, kilimo, amani na usalama.

Aidha, amesema nchi hizo hususani Tanzania, imenufaika na miradi mingi ya nchi za Nordic ikiwamo Kituo cha Elimu Kibaha (Kibaha Education Centre) na Kituo cha Utafiti cha Kilimo Uyole.

“Nchi za Nordic zilitusaidia kujenga vyuo vya ufundi na pia kwenye kampeni za kufuta ujinga (Illiteracy Campaign Programme), iliyotekelezwa miaka ya ‘70 na kuiwezesha Tanzania kufuta ujinga kwa ailimia 98 na hivyo kuwa nchi za kwanza Afrika kufikia kiwango hicho, sina hakika kama kiwango hicho kimeshafikiwa na nchi nyingine.

“Leo nataka niwashukuru kwa sababu na mimi ni product ya wanufaika wa nchi za Nordic kwa sababu digrii yangu ya kwanza kwa miaka yote mitatu nikifabnya thesis na research zilitolewa fedha na nchi ya Norway kwa kupiftia Shirika la Norad kwa hiyo na mimi nawashukuru.

“Kwa kuzingatia hayo yote napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika na tunawaomba mawaziri wetu wa mambo ya nje mfikishe salamu zetu kwa nchi zenu,” amesema.

Mtanzania

Medium of communication ilikuwa ipi? mbona hamsemi?
 
Hivi alishawapa majibu wale wa Haki za binadamu au bado? Atupeajibu kwanza.
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania Endelea kuchapa kazi

Matunda ya kuwa mwenyekiti wa sadic yanaonekana Sasa
Hivi na wazazi wako huwa unawaambia hongera? Make tangu asubuhi hii ni hongera ya 100 kwa wanaume wenzako ila kwa Wazazi wako hata salamu hakuna
 
Kuna wanafunzi wanajisaidia vichakani unadai Tanzania ji Tajiri? Wewe hapo ulipo Wazazi wako wana umasikini wa kutisha kule kijijini. Hahaa acha ujinga wewe
Mawaziri wa nchi tajiri zaidi Africa Wakutana wakiongozwa na nchi mwenyeji Tanzania. Mungu ibariki Africa Maendeleo hayana Chama....

Kuanzia sasa hatutaki tena misaada ya Mabeberu #MATAGA View attachment 1257644
 
Anaipaisha wapi? Kwenye vyombo vya habari?

Mnauona umasili wa ndugu zenu kule kijijini?
Make Tanzania great Again

Hatuna wasiwasi chini ya Mzalendo Magufuli

Anaipaisha Tanzania

Waziri moja wa Norway ametokwa na machozi baada ya kuonana na kiongozi bora Magufuli

Amesema anatamani kuwa Mtanzania
 
Nashangaa. Nenda Vijijiini uone umasikinj Kiongozi. Aisee unaweza lia eti

Back
Top Bottom