Mkutano wa CAF wapitisha maombi ya Zanzibar kuwa mwanachama huru

Mungu ibariki zanzibariiiiiiii wabaliki Viongozi wakeee Hekima Umoja na amani hizi ni ngao zetu Zanzibariii na watu wake ibariki zanzibariii ......
 
Popote tu wakasimamishe bendera yao, wawe wanachama kila shirikisho, sioni shida.

Swali ni je? Gharama hizo....atabeba nani???
Refer "UMEME".
 
Reactions: Qj_
Wao wana wimbo wao na bendera yao,hawajaiba kama sisi tulioiba Nkosi si kereli.
 
Tulikosea kwenye katiba mpya maana ndio sehemu pekeee ambao tungeliweka mambo sawa bila kuchekwa na dunia, tukaipoteza!
Tangu 1964 safari imekuwa ya kulazimishana hadi wengine wamefia kwenye vifungo vya nyumbani, badala ya kueleza mambo ya msingi viongozi wanatumia hotuba nzima kueleza kuwa sijui nchi au sio nchi. Haya mambo inabidi yawe wazi na dalili zilivyo muungano wetu hauwezi kusurvive!
 
Wachezaji Wote wanatokea bara...


Ngoja tuwafanyie fitina muozee benchi
 
Reactions: Qj_
Great Britain *Uingereza) ni muungano wa Visiwa vya Scotland, Wales na Ireland. Hapa kila kisiwa ni mwanachama wa chama cha Mpira Ulaya; Sasa kuna ubaya gani kwa Zanzibar?
Ni kwasababu ya Uelewa Wako Muungano wetu uko Tofauti sana na Great Britain.
 
Dalili za Mvua ni mawingu hata kama mnatumia vibatari kazeni hapo hapo
 
Game kati ya Zanzibar na SISI, sisi tutajiiita Tanzania Bara kwa unafki wetu!
Ule mwaka kilimanjaro stars na zanzibar herous wamekutana kombe la challenge super sport wakionesha mubashara waliandika " Tanzania vs Zanzibar"
 
mkileta fyokofyoko mtakiona cha mtema mkuni...
 
Acha ushamba mkuu! Angalia namna UK ilivyo! Wales, England na Scotland vinajitegemea! Soma uelimike sio kukariria mitihani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…