Mkutano wa CAF wapitisha maombi ya Zanzibar kuwa mwanachama huru

Mkutano wa CAF wapitisha maombi ya Zanzibar kuwa mwanachama huru

Hongera Zanzibar kwa hatua kubwa kuelekea Uhuru kamili. Sasa muende FIFA mkifanikiwa huko mmalizie UN . Mengine yatajisawazisha yenyewe tu. Mkifikia hapo mtakuwa mmetusaidia sana kurejesha "Tanganyika" yetu na kuhitimisha unafiki wa wanasiasa kuhusu Muungano.
 
Hapo patamu sana.Itabidi tufanye kama UK.England,Scotland,Wales kila nchi na wimbo na bendera yake.Serikali itabidi ilitoe ufafanuzi.Hivi hawa CAF wamewasiliana na Serikali yetu kabla ya kutoa uamuzi.Naona una kila.Chembe ya kuvunja muungano wetu.
Serikali ya Muungano nayo ilishiriki kupigania Zanzibar ipewe uanachama CAF, ndiyo maana TFF ilipiga kampeni. Zanzibar tayari wana nyimbo na bendera, hata Tanganyika ina nyimbo na bendera kiasi cha kurudishwa tu. Ila sema tunapaswa kutumia Tanzania Bara au Tanganyika? Unafiki utaanzia hapa!
 
Serikali ya Muungano nayo ilishiriki kupigania Zanzibar ipewe uanachama CAF, ndiyo maana TFF ilipiga kampeni. Zanzibar tayari wana nyimbo na bendera, hata Tanganyika ina nyimbo na bendera kiasi cha kurudishwa tu. Ila sema tunapaswa kutumia Tanzania Bara au Tanganyika? Unafiki utaanzia hapa!
Haa haa Asante Mpweke kwa taarifa.Tusubiri tuone
 
Jina"Tanzania" lina herufi za Zanzibar(Zan) hivyo inabidi TFF sasa iwe na maana ya "Tanganyika"Football Federation. Hongera Zanzibar, sasa muende UN kudai kiti chenu. Hayati Mchungaji Mtikila angefurahia mno hatua hii.
 
Shirikisho la soka la afrika kuanzia leo, Zanzibar nayo ni mwanachama huru.

Maswali:
1. Je, Wachezaji wa zanzibar wanaochezea huku bara watakua na vibali maalum na vilevile wa bara waliopo znz watakua wana vibali maalum au itakuaje?

2. Kwahiyo zanzibar sasa ishakua nchi?

3. Maana wakienda kucheza nje ya nchi watapandisha bendera ya Zanzibar au ya muungano?

Mwisho: ahmmed ahmmed. ndio RAIS wa caf mpya wakutoka nchini madagaska good nice.
 
Sasa kiCAF Zanzibar ni mamlaka kamili. Wachezaji wa Zanzibar watahitaji vibali kucheza Bara
 
Watakuwa ni sawa na wachezaji wengine wa kigeni.
 
Na sisi tutatumia upi coz itakuwa sio timu ya Tanzania tena bali Tanganyika
Watarudishiwa tu kiti chao cha UN kwani bado kipo
180213.jpg
 
Hongera kwao....inakaribia miaka saba sasa tangu watume maombi yao.
Naiona Zanzibar ikifanya vizuri kuliko Tanganyika Stars!

Sasa ikitokea tunacheza nao katika mashindano ya Afcon.......timu kutoka Tanganyika itapeperusha bendera gani?
Itaimba wimbo upi wa Taifa
Zanzibar ina rais, bendera, wimbo wake
 
Back
Top Bottom