Mkutano wa dharura waitishwa NEC, Makonda atatenguliwa rasmi Uenezi, Mwenyekiti alivunja Katiba ya chama kumwengua

Mkutano wa dharura waitishwa NEC, Makonda atatenguliwa rasmi Uenezi, Mwenyekiti alivunja Katiba ya chama kumwengua

Anhaaa, wanamtoa Uenezi halafu ndio wanamwapisha RC

Kama uetuzi wa u-RC hauna tatizo, kwa nini wanamtoa Uenezi ????
Sioni tatizo! Kuna mambo mawili; hoja ya msingi ni kukiukwa taratibu. Nikadefend
Anhaaa, wanamtoa Uenezi halafu ndio wanamwapisha RC

Kama uetuzi wa u-RC hauna tatizo, kwa nini wanamtoa Uenezi ????
Sioni tatizo! Nilimdefend Mhe. Rais kwa madai kakiuka katiba. Nikasema taratibu za kikatiba mbona zinaendelea! Pili, kuondolewa uenezi kwa uteuzi wa URC pia sioni shida.

Cheo ni dhamana! Pia, Mhe. Rais ndiye alimteua na anajua kwa nini amefanya hivyo. Mhe. Makonda bado ni kijana. Kuna kesho yake nzuri tu. 🙏🙏🙏
 
ASIYEKUTEUA HAWEZI KUKUTENGUA

KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI
TOLEO LA 2022

IBARA YA 102

Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa
zitakuwa zifuatazo:-

KIFUNGU CHA 12
Kuchagua Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa wa Itikadi na Uenezi

KIFUNGU CHA 21
Kumwachisha au kumfukuza Uongozi
kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa
mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu
ya CCM ya Taifa.

=================================

CCM leo imeitisha kikao cha dharura cha NEC kwa nia ya ku save face ya Mwenyekiti, yani kufunika mchemko wa kuvunjwa Katiba ya CCM uliofanywa na Mwenyekiti. Watatengua nafasi ya Makonda na kuteua Mwenezi mpya. Lakini Mwenyekiti alishamtengua kivyake vyake tayari na kumfanya RC Arusha

Viongozi wasipofata taratibu, sheria, kanuni, itifaki za chama na serikali, wanatuma ujumbe kwa wengine wote nchini yao kwamba kiongozi ana mamlaka ndani ya eneo lake kufanya lolote analotaka....
CCM gani ambayo mwenyekiti anahitaji kusave nafasi yake? Vijana wa leo huwa wanatembea vichwa vyao vikiwa usingizini
 
Naamini kazi mpya inaanza pale mteuliwa anapoapishwa, kwa maana nyingine naweza kusema Makonda bado anashikilia funguo za uenezi mpaka sasa, akishapewa kazi hiyo mwingine, ndipo na Makonda atakabidhi ofisi.

This applies hata kule Arusha kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mpaka sasa ofisi ile haimjui Makonda, kwa maana hiyo funguo za ofisi bado anazo Mongela, tangazo la uteuzi haliwezi kuendana na kuanza kwa utekelezaji wa majukumu hapo hapo, ile ni kama alert tu, ndio maana kuna viapo.

Hivyo sioni popote palipoharibika.
 
Leo hamjaanza kwa kumshukuru Mama Samia kwa kumtengua zero brain?
 
Hatimaye member mwenzetu wa JF ameteuliwa kuwa mwenezi wa CCM. Hongera Lucas
 
Katiba ya CCM ni kikaratasi tu
Kwa sauti ya mwenyekiti wa chama.
 
Shamba la bwana heri, ng'ombe wa bwana heri.....
 
ASIYEKUTEUA HAWEZI KUKUTENGUA

KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI
TOLEO LA 2022

IBARA YA 102

Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa
zitakuwa zifuatazo:-

KIFUNGU CHA 12
Kuchagua Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa wa Itikadi na Uenezi

KIFUNGU CHA 21
Kumwachisha au kumfukuza Uongozi
kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa
mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu
ya CCM ya Taifa.

=================================

CCM leo imeitisha kikao cha dharura cha NEC kwa nia ya ku save face ya Mwenyekiti, yani kufunika mchemko wa kuvunjwa Katiba ya CCM uliofanywa na Mwenyekiti. Watatengua nafasi ya Makonda na kuteua Mwenezi mpya. Lakini Mwenyekiti alishamtengua kivyake vyake tayari na kumfanya RC Arusha

Viongozi wasipofata taratibu, sheria, kanuni, itifaki za chama na serikali, wanatuma ujumbe kwa wengine wote nchini yao kwamba kiongozi ana mamlaka ndani ya eneo lake kufanya lolote analotaka....
Kama ni kumtengua Makonda, mimi CCM niko tayari kumsamehe Mwenyekiti, hata kama hajakosea
 
ASIYEKUTEUA HAWEZI KUKUTENGUA

KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI
TOLEO LA 2022

IBARA YA 102

Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa
zitakuwa zifuatazo:-

KIFUNGU CHA 12
Kuchagua Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa wa Itikadi na Uenezi

KIFUNGU CHA 21
Kumwachisha au kumfukuza Uongozi
kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa
mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu
ya CCM ya Taifa.

=================================

CCM leo imeitisha kikao cha dharura cha NEC kwa nia ya ku save face ya Mwenyekiti, yani kufunika mchemko wa kuvunjwa Katiba ya CCM uliofanywa na Mwenyekiti. Watatengua nafasi ya Makonda na kuteua Mwenezi mpya. Lakini Mwenyekiti alishamtengua kivyake vyake tayari na kumfanya RC Arusha

Viongozi wasipofata taratibu, sheria, kanuni, itifaki za chama na serikali, wanatuma ujumbe kwa wengine wote nchini yao kwamba kiongozi ana mamlaka ndani ya eneo lake kufanya lolote analotaka....
Rais hakutengua uteuzi wa Makonda kama mwenezi bali yeye alimteua kuwa RC, kitendo cha kuwa RC kinamuondolea sifa ya kuwa mwenezi hivyo kulazimu NEC kukutana kujaza nafasi ya mwenezi ambayo iko wazi.
Mwenyekiti hana mamlaka ya kumtengua katibu yeyote wa NEC kikatiba ila alichofanya ni technical utenguzi kwa kutumia mamlaka ya urais kumteua kuwa RC.
 
Imeshatokea Na Mama Mitano Tena Anaupiga Mwingi Sana Mpaka Unatoka Nje
 
Sawa, nakuelewa! Tumkosoea kwa fact basi! Sasa mtu anasemaje Mhe. Rais kavunja katiba ya Chama wakati taratibu zenyewe za Katiba zinaendelea? Kikao cha Chama kitaanza na kufuatia uapisho.🙏🙏🙏
Kipi kilipaswa kuanza, ama kikao hiki cha dharula ili kojadili nyongeza ya majukumu ya mwenezi au hivi alivyopewa halafu kikao ndo kifuate kuweka muhuri wa Mwenyekiti?

Ingawa sijaisoma vizuri katiba ya ccm hapa upo ukakasi, maana hata kama Mwenyekiti alikuwa anamhitaji Makonda ktk nafasi nyingine ilikuwa vizuri zaidi kuanza na japo kikao cha dharula kama hiki ili walau wajumbe wapate kutia baraka hata kama hawawezi kupinga maamuzi ya Mwenyekiti. Hii inaipa halmashauri/ kamati heshima na kujiona kuwa wametekeleza wajibu hata kama ni usanii.
 
Back
Top Bottom