Mkutano wa dharura waitishwa NEC, Makonda atatenguliwa rasmi Uenezi, Mwenyekiti alivunja Katiba ya chama kumwengua

Mkutano wa dharura waitishwa NEC, Makonda atatenguliwa rasmi Uenezi, Mwenyekiti alivunja Katiba ya chama kumwengua

Mwenyekiti hajamtengua msemaji wa chama ila kamuongezea jukumu na sijaona pahali pameandikwa katenguliwa uenezi ila kateuliwa kuwa mkuu wa mkoa na wala sio kosa wala hajakiuka katiba msipotoshe
Mnateseka sana kmmmk. Kwisha habari yenu. Tuliwaambia jamaa yenu hafugiki. Na huko chuga ni suala la muda tu
 
Kipi kilipaswa kuanza, ama kikao hiki cha dharula ili kojadili nyongeza ya majukumu ya mwenezi au hivi alivyopewa halafu kikao ndo kifuate kuweka muhuri wa Mwenyekiti?

Ingawa sijaisoma vizuri katiba ya ccm hapa upo ukakasi, maana hata kama Mwenyekiti alikuwa anamhitaji Makonda ktk nafasi nyingine ilikuwa vizuri zaidi kuanza na japo kikao cha dharula kama hiki ili walau wajumbe wapate kutia baraka hata kama hawawezi kupinga maamuzi ya Mwenyekiti. Hii inaipa halmashauri/ kamati heshima na kujiona kuwa wametekeleza wajibu hata kama ni usanii.
Kumbuka Mhe. Makonda hajaapishwa pia, taarifa ya Ikulu haijasema kama kaondolewa katika nafasi ya Uenezi! Ndiyo maana nimesema kama ataondolewa basi hakuna sehemu Mhe. Rais atakuwa amekiuka Katiba. Utaratibu huu pia ulitumika kwa Mhe. Sophia Mjema. So kuhusu nini kilipaswa kuanza; bado uamuzi wa Mhe. Rais uko sawa kama ulivyo.🙏🙏🙏
 
Kumbuka Mhe. Makonda hajaapishwa pia, taarifa ya Ikulu haijasema kama kaondolewa katika nafasi ya Uenezi! Ndiyo maana nimesema kama ataondolewa basi hakuna sehemu Mhe. Rais atakuwa amekiuka Katiba. Utaratibu huu pia ulitumika kwa Mhe. Sophia Mjema. So kuhusu nini kilipaswa kuanza; bado uamuzi wa Mhe. Rais uko sawa kama ulivyo.🙏🙏🙏
Tuache katiba maana inaweza kuwa na shimo kwamba haielezi kinagaubaga juu ya jambo hili. Ila tujadili ktk hali ya kimantiki, je ni busara kuikalisha halmashauri ipendekeze na kupitisha mteule wa chama kisha huyu mteule akawa anaweza kufukuzwa kwa namna yoyote bila halmashauri iliyomjadili kuhusishwa eti wahushwe baada ya kuondolewa?
 
Viongozi wasipofata taratibu, sheria, kanuni, itifaki za chama na serikali, wanatuma ujumbe kwa wengine wote nchini yao kwamba kiongozi ana mamlaka ndani ya eneo lake kufanya lolote analotaka....[/SIZE][/FONT]
Wanaanzaga very humble, baadae, wananza kuota mapembe!, yanachomoza mdogo mdogo, yasipodhibitiwa mapema,
images (15).jpeg

yatakuwa makubwa kama ya ngomb'e wa ankole, yatakuwa na ncha kali..., yatachoma hayo!
P
 
Tuache katiba maana inaweza kuwa na shimo kwamba haielezi kinagaubaga juu ya jambo hili. Ila tujadili ktk hali ya kimantiki, je ni busara kuikalisha halmashauri ipendekeze na kupitisha mteule wa chama kisha huyu mteule akawa anaweza kufukuzwa kwa namna yoyote bila halmashauri iliyomjadili kuhusishwa eti wahushwe baada ya kuondolewa?
Katika hiyo mantiki; anayepeleka jina lake lijadiliwe ni Mhe. Rais na Mwenyekiti wa Chama. Ndiyo maana nimesema kwanza, hakuna sehemu hadi hivi sasa Mwenezi ameondolewa. Kama kutakuwa na uamuzi huo basi utaratibu utakuwa sawa na uliotumika kumteua. Kitu kimoja tu; sioni mantiki kumlaumu Mhe. Raia kama alivyosema mleta mada.
 
ASIYEKUTEUA HAWEZI KUKUTENGUA

KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI
TOLEO LA 2022

IBARA YA 102

Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa
zitakuwa zifuatazo:-

KIFUNGU CHA 12
Kuchagua Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa wa Itikadi na Uenezi

KIFUNGU CHA 21
Kumwachisha au kumfukuza Uongozi
kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa
mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu
ya CCM ya Taifa.


=================================

CCM leo imeitisha kikao cha dharura cha NEC kwa nia ya ku save face ya Mwenyekiti, yani kufunika mchemko wa kuvunjwa Katiba ya CCM uliofanywa na Mwenyekiti. Watatengua nafasi ya Makonda na kuteua Mwenezi mpya. Lakini Mwenyekiti alishamtengua kivyake vyake tayari na kumfanya RC Arusha

Viongozi wasipofata taratibu, sheria, kanuni, itifaki za chama na serikali, wanatuma ujumbe kwa wengine wote nchini yao kwamba kiongozi ana mamlaka ndani ya eneo lake kufanya lolote analotaka....
Hizo huwa ni formalities tu !
Lakini ukweli utabaki pale pale !
Mwenyekiti ndio kila kitu na anaweza kufanya chochote !!🙏🙏
 
Mkuu,

Kwa kanuni ipi?

Mbona Mwenyekiti wa CCM ni Rais tayari?

Ni kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za CCM.

RAIS, au kiongozi yeyote wa serikali, hawezi kuwa kiongozi ndani ya chama bila idhini ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Mwenyeki hakupata idhini ya Kamati Kuu. Ndo maana Makonda kaitishiwa kikao NEC wamtengue haraka.
 
Samia kakamilisha the dirty job, kamuondoa Makonda kinguvu.

The take home lesson ni kuwa KATIBA ya CCM haina nguvu mbele ya Mwenyekiti.

Siku Mwenyekiti akiona Katibu Mkuu Kinana anamzibia mishe zake CCM (kumbuka Samia anapenda sana viongozi vitoto vitoto vinavyomwamkia Shikamoo Mama akiingia kwenye kikao), cha kufanya ni kumteua Kinana kuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa au Kamishna wa Tume ya Rasilimali watu na utawala serikalini.

Ni somo juu ya uandishi wa Katiba zetu kwenye jamii za watu wasioheshimu Katiba.
 
Mpaka sasa Makonda Bado ni Katibu wa NEC itikadi na Uenezi maana hakuna mahali popote panaposema kaenguliwa, katumbuliwa au kaachishwa ila kilichofanyika ni kuteuliwa ukuu wa mkoa
KWahiyo uenezi una nafasi mbili? Kwamba Makonda bado yumo na Makala naye yumo kwenye nafasi hiyo?
 
Back
Top Bottom