Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]


Du! Kiby umeniacha hoi saaana . . . msisitizo wako natumaini utaungwa mkono na Wadau. Nashauri wewe na WoS muwe katika kamati maalumu "Task Force" au Kikosi kazi cha kushughulikia suala hili ili tuweze kupata mapendekezo makini.
 
Mwenyekiti..uteuzi huu ni batili..huna mamlaka ya kujipa ujiko wa uenyekiti..kwa msingi huo huwezi kuniteua.Teuzi hizi nazo zinafanya kazi nzima iwe batili

WoS tumekubaliana kuwa lugha ya matusi na kashfa na kejeli isiwepo. Tunataka uvumilivu wa kisiasa. Sasa ukisema "Batili" sijui "Ujiko" huoni kuwa unanitusi? Mimi si sawa na baba yako . . . tafadhali simamia hoja zaako tu . . . Teeh teee haaa haaa

Sasa tuje kwenye hoja ya msingi . . . Kwa heshima na taadhima naomba nipendekeze kuwa wewe na kiby muwe katika hiyo kamati . . . Naona wadau wote hapa jangwani wanasema "Saaaaawwwwaaaaa" kwa hiyo yunaomba ukubali wenu . . .
 

Nimekusoma Kitumbo . . . So hili nalo ni zuri sana na tunaliingiza katika katiba . . . na hivyo kuimarisha hoja kuwa na nguvu ya "Kuunda katiba Mpya"

Vipi katika suala la Umasikini wa Watanzania? Hii si agenda kuu?
 
Mi naomba atakayechaguliwa kwanza atuambie hadhi ya Zanzibar ni nchi ama si nchi?:confused2::confused2:

Kaizer, kwanza umekuja hapa Jangwani umechelewa, halafu nakuona kama una Beer Can . . . Ni sawa? halafu unaongea wakati wengine wanaongea na hujapewa ruhusa . . . Jamani tuwe na uvumilivu wa kisiasa kwa kupeana muda . . .

Sawa. hata hivyo hoja yako ni ya msingi. Kwa hiyo kuna issues katika Muungano. Sasa ufumbuzi wake ni nini? Au tuitishe "Kura ya Maoni Juu ya Muundo Wa Muungano"?
 

Ni kweli inachanganya . . . . niliona kuna mwanachama moja hapa Dr. Mvungi alilitolea ufafanuzi wa kina.

Kwa sasa kwa kuwa Rais wa ZNZ bado hana mamlaka ya Ki-Nchi Nje ya Tanzania, labda nalo liingie katika mjadala mpana wa Muungano.
 
Mimi nashauri ipatikane tume huru ya uchaguzi ambayo haitachaguliwa na rais wala kuwajibika chini ya utawala ulio madarakani.

Twahitaji tume itakayochaguliwa ithibitishwe na bunge na kuwajibika kwa bunge.


Asante Mchukia Ufisadi . . . hii ni hoja ya Nguvu. Tunaiweka hivi: Chama kitakachoingia madarakani "Kiunde Tume Huru ya Uchaguzi itakayo wajibika kwa Bunge". Pia hili nalo liingie katika katiba ili lisije likachakachuliwa.
 
kama maswala ya nchi hii mengine ni "nyeti" na yanaangaliwa na watu ambao wengi si wataalam na wanaingiza nchi ktk umaskini mkubwa kwa wanainchi mana hainiingii akilini Tz ni ya ngapi sijui ktk madini fulani,maliasili zimejaa nchi zingine hakuna nk nk,basi tunaitaji uwepo/matumizi/mchango wa wataalamu waliobobea ktk fani mbalimbali na washiliki na kuamua ktk mustakhabali wa nchi yetu maana wataalam wetu wamewekwa kapuni na wanasaidia kuendeleza nchi zingine.
shame
 

Babu M nimekusoma. Hivi wewe ni moja wa Wamiliki wa Bank M?

Hoja zako zote ni za Msingi na tutazipokea kama zilivyo katika maazimio ya Mkutano.

Asante.
 

Objection!
1. Sijatumia lugha ya matusi
2. "Batili" na "Ujiko" siyo matusi wala kejeli - Nitaomba mwongozo kutoka kwa taasis y auchunguzi wa kiswahili au BAKITA ( wapo wataalamu wa kiswahili JF akina MMKJJ na wengineo watupe ufumbuzi.
3. Siwezi kukubali uteuzi kabla ya kusafisha jina langu lililochafuliwa na wewe mwenyekiti na usipofanya hivyo ndani ya siku saba nitalazimika kuchukua hatua za kisheria dhidi yako na utawajibika kwa matokeo yake.
 
Hii JF ya wannandugu nini? maana Asubuhi hii nimetuma post yangu kuwa nimefungua tu naona meseji hii ikisema mkutano wana JF online sasa nikatuma meseji sawa mpka sasa nikifuatilia siiioni Je Mods ameifuta au nini Max nielezee kwa kina

Kamanda OP, hapana JF si ya wanandugu. Ni ya wote ambao "They Dare To Talk Openly" hakuna mizengwe wala kuchakachua hapa. labda tu ni matatizo ya kiufundi upande wako au wa JF.

Tafadhali ibandike hojaa yako hapa . . .
 
Naomba majibu ndani ya masaa sita yajayo alaa Mods acha ubaguzi sisi tupo mstari wa Mbele kupinga Ufisadi kumbe wewe unausapot na kuuleta huku
:fencing:


OP lugha ya matusi si njema tafadhali . . . tutumie lugha ya kistaarabu tu kama tulivyokubaliana katika maadili ya kuendesha huu mkutano
 
My best three priorities would be:
  • Health Insurance kwa kila Mwananchi - Wananchi wote watanzania wawe na kadi za bima na hospitali zote ziwe zinakubali aina zote za Health Insurance. Na hili liwekwe kwenye katiba. Government iwe responsible kulipia sehemu ya hiyo gharama kwa mwananchi wa chini
  • Kukuza wigo wa ukusanyaji mapato na usimamizi thabiti wa hayo mapato - Serikali ibane matumizi kwa kadiri itavyowezekana kwa mambo yasiyo ya lazima na kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato kwa kuja na vyanzo vipya vya mapato; mfano kwenye nyanja ya burudani - movies, musics, selling of albams, etc. Kupunguza vikao visivyo vya lazma na kila kikao kinapoitishwa kiwe na tija inayopimika, etc. Hela zinazo patikana ziongezwe kwenye sekta ya afya na mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na SME
  • Elimu bure mpaka kidato cha nne. Na iwe ni lazima kila mwananchi afikie elimu hiyo.
 
Vipi kuhusu wanaotia na kutiwa mimba ,zaidi likihusishwa na madenti ,Ili suala watalitatua vipi kwani kusema kweli hali inatisha haina tofauti na ujambazi.


Wewe unashauri nini Mwiba . . . hoja yako ni moto hasa ukizingatia kuwa hii issue inawashinda walio wengi . . . I mean kujizuia (au wapwa wa lile jukwaa mnasemaaje"?
 
Last edited by a moderator:

Kijana acha vurugu tafadhali? Au nikuitie vijana wa Kova?

hata hivyo pointi zako zina mantiki sana:

La kwanza nadhani Tutaliingiza katika Sheria za Uchaguzi "So"Tunataka Sheria Za Uchaguzi ambazo zitatoa ushindani sawa"

La pili ni la Kikatiba. Kuwa Uwakilishi/Ubunge/Siasa iwe ni kazi ya Kujitolea. Hili naomba kwanza tupate maoni ya wengine.

La mwisho ni la kikatiba "Kupunguza Madaraka ya Rais" na Pia "Mawaziri/RC/DC wawajibike kwa Bunge" Nimekusoma.

Ni sawa?
 


Asante Aza . . . Hili tuliweke hivi "Usimamizi Mzuri na Utumiaji wa Rasilimali Zetu kwa faida ya wote katika Kuondoa umasikini"

Hapo vipi?
 

Mkuu nadhani nafasi ya mkurugenzi wa TBC itangazwe ili mtanzania yeyote mwenye uwezo aombe na chombo huru kitumike kufanya usaili. Baada ya hapo awe anareport kwa bunge na sio rais.
 

Kova Please . . .
Todo . . . Naomba TBC Mkatishe Matangazo . .
Wana JF kama hamlaani kitendo hiki mimi naachia ngazi chagueni mratibu mwingine . . .

Binti wewe kabila gani kwanza? dini gani wewe? Ooops . . . kumbe tumekataa ukabila na udini . . .

Sasa dear sikiliza basi, kuwa soft kidogo ili mambo yaende mbele . . . najua unategemea kitu kidogo labda. Mimi siwezi toa. . . . niko kimaadili zaidi . . . .

Haaa haaa hapo vipi?

Unda kamati basi tufunge mjadala.
 
Mwenyekiti tangu jana mimi nimenyoosha mkono umenitosa. Tatizo langu kubwa liko kwenye usimamizi wa rasilimali za taifa. Tuje ni mikakati endelevu ya kuhakikisha rasilimali tulizonazonazo kama madini, mbuga za wanyama n.k. zinaleta manufaa ya kweli kwa nchi na watanzania wa kawaida.
 

Du Kabengwe . . . hizi zote zimekaa vizuri. Tutaziweka katika majumuisho:
Bima ya Matibabu Kwa wote
Kupanua Wigo Wa Kukusanya kodi
Elimu Bure ya Msingi hadi kidato cha Nne
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…