Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,693
- 1,702
- Thread starter
- #121
.
Ee ipo nchi inafanya hivyo. China fisadi yeyote anaefisadi kwa kuhujumu uchumi anauawa hadhadhani mpaka kufa. Na mara nyingi huku kwetu utawasikia viongozi wakiyasifia maendelea ya haraka ya china bila kujua kwamba yanasababishwa na sheria kali zilizopelekea viongozi kuheshimu maadili ya uongozi. Kuhusu haki za binadamu ni kwamba sheria ya maumbile inaongozwa na kanuni ya uhai ambayo ni, ili kuwe na uhifadhi wa uhai ni lazima viumbe wengine wafe kwa ajili ya vingine. Sisi tunaishi kwa sababu wapo samaki, mbuzi, kuku, ngombe nk waliokufa. Na kama ukosefu wa maji, umeme, dawa, makazi bora nk vimesababisha walalahoi wengi kufa kisa ni mmoja au wachache wamefisadi pesa na miundombinu, kwa nini wasife ili kunusuru jamii ya walio wengi? NINACHOMAANISHA HAPA NI 'HAKUNA HAKI YA MTU MMOJA IKIWA HAKI HIYO INADHULUMU HAKI ZA WALIO WENGI. Mratibu mie bado nasisitiza tena nisiposikilizwa kakhyanani ntavuruga mkutano!!
Du! Kiby umeniacha hoi saaana . . . msisitizo wako natumaini utaungwa mkono na Wadau. Nashauri wewe na WoS muwe katika kamati maalumu "Task Force" au Kikosi kazi cha kushughulikia suala hili ili tuweze kupata mapendekezo makini.