Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

.
Ee ipo nchi inafanya hivyo. China fisadi yeyote anaefisadi kwa kuhujumu uchumi anauawa hadhadhani mpaka kufa. Na mara nyingi huku kwetu utawasikia viongozi wakiyasifia maendelea ya haraka ya china bila kujua kwamba yanasababishwa na sheria kali zilizopelekea viongozi kuheshimu maadili ya uongozi. Kuhusu haki za binadamu ni kwamba sheria ya maumbile inaongozwa na kanuni ya uhai ambayo ni, ili kuwe na uhifadhi wa uhai ni lazima viumbe wengine wafe kwa ajili ya vingine. Sisi tunaishi kwa sababu wapo samaki, mbuzi, kuku, ngombe nk waliokufa. Na kama ukosefu wa maji, umeme, dawa, makazi bora nk vimesababisha walalahoi wengi kufa kisa ni mmoja au wachache wamefisadi pesa na miundombinu, kwa nini wasife ili kunusuru jamii ya walio wengi? NINACHOMAANISHA HAPA NI 'HAKUNA HAKI YA MTU MMOJA IKIWA HAKI HIYO INADHULUMU HAKI ZA WALIO WENGI. Mratibu mie bado nasisitiza tena nisiposikilizwa kakhyanani ntavuruga mkutano!!

Du! Kiby umeniacha hoi saaana . . . msisitizo wako natumaini utaungwa mkono na Wadau. Nashauri wewe na WoS muwe katika kamati maalumu "Task Force" au Kikosi kazi cha kushughulikia suala hili ili tuweze kupata mapendekezo makini.
 
Mwenyekiti..uteuzi huu ni batili..huna mamlaka ya kujipa ujiko wa uenyekiti..kwa msingi huo huwezi kuniteua.Teuzi hizi nazo zinafanya kazi nzima iwe batili

WoS tumekubaliana kuwa lugha ya matusi na kashfa na kejeli isiwepo. Tunataka uvumilivu wa kisiasa. Sasa ukisema "Batili" sijui "Ujiko" huoni kuwa unanitusi? Mimi si sawa na baba yako . . . tafadhali simamia hoja zaako tu . . . Teeh teee haaa haaa

Sasa tuje kwenye hoja ya msingi . . . Kwa heshima na taadhima naomba nipendekeze kuwa wewe na kiby muwe katika hiyo kamati . . . Naona wadau wote hapa jangwani wanasema "Saaaaawwwwaaaaa" kwa hiyo yunaomba ukubali wenu . . .
 
Katika katiba mpya, swala la "balance and checks" liangaliwe kwa makini. Vyombo vya kusimamia maadili viwajibike kwa bunge na sio kiongozi wa Serikali mf. PCCB, Mawaziri wasiwe wabunge, wabunge wasiwe na majukumu ya executives...kama kuongoza bodi za mashirika

Nimekusoma Kitumbo . . . So hili nalo ni zuri sana na tunaliingiza katika katiba . . . na hivyo kuimarisha hoja kuwa na nguvu ya "Kuunda katiba Mpya"

Vipi katika suala la Umasikini wa Watanzania? Hii si agenda kuu?
 
Mi naomba atakayechaguliwa kwanza atuambie hadhi ya Zanzibar ni nchi ama si nchi?:confused2::confused2:

Kaizer, kwanza umekuja hapa Jangwani umechelewa, halafu nakuona kama una Beer Can . . . Ni sawa? halafu unaongea wakati wengine wanaongea na hujapewa ruhusa . . . Jamani tuwe na uvumilivu wa kisiasa kwa kupeana muda . . .

Sawa. hata hivyo hoja yako ni ya msingi. Kwa hiyo kuna issues katika Muungano. Sasa ufumbuzi wake ni nini? Au tuitishe "Kura ya Maoni Juu ya Muundo Wa Muungano"?
 
Jibu lilishatolewa....ina maana hadi sasa tulishapewa position ya serikali kuwa Zanzibar siyo nchi... ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano....( japo hata mimi bado nachanganyikiwa maana kama ni sehemu ya Muungano, na hapo hapo ina rais wake, bendera yake, Baraza lake la wawakilishi etc...inakuwaje, lakini coercive instruments of the State kama polisi, jeshi, etc hawana vya kwao)

Ni kweli inachanganya . . . . niliona kuna mwanachama moja hapa Dr. Mvungi alilitolea ufafanuzi wa kina.

Kwa sasa kwa kuwa Rais wa ZNZ bado hana mamlaka ya Ki-Nchi Nje ya Tanzania, labda nalo liingie katika mjadala mpana wa Muungano.
 
Mimi nashauri ipatikane tume huru ya uchaguzi ambayo haitachaguliwa na rais wala kuwajibika chini ya utawala ulio madarakani.

Twahitaji tume itakayochaguliwa ithibitishwe na bunge na kuwajibika kwa bunge.

Asante Mchukia Ufisadi . . . hii ni hoja ya Nguvu. Tunaiweka hivi: Chama kitakachoingia madarakani "Kiunde Tume Huru ya Uchaguzi itakayo wajibika kwa Bunge". Pia hili nalo liingie katika katiba ili lisije likachakachuliwa.
 
kama maswala ya nchi hii mengine ni "nyeti" na yanaangaliwa na watu ambao wengi si wataalam na wanaingiza nchi ktk umaskini mkubwa kwa wanainchi mana hainiingii akilini Tz ni ya ngapi sijui ktk madini fulani,maliasili zimejaa nchi zingine hakuna nk nk,basi tunaitaji uwepo/matumizi/mchango wa wataalamu waliobobea ktk fani mbalimbali na washiliki na kuamua ktk mustakhabali wa nchi yetu maana wataalam wetu wamewekwa kapuni na wanasaidia kuendeleza nchi zingine.
shame
 
1) Hakuna kiongozi yoyote kutibiwa nje ya nchi kwa gharama za serikali-Itasadia kuboresha hospitali zetu.

2)Marufuku kwa serikali kununua vitu nje ya nchi ambavyo vinaweza kupatia hapa hapa nchi,mfano samani.

3)Mikataba na matumizi ya serikali iwe kwenye public domain, mfano safari za rais.

Babu M nimekusoma. Hivi wewe ni moja wa Wamiliki wa Bank M?

Hoja zako zote ni za Msingi na tutazipokea kama zilivyo katika maazimio ya Mkutano.

Asante.
 
WoS tumekubaliana kuwa lugha ya matusi na kashfa na kejeli isiwepo. Tunataka uvumilivu wa kisiasa. Sasa ukisema "Batili" sijui "Ujiko" huoni kuwa unanitusi? Mimi si sawa na baba yako . . . tafadhali simamia hoja zaako tu . . . Teeh teee haaa haaa

Sasa tuje kwenye hoja ya msingi . . . Kwa heshima na taadhima naomba nipendekeze kuwa wewe na kiby muwe katika hiyo kamati . . . Naona wadau wote hapa jangwani wanasema "Saaaaawwwwaaaaa" kwa hiyo yunaomba ukubali wenu . . .

Objection!
1. Sijatumia lugha ya matusi
2. "Batili" na "Ujiko" siyo matusi wala kejeli - Nitaomba mwongozo kutoka kwa taasis y auchunguzi wa kiswahili au BAKITA ( wapo wataalamu wa kiswahili JF akina MMKJJ na wengineo watupe ufumbuzi.
3. Siwezi kukubali uteuzi kabla ya kusafisha jina langu lililochafuliwa na wewe mwenyekiti na usipofanya hivyo ndani ya siku saba nitalazimika kuchukua hatua za kisheria dhidi yako na utawajibika kwa matokeo yake.
 
Hii JF ya wannandugu nini? maana Asubuhi hii nimetuma post yangu kuwa nimefungua tu naona meseji hii ikisema mkutano wana JF online sasa nikatuma meseji sawa mpka sasa nikifuatilia siiioni Je Mods ameifuta au nini Max nielezee kwa kina

Kamanda OP, hapana JF si ya wanandugu. Ni ya wote ambao "They Dare To Talk Openly" hakuna mizengwe wala kuchakachua hapa. labda tu ni matatizo ya kiufundi upande wako au wa JF.

Tafadhali ibandike hojaa yako hapa . . .
 
Naomba majibu ndani ya masaa sita yajayo alaa Mods acha ubaguzi sisi tupo mstari wa Mbele kupinga Ufisadi kumbe wewe unausapot na kuuleta huku
:fencing:

OP lugha ya matusi si njema tafadhali . . . tutumie lugha ya kistaarabu tu kama tulivyokubaliana katika maadili ya kuendesha huu mkutano
 
My best three priorities would be:
  • Health Insurance kwa kila Mwananchi - Wananchi wote watanzania wawe na kadi za bima na hospitali zote ziwe zinakubali aina zote za Health Insurance. Na hili liwekwe kwenye katiba. Government iwe responsible kulipia sehemu ya hiyo gharama kwa mwananchi wa chini
  • Kukuza wigo wa ukusanyaji mapato na usimamizi thabiti wa hayo mapato - Serikali ibane matumizi kwa kadiri itavyowezekana kwa mambo yasiyo ya lazima na kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato kwa kuja na vyanzo vipya vya mapato; mfano kwenye nyanja ya burudani - movies, musics, selling of albams, etc. Kupunguza vikao visivyo vya lazma na kila kikao kinapoitishwa kiwe na tija inayopimika, etc. Hela zinazo patikana ziongezwe kwenye sekta ya afya na mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na SME
  • Elimu bure mpaka kidato cha nne. Na iwe ni lazima kila mwananchi afikie elimu hiyo.
 
Vipi kuhusu wanaotia na kutiwa mimba ,zaidi likihusishwa na madenti ,Ili suala watalitatua vipi kwani kusema kweli hali inatisha haina tofauti na ujambazi.

Wewe unashauri nini Mwiba . . . hoja yako ni moto hasa ukizingatia kuwa hii issue inawashinda walio wengi . . . I mean kujizuia (au wapwa wa lile jukwaa mnasemaaje"?
 
Last edited by a moderator:
M/kiti mkono wangu nimenyoosha mda mrefu bado naona siruhusiwi, basi napora mike kinguvu kwani haki haiombwi bali inachukuliwa.
Katika katiba mpya pia napendekeza iwe ma marufuku kama hivi:-
Ni marufuku mtu/taasisi/kampuni kutoa misaada kwa mtu mmoja mmoja, mfano kumpa kiroba cha unga, bati,sment, pocket money nk,labda iwe tu ni kwa dharura. Badala yake misaada itaelekezwa kwenye vikundi/taasisi ili kuwezesha miundombinu inayoweza kuharakisha maendeleo endelevu katika sector zote.
-Ni marufuku kwa kazi ya siasa kulipwa mshahara. Badala yake itakuwa ni kazi ya kujitolea na kitakachotolewa ni posho ya vikao tu. Mishahara minono na yenye kushawishi itaelekezwa kwenye ajira za kitaaluma ili kuepusha taaluma kukimbiwa na kusababisha taifa lisilozalisha ila kupiga domo mda mwingi.
-Ni marufuku watendaji wa serikali mfano wakuu wa mikoa/wilaya nk, kujihusisha na siasa. Kwa kuwezesha hili wasiteuliwe na rais badala yake wachaguliwe na wananchi na kuwajibika bungeni.

Kijana acha vurugu tafadhali? Au nikuitie vijana wa Kova?

hata hivyo pointi zako zina mantiki sana:

La kwanza nadhani Tutaliingiza katika Sheria za Uchaguzi "So"Tunataka Sheria Za Uchaguzi ambazo zitatoa ushindani sawa"

La pili ni la Kikatiba. Kuwa Uwakilishi/Ubunge/Siasa iwe ni kazi ya Kujitolea. Hili naomba kwanza tupate maoni ya wengine.

La mwisho ni la kikatiba "Kupunguza Madaraka ya Rais" na Pia "Mawaziri/RC/DC wawajibike kwa Bunge" Nimekusoma.

Ni sawa?
 
kama maswala ya nchi hii mengine ni "nyeti" na yanaangaliwa na watu ambao wengi si wataalam na wanaingiza nchi ktk umaskini mkubwa kwa wanainchi mana hainiingii akilini Tz ni ya ngapi sijui ktk madini fulani,maliasili zimejaa nchi zingine hakuna nk nk,basi tunaitaji uwepo/matumizi/mchango wa wataalamu waliobobea ktk fani mbalimbali na washiliki na kuamua ktk mustakhabali wa nchi yetu maana wataalam wetu wamewekwa kapuni na wanasaidia kuendeleza nchi zingine.
shame

Asante Aza . . . Hili tuliweke hivi "Usimamizi Mzuri na Utumiaji wa Rasilimali Zetu kwa faida ya wote katika Kuondoa umasikini"

Hapo vipi?
 
Agenda Nyingine, ambayo ni muhimu sana, nikuvifanya vyombo vya Umma, kuwa vya Umma kweli, si mali ya CCM , KIMWENENDO NA KIMTAZAMO.hapa nikuiondoa sekta ya UMMA katika soko la biashara , maana wanapokea kodi zetu, haiwezekani wapigania soko moja na vyombo vya habari binafsi.pia Mkurugenzi wa TBC ateuliwe na Rais ila athibitishwe na chombo huru.

Mkuu nadhani nafasi ya mkurugenzi wa TBC itangazwe ili mtanzania yeyote mwenye uwezo aombe na chombo huru kitumike kufanya usaili. Baada ya hapo awe anareport kwa bunge na sio rais.
 
Objection!
1. Sijatumia lugha ya matusi
2. "Batili" na "Ujiko" siyo matusi wala kejeli - Nitaomba mwongozo kutoka kwa taasis y auchunguzi wa kiswahili au BAKITA ( wapo wataalamu wa kiswahili JF akina MMKJJ na wengineo watupe ufumbuzi.
3. Siwezi kukubali uteuzi kabla ya kusafisha jina langu lililochafuliwa na wewe mwenyekiti na usipofanya hivyo ndani ya siku saba nitalazimika kuchukua hatua za kisheria dhidi yako na utawajibika kwa matokeo yake.

Kova Please . . .
Todo . . . Naomba TBC Mkatishe Matangazo . .
Wana JF kama hamlaani kitendo hiki mimi naachia ngazi chagueni mratibu mwingine . . .

Binti wewe kabila gani kwanza? dini gani wewe? Ooops . . . kumbe tumekataa ukabila na udini . . .

Sasa dear sikiliza basi, kuwa soft kidogo ili mambo yaende mbele . . . najua unategemea kitu kidogo labda. Mimi siwezi toa. . . . niko kimaadili zaidi . . . .

Haaa haaa hapo vipi?

Unda kamati basi tufunge mjadala.
 
Mwenyekiti tangu jana mimi nimenyoosha mkono umenitosa. Tatizo langu kubwa liko kwenye usimamizi wa rasilimali za taifa. Tuje ni mikakati endelevu ya kuhakikisha rasilimali tulizonazonazo kama madini, mbuga za wanyama n.k. zinaleta manufaa ya kweli kwa nchi na watanzania wa kawaida.
 
My best three priorities would be:
  • Health Insurance kwa kila Mwananchi - Wananchi wote watanzania wawe na kadi za bima na hospitali zote ziwe zinakubali aina zote za Health Insurance. Na hili liwekwe kwenye katiba. Government iwe responsible kulipia sehemu ya hiyo gharama kwa mwananchi wa chini
  • Kukuza wigo wa ukusanyaji mapato na usimamizi thabiti wa hayo mapato - Serikali ibane matumizi kwa kadiri itavyowezekana kwa mambo yasiyo ya lazima na kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato kwa kuja na vyanzo vipya vya mapato; mfano kwenye nyanja ya burudani - movies, musics, selling of albams, etc. Kupunguza vikao visivyo vya lazma na kila kikao kinapoitishwa kiwe na tija inayopimika, etc. Hela zinazo patikana ziongezwe kwenye sekta ya afya na mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na SME
  • Elimu bure mpaka kidato cha nne. Na iwe ni lazima kila mwananchi afikie elimu hiyo.

Du Kabengwe . . . hizi zote zimekaa vizuri. Tutaziweka katika majumuisho:
Bima ya Matibabu Kwa wote
Kupanua Wigo Wa Kukusanya kodi
Elimu Bure ya Msingi hadi kidato cha Nne
 
Back
Top Bottom