Agenda zangu kuu 2010:
1. KUANDIKA KATIBA MPYA: Mchakato uanze ndani ya mwaka mmoja tangu kuingia madarakani. Katiba iandikwe na wadau wanaowakilisha makundi mengi iwezekanavyo. Hapa ndipo tunaweza kuweka vifungu vinavyotoa maelekezo muhimu ya jinsi ya kuongoza nchi,ulinzi wa raslimali zetu, uadilifu, vita dhidi ya ufisadi (zero tolerance kwa mafisadi), n.k.
2. ELIMU: Elimu bora kwa kila Mtanzania katika wigo mpana (ubora wa elimu, walimu, vifaa vya kufundishia, mazingira elimu inakotolea n.k.). Pia suala la utafiti na ugunduzi lipewe kipaumbele si kwa maneno tu bali kwa sera, sheria na budget.
3. KILIMO: Kilimo katika mtazamo wa uzalishaji na uendelezaji wa viwanda badala ya uchuuzi na utumikishaji wa wakulima.
4. MIUNDOMBINU: Hapa ni kuweka mkazo si kwenye wingi tu bali ubora wa miundombinu yetu.
5. ELIMU, ELIMU ELIMU, ELIMU........ ++++++++ AFYA.