Uchaguzi 2020 Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM: Dkt. Hussein Ally Mwinyi achaguliwa Kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM. Membe afukuzwa rasmi

Uchaguzi 2020 Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM: Dkt. Hussein Ally Mwinyi achaguliwa Kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM. Membe afukuzwa rasmi

Mpaka pale wajumbe wa Zanzibar watakapoku watakapokuwa na wingi wa kutosha kujiamulia hatma ya Rais wao, wataendelea kuburuzwa na wajumbe wa Bara miaka yote wao wataendelee kushangilia tu, CCM juu..CCM juu...
 
CHADEMA kwa sasa wamekuwa wachambuzi wa Siasa za ndani ya CCM!

Suala la Urais wa Zanzibar ndani ya CCM kwa sasa ni hoja iliyofungwa jana.

Mtu mwenye akili timamu anajua Dk Hussein Mwinyi ni Rais mtarajiwa wa Zanzibar!
 
Ifike mda hata wale ccm maslahi waungane na wazanzibari wenzao kujikomboa kama walivyojaribu 2009 chini ya Karume Jr.
Vyenginevyo wakubali tu kutawaliwa chini ya mwinyi ni mbili kuelekea moja maana yake ndo wameyazika mapinduzi rasmi.
Yupo kwa mslahi ya waliomchagua, si mzanzibari halisi na hata hayo mapinduzi ya 1964 hayajui.
Sijui wanakwama wapi ccm wa Zanzibar jinsi wanavotumika kosa kubwa walilifanya walipounganisha ASP na TANU maamuzi yakahamia dodoma sijui wanajiaikiaje sasa inauma kwa kweli.
 
Ukweli ndiyo huu kuhusu mchakato wa kupata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM kwenye mkutano wa halmashauri kuu ulioketi.

Kura zote zilizopigwa ni 164
Hakuna kura iliyoharibika.
Wajumbe wa halmashauri kuu Tanzania bara walikuwa ni 129.
Wajumbe wa halmashauri kuu Tanzania visiwani walikuwa ni 35
Kura halali za Dkt. Hussein Mwinyi zilikuwa 129.
Dkt. Khalid na Vuai Nahodha wakagawana kura 35 za wajumbe wa Zanzibar.


Maendeleo hayana vyama.
Aiseee, mbona kama ramli chonganishi hivi mkuu.
 
CHADEMA kwa sasa wamekuwa wachambuzi wa Siasa za ndani ya CCM!

Suala la Urais wa Zanzibar ndani ya CCM kwa sasa ni hoja iliyofungwa jana.

Mtu mwenye akili timamu anajua Dk Hussein Mwinyi ni Rais mtarajiwa wa Zanzibar!
Mgombea wa watanganyika
 
Wapiga kura walikua 164, wazanzibari wako 35 katika wapiga Kura wote,
hakuna kura iliyoharibika,
129 + 35 =164,
Umegundua nini hapa ?

KURA za Dkt. Khalid 19
KURA za Shamsi 16
Jumla 35 👉🏽 Zanzibar

Hussein Mwinyi 129 zote za Bara. https://t.co/hsV8JwuDH8
Una uhakika upi kuwa hizo kura 35 za hao wagombea wawili zote zimepigwa na wazanzibar pekee?
Au kura zilitaja majina pale?
Lete ushahidi kuwa wazanzibar walikuwa ni 35 pekee.
Kama wazanzibar hawamtaki kama unavosema huko kwao kwenye kura za maoni kapita pitaje hadi jina lake kuwa miongoni mwa majina 3 yaliyo letwa huku bara?
Uje na ushahidi sio porojo mkuu.
 
Kwenye mikutano huwa nasikia kauli mbiu ya "Mapinduzi Daima"....hii kauli iko siku itatimia kwa mara nyingine tena.
 
CHADEMA kwa sasa wamekuwa wachambuzi wa Siasa za ndani ya CCM!

Suala la Urais wa Zanzibar ndani ya CCM kwa sasa ni hoja iliyofungwa jana.

Mtu mwenye akili timamu anajua Dk Hussein Mwinyi ni Rais mtarajiwa wa Zanzibar!
Na hili ndio kosa kubwa wanalofanya tumeshauri mara nyingi sana humu kuwa huu sio wakati wa kuendekeza siasa za matukio kusubiri ccm wamefanya nini ndio na wao wapate hoja matokeo yake wanayumbishwa sana na siasa za ndani ya ccm.
Wasimame wao kama wao ila hiki wanachokifanya kwasasa hakina mashiko kabisa.
 
Wazanzibari hata siwaelewi; yaani wana jeshi, mahakama, wimbo wa taifa lao, na bunge.

Lakini pamoja na mbwembwe zao zote hizo, Rais wao anachaguliwa Dodoma, Tanzania Bara, sijui wanakwama wapi?!.

Hii ni sawa na baba wa familia kuwa na nyumba yako, unaacha pesa ya matumizi kila siku, lakini chakula kinapikwa kwa jirani, na umeshazoea kwenda kula huko.
[emoji23][emoji23]

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Kuna kijana amezuiwa kupewa maiti ya mkewe hapo Muhimbili National Hospital mpaka atakapolipa shilingi 1,470,800.

Wasamaria walimsaidia kuchimba kaburi ili amhifadhi marehemu mkewe lakini kutokana na kuwekewa ngumu na serikali ya wanyonge, wamelazimika kufukia kaburi kisha kumchangia fedha za nauli kijana huyo ili arejee kwao Mtwara.

Hivi sasa huyo bwana yuko njiani akielekea makwao akiwa amebeba kichanga cha wiki tatu na maiti ya mkewe ikiendelea kushikiliwa hapo Muhimbili.

Huyu ni mmoja kati ya wapiga kura mnaowategemea. Kwa hakika hakuna chama cha kidhalimu duniani kinachoweza kuishinda CCM.

Kama umeguswa wasiliana na huyu mnyonge anayeteseka kwa kunyimwa mwili wa mpendwa wake kwa namba ya simu 0778 140 361
Hivi kwann "umnyime mtu mwili wa marehemu?"
Duh

JESUS IS LORD[emoji120]
 
I'm jus thinking!
Baada ya Magu atakuja nani,na baada ya Hussein mwinyi atakuja nani tena!?

Nawaza tu yaani!

JESUS IS LORD[emoji120]
 
CHADEMA kwa sasa wamekuwa wachambuzi wa Siasa za ndani ya CCM!

Suala la Urais wa Zanzibar ndani ya CCM kwa sasa ni hoja iliyofungwa jana.

Mtu mwenye akili timamu anajua Dk Hussein Mwinyi ni Rais mtarajiwa wa Zanzibar!
Mie nadhani sio suala la CHADEMA kuwa wachambuzi wa siasa ndani ya CCM. Hapa hoja ni siasa tu, ingekuwa mahubiri ya injili si dhani kama CHADEMA wangeichambua.

Nadhani hata wewe ni mmoja wa wanojadili siasa za vyama vingine ikiwamo CHADEMA.

Tumeshuhudia kwenye chaguzi za CHADEMA namna gani chama kama CCM wamekuwa wakijadili siasa ndani ya CHADEMA huko.

Leo pia mwenyekiti katika mkutano mkuu wa CCM Dodoma pale amepiga vijembe siasa za upinzani.

Hayo ndiyo maisha ya siasa,tunajadili tu ziwe za bara,visiwani,ukanda,upinzani uchwara,upinzani.. Ili mradi hatuijadili injili kwenye siasa.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Rais wetu Magufuli.

Mungu tubariki tupate viongozi sahihi katika uchaguzi mwaka huu,waweze kumsaidia Rais wetu katika ngwe yake ya mwisho kusukuma maendeleo kwa wananchi.
 
Dr Shein alikua mtu wa bara?
Fuatilia historia yake uone,hawataki mtu ambaye aliyezaliwa na kukulia zanzibar 100% ,Dr Shein alitolewa mfukoni mwa Mkapa!! Awali alikuwa hajawai kufanya/kujishughulisha na siasa!!
 
Back
Top Bottom