Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Wakuu leo Mheshimiwa J Kikwete anatarajiwa kufanya mkutano wa kampeni mjini Arusha muda wa saa 10 jioni kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheckh Amri Abeid.Tayari shamra shamra za mkutano wake wa kampeni zimeshaanza tangu saa 3 asubuhi,Mabasi yamekuwa yakifanya kazi ya kusomba watu kutoka maeneo ya Monduli,Simanjiro,Arumeru,Kia,Nduruma na maeneo mbali mbali nje ya mji wa Arusha.
Nimeshuhudia vikundi vingi vya kwaya,ngoma na wanamuziki wa kizazi kipya wakijumushwa kwenye kampeni za Mungwana.Nimejaribu kuangalia gharama za kufanikisha kampeni kwa kukisia mji wa Arusha pekee si chini ya tsh 200 milioni.Upande wa sare, bendera na picha za wagombea udiwani,ubunge na urais ni wakushangaza.
Wakuu hivi hakuna namna tunaweza kufanya kampeni zetu bila kutumia gharama kubwa ?.Kwanini hizi fedha hazipelekwi kwa wananchi kutatua matatizo ya afya,elimu na miundombinu.Vipi sheria ya matumizi wakati wa kampeni inazingatiwa kweli au ni changa la macho tu.