Elections 2010 Mkutano wa kampeni arusha jakaya kikwete

Elections 2010 Mkutano wa kampeni arusha jakaya kikwete

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Wakuu leo Mheshimiwa J Kikwete anatarajiwa kufanya mkutano wa kampeni mjini Arusha muda wa saa 10 jioni kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheckh Amri Abeid.Tayari shamra shamra za mkutano wake wa kampeni zimeshaanza tangu saa 3 asubuhi,Mabasi yamekuwa yakifanya kazi ya kusomba watu kutoka maeneo ya Monduli,Simanjiro,Arumeru,Kia,Nduruma na maeneo mbali mbali nje ya mji wa Arusha.

Nimeshuhudia vikundi vingi vya kwaya,ngoma na wanamuziki wa kizazi kipya wakijumushwa kwenye kampeni za Mungwana.Nimejaribu kuangalia gharama za kufanikisha kampeni kwa kukisia mji wa Arusha pekee si chini ya tsh 200 milioni.Upande wa sare, bendera na picha za wagombea udiwani,ubunge na urais ni wakushangaza.

Wakuu hivi hakuna namna tunaweza kufanya kampeni zetu bila kutumia gharama kubwa ?.Kwanini hizi fedha hazipelekwi kwa wananchi kutatua matatizo ya afya,elimu na miundombinu.Vipi sheria ya matumizi wakati wa kampeni inazingatiwa kweli au ni changa la macho tu.
 
Nimepita muda si mrefu mitaa ya ofisi ya ccm mkoa, nimeona jinsi bodaboda wanasubiria ulaji wao waanze kupita mitaani kwa mbwembwe.
kweli kampeni za JK zinaifilisi Nchi
 
Naona tumelala bado,ndio maana hawa jamaaa wanatumia watakavyo.Tusikate tamaa,tutashinda tu pamoja na pesa zao.
 
Nimeongea na dogo Arusha ni Taxi dereva, kumbe ni kweli bwana unaweka bendera ya CCM kwenye gari unaenda kituo cha Mafuta pale Mianzini unawekewa mafuta ya 10,000! Ama kweli CCM wanapesa inawanaitumia isipofaaa
 
KULA CCM KURA CHADEMA.... Msemo wa Belinda Jacob
 
Yaani kama una TAXI hata kama wewe ni CHADEMA, ukienda tu Petrostation wanakujazia mafuta ya 10,000/..????

Ningelikuwa ninakuja na kubadili namba ya gari na kurudi tena kujaza mafuta. Hadi mwisho naanza kuazima na namba za majirani na mwisho wa siku ninajaza mafuta ya kama laki tano hivi.....
 
Boda boda wanawekewa mafuta full tank na tsh 10,000/= kwa masharti ya kuvaa t shirt,kapelo na kupachika bendera kwenye pikipiki !.
 
Ha ha ha ndo hao wanaolipwa kwenda mkutanoni ndo wanaitwa ushindi wa zaidi ya 80% na Kinana? Raha ni kwa hao walioshika mikoba ya kuhonga hizo elfu kumi kumi. Hela zisizo na hesabu wala marejeo wow!
 
Boda boda wanawekewa mafuta full tank na tsh 10,000/= kwa masharti ya kuvaa t shirt,kapelo na kupachika bendera kwenye pikipiki !.

Katika hali ya kudhiti fedha zao zisiliwe bure boda boda zimepangiwa njia za kupita ambako wako watu wanohakiki namba za pikipiki na kama wamevaaa uniform [kofia,bendera,fulana] na kama wanapiga honi kwa fujo.Hela nyingine bwana heri za mtunza maiti
 
Ukiona chama kinawalaghai wapigakura kwa t-shirt, khanga, buku 10 na kukusanya wananchi kwa mabasi ili waje kwenye mikutano yao ujuie kimechokwa na hakina mvuto unapaswa ukiogope kama ugonjwa wa ukoma.
 
wanatumia pesa nyingi wanajua wakiingia madarakani zote zitarudi tena na zaidi - hizo zote ni contact moja tu ya mgodi wa dhahabu. Kweli Tanzania bado usingizi ni mnene.

Bodaboda na Taxi drivers ni sherehe tupu, - wenye mabasi nao ni mtaji maana unapewa hesabu ya siku mbili kufanya kazi ya siku moja ccm imeshalipa.

Je hiki chama kinaweza kweli kutokomeza rushwa? namkumbuka marehemu Kolimba (RIP) alishagundua mapema kwamba CCM hakuna dira wala mwelekeo - sasa hivi watanzania ndiyo tunashituka kwamba tumelipanda gari lisilo na break, tairi vipara,halina taa na dereva kalewa mnazi - kazi tunayo.
 
mkuu hizo pesa wanazotumia sio zao, ni za wanachi maskini... zunguka mahospitalini sasa uone kama kuna madawa na vifaa vya maabara

pesa ya maskini inagawiwa kama pipi kwa madereva taxi
 
Mheshimiwa anajua kuwa hadhara kubwa anayoihutubiwa wamefika kwa kuwa wamelipwa na si mapenzi kwa chama? Nasema hii kwa sababu kama anapata mapokezi ya nguvu mwisho wa siku aambiwe kura hazikutosha hatakubali.
 
Katika hali ya kudhiti fedha zao zisiliwe bure boda boda zimepangiwa njia za kupita ambako wako watu wanohakiki namba za pikipiki na kama wamevaaa uniform [kofia,bendera,fulana] na kama wanapiga honi kwa fujo.Hela nyingine bwana heri za mtunza maiti

Ngongo...TUKO PAMOJA!

Mi hata sijatoka kabisa nje ya ofisi, japo nasikia mchanganyiko wa makelele ya kuudhi sana !

ENDElea kuleta haya mambo, maana ni vituko vinavyotakiwa kukaa kwenye maktaba kwaajili ya vizazi vijavyo!

Ama kweli wananchi wengi sana wamefungwa ufahamu kwa kiasi cha kutisha!..wanashindwaje kuelewa kwamba fedha hizo ni zao, na zinaliwa na wachache, inagharimu nini kujua hilo?
 
mkuu hizo pesa wanazotumia sio zao, ni za wanachi maskini... zunguka mahospitalini sasa uone kama kuna madawa na vifaa vya maabara

pesa ya maskini inagawiwa kama pipi kwa madereva taxi

Wanaopewa hizo pesa ni Watanzania na wanaokosa tiba ni Watanzania shida iko wapi? Aliyepokea buku 10 si atamtibu mama, baba, bibi, babu hata kwa kuwachemshia mwarobaini?
 
Wanajimu wanadai leo ataanguka Arusha! Labda abaki kwenye gari ila akipanda kwenye mimbali ...Aiseeeeeeeee! Picha picha jamani
 
Wanaopewa hizo pesa ni Watanzania na wanaokosa tiba ni Watanzania shida iko wapi? Aliyepokea buku 10 si atamtibu mama, baba, bibi, babu hata kwa kuwachemshia mwarobaini?
nimepata hiyo mockery yako....

Tatizo nambari wani la CCM ni vipaumbele.... hata hizo buku kumi wanazotoa zinathibitisha hivyo!!! How will they account for that money?? watajuaje ni wangapi wamepewa na katika hao wagawaji pesa (kampeni menejaz) ni wangapi wamedhulumu?

Its a sad reality lakini CCM wanajifanya akina Puff Daddy kumwaga pesa kwenye kumbi za starehe, very sad reality
 
Back
Top Bottom