Elections 2010 Mkutano wa kampeni arusha jakaya kikwete

Elections 2010 Mkutano wa kampeni arusha jakaya kikwete

Ccm....ccm....ccm.....shika hataaamu!!
 
Wakuu uwanja wa kumbukumbu Shekh Amri Abeid una uwezo wa kuchukua watu takribani 14,000.Niko uwanjani muda huu nashangaa kukuta uwanja haujafurika yapo maeneo mengi hakuna watu kabisa najaribu kuuliza watu wachache naambiwa wapangaji wa ratiba wamechemsha kupita maelezo wamesomba watu tangu asubuhi saa 3 njaa zimewasambaratisha.Ratiba za muungwana zimewachanganya muda huu wa saa 10:25 jioni bado yuko Usa river antegemewa kufika Arusha mjini saa 11 jioni.Hali iliyoko hapa uwanjani ni ya simanzi wanamuziki wanajitahidi kuwaburudisha watu ili wasikimbie wote.

Thank God mipango yao ya kilaghai inazidi kuvurugika.
 
Yeh JK kafunika ndugu!! CHADEMA HAWANA CHAO MWAKA HUU

Mpaka sasa saa 5:18 bado hajaingia uwanjani sasa unaposema kafunika nashindwa kukuelewa kabisa.Watu wanazidi kuondoka uwanjani baada ya kusubiri kwa muda mrefu sana.
 
jamani nipo uwanjani me nilikuwa naona tu kwenye tv campeni za CCM lakini hamna kitu mpaka watu wanaenda kukodishwa aisee je wanalipwa au wanapewa maji tu na biskuti tujiangalie watanzania tubadilike tujue wapi tunakwenda bado dakika 8 campeni zikwishe sijui imekuwaje poleni CCM hayo ni yangu kwa leo
 
Wakuu mkutano wa wa CCM Arusha umehairishwa baada ya Muungwana kushindwa kutokea uwanjani.Hii ni aibu kubwa sana kwa CCM mkoa wa Arusha hasa ukizingatia maandalizi
 
jamani nipo uwanjani me nilikuwa naona tu kwenye tv campeni za CCM lakini hamna kitu mpaka watu wanaenda kukodishwa aisee je wanalipwa au wanapewa maji tu na biskuti tujiangalie watanzania tubadilike tujue wapi tunakwenda bado dakika 8 campeni zikwishe sijui imekuwaje poleni CCM hayo ni yangu kwa leo

Karibu jamvini
 
acha tu ni aibu sana ratiba za CCM azieleweki kama mweshimiwa amechoka nijambo lakuwaambia watu sio kuwaweka mpaka sasa na je nauliza kuhusu ratiba ya arusha mjini kw CCM ndo imekwisha maana hatujui hata ilani ya CCM?
 
Mimi Niko Hapa Sterio Hotel Kuna Ka Ujasiliamali ninafanya Yaani saa 5 mpaka sasa ni makelele tu Muungwa Ndo nimesikia ving'ora nje!! Shit! Too Much noice na sijui watu hawana kazi za kufanya mpaka karne hii unawekwa juani for 7 hours!!! I do know tutafika lini
 
Wakuu Muungwana anaingia muda huu uwanjani watu kibao wameshaondoka
 
Naomba kujuzwa muda wa kampeni unaisha saa ngapi ?.Niliwahi kuambiwa muda wa kampeni mwisho saa 12 jioni.iweje Muungwana aanze kampeni saa 12 05 jioni au sheria zinawekwa pembeni kwa CCM.
 
aisee ni aibu sana kwa utaratibu wa CCM arusha sijui kwingine ndo kampeni ndo zimeanza sasa hivi sijui anamuda wa kutuambia kilichopo kwenye ilani ya CCM na sijui atatumia muda gani its real crazy wanajamii
 
any updates kwa mlio arusha??
aisee ni aibu sana kwa utaratibu wa CCM arusha sijui kwingine ndo kampeni ndo zimeanza sasa hivi sijui anamuda wa kutuambia kilichopo kwenye ilani ya CCM na sijui atatumia muda gani its real crazy wanajamii
 
Wakuu leo Mheshimiwa J Kikwete anatarajiwa kufanya mkutano wa kampeni mjini Arusha muda wa saa 10 jioni kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheckh Amri Abeid.Tayari shamra shamra za mkutano wake wa kampeni zimeshaanza tangu saa 3 asubuhi,Mabasi yamekuwa yakifanya kazi ya kusomba watu kutoka maeneo ya Monduli,Simanjiro,Arumeru,Kia,Nduruma na maeneo mbali mbali nje ya mji wa Arusha.

Nimeshuhudia vikundi vingi vya kwaya,ngoma na wanamuziki wa kizazi kipya wakijumushwa kwenye kampeni za Mungwana.Nimejaribu kuangalia gharama za kufanikisha kampeni kwa kukisia mji wa Arusha pekee si chini ya tsh 200 milioni.Upande wa sare, bendera na picha za wagombea udiwani,ubunge na urais ni wakushangaza.

Wakuu hivi hakuna namna tunaweza kufanya kampeni zetu bila kutumia gharama kubwa ?.Kwanini hizi fedha hazipelekwi kwa wananchi kutatua matatizo ya afya,elimu na miundombinu.Vipi sheria ya matumizi wakati wa kampeni inazingatiwa kweli au ni changa la macho tu.

hivi hao watu waliotolewa mbali wanalipwa nini jamani maana toka asubuhi au ni wana skauti wa CCM
 
Back
Top Bottom