Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

We Acha tu!
Katiba mpya haijadiriki endapo tutapuuza suala la muungano kujadiriwa kwa ukweli na uwazi. Hapa nyuma nilikuwa sijui sababu za kuungana ila leo nimesoma raiamwema (toleo la wiki hii) wamenifumbua macho barabara. Muundo uliopo wa muungano haukubaliki, kuwa na serikali moja tunakaribisha vita, suluhu ni kuwa na serikali tatu ili kunurusu muungano wetu. Hili si fumbo la imani kwa sababu wapo watu walioshuhudia muungano na wangali hai hivyo lazima tuambiwe ukweli watanzania, zama za kunong'ona zimeshapita. Naomba tujadili hili ndugu watanzania!
 
Pengo atoa onyo

Ataka wanasiasa kutohusisha dini na siasa

Na Waandishi wetu

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, amevitaka vyama vya siasa na serikali kwa ujumla kuacha mara moja kuwazuia watu wanaodaiwa kuwa mafisadi kwenda kupata huduma za kiroho.

Pengo alitoa rai hiyo jana alipozungumza na Tanzania Daima baada ya kuhitimisha ibada ya misa takatifu ya sikukuu ya Pasaka katika Kanisa la Mt Vinsent wa Paulo, wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.

Alisema Kanisa Katoliki kamwe halitamfukuza mtu yeyote anayedaiwa kuwa ni fisadi ili mradi ni muumini wa kanisa hilo na kuwa kanisa litampokea iwapo atahitaji huduma zozote za kiroho.

“Kanisa Katoliki halitamfukuza mtu yeyote yule anayedaiwa na serikali au chama kuwa ni fisadi eti asipate huduma zinazomstahili! Kanisa litampokea iwapo ni muumini mzuri na amekwenda kwa ajili ya kupata huduma za kiroho,” alisema.

Alisema vyombo vya dini viko kwa ajili ya kutoa huduma za kiroho, hivyo visihusishwe na vyama vya kisiasa na kuwa Yesu alikuja duniani kwa ajili ya wenye dhambi na ndio maana alikufa msalabani, ili kuwaokoa.

“Natoa wito kwa serikali na vyama vyote vya siasa kutohusisha dini na siasa kama kuna mtu anayedaiwa kuwa ni fisadi na anataka kujisafisha kwa lengo la kutubu au anahitaji huduma nyingine yoyote ya kanisa huku akiwa ni muumini.

Wamuache aende kupata huduma kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi, hivyo kutubu ni kuacha kutenda ufisadi na kuwa mtu safi; wasiwazuie!” alisema Kardinali Pengo.

Kadinali Pengo alisema kumtenga mtu ambaye ni muumini kwa sababu za kile kinachoitwa ufisadi ni kosa ikiwa kanisa ni chombo kinachopaswa kumsaidia aweze kuwa mtu mwema.

“Kumtenga mtu ni kosa. Mbona Yesu hakumkataa Maria Madgalena na Zakayo mtoza ushuru sasa iweje leo kanisa liwatenge watu wanaodaiwa kuwa ni mafisadi huku wakiwa ni waumini wa kanisa?

“Kamwe kanisa halikubaliani na hilo, kanisa hutoa huduma za kiroho na lengo ni kumfanya mtu awe mwema sasa tutamkataaje mwenye dhanbi ikiwa Yesu mwenyewe aliwapokea na kuwafundisha kisha wakawa watu wema iweje leo tuwakatae?” alihoji Kadinali Pengo.

Aidha, alisema iwapo mtu hakubaliki katika chama si kweli kuwa na katika kanisa hakubaliki kwa kuwa chama na kanisa ni vitu viwili tofauti.

Alisema vyama vinahitaji watu wasafi, lakini kanisa linahitaji wenye dhambi (watu wachafu) ili wapate kutubu na kumrudia Mungu ndio maana Yesu alikuja kwa ajili ya watu wagonjwa na si wazima.

“Ikiwa Yesu alikuja kwa ajili ya wagonjwa na si watu walio wazima na tena wenye afya ambao hawahitaji tabibu itakuwaje mwenye dhambi asimrudie Mungu? Inawezekana kweli mtu akawa mbaya kwenye chama lakini akawa mzuri kanisani. Je utaweza kumtenga mtu huyo na je utamjuaje kama kweli kule alikotoka alitenda kosa hilo? Zaweza kuwa njama tu za watu serikalini au katika siasa.

Hapana Kanisa Katoliki lisihusishwe na hilo,” alisema.
Kauli ya Kardinari Pengo imekuja siku chache baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kusema mafisadi walioenguliwa na chama hicho wanataka kuwatumia viongozi wa dini ili kujisafisha.

Katika ibada aliyoiongoza Kardinari Pengo aliwataka waumini wa dhehebu Katoliki kuliombea taifa liwe na amani pamoja na machafuko ya kisiasa yanayozidi kutokea katika bara la Afrika na duniani kosa sanjari na majanga yanayotokea.

Naye Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, ameelezea wasiwasi wake juu ya uundwaji wa Katiba mpya kutokana na kuendeshwa kwa misingi ya kichama badala ya maslahi ya taifa.

Akihubiri katika misa maalum ya Sikukuu ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, alisema uudwaji wake umeonyesha shaka na wasiwasi mkubwa kutokana na kuanza kwenye misingi mibovu.

“Katiba mpya ni sheria mama ya nchi, hivyo haina budi kumgusa kila mtu nchini, kanisani na hata ndani ya jamii inayotuzunguka, lakini naona tayari imeanza kutawaliwa na itikadi za kisiasa,” alisema Nzigilwa.

Akihubiri huku akisikilizwa kwa makini na waumini waliofurika katika ibada hiyo, alisema Katiba ni jambo kubwa lenye kuonyesha mustakabali wa nchi: kutetea wanyonge, kuleta haki na usawa, hivyo isiandaliwe kwa misingi ya chama fulani cha siasa.

Alisema endapo Katiba inataendeshwa kama ilani ya chama fulani cha siasa ni wazi kwamba taifa litakuwa njia panda na kuelekea mahali pabaya zaidi.

“Endapo chama tawala kinaandaa Katiba mpya kwa ilani yao, ni wazi chama hicho kitaweka vipengele vya kujipendelea chenyewe ili kibaki madarakani, na upinzani kadhalika, utaleta vipengele kwa maslahi yake binafsi yakiwemo ya kumwondoa aliye madarakani. Hatutaki hili litokee sasa.

“Iandikwe katiba yenye kuweka mbele maslahi ya taifa, inayogusa maisha ya wananchi wa mijini na vijijini, na kila mwananchi lazima ashiriki katika jambo hilo,” alisema.

Askofu huyo alisema Katiba mpya itakayoundwa lazima iwe yenye uwazi kwa watu wa rika zote na isiyomlinda mtu au kundi fulani la watu na chama.

Alisema hakuna ubishi kwamba baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye katiba ya sasa havistahili kunyofolewa, lakini yale yasiyofaa lazima yaondolewa kwa ajili ya maslahi ya watu wote.

Askofu huo pia alitumia muda huo kuonya juu ya baadhi ya watu walioko katika jamii kutumia pesa kwa ajili ya kuficha ukweli.

Akinukuu kifungu katika Biblia kinachosema ‘walinzi walitumia pesa kwa ajili ya kuficha ukweli wa ufufuko wa Yesu’, alisema ni jambo la hatari kwa jamii na taifa kwa ujumla, kwani iko siku ukweli wa mambo utawekwa wazi.

Alisema watendaji wa serikali wanapaswa kujihoji ni kwa kiasi gani wanatimiza mapenzi ya Mungu katika kuwatendea wenzao haki.

Aidha, aliwataka waumini wa Kikristo na Watanzania kwa ujumla kuitumia Sikukuu ya Pasaka kurejea matendo mema ikiwa ni pamoja na kuheshimiana na kudumisha amani.

Akizungumzia kudumishwa kwa amani, alisema taifa kwa sasa linakabiliwa na hofu mbalimbali na kuongeza kuwa hofu hizo zinatokana na wananchi na viongozi walioko madarakani kutomtii Mungu ipasavyo.

Alisema hofu hizo ndizo zinasababisha kutoweka kwa amani ya utulivu wa nchi, kutokana na Mungu kuwa mbali na wanadamu wake.

Alifafanua juu ya hilo, alisema Pasaka maana yake ni upatanisho kati ya makundi mbalimbali yanayopingana ndani ya jamii.

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustine Shao, amesema matarajio ya wananchi baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huenda yasifikiwe kutokana na kutokuwepo nia ya dhati ya kuleta mabadiliko hayo.

Askofu Shao alisema hayo juzi usiku katika mkesha wa ibada ya Pasaka katika kanisa la Minara miwili Shangani Mjini Zanzibar.

Alisema baada ya uchaguzi mkuu uliopita wananchi wengi walitarajia serikali ya umoja wa kitaifa italeta mabadiliko makubwa ikiwemo unafuu wa hali za maisha ya wananchi wake.

“Tunaweza kusema tuliyoyatarajia kwa kiwango kikubwa huenda yasifikiwe kwa sababu wengi wetu hatujaona nia ya dhati ya kutaka mabadiliko na utayari wa kupokea mawazo na changamoto za wengine,” alisema askofu huyo.

Alisema wananchi walitarajia kuona nguvu mpya na ubunifu mpya kwa kuzingatia rika na vipaji kuanzia ngazi za wilaya mikoa hadi wizara, ili kuharakisha maendeleo ya Zanzibar.

Hata hivyo alisema mabadiliko yaliyofanyika katika serikali ya umoja wa kitaifa ni mabadiliko ya nafasi kwa viongozi wale wale mabadiliko ambayo hayana tija katika kuharakisha maendeleo ya nchi.

Askofu Shao alisema mabadiliko hayo ni sawa na mwalimu mzembe kumhamisha shule moja na kumpeleka shule nyingine, jambo ambalo haliwezi kubadilisha uwajibikaji wake.

Wakati huohuo, Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, limesema wakati umefika kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushughulikia tatizo la mfumko wa bei uliojitokeza katika soko la ndani ya Zanzibar.

Alisema tatizo hilo linaendelea kuathiri wananchi wenye kipato cha chini, huku serikali ikiwa imekaa kimya.
 
Wanasiasa wahofia hatima ya Muungano Send to a friend Monday, 25 April 2011 23:58

Raymond Kaminyoge na Fredy Azzah
WAKATI Tanzania leo ikiadhimisha miaka 47 ya Muungano, baadhi ya wanasiasa nchini wameonyesha wasiwasi kuhusu hatima yake na kutaka mjadala wa Katiba unaoendelea nchini, utumike kuunusuru.Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jana wanasiasa hao walisema, kuna kila dalili za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuvunjika muda mfupi ujao kama hakutakuwa na mkakati maalumu wa kuunusuru.

Mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombare Mwiru amewataka Watanzania kuuenzi Muungano kwa kuendeleza umoja na amani katika jamii: "Tanzania ni moja na sisi (Watanzania) ni wamoja, hakuna haja ya kulumbana kiasi cha kugawanyika katika kipindi hiki ambacho mataifa mengi yanataka kuungana.

"Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema mjadala wa Katiba unaoendelea sasa nchini, unapaswa pia utumike kujadili muundo mpya wa muungano ambao utaondoa malalamiko."Watu wapewe uhuru wa kujadili muundo wa Muungano wao ili kuondokana na kasoro ambazo zimekuwa zikilalamikiwa, hiyo itasaidia kuwa na Muungano imara zaidi," alisema Mbatia.

Kwa mujibu wa Mbatia, Muungano ni kitu adhimu na si vyema kuzungumzia kuuvunja katika kipindi hiki ambacho nchi nyingi duniani, zinataka kuungana ili kuwa na nguvu ya pamoja."Kwa kweli nitamshangaa mtu anayezungumzia kuvunja muungano katika kipindi hiki ambacho mataifa mengi duniani, yanafikiria kuungana.

Jambo la msingi hapa ni kuumarisha kwa kuondoa kasoro zilizopo," alisema.Mbatia alisema hilo litawezekana ikiwa watu watapewa uhuru wa kujadili masuala mbalimbali yanayouhatarisha.Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni silaha kubwa katika mapambano dhidi ya umaskini.

Hata hivyo, alisema kumekuwa na viashiria vinavyohatarisha uwapo wake na kusema busara inatakiwa kutumika ili kuunusuru.Mrema alisema moja ya viashiria vya kuvunjika kwa Muungano ni kauli za hivi karibuni kuhusu Muswada wa Katiba kwamba Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein hakushirikishwa kuuandaa.

"Wanasahau kwamba Rais Kikwete ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyechaguliwa na Watanzania wote, wakiwamo Wazanzibari," alisema Mrema na kuongeza:"Kwa hiyo hizi ni kasoro zinazoashiria kuvunjika kwa muungano kama hazitadhibitiwa. Tunahitaji mazungumzo ili kujadili kero zinazolalamikiwa." Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei alisema Muungano wa kulazimishana hauwezi kuwaletea matunda Watanzania.

"Wazanzibari wanaona kama vile tunawalazimisha katika Muungano. Wanaona kwamba watu wa bara ndiyo wanaofaidika zaidi nao.

Katika majadiliano ya Katiba mpya, Muungano ujadiliwe kwa uwazi ili kama Wazanzibari hawautaki tuuvunje, tusilazimishane, vinginevyo kila siku tutakuwa katika matatizo."Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwataka wananchi kuzungumzia pia mambo mazuri yaliyopo kwenye Muungano badala ya kujadili yaliyo mabaya pekee.

Alisema kwa kuzungumza mambo mabaya pekee, kunawafanya vijana na watoto kukua wakiwa na dhana kuwa, Muungano hauna jambo lolote jema."Tujivunie mengi mema yaliyo kwenye Muungano kuliko kutumia muda mwingi kila tunapokutana kuzungumzia mabaya tu.

Mazuri ya Muungano pia, yazungumzwe," alisema Nape.Alisema Watanzania wanatakiwa kuadhimisha miaka 47 ya Muungano kwa furaha na kujiamini kwa kuwa mbali na kuwa ni Muungano wa muda mrefu, umewaunganisha Watanzania na kudumisha upendo miongoni mwao.
 
Pengo avunja ukimya kuhusu uhusiano wa Katoliki na Serikali ya JK Send to a friend Monday, 25 April 2011 23:43

Joseph Zablon
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amezungumzia uhusiano wa kanisa hilo na Serikali, akikanusha tuhuma kwamba maaskofu wake wanatumiwa na mafisadi kumchafua Rais Jakaya Kikwete na familia yake.Kardinali Pengo alisema kuwa hakuna askofu yeyote wa kanisa hilo anayetumiwa na watuhumiwa wa ufisadi kumchafua Rais Kikwete na Serikali yake kama baadhi ya watu wanavyodai.

Kardinali Pengo alisema hayo jana katika Ibada ya Jumatatu ya Pasaka iliyofanyika katika Parokia Kristu Mfalme Tabata ikikutanisha pia kwaya zote za kanisa hilo jimboni humo."Kanisa limeshtakiwa kuwa lipo kinyume na utawala uliopo madarakani hivi sasa na kuna uzushi kuwa eti maaskofu wake, wanawaandaa wapinzani kuchukua madaraka ya kuongoza taifa," alisema Kardinali Pengo.

Kardinali Pengo alisema maneno hayo ni uzushi usiokuwa na msingi kwani kanisa hilo halina na halipaswi kuwa na upande wowote katika masuala ya utawala wa dunia.Alisema kauli hizo alizodai za uzushi, ni hatari kwa kuwa zinalifanya kanisa hilo lionekane kuwa chombo cha kuziendeleza mamlaka za kisiasa au linapingana na watawala.

Akitumia maandiko ya matakatifu ya Biblia, Kardinali Pengo alisema kinachotokea sasa ni kama kilichotokea wakati wa Kristu katika utawala wa Herode, Yesu Kristu alishutumiwa kwa kula na kunywa na watoza ushuru."Hata Yesu alipokuwa karibu na watoza ushuru, alionekana kama kibaraka wa utawala wa Rumi wakati huo na kuna ambao walimwona anakufuru kwa kushirikiana na watu hao ambao ni chukizo," alisema Pengo.

Alisema kama ilivyokuwa kwa Kristu ambaye aliwajibu waliomchukia kuwa hakuja kwa ajili ya wenye haki bali wenye dhambi, Kanisa Katoliki halitawatenga wala kuwazuia makanisani wanasiasa watakaofukuzwa kwenye vyama vyao kwa tuhuma za ufisadi.

"Hatutamtenga mtu au kumzuia asije kanisani kisa tu amefukuzwa katika chama chake cha siasa," alisema Kardinali Pengo na kuongeza:
"Kufanya hivyo ni kuwanyima ya huduma za kiroho. Hata mimi siwezi kuacha kumwungamisha mtu ambaye amefukuzwa katika chama chake kwa sababu za ufisadi, kwani kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya Yesu Kristu ambaye alikuja duniani kwa ajili ya wenye dhambi.

"Pengo alisema binafsi anasikia machache lakini waumini hao watakuwa wanasikia mengi kwa kuwa ndiyo waliopo mitaani na huko ndipo wanapogombea madaraka ya kisiasa.Alisema huyasikia yanapopelekwa kwake na walioshindwa kuyamaliza huko mtaani na kwamba anaamini wanasikia mengi, lakini akasisitiza kwamba msimamo wa kanisa ni kuwa halitakuwa na upande katika utawala wa kidunia kama alivyokuwa Kristu.

"Litakuwa jambo baya sana na kwenda kinyume na mafundisho ya Kristu kama muumini wa namna hiyo atanifuata, halafu nikamweleza kuwa akanunue silaha," alisema Pengo na kuongeza kuwa atamshauri kulingana na maandiko na si vinginevyo.Pengo aliwataka waumini wa kanisa hilo kutafakari na kuliombea taifa amani hasa katika kipindi hiki ambacho alikifananisha na nyakati za kuzaliwa kwa Yesu ambapo alituhumiwa, kusulubiwa, kifo chake hadi alipofufuka na kuendelea kulitangaza jina la Bwana.

Ingawa Askofu Pengo hakumtaja mtu wala taasisi inayotoa madai hayo dhidi ya Kanisa, Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye amewahidi kukaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa dini, wanatumiwa na mafisadi kwa ajili ya kumchafua Kikwete na Serikali yake kwa minajili ya kutaka kuingia madarakani.

Nape alitoa madai hayo Aprili 16, mwaka huu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Bakhresa Manzese, Dar es Salaam.Alisema mafisadi wametangaza vita ya kumchafua mwenyekiti wa chama hicho na familia yake kupitia vyombo vya habari hata baadhi ya viongozi wa dini na makanisa.Nnauye alisema wamegundua mpango huo na kwamba wanatangaza kuamua kupambana nao hadi wang'oke ndani ya CCM.
 
JK:Wanaohubiri udini hawaitakii mema Tanzania Send to a friend Monday, 25 April 2011 10:23

kikweteutabiri.jpg
Rais Kikwete

Ibarahim Bakari
RAIS Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kuwapuuza wanaotaka kuwagawa Watanzania kwa kisingizio cha dini zao akisema hao hawalitakii mema taifa.Alisema hayo jana alipokuwa akizungumza kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

"Tusiwasikilize wanaotaka kuwagawa Watanzania kwa dini zao, hawa wanapandikiza mbegu za chuki za udini na kama inawezekana tufanye kila njia kuwaepuka... hata Mwalimu Nyerere alipinga udini akataja dhambi nne akasisitiza dhambi ya udini ni mbaya," alisema.

Alisema dini haijawa kitu cha kutugawa, kutuchonganisha na kutukosanisha kwani zote zilitumika kudai uhuru mwaka 1961 na Mapinduzi ya Zanzibar mnamo mwaka 1962: "Kikubwa Watanzania tusifanye makosa kuvuruga amani, dini zisitumike kutuvuruga...," alisema Kikwete na kuitikiwa Ameen.

Awali, Askofu Onesmo Ndegi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), alisema Mungu amempa Rais Kikwete ujasiri wa kuvua gamba na kwamba hatua hiyo ya Rais ni maelekezo yanayotoka kwa Mungu.

"Tunachotaka kuona ni gamba kuvuliwa kikwelikweli na wasaidizi aliowaweka tuna imani watamsadia katika kuweka mambo sawa," alisema kabla ya Rais Kikwete kuwashukuru watu kuunga mkono hatua hiyo ya CCM kujikuvua gamba.

Naye Askofu Samuel Kameta pia wa TAG, alisema wakati umefika kwa kila Mtanzania kuwanyooshea kidole mafisadi na wala rushwa... "Tushirikiane kuwafichua mafisadi, tusiwaonee haya na Tanzania bila ufisadi inawezekana."
 
Wazanzibari wazidi kuchokonoa Muungano Send to a friend Monday, 25 April 2011 20:40

Elias Msuya
KUNDI la wazee wanaodai kuwakilisha mikoa mitano ya Zanzibar, limemwandikia Rais Jakaya Kikwete, barua ya malalamiko kuhusu Muungano na kumtaka atimize ahadi zake za kuondoa kero za chombo hicho, kabla ya kumaliza kipindi chake cha uongozi wa taifa.

Barua hiyo ya Aprili 21 mwaka huu, imekuja wakati Watanzania leo wanasherehekea miaka 47 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Maadhimisho hayo yatafanyikia katika uwanja wa Aman, mjini Zanzibar.Katika barua hiyo, kundi hilo limeelezea kusikitishwa juu ya kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo wa konokono wa Rais Kikwete ,katika kushughulikia ahadi zake za kuzimaliza kero za Muungano.

"Kwa masikitiko makubwa hatuna budi kufikisha kilio chetu kwako wewe rais wetu ambaye upo katika kipindi chako cha pili na cha lala-salama kikatiba, katika kuliongoza taifa hili bila ya mafanikio juu ya ahadi zako ulizotoa kuhusu kuzimaliza kero za Muungano baina ya watu wa Zanzibarna wa Ttanganyika," ilisema sehemu ya barua hiyo.

Barua hiyo imeongeza kuwa wakati Rais Kikwete alipokwenda visiwani kuomba kura kwa mara ya kwanza mwaka 2005, alipewa ushirikiano pale alipowaahidi Wanzanzibari kwamba, angezipatia ufumbuzi kero zote za Muungano.

Wazee hao, walitaja mambo ambayo Rais Kikwete aliahidi kuyatekeleza alipokuwa akilihutubia Bunge Desemba 30 mwaka 2005 kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa pande zote mbili za Muungano, zinafaidika na kuridhishwa na Muungano.

Hali kadhalika kukuza demokrasia itakayoendeshwa kwa misingi ya utawala bora, utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu.

"Licha rais na serekali yako kushindwa kuyatekeleza mambo makuu matatu uliyoyapa kipaumbele katika awamu yako ya kwanza, lakini pia hukujisikia aibu kuwaeleza Watanzania kupitia Bunge jipya la kumi kwamba mambo yale uliyoyaahidi katika Bunge lililopita bado yataendelea kuwa ndiyo majukumu yako ya msingi katika kipindi chako hiki cha pili,"imesema barua hiyo.

Wamegusia pia viaumbele 13 alivyovitoa Rais Kikwete, alipokuwa akilihutubia Bunge mwishoni mwa mwaka jana, ambavyo ni pamoja na kuwa na nchi yenye umoja, amani, na usalama na muungano ulioimarika.

Walisema hata hivyo vipaumbele hivyo, vinakwamishwa na rasimu ya katiba mpya iliyoandaliwa bila hata kufuata kanuni na sheria za muungano.

"Je, ndio kutaka kuimarisha umoja, amani na usalama wa kweli? Huu ndio utawala bora, utawala wa sheria wa demokrasia yenye kujali haki za binadamu Au huu ndio mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa muungano wetu unaendelea kudumu na kuimarika," ilihoji sehemu ya barua hiyo.

Wazee hao wameunga mkono hatua ya Wazanzibari kuukataa muswada wa marejeo ya katiba na kutoa pongezi kwa wananchi hao.

"Rais, tunakuomba kwa heshima zote wewe na serekali yetu ya muungano; tafadhalini sana sana msikie kilio cha wazanzibari. Tunajua asili na tabia yako wewe si mtu wa pupa, jazba na hamaki. Tabia yako imepambwa na busara, hekima, usikivu na utaratibu, sifa ambazo ni sawa na lulu na ndizo zinazokutofautisha sana wewe na baadhi ya viongozi waliotangulia," ilisisitiza barua.

Walisisitiza Wazanzibari wanataka mabadiliko makubwa ndani ya Muungano, kwa sababu makubaliano ya muungano huu yamekiukwa na hivyo kuweka kasoro kubwa katika uhalali wake.

"Sisi tunaamini kwamba huu ni wakati muafaka na mnasaba wa kuujadili muungano upya. Na baadaye watu wa Zanzibar na watu wa Tanganyika,wapewe fursa ya pekee ya kuulizwa kuhusu Muungano upi wanaoutaka. Majibu yatakayotoka katika pande zote mbili ndiyo yapewe kwa tume ili yafanyiwe kazi inayostahiki." alisema.

Wamekumbushia pia mpango uliokuwepo wakati wa serekali ya Rais Ali Hassan Mwinyi, ambapo aliyekuwa Waziri mkuu wake, John Malecela alishakamilisha na kulieleza Bunge juu ya nia ya kuwapo kwa muswaada wa kuanzishwa kwa serekali yaTanganyika, lakini baadaye Mwalimu Nyerere alitumia uwezo wa chama na kulilazimisha Bunge lisiujadili.
 
Comments

#3 rutashubanyuma 2011-04-26 08:35 Muungano huu umepitwa na wakati. Hatuna sababu za karne ya ishirini na moja kuutetea hata kidogo haswa ukizingatia ya kuwa EAC, SADC na COMESA zinajiandaa kuanzisha mashirikisho ya kisiasa na kiuchumi.....................ni vyema tukaacha kukariri sababu za mwaka 1967 kuhalalisha muungano katika karne ya 21...................Jibu ni kuuvunja na Tanganyika na Zanzibar zikajiunga kwenye EAC kama nchi huru kama ilivyo kwa Rwanda na Burundi ambazo ni ndogo mno...........................
Quote

0 #2 Mangi Lelo 2011-04-26 07:20 Wazenji nyinyi fanyeni kwa nguvu muondoke kwenye Muusokomano musikubali kutawaliwa tena...Eboooo
Quote

0 #1 A 2011-04-26 06:53 Muukubali mtake msitake. Si mmekubali wenyewe tangu miaka 47 iliyopita na munagutuka leo na kuanza kupiga kelele baada ya kuona kisiwa chenu kimeshamezwa? Nani aliyezawadiwa anakubali kuirejesha zawadi? Mzanzibari mmoja kiongozi hivi karibu alitamka waziwazi kuwa hao wanaoupinga muungano ni wahuni. Mnayaona mambo hayo?
Quote

Refresh comments list
 
Viongozi chanzo cha vurugu za Muungano
• Wazanzibari 10 wahaha kuisaka hati

na Hellen Ngoromera

amka2.gif
MHADHIRI mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azaveli Lwaitama, amewaponda viongozi wa serikali kuwa ni wanafiki na ndio chanzo cha chokochoko za Muungano.
Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akihojiwa katika kituo cha televisheni cha ITV katika mada iliyohoji ikiwa Muungano unaenziwa kwa vitendo.
Kwa mujibu wa msomi huyo wananchi hawana matatizo kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini wanaoshabikia suala hilo ni viongozi na kwamba wanafanya hivyo kwa maslai yao.
"Viongozi wengi walioko madarakani hasa wa Chama tawala cha Mapinduzi(CCM) hawawezi kutetea alichokianza Mwalimu (Hayati) Julius Nyerere kuhusu Muungano wetu," alisema Dk. Lwaitama.
Kwa mujibu wa Dk. Lwaitama viongozi hao ambao aliwaita wanafiki wameugeuka Muungano hali ambayo inasababisha mgongano.
Alisema anayefikiria kuuvunja ni mpumbavu na kwamba kufanya hivyo ni kujidhoofisha na kwamba kinachohitajika sasa ni kuwa na serikali mbili na baada ya kutoka hapo iwepo moja na si vinginevyo.
"Anayefikiria kuuvunja Muungano ni mpumbavu… kuwa na serikali tatu ni kuvunja Muungano na hakuna haja ya akufanya hivyo, wanaochokoza kuhusu Muungano ni viongozi wetu.
"…Hivi leo Mwalimu Nyerere akifufuka na kuona hali inavyokwenda kuhusu Muungano atasemaje? Viongozi hawa wajiuzulu kwa sababu hakuna wanachotetea kuhusu Muungano, wengi wao ni wafanyabiashara na wanatumia mwanya kupata uongozi ili kuendeleza biashara zao," alisema Dk. Lwaitama.
Naye Remigus Mbawala ambaye ni mzee wa siku nyingi alisema hakuna haja ya wananchi kuzuiwa kuuzungumzia Muungano kwani kwa kufanya hivyo kunauwezesha ulete tija.
Alisema ili kuwezesha mambo mengi kwenda sawa kuna haja kulifanya baraza la mawaziri kuwa dogo ili kuwezesha fedha zinazotumika kuhudumia baraza hilo la mawaziri zikafanyie mambo ya maendeleo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, alisema Muungano lazima ujadiliwe kwani kwa kufanya hivyo kunalifanya taifa kuwa moja.
Alisema kwa sasa maadili ya viongozi wa zamani yamepitwa na wakati na kwamba enzi za CCM zimepitwa na wakati hivyo wawaachie wengine.
Alishangazwa na kule taifa linakoelekea na kusema kuwa ingawa linatimiza miaka 47 ya Muungano bado linategemea misaada ya wahisani.
"La muhimu kutazama ni kwamba ndani ya nchi Watanzania wanahitaji taifa la aina gani," alisema Mtatiro aliyekuwa mgombea ubunge wa Ubungo.
Wakati huo huo, Mauwa Mohamed kutoka Zanzibar anaripoti kuwa kundi la 10, Wazanzibari walioanzisha mchakato wa kudai hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wameapa kuendelea na juhudi za ndani na mahakama ya kimataifa kuupinga.
Kundi hilo linaongozwa na Rashid Salum Addiy lilianza harakati za kudai mkataba wa Muungano wenye saini mbili za Nyerere na Karume mwaka 2005 katika Mahakama Kuu ya Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar bila mafanikio.
Dai katika Mahakama Kuu lilitupwa kwa kile kilichoelezwa kwamba walalamikaji wameshindwa kujenga hoja zao katika misingi ya kisheria. Mwanasheria Mkuu naye alisema ofisi yake haikuwa na nakala ya makubaliano.
Akizungumza na gazeti hili, Rashid alisema kuwa kundi lake limekusudia kuendelea na madai yao ambapo mwishoni mwa mwaka jana walipeleka notisi katika Mahakama ya Kimataifa (ICJ) kutaka kuishtaki Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kuridhia Muungano uliopo kinyume na misingi ya kisheria huku wakidai kuwa uwepo wake si halali.
Rashid alisema tayari ameshawasilisha hati ya kuishtaki SMZ kupitia wakili wa kampuni ya J.C. Chidzipha & CO.Advocates yenye ofizi zake Mombasa, nchini Kenya iliyowasilishwa Oktoba 19, 2010.
Lengo la kuishtaki serikali ni kupata hati ya Muungano ambapo kundi hilo limesema tayari limeshajibiwa barua hiyo na Mahakama ya Kimataifa na sasa wanaendelea kukusanya vielelezo vinavyohitajika mahakamani ikiwemo saini za wananchi wasiopungua 200 wa Unguja na Pemba.
"Tulipowasilisha barua yetu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ili watupatie hati ya siri ya mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar walikaa kimpya- hawakutujibu-mpaka tulipoamua kuwapeleka mahakamani ndipo wakatujibu kwamba serikali haina hati hiyo.
"Ofisi yangu haikuweka kumbukumbu ya nakala ya hati ya mkataba wa asili (original) wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo Aprili 26, 1964," alinukuu barua ya Juni 22, 2005 iliyowekwa saini na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati huo, Iddi Pandu Hassan.
 
Kwa hili LHRC wamenena
ban.mtazamo.jpg

Asha Bani​

amka2.gif
HIVI karibuni wanaharakati wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) walitoa tathmini yao juu ya uendeshwaji wa shughuli za Bunge linaloongozwa na Spika, Anne Makinda.
LHRC walimtaka Spika kusimamia vema kanuni ili kusije kutokea tena vurugu ambazo zitasababisha uvunjifu wa amani ndani ya Bunge.
Sina budi kusema naungana na LHRC katika hili na pia kumtaka spika kutowapinga wanaharakati hao kwa kuwa wameweza kuona mbali jinsi Bunge linavyoendeshwa na kusema lolote linaweza kuja kutokea hapo baadaye.
Ni imani yangu kila mbunge aliyepo mjengoni yuko kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi na si vinginevyo.
Lakini kunapotokea matatizo ya hapa na ple na kusababisha muda mwingi kwa wabunge hao kujadili mambo yasiyo ya lazima wanawavunja moyo wananchi ambao wamewachagua.
Sina maana kuwa Bunge halifanyi kazi, la hasha! Lakini maana yangu ni kwamba wabunge wetu wanapokuwa bungeni wanatakiwa kuacha mambo ya kishabiki, yasiyo na maana ili waweze kujadili mambo yatakayoweza kulisaidia taifa na wananchi wake.
Naungana na wanaharakati hao pamoja na hivi karibuni nilipomsikia aliyekuwa Spika wa Bunge, Pius Msekwa, akisema kuwa kama mtu unakuwa spika ni lazima uzifahamu kanuni na sheria mbalimbali za Bunge, vinginevyo unaweza kufanya vitu visivyokuwa na maana na wakati mwingine kupindisha kanuni kwa masilahi ya wachache.
Pia nafahamu kuwa kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa na idadi kubwa ya wabunge, ndiyo sababu inayosababisha kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine kwa upande wangu naona wanafanya maamuzi ambayo si sahihi.
Nasema hivyo kutokana na idadi hiyo kubwa kupitisha baadhi ya maadhimio kwa kelele za ‘ndiyo' maazimio ambayo hayana maana wala tija kwa taifa, lakini wao kwa ushabiki wanaitikia bila kujali na kuondoa maana ya uwakilishi wa wananchi bungeni.
Suala hilo pia ndilo linalotuumiza katika uchaguzi wa viongozi mbalimbali katika Bunge, ambao mara nyingi wamekuwa wakipitishwa kutokana na wingi wa wabunge wa CCM, hali ambayo inasababisha kuwa na watendaji ambao hawana uwezo.
Sitaki kusema kuwa maamuzi ya wabunge kumpitisha Spika Anne Makinda hayakuwa na maana, lakini nimeona chaguzi mbalimbali zikipitisha watu ambao hawana uwezo kutokana na kuwa na ushabiki usiokuwa na maana pia.
Mfumo huo ambao mimi binafsi nauita wa ‘wengi wape', unasababisha kila Bunge, spika kutoka katika chama tawala, hali ambayo si sahihi.
Kwa sababu wakati mwingine hoja za wapinzani ni kwamba huwa wanapingwa kila kukicha.
Jambo ambalo nimekuwa nikilishuhudia licha ya kuwaunga mkono wanaharakati, ni la hoja iliyokuwa imetolewa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, dhidi ya muswada wa uendeshaji wa mahakama huku akieleza kuwa unahatarisha uhuru wa Mahakama lakini alipingwa na wabunge wa CCM.
Mbali na hayo, mengine ni spika kuchukua uamuzi wa kujadili miswada mbalimbali kuwa dharura, hivyo kusababisha kuipa muda mfupi bila kufikiria umuhimu wake, jambo ambalo hata wanaharakati waliliongelea, mfano ni mjadala wa muswada wa marejeo ya Katiba.
Kwa kweli kama spika katika Bunge lijalo hatakuwa makini, nafikiri lazima kutokee machafuko.
Ni lazima afuate kanuni, Bunge hili si sawa na mabunge yaliyopita ya ndiyo na hewala kwa kila jambo hata ambalo halina mantiki kitaifa, wao ni ‘ndiyo' na hoja hupitishwa bila ya wabunge kuhoji kitu.
Jambo la ajabu na aibu ni pale wabunge wakitumia vipaza sauti kutoa maneno ya kashfa, maudhi na kejeli, lakini kwa hili pia siwezi kuwalaumu sana wabunge ingawa wao wameshindwa kuzuia hisia zao lakini haya yote ni zigo la spika ambaye kwa namna moja ama nyingine angekuwa katika mstari wa mbele kunyoosha kanuni yasingetokea.
Wabunge walitumia lugha za maudhi zikiwamo za kuzomea kama zilivyonukuliwa na kituo hicho ingawa kwa kila mtu aliyesikiliza Bunge kwa siku hiyo aliweza pia kusikia maneno hayo ya aibu kama "haoooo...wamezoea...funga mlango tupigane."
Kitu kingine ninachoweza kuzungumzia ni kutokana na kila mwananchi kufahamu kuwa amemchagua mwakilishi wake bungeni kutoa kero za jimbo na taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa LHRC kumekuwepo na mahudhurio hafifu ya wabunge wa CCM licha ya vyama vya upinzani kuwa na idadi ndogo ya wawakilishi, lakini wameonekana kuwa sawa kutokana na mahudhurio hayo na wakati mwingine kuingia ukumbini humo wakati wa kupitisha hoja kwa makelele ya ‘ndiyo', huku wakiwa wanapitisha hoja ambazo hazina maana wala mantiki.
 
MIAKA 47 YA MUUNGANO: Kero zilizopo ziondolewe
ban.blank.jpg

Julius Kunyara​

amka2.gif
LEO tunasherehekea mwaka wa 47 wa kuzaliwa kwa Muungano wa Tanzania.
Siku kama ya leo nchi mbili za Tanganyika na Unguja ziliungana mwaka 1964 na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waasisi wa Muungano wetu walikuwa marais, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa upande wa Tanganyika na hayati Aman Abeid Karume kwa Visiwa vya Unguja na Pemba.
Muungano huu umetuletea mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na maendeleo na amani isiyoyumba miongoni mwa wananchi.
Hata hivyo kumekuwa na malalamiko kutoka kila upande kudai kwamba upande mmoja unafaidika na Muungano kuliko mwingine, lakini masuala hayo yamefanyiwa kazi na mengine bado yanafanyiwa kazi na viongozi wetu.
Muungano wa Tanzania uliwezekana baada ya Tanganyika kupata uhuru Desemba 9, 1961, huku Visiwani wakipata Uhuru Januari 12, 1963.
Tangu kuasisiwa Muungano Aprili 26, 1964 ambao ndio uliozaa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kumekuwa na sifa nyingi.
Moja ya sifa hizo ni ile ya kuwa nyenzo au kitambulisho cha umoja wa kitaifa nchini Tanzania.
Hata hivyo Muungano huo una kasoro za msingi za kimaumbile. Kasoro hizo ni miongoni mwa sababu za Muungano kuwa na kero sugu.
Kasoro hizo za maumbile ni kuwapo kwa masuala ya msingi ya kikatiba ambayo hayana majibu kutoka ndani ya Katiba, sheria, sera na hata kutoka kwa watendaji.
Baadhi ya kero za Muungano
Katika kutekeleza shughuli za Muungano matatizo kadhaa yamejitokeza ambayo yamesababisha kuwapo kero za Muungano.
Siku za mwanzo kabisa za Muungano lilijitokeza tatizo mwaka 1965 wakati jambo jipya la Muungano lilipoongezwa katika orodha ya mambo ya Muungano bila ya makubaliano baina ya serikali hizi mbili.
Mawasiliano yaliopo katika kumbukumbu baina ya Waziri wa Fedha wa Zanzibar na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Muungano yanaonyesha kuwa mawazo ya Serikali ya Zanzibar katika uundaji wa Benki Kuu hayakusikilizwa.
Baada ya mwelekeo wa kuwa na Shirikisho la Afrika Mashariki kufifia, nchi za Afrika Mashariki zikitanguliwa na Uganda zilichukua hatua za kuanzisha Benki Kuu zao hata kabla ya kuivunja rasmi Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki.
Katika hali hiyo, ndipo Serikali ya Muungano ilipochukua hatua za haraka za kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) bila ya maafikiano rasmi na Zanzibar na hivyo kusababisha Zanzibar kukosa haki zake katika Bodi ya Sarafu na ndani ya Benki Kuu ya Tanzania.
Kutokana na hatua hiyo, Rais wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume aliunda kamati ya watu 12 ikiongozwa na mtaalam wa masuala ya benki, E. Ebert, ili kuishauri serikali juu ya kuanzisha Benki ya Serikali ya Zanzibar. Kamati hiyo iliwasilisha ripoti yake mwishoni mwa mwaka 1965.
Ripoti hiyo pamoja na mambo mengine ilipendekeza kuwa benki hiyo iwe ndiyo benki ya serikali na itumike kusimamia hesabu za (accounts) serikali.
Kamati ilipendekeza hadi ifikapo Julai, 1966 ‘accounts’ zote za serikali ziwe zimehamishiwa katika benki hiyo.
Hapo ndipo ilipoanzishwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), iliyoendelea kuwa ndiyo Benki ya SMZ hadi mwaka 2001 wakati BoT ilipoanza rasmi kuwa benki inayotumiwa na Serikali ya Zanzibar.
Hivyo pamoja na kuwapo BoT kama chombo cha Muungano, lakini kuanzia Awamu ya Kwanza hadi ya Tano za Serikali ya Zanzibar, haikutumia benki hiyo.
Serikali ya Muungano ilikuwa siku zote ikililalamikia jambo hilo. Wakati wa Awamu ya Pili ya Serikali ya Zanzibar, matatizo ya Muungano yalijitokeza zaidi.
Rais Aboud Jumbe alionekana dhahiri kutoridhishwa hata kidogo na mwenendo wa Muungano.
Mbali ya kutafuta mtaalamu wa sheria kutoka Ghana, Bashir Swanzi, ili kujenga hoja ya kukiukwa kwa Katiba ya Muungano na kupendekeza hatua za kisheria za kuondoa kasoro hizo, alisababisha kuanguka kwake katika uongozi.
Lakini yeye binafsi alichukizwa sana na mambo ya Muungano yanavyoendeshwa bila ya kufuata Katiba.
Kisheria shughuli yoyote isiyo ya Muungano haiwezi kufanywa bila ya ridhaa ya Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika au na Serikali ya Muungano kwa niaba ya Tanzania Bara.
Mpango wa Serikali ya Muungano kuwakilisha pia Tanzania Bara umeleta wasiwasi katika miaka kadhaa, hasa ya hivi karibuni.
Muungano au umoja hauwezi kuimarishwa kwa upande mmoja kutwaa madaraka ambayo ni ya pande mbili za umoja huo.
Huu ni ushahidi wa wazi kuwa pamoja na viongozi wakuu wa Muungano kuupenda Muungano lakini waliona kasoro za wazi za utekelezaji wa Muungano miaka mingi iliyopita.
Hatua zilizochukuliwa kuondoa kero
Katika Awamu ya Tatu na Nne, mbali ya mambo ya Muungano kuongezeka, juhudi za kusawazisha kasoro za Muungano ziliendelea.
Njia kubwa iliyotumika ilikuwa ile ya vikao vya pamoja baina ya Serikali ya Muungano na Zanzibar.
Vikao hivyo viliongozwa na Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi. Katika Awamu ya Tano, serikali ilichukua hatua nyingi zaidi kuliko awamu yoyote kushughulikia kasoro za Muungano.
Dk. Salmin Amour hakuwa akificha hisia zake za kutoridhishwa na utekelezaji wa Muungano.
Miongoni mwa mambo aliyoyawekea msimamo ni kutaka kuwe na uwazi na masawazisho ya masuala ya kiuchumi, kupunguzwa mambo ya Muungano yasiyo ya lazima na suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kuna taaarifa za kuaminika kuwa wiki chache kabla ya kutiwa saini Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Salmin Amour alimwandikia waraka maalumu Rais Benjamin Mkapa, kueleza msimamo na mtazamo wa Zanzibar juu ya uwakilishi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Awamu ya Sita ya Serikali ya Zanzibar inajulikana wazi kwa msimamo wake juu ya suala la uchimbaji wa mafuta – msimamo ambao iliurithi kutoka Awamu ya Tano.
Mbali ya suala hilo, iliunda kamati ya wataalamu katika siku za mwanzo za kuingia madarakani. Kamati ilichambua kasoro za Muungano na kupendekeza mambo ya kubaki katika Muungano, ya kupunguzwa, ya kuongezwa pamoja na utaratibu wa kuendesha masuala ya Muungano kisera, kiutawala na katika kutunga sheria za Muungano.
Miongoni mwa mapendekezo mahususi ya kamati ilikuwa ni pamoja na Bunge la Tanzania kuwa na sehemu mbili – ‘Lower House,’ itakayoshughulikia mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara, ambapo wabunge wa Zanzibar hawatashiriki na ‘Upper House’ itakayoshughulikia mambo ya Muungano tu na itakuwa na uwakilishi sawa baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.
SMZ pekee ama kwa kushirikiana na Serikali ya Muungano, zimechukua hatua kadhaa za kutafuta ufumbuzi wa kero za Muungano.
Kwa upande wa SMZ, miongoni mwa hatua ilizochukua na zinazojulikana ni pamoja na kuunda kamati mbalimbali.
Miongoni mwa kamati zilizoundwa na SMZ kushughulikia kero za Muungano kati ya mwaka 1990 na 2003 ni pamoja na Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992, Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamati ya Shamhuna, 1997), Kamati ya Rais Kuchambua Ripoti ya Kisanga (Kamati ya Salim Juma), Kamati ya Rais ya Kuandaa Mapendekezo ya SMZ juu ya Kero za Muungano. (Kamati ya Ramia, 2000) na Kamati ya BLM juu ya Sera ya Mambo ya Nje.
Nyingine ni Kamati ya Rais ya wataalamu juu ya kero za Muungano (2001), Kamati ya BLM ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kamati ya Mafuta, Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu.
Mbali ya baadhi ya kamati hizo za SMZ peke yake; Serikali ya Muungano na SMZ zimeunda tume, kamati na kuajiri wataalamu mbalimbali ili kutafuta suluhisho la kero mbalimbali za Muungano.
Aidha, SMZ na Serikali ya Muungano zimefanya vikao vya pamoja visivyopungua 80 katika ngazi mbalimbali ili kuzungumzia kero za Muungano.
Aidha, serikali hizi mbili; mwaka 1994 ziliomba msaada wa IMF ili kuzishauri kuhusiana na BoT, mgawano wa misaada na uhusiano wa kifedha.
Kwa maoni yangu, kiini cha tatizo ni mfumo wa serikali mbili. Ingawa mfumo huo kweli umechangia, lakini hilo bado ni jibu rahisi kwa suala gumu.
Katika Muungano wa Tanzania; Zanzibar na Tanganyika ziliungana kwa baadhi ya mambo tu na si mambo yote na ndiyo maana kuna orodha ya mambo ya Muungano.
Aidha, Ibara ya 64 ya Katiba ya Muungano inaeleza wazi kuwa Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria kwa mambo ya Zanzibar yasiyokuwa ya Muungano.
Hivyo ilitarajiwa kwamba, kwa vile pande hizi zimeungana kwa baadhi ya mambo tu, kanuni ya msingi ni kuwa pande hizo lazima ziwe na kauli sawa kuhusiana na mambo ya Muungano katika sera, utawala na katika kuyatungia sheria.
Aidha, ziwe na kauli sawa katika kuongeza na kupunguza mambo ya Muungano na Katiba, pamoja na kuweka bayana jambo hilo.
Ni maoni yangu kwamba iwapo viongozi watazingatia kasoro zinazoyumbisha Muungano na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu, wananchi hawatakuwa na malalmiko yoyote baina ya pande mbili (Tanganyika na Visiwani).
Pamoja na kuwapo kero nyingi, pengine tangu kuanzishwa kwa Muungano, naamini tiba mwafaka ikipatikana kero zitaondoka katika jamii yetu.

h.sep3.gif

Kwa maoni na ushauri:
Simu 0715 715271 au kunyara@gmail.com
 
Warioba ashangaa Muswada kupelekwa kwa wananchi

Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 26th April 2011 @ 08:13 Imesomwa na watu: 239; Jumla ya maoni: 0

Habari Zaidi: Maiti watano ajali ya Fuso watambuliwa
Waliokufa mlipuko lori la mafuta wafikia 16
Benki ya Dunia yafafanua utoaji mikopo
Ban Ki-moon awapongeza Watanzania
Same kuajiri watumishi wapya 120
Walimu Sikonge wakopeshwa bil 1.7/-
'Shule za msingi wafundishwe Ukimwi'
Ukonga walia na daraja
Mgambo adaiwa kuua
Mwanafunzi adaiwa kutumia silaha kupora
Ajali zaua watu wawili Dar es Salaam
Warioba ashangaa Muswada kupelekwa kwa wananchi
Kikwete kuongoza sherehe za Muungano leo
Mtoto adaiwa ‘kumdhulumu' nyumba Polisi
Askofu: Bunge sasa ni kama shule ya msingi
‘Ndiyo' ya Pinda Ilivyotunisha misuli Upinzani bungeni
JK: Sitamuonea mtu kujivua gamba
Kanisa lakemea Katiba mpya kugeuzwa Ilani
Ajali ya Fuso yaua saba
Vunjo wampigia debe Kimaro kwa JK

Habari zinazosomwa zaidi: Balaa lingine kwa Chenge
Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
‘Housigeli' anataka kuniharibia ndoa
Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
Vatican yamvua jimbo Askofu
Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
WAZIRI Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, amesema hakukuwa na haja ya kupeleka Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011 kwa wananchi kwa kuwa wabunge ni wawakilishi wao.

Ameshangaa baadhi ya watu vikiwamo vyombo vya habari, kuvalia njuga suala la Muswada huo kama vile ni mara ya kwanza kuwa na Muswada wa Katiba nchini, na kuonya kuwa watu hao hawalitakii mema Taifa.

Wakati Warioba akieleza hayo, Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, amesema tayari Muswada huo umeshaandikwa kwa Kiswahili na Serikali itatoa ratiba ya elimu kwa wananchi kote nchini kuhusu kilichomo kwenye Muswada ili kuondoa upotoshaji.

Warioba akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, alisema haoni sababu ya Muswada huo kupigiwa kelele, kwa kuwa tayari Serikali imeshaufikisha bungeni na haukuwa Muswada wa Katiba mpya, hivyo Bunge ndilo lenye mamlaka nao.

"Hivi naomba mjihoji kwanza, hasa nyie waandishi wa habari, ni mara ya kwanza kuwa na ‘bill (muswada)' nchini? Kwa nini huu uwe mgumu, kwa nini wananchi ndio waamue wakati Bunge lipo kwa ajili yao? Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, ni Muswada gani wa Katiba ulipelekwa kwa wananchi hivi?"

Alihoji Jaji Warioba. Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Katiba na Sheria, alihoji suala hilo na kubainisha kuwa ilikuwa ni kazi ya Bunge kuamua na si wananchi.

Waziri Mkuu huyo mstaafu hata hivyo aliipongeza Serikali kwa kuwa sikivu wakati wote, pale wananchi wanapolalamika na kuitaka iandae utaratibu mzuri wa kuwezesha wananchi kutoa maoni wakati utakapofika.

Muswada huo uliwasilishwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge Dodoma kwa Hati ya Dharura, lakini kabla ya kusomwa mara ya pili, wananchi walipata fursa ya kutoa maoni katika vituo vya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar, lakini kuliibuka vurugu zillizosababisha muda zaidi kutolewa kwa wananchi na wadau kutoa maoni yao hadi Bunge la Juni.

Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa na wananchi ni baadhi ya makatazo ndani ya Muswada huo kuhusu kutozungumzia suala la Muungano, urais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, lakini hata hivyo haukatazi mambo hayo kujadiliwa, ila itakapotokea hatari ya kutaka yaondolewe kabisa.

Muswada huo uliotakiwa pia kuandikwa kwa Kiswahili, ulikuwa ni wa kuwezesha kuundwa kwa Tume itakayoratibu mchakato wa wananchi kutoa maoni kuhusu Katiba mpya na si wa Katiba mpya kama ilivyokuwa ikielezwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa.

Akifafanua, Warioba alisema suala la kuandaa utaratibu ukataowezesha wananchi kutoa maoni vizuri ni jukumu la viongozi, lakini kutoa maoni mchakato utakapofika ni jukumu la wananchi wote.

Alivionya vyombo vya habari kuacha kuangalia mambo ya jazba pekee badala yake waisaidie jamii kuelewa kilichomo ndani ya Muswada na kuwakumbusha kuwa hakuna wakati ambapo Muswada wa Katiba kati ya marekebisho 14 na Katiba mpya tano zilizowahi kufanyika tangu Uhuru, ulipelekwa kwa wananchi.

Kuhusu suala la muda kama unatosha kukusanya maoni, kwa kuwa utaratibu huwa si chini ya miezi sita na vituo vitatu (Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar) badala ya nchi nzima, Warioba alisema hana maoni kuhusu suala hilo, kwa kuwa huu si wakati wa kukusanya maoni ya Katiba mpya bali utaratibu wa awali.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge ya 114 (4) kuhusu utaratibu katika Kamati za Kudumu za Bunge, ikiwamo ya Katiba, Sheria na Utawala, itafanya mikutano yake ya kawaida Dodoma, Dar es Salaam au Zanzibar.

Kombani akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, alisema tayari Serikali imeutafsiri Muswada huo kwa Kiswahili na upo mikononi mwa Spika, Serikali itahusika kutoa elimu kwa wananchi kote nchini kuhusu nini kilichomo katika Muswada huo.

"Tutashirikiana na vyombo vya habari kuueleza Muswada huo, sasa hivi lazima hatua inayofuata ni kuutoa katika gazeti la Serikali na tutatoa utaratibu wa namna tutakavyotoa elimu nchi nzima, tunataka wananchi wajue kuwa huu si Muswada wa Katiba bali ni wa mchakato wa kuunda Tume," alisisitiza Kombani.

Kumekuwa na kutoelewana tangu Muswada huo uwasilishwe bungeni huku baadhi ya vyama vya siasa vikieleza waziwazi kuupinga kwa kuandaa maandamano, ambayo yalizimwa na hatua ya Serikali kuondoa Hati ya Dharura ili kuipa nafasi Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kupokea mapendekezo zaidi.
 
Warioba ashangaa Muswada kupelekwa kwa wananchi

Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 26th April 2011 @ 08:13 Imesomwa na watu: 239; Jumla ya maoni: 0

http://habarileo.co.tz/kitaifa/?n=822
WAZIRI Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, amesema hakukuwa na haja ya kupeleka Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011 kwa wananchi kwa kuwa wabunge ni wawakilishi wao.

Ameshangaa baadhi ya watu vikiwamo vyombo vya habari, kuvalia njuga suala la Muswada huo kama vile ni mara ya kwanza kuwa na Muswada wa Katiba nchini, na kuonya kuwa watu hao hawalitakii mema Taifa.

Wakati Warioba akieleza hayo, Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, amesema tayari Muswada huo umeshaandikwa kwa Kiswahili na Serikali itatoa ratiba ya elimu kwa wananchi kote nchini kuhusu kilichomo kwenye Muswada ili kuondoa upotoshaji.

Warioba akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, alisema haoni sababu ya Muswada huo kupigiwa kelele, kwa kuwa tayari Serikali imeshaufikisha bungeni na haukuwa Muswada wa Katiba mpya, hivyo Bunge ndilo lenye mamlaka nao.

“Hivi naomba mjihoji kwanza, hasa nyie waandishi wa habari, ni mara ya kwanza kuwa na ‘bill (muswada)’ nchini? Kwa nini huu uwe mgumu, kwa nini wananchi ndio waamue wakati Bunge lipo kwa ajili yao? Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, ni Muswada gani wa Katiba ulipelekwa kwa wananchi hivi?”

Alihoji Jaji Warioba. Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Katiba na Sheria, alihoji suala hilo na kubainisha kuwa ilikuwa ni kazi ya Bunge kuamua na si wananchi.

Waziri Mkuu huyo mstaafu hata hivyo aliipongeza Serikali kwa kuwa sikivu wakati wote, pale wananchi wanapolalamika na kuitaka iandae utaratibu mzuri wa kuwezesha wananchi kutoa maoni wakati utakapofika.

Muswada huo uliwasilishwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge Dodoma kwa Hati ya Dharura, lakini kabla ya kusomwa mara ya pili, wananchi walipata fursa ya kutoa maoni katika vituo vya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar, lakini kuliibuka vurugu zillizosababisha muda zaidi kutolewa kwa wananchi na wadau kutoa maoni yao hadi Bunge la Juni.

Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa na wananchi ni baadhi ya makatazo ndani ya Muswada huo kuhusu kutozungumzia suala la Muungano, urais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, lakini hata hivyo haukatazi mambo hayo kujadiliwa, ila itakapotokea hatari ya kutaka yaondolewe kabisa.

Muswada huo uliotakiwa pia kuandikwa kwa Kiswahili, ulikuwa ni wa kuwezesha kuundwa kwa Tume itakayoratibu mchakato wa wananchi kutoa maoni kuhusu Katiba mpya na si wa Katiba mpya kama ilivyokuwa ikielezwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa.

Akifafanua, Warioba alisema suala la kuandaa utaratibu ukataowezesha wananchi kutoa maoni vizuri ni jukumu la viongozi, lakini kutoa maoni mchakato utakapofika ni jukumu la wananchi wote.

Alivionya vyombo vya habari kuacha kuangalia mambo ya jazba pekee badala yake waisaidie jamii kuelewa kilichomo ndani ya Muswada na kuwakumbusha kuwa hakuna wakati ambapo Muswada wa Katiba kati ya marekebisho 14 na Katiba mpya tano zilizowahi kufanyika tangu Uhuru, ulipelekwa kwa wananchi.

Kuhusu suala la muda kama unatosha kukusanya maoni, kwa kuwa utaratibu huwa si chini ya miezi sita na vituo vitatu (Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar) badala ya nchi nzima, Warioba alisema hana maoni kuhusu suala hilo, kwa kuwa huu si wakati wa kukusanya maoni ya Katiba mpya bali utaratibu wa awali.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge ya 114 (4) kuhusu utaratibu katika Kamati za Kudumu za Bunge, ikiwamo ya Katiba, Sheria na Utawala, itafanya mikutano yake ya kawaida Dodoma, Dar es Salaam au Zanzibar.

Kombani akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, alisema tayari Serikali imeutafsiri Muswada huo kwa Kiswahili na upo mikononi mwa Spika, Serikali itahusika kutoa elimu kwa wananchi kote nchini kuhusu nini kilichomo katika Muswada huo.

“Tutashirikiana na vyombo vya habari kuueleza Muswada huo, sasa hivi lazima hatua inayofuata ni kuutoa katika gazeti la Serikali na tutatoa utaratibu wa namna tutakavyotoa elimu nchi nzima, tunataka wananchi wajue kuwa huu si Muswada wa Katiba bali ni wa mchakato wa kuunda Tume,” alisisitiza Kombani.

Kumekuwa na kutoelewana tangu Muswada huo uwasilishwe bungeni huku baadhi ya vyama vya siasa vikieleza waziwazi kuupinga kwa kuandaa maandamano, ambayo yalizimwa na hatua ya Serikali kuondoa Hati ya Dharura ili kuipa nafasi Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kupokea mapendekezo zaidi.
 
Kingunge: Wanaopinga Muungano wapuuzwe

na Mwandishi wetu

amka2.gif
MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru, amewataka wananchi kuwapuuza watu wanaopinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza na shirikisho la vyuo vikuu Dar es Salaam, katika Ofisi za chama hicho wilaya ya Kinondoni mwanasiasa huyo aliwashangaa watu mbalimbali wakiwemo wasomi wanaovaa kofia za hadhi ya uprofesa kisha kuupinga Muungano.
Kwa mujibu wa Kingunge, wanaopinga Muungano huo ni waroho wa madaraka ambao huona nafasi za uongozi zikiwemo za uwaziri na ubalozi zinakuwa chache hivyo wanatumia nafasi hiyo kuupinga ili waweze kujitwalia madaraka.
"Mimi nashangaa kwa nini watu wanaupinga Muungano, hawa wanatakiwa kupuuzwa.
Watanzania wanatakiwa kudumisha Muungano kwa kuwa wanaoupinga ni wale ambao wanataka madaraka ya kuwa viongozi na kwamba wanaona Muungano ukiendelea nafasi za uongozi zitaendelea kuwa chache," alisema Kingunge.
Alisema Muungano ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na viongozi kupitia Baraza la Mapinduzi na la Kutunga Sheria kuuidhinisha Muungano huo.
Alihoji sababu ya Muungano wa Tanzania kutokuwa na sura ya ile ya Uingereza na Marekani ambao wameungana na Muungano wao kuwa imara.
Alisema kinachotakiwa ni kwa taifa kudumisha uzalendo huku akitolea mfano uzalendo waliokuwa nao waasisi wa Muungano huo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume kwa kuwa hawakuwa na tamaa ya vyeo wala madaraka.
Kingunge pia alisisitiza kuwa na haja ya vijana kufundishwa historia ya Muungano ili wajue wanakotoka na wanakokwenda ili kutoyumbishwa na watu wasioupenda Muungano huo.

h.sep3.gif
 
Kingunge: Wanaopinga Muungano wapuuzwe

na Mwandishi wetu

amka2.gif
MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru, amewataka wananchi kuwapuuza watu wanaopinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza na shirikisho la vyuo vikuu Dar es Salaam, katika Ofisi za chama hicho wilaya ya Kinondoni mwanasiasa huyo aliwashangaa watu mbalimbali wakiwemo wasomi wanaovaa kofia za hadhi ya uprofesa kisha kuupinga Muungano.
Kwa mujibu wa Kingunge, wanaopinga Muungano huo ni waroho wa madaraka ambao huona nafasi za uongozi zikiwemo za uwaziri na ubalozi zinakuwa chache hivyo wanatumia nafasi hiyo kuupinga ili waweze kujitwalia madaraka.
“Mimi nashangaa kwa nini watu wanaupinga Muungano, hawa wanatakiwa kupuuzwa.
Watanzania wanatakiwa kudumisha Muungano kwa kuwa wanaoupinga ni wale ambao wanataka madaraka ya kuwa viongozi na kwamba wanaona Muungano ukiendelea nafasi za uongozi zitaendelea kuwa chache,” alisema Kingunge.
Alisema Muungano ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na viongozi kupitia Baraza la Mapinduzi na la Kutunga Sheria kuuidhinisha Muungano huo.
Alihoji sababu ya Muungano wa Tanzania kutokuwa na sura ya ile ya Uingereza na Marekani ambao wameungana na Muungano wao kuwa imara.
Alisema kinachotakiwa ni kwa taifa kudumisha uzalendo huku akitolea mfano uzalendo waliokuwa nao waasisi wa Muungano huo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume kwa kuwa hawakuwa na tamaa ya vyeo wala madaraka.
Kingunge pia alisisitiza kuwa na haja ya vijana kufundishwa historia ya Muungano ili wajue wanakotoka na wanakokwenda ili kutoyumbishwa na watu wasioupenda Muungano huo.

h.sep3.gif
 
Turekebishe kasoro za Muungano

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
TANZANIA jana iliadhimisha miaka 47 ya Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Aman Abeid Karume Aprili 26, 1964.
Sherehe za kilele cha maadhimisho hayo yaliyofana, zilifanyika katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete, alikagua gwaride la heshima.
Tunaungana na Watanzania wote kusherehekea maadhimisho haya na tunautakia kila la kheri Muungano huo udumu kwa manufaa ya serikali zetu.
Lakini wakati tukiadhimisha miaka 47, yapo mafanikio makubwa yaliyofikiwa chini ya Muungano huo, lakini pia zipo changamoto lukuki ambazo wakati fulani ziliutikisa Muungano wetu kiasi cha kutaka kuvunjika.
Pamoja na kasoro zilizopo, bado Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kupigiwa mfano barani Afrika kwa kuwa ndio pekee ambao umedumu.
Zipo nchi barani Afrika mara baada ya kupata Uhuru kutoka kwa wakoloni, zilijaribu kuungana, lakini zilishindwa kutokana na sababu mbalimbali.
Nia ya kuungana ilikuwa nzuri kwa lengo la kuwa na taifa moja la Waafrika kama dhana hiyo ilivyoasisiwa na baadhi ya viongozi waasisi wa Afrika wakiwemo Hayati Kwame Nkrumah wa Ghana na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa bahati nzuri Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeweza kuwaunganisha wananchi wa pande mbili kwa kuwa na utaifa mmoja kwa miaka mingi sasa. Umri wa miaka 47 ni umri wa mtu mzima.
Katika umri huo wa nusu karne wa Muungano wetu kuna faida nyingi zilizopatikana ambazo sio rahisi kuzitaja zote kuliko changamoto.
Changamoto kadhaa zimekuwa zikijitokeza na jitihada kuchukuliwa kuzitafutia ufumbuzi.
Yapo mambo ambayo tume kadhaa zilizoundwa ziliwahi kuyabainisha kwa mfano Tume za Jaji Nyalali na Jaji Kissanga ambayo hata hivyo hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Kwa bahati nzuri maadhimisho ya miaka 47 yamefanyika sambamba na mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wananchi wako tayari kutoa mawazo yao kupitia njia mbalimbali kama mikutano, semina, makongamano na warsha.
Kwa upande wake, serikali ilishaandaa muswada wa marejeo ya Katiba ya mwaka 2011 na kupanga kuuwasilisha katika mkutano wa tatu wa Bunge ulioahirishwa Aprili 16.
Kasoro moja iliyojitokeza hivi karibuni wakati wa mchakato wa kuunda Katiba mpya ni kwamba upande mmoja wa Muungano, yaani Zanzibar, haukushirikishwa wakati ni sehemu inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi waandamizi wa serikali ya Zanzibar wakati wa kuchangia maoni yao kwa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala, walisema wazi kuwa Zanzibar haikushirikishwa na kwamba hata Rais wake ameachwa nje katika mchakato wa kuunda Tume ya Katiba na kumwachia jukumu hilo Rais wa Jamhuri ya Muungano pekee. Hilo ni kosa.
Malalamiko hayo na mengine hayapaswi kuachwa hivihivi bila kushughulikiwa kabla ya kuundwa kwa Tume ya Katiba, vinginevyo huko mbele yanaweza kujitokeza malalamiko ambayo yatauweka rehani Muungano badala ya kuuboresha.
Ikitengenezwa Katiba nzuri inayozingatia maslahi ya pande zote za Muungano ndiyo njia pekee itakayoondoa kero zote za Muungano huo
 
Miaka 47 ya Muungano: Bado ni nguzo ya taifa
ban.blank.jpg

Emmanuel Shilatu​

amka2.gif
AFRIKA haikuwa na mipaka ya nchi ndogo ndogo kama ilivyo hii leo, mpaka wakoloni walipokuja na kuigawa, ambapo leo hii tunaita nchi kupitia mkutano wao batili wa Berlin 1886, kwani hakuhusishwa Mwafrika yeyote yule.
Lengo kuu ni kuweza kututawala kirahisi ambapo kukaibuka Tanganyika waliyopewa Wajerumani na Zanzibar ikapewa Sultan wa Oman huku akisimamiwa na Waingereza. Sultan wa Oman aliingia Zanzibar tangu mwaka 1832 kutokana na kuvutiwa na marashi ya Zanzibar.
Baada ya Mjerumani kushindwa vita ya Kwanza ya Dunia na Waingereza ilimfanya kupokonywa himaya zake, Tanganyika ikiwemo. Hatimaye Watanganyika walipata uhuru wao 9, Desemba 1961 kutoka kwa Waingereza, nao wananchi wa Zanzibar walifanya mapinduzi ya kung'oa ruba ya utawala wa kisultani 12, Januari 1964.
Ikumbukwe harakati za kulikomboa Bara la Afrika miaka ya 1950 zilikuwa zikiongozwa na shujaa Kwame Nkurumah aliyeiwezesha nchi yake ya Ghana kupata uhuru wake mwaka 1957, hali iliyochochea nchi nyingine kutafuta uhuru wao akiwa na lengo la kuleta na kujenga umoja wa nchi za Afrika kwa mkupuo.
Lakini Mwalimu Nyerere akiwa na Mtazamo tofauti wa kuiunganisha Afrika kwa awamu na alianzia na wazo la kuunganisha Afrika Mashariki. Jitihada zake ziligonga mwamba kwa marais wa nchi hizo ambao ni Jomo Kenyata (Kenya) na Milton Obote wa (Uganda) ambao walikinzana kimtazamo na Mwalimu.
Baadaye Mwalimu alipata wazo lingine la kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kwa awamu hii Rais Abeid Karume (wa Zanzibar kwa kipindi hicho) alikubali wazo lake ambalo hatimaye lilizaa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ni miaka 47 imepita tangu jahazi lililowabeba Watanganyika na Wazanzibari liweke historia ya kung'oa nanga mara baada ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kuzaliwa rasmi mnamo Aprili 26,1964. Hii ilitokana na ujasiri, ushupavu na nia ya dhati waliyokuwa nayo waasisi wa Muungano huu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika) na Abeid Aman Karume (Zanzibar).
Hatua hiyo ilifikiwa kutokana na mtiririko wa kimazingira na mahusiano ambayo yalishabihiana kama si kufanana kabisa kwa pande zote mbili (Tanganyika na Zanzibar).
Zipo sababu za kijiografia, kisayansi, kitamaduni na kihistoria zilizochangia huu muungano wetu.
Kutokana na sababu za kijiografia na kisayansi inaaminika kabisa kwamba Visiwa vya Zanzibar (Pemba na Unguja) vilikuwa vimeungana na hata kushikamana kwa pamoja pembezoni mwa pwani ya ardhi ya Tanganyika. Hivyo tangu awali tulikuwa ni kitu kimoja, tulio katika ardhi moja na ya pamoja.
Pia kuna historia (isiyo na shaka) ya muingiliano wa kiutamaduni baina ya Wakazi wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hali nzima ya kuoa ama kuolewa ilizidi kushamiri baina yao.
Halikadhalika harakati za kudai ukombozi wa uhuru wetu ili tuweze kujitawala wenyewe kutoka kwa dudu la wakoloni nazo zilichangia kutuunganisha. Inaaminika (na ndiyo ilivyo) ya kuwa asilimia kubwa ya Wazanzibari walishiriki kwenye harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Mwingereza ambapo kutokana na nia, ushupavu na nguvu ya pamoja walifanikiwa kupata uhuru wa Tanganyika mnamo Desemba 9, 1961.
Lakini pia licha ya asilimia kubwa ya Wazanzibar kushiriki katika mchakato wa Mapinduzi ya Zanzibar lakini pia kulikuwepo na asilimia kubwa ya mchango wa ushiriki kutoka kwa Watanganyika. Hatimaye matunda yake yalionekana ya mapinduzi matukufu yaliyofikia kilele katika Uwanja wa Gombani Pemba yaliyofanyika Jamhuri 12, 1964, baada ya kuchoshwa na hila na ghiliba za Waarabu uliotamalaki visiwani humo kwa zaidi ya karne mbili na hatimaye waliwaacha wazalendo watwana katika ardhi yao.
Pia tusisahau lengo na nia ya dhati aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere ya kutaka kuiunganisha Afrika mzima kwa hatua lakini jitihada zake zilianza kuzaa matunda ambayo hayatakaa yatokee tena Afrika kwa kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Aprili 22, 1964, marais wa nchi hizi mbili ambazo sasa zinaunda Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (wa Jamhuri ya Tanganyika) na Abeid Aman Karume (wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar ) walitia sahihi mkataba wa kimataifa wa kuunganisha nchi zao, unaojulikana kama "Hati ya Muungano" (Articles of union) na hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ama United Republic of Tanganyika and Zanzibar (URTZ).
Kutokana na kuyapiku majina ya Tangibar na Tanzani yaliyokuwa kwenye mchakato wa ushindano wa jina halisia litakalotumika , mnamo Octoba 1964, lilitangazwa jina la Tanzania mbele ya Baraza la mawaziri wa serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mwalimu Nyerere.
Neno TANZANIA linatokana na muunganiko wa herufi TAN- kuwakilisha Tanganyika, ZAN- kuwakilisha Zanzibar, na herufi IA -zilichukuliwa kutoka kwenye Tanganyika na Zanzibar kama viwakilishi vinavyokamilisha Muungano.
Kama nilivyodokeza kwamba Muungano wa Tanzania ulifikiwa kwa kutiwa sahihi mkataba unaoitwa Hati ya Muungano (Articles of the Union) na wakuu wa nchi hizi mbili, Mwalimu Nyerere (Tanganyika) na Abeid Karume (Zanzibar) Aprili 22,1964 na kuridhiwa na mabunge ya nchi hizo Aprili 25,1964 na hatimaye kuwa sheria ya Muungano ya (Acts of Union) ya mwaka 1964.
Kimsingi sheria ya Muungano ndiyo iliyoanzisha na ndiyo iliyopewa haki ya chombo cha kikatiba kinachodhibiti katiba zote mbili za Serikali ya Muungano.
Mwanzoni kabisa Hati ya Muungano (Articles of Union) iliyomo ndani ya sheria ya Muungano iliorodhesha na hata kudadavua mambo 11 ya Muungano. Mambo hayo ni kama vile: Mambo ya nchi za nje, Ulinzi na usalama (lakini si usalama wa Taifa); Polisi, Uraia, Uhamiaji, mikopo na biashara za nchi za nje, utumishi katika Serikali ya Muungano, kodi ya mapato, usimamizi wa fedha, Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu.
Kwa nia safi na malengo mazuri yanayojitokeza Hati ya Muungano imekuwa ikiboreshwa zaidi kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele kwa malengo kusudi ya kuleta umoja, mshikamano, amani na utulivu wetu ule ule tulioanza nao awali. Ndiyo maana mtu timamu hatoshangaa sana kuona Hati ya Muungano ikiendelea kuboreshwa kila siku (na itaendelea hivyo) ambapo ilianzia na mambo 11 ambapo hii leo yamefikia takriban 23.
Mengineyo ama baadhi ya yale yalioongezeka ni kama vile; Noti; Elimu ya juu, maliasili na mafuta (mafuta) yasiyochujwa, bidhaa za mafuta na gesi asilia, ya mwaka 1968; Baraza la Mitihani ya Taifa; utafiti; utabiri wa hali ya hewa; Takwimu, Mahakama ya Rufaa ya juu ya mwaka 1979; pamoja na uandikishwaji wa vyama vya kisiasa.
Tusisahau mwaka 1965 iliundwa katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The Interim Constitution of The United Republic of Tanzania) mpaka kufikia mwaka 1977 ndipo ilipoundwa Katiba ya kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo inaendesha nchi.
Mwaka huo huo wa 1977 yaani miaka 13 baada ya Muungano kutokea kulikuwa na muungano wa vyama vikubwa viwili kuungana kutoka pande zote mbili (Bara na Visiwani). Vyama hivyo ni TANU (Tanganyika African National Union) pamoja na ASP (Afro Shiraz Party) cha Zanzibar kuungana na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua ama vitendo na mafanikio hayo si tu kwamba yalidumisha bali hata yaliendeleza kukuza Muungano wetu ambao Jahazi lake liligubikwa na misukosuko ya mawimbi makubwa baharini uliojaa uzito wa mambo mbalimbali uliokuja kwa sera ya kero zilizoleta chokochoko mbalimbali katika Muungano wetu., ambao hatutakiwi kamwe kuusahau maishani mwetu.
Tusisahau mchezo mchafu uliojaa rafu za kutisha uliotaka kufanywa na Bunge miaka ya 1990 na 1992 ya kutaka kuyakubali madai yaliyotolewa na kundi la G55 ambalo lilitaka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika, hali hii ingetuvuruga kwani ilihitaji uwepo na serikali tatu yaani Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakika yatupasa tuzishukuru hekima na busara za Mwalimu kwa kutuokoa na chokochoko ya kero hii.
Pia tusiisahau kero ama chokochoko nyingine ya Muungano wetu iliyoibuka Desemba 1, 1992, ambayo Zanzibar ilitaka kujiunga na umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) kama nchi nje ya Muungano.
Tuendelee kukumbuka ni kwa jinsi gani Zanzibar iliyokuwa inasaka ukuu nje ya Muungano kwa kuibua madai ya Bendera ya Taifa lake (Zanzibar), Wimbo wa Taifa, na Nembo yao ya Taifa.
Kwa nyakati tofauti tofauti tumekuwa tukisikia baadhi ya Wazanzibari walio wachache wakiilalamikia hali nzima ya ongezeko la mambo kwenye Hati ya Muungano (Articles of Union) kutoka mambo 11 hadi kufikia 23, ambalo ni sawa na ongezeko la mambo 12 ambao kwa baadhi yao hawaoni umuhimu wa uwepo wake na hata kutishia kujitoa. Ila asilimia kubwa ya Wazanzibari wanayaunga mkono, hali iliyosababisha hoja ya wachache kuzidiwa nguvu.
Pia tumekwisha kusikia jinsi gani Wazanzibari wanavyotaka jambo la maliasili ya mafuta pamoja na mafuta yasiyochujwa na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia iondolewe katika masuala ya Muungano ili Zanzibar kunufaika zaidi na maliasili zake.
Kukuru kakara za Wazanzibari zinatokana na madai yao ya kuwa Tanganyika (Bara) imeimeza Zanzibar (Visiwani) katika masuala mazima yahusuyo Muungano. Ikumbukwe ubaguzi wa dhana ya Tanganyika umeimeza Zanzibar si ya kweli na hii imebainishwa katika Katiba ya Muungano kuwa kuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano na seerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayani mapenzi ya dhati waliyoonyesha kwa Wazanzibari kwa kuwaruhusu wawe na serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ikumbukwe Serikali ya Muungano inaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaongozwa na Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar na chombo chao cha kutunga sheria kinaitwa Baraza la Wawakilishi.
Ndugu zangu hali ya kupuuzia na hata kuuchezea Muungano wetu ni hatari sana tena ni dhambi iliyotukuka. Mathalani Wazanzibari wakiamua kujiengua kwenye huu Muungano ili wawe kivyao vyao, hawatabaki salama. Mwalimu Nyerere alishawahi kusema ya kuwa "wakifika kwenye hatua hiyo watagundua kuwa ndani yao kuna Wazanzibari na Wazanzibara."
Nao wataamua kuwafukuza wale wa Wazanzibara, lakini hiyo haitakuwa mwisho. Punde si punde watajigundua kuwa nao (Wazanzibari) wamegawanyika kwani kuna Wapemba na Waunguja, na wakifikia hapo pia hawatakuwa salama ni lazima machafuko yatatokea.
Daima Wazanzibari watambue ya kuwa dhambi ya kutokutamalaki kwa dhana ya Unguja na Pemba unatoka na kufunikwa na kivuli cha mwamvuli cha Muungano. Hivyo umoja, mshikamano, amani na utulivu wao unategemea sana uwepo wa nguzo hii imara ya Muungano huu tulionao.
Vivyo hivyo kwa watu wa Bara (Tanganyika) ni rahisi kwao kutafunwa na dhambi ile ile ya ubaguzi watakayo ianzisha nje ya uwepo wa Muungano ni rahisi sana kwa ukabila, udini, ukanda na hata U-rangi kutamalaki ndani ya jamii wakishafikia hapo, hawatabaki salama kwani watachafuana tu.
Muungano huu tulionao unawafanya wale wageni, mataifa ya nje na watu wote wenye hila, donge, roho ya korosho kuogopa kutugusa na kutuvuruga kutokana na kuwepo kwa nguvu kubwa ya umoja, ushirikiano na mshikamano baina yetu.
Muungano huu wetu unatupatia fursa kubwa ya uhuru wa kusafiri kwa pande zote iwe ni bara ama ni visiwani. Leo hii ni rahisi sana kwa mtu wa bara kwenda Visiwani na hata wale wa Visiwani kuja Bara kwa uhuru zaidi kwani Uhuru huo wa uwepo wa nafasi hiyo umeshalipiwa na huu Muungano wetu tulionao.
Kutokana na uwepo wa uhuru wa kusafiri usio na mipaka baina yetu, pia Muungano wetu tulionao unazidi kutuongezea fursa na nafasi zaidi ya uwanja mpana wa ufanyaji biashara. Hali hii imesababisha uwepo wa mzunguuko mkubwa wa pesa ndani yetu kwani si jambo la ajabu kuona pesa zikitoka Visiwani (Zanzibar) kuja Bara (Tanganyika) kupitia mabadilishano ya bidhaa kama vile nafaka, kahawa, matunda, vipuri vya magari na kadhalika.
Pia si jambo geni tena kwa sasa kuona pesa zikivuka bahari na kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya ufanyaji ama ununuzi wa biashara kama vile magari, nazi, karafuu, tende na kadhalika.
Ndugu zangu, mpaka sasa natafuta jibu na bado sijalipata la huu Muungano wetu una ubaya gani kwetu? Muungano huu tulionao ni nguzo ya uwepo wa umoja, mshikamano, amani na utulivu hapa nchini Muungano wetu hautunyimi fursa ya kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, ama kutoka himaya moja kwenda himaya nyingine; Muungano huu hautukatazi kabisa nafasi ya mwingiliano baina ya tamaduni moja na tamaduni nyingine bila kujali ni wa Bara ama Visiwani.
Muungano huu unatuzidishia fursa ya mianya ya uwanja mpana tena usio na kikomo wa ufanyaji biashara, Muungano huu hautubagui au kuwa na upendeleo wa upatikanaji wa elimu bora, huduma za kijamii bora, Muungano hautugawi wala kuwa na upendeleo, bali umejaa uwiano sahihi wa upatikanaji wa mambo yote ya msingi yaliyomo ndani ya "Hati ya Muungano" (Articles of union). Muungano huu ni nguzo imara katika muktadha mzima wa nyanja za kimaisha yetu. Tatizo la huu Muungano wetu ni lipi hasa?
Ni ukweli uliodhahiri kuwa haitatokea Muungano kama huu (wa Tanganyika na Zanzibar) hapa barani Afrika, umoja ushirikiano, amani na utulivu ni sehemu mojawapo ya manufaa ya Muungano huu. Chini ya tawala za serikali zilizopo madarakani, yaani chini ya mwamvuli wa chama tawala CCM, Muungano wetu umeendelea kuwa imara na wenye tija kwa manufaa ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.
Njia mojawapo ya kuwaenzi vyema waasisi wetu ni kwa kuudumisha Muungano wetu. Watanzania yatupasa tuenzi Muungano wetu kwa kuulinda na kuudumisha kwa vitendo, kwani ni nguzo na fahari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika. Naomba kutoa hoja.

h.sep3.gif

0717-488 622
 
Miaka 47 ya Muungano: Bado ni nguzo ya taifa
ban.blank.jpg

Emmanuel Shilatu​

amka2.gif
AFRIKA haikuwa na mipaka ya nchi ndogo ndogo kama ilivyo hii leo, mpaka wakoloni walipokuja na kuigawa, ambapo leo hii tunaita nchi kupitia mkutano wao batili wa Berlin 1886, kwani hakuhusishwa Mwafrika yeyote yule.
Lengo kuu ni kuweza kututawala kirahisi ambapo kukaibuka Tanganyika waliyopewa Wajerumani na Zanzibar ikapewa Sultan wa Oman huku akisimamiwa na Waingereza. Sultan wa Oman aliingia Zanzibar tangu mwaka 1832 kutokana na kuvutiwa na marashi ya Zanzibar.
Baada ya Mjerumani kushindwa vita ya Kwanza ya Dunia na Waingereza ilimfanya kupokonywa himaya zake, Tanganyika ikiwemo. Hatimaye Watanganyika walipata uhuru wao 9, Desemba 1961 kutoka kwa Waingereza, nao wananchi wa Zanzibar walifanya mapinduzi ya kung’oa ruba ya utawala wa kisultani 12, Januari 1964.
Ikumbukwe harakati za kulikomboa Bara la Afrika miaka ya 1950 zilikuwa zikiongozwa na shujaa Kwame Nkurumah aliyeiwezesha nchi yake ya Ghana kupata uhuru wake mwaka 1957, hali iliyochochea nchi nyingine kutafuta uhuru wao akiwa na lengo la kuleta na kujenga umoja wa nchi za Afrika kwa mkupuo.
Lakini Mwalimu Nyerere akiwa na Mtazamo tofauti wa kuiunganisha Afrika kwa awamu na alianzia na wazo la kuunganisha Afrika Mashariki. Jitihada zake ziligonga mwamba kwa marais wa nchi hizo ambao ni Jomo Kenyata (Kenya) na Milton Obote wa (Uganda) ambao walikinzana kimtazamo na Mwalimu.
Baadaye Mwalimu alipata wazo lingine la kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kwa awamu hii Rais Abeid Karume (wa Zanzibar kwa kipindi hicho) alikubali wazo lake ambalo hatimaye lilizaa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ni miaka 47 imepita tangu jahazi lililowabeba Watanganyika na Wazanzibari liweke historia ya kung’oa nanga mara baada ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kuzaliwa rasmi mnamo Aprili 26,1964. Hii ilitokana na ujasiri, ushupavu na nia ya dhati waliyokuwa nayo waasisi wa Muungano huu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika) na Abeid Aman Karume (Zanzibar).
Hatua hiyo ilifikiwa kutokana na mtiririko wa kimazingira na mahusiano ambayo yalishabihiana kama si kufanana kabisa kwa pande zote mbili (Tanganyika na Zanzibar).
Zipo sababu za kijiografia, kisayansi, kitamaduni na kihistoria zilizochangia huu muungano wetu.
Kutokana na sababu za kijiografia na kisayansi inaaminika kabisa kwamba Visiwa vya Zanzibar (Pemba na Unguja) vilikuwa vimeungana na hata kushikamana kwa pamoja pembezoni mwa pwani ya ardhi ya Tanganyika. Hivyo tangu awali tulikuwa ni kitu kimoja, tulio katika ardhi moja na ya pamoja.
Pia kuna historia (isiyo na shaka) ya muingiliano wa kiutamaduni baina ya Wakazi wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hali nzima ya kuoa ama kuolewa ilizidi kushamiri baina yao.
Halikadhalika harakati za kudai ukombozi wa uhuru wetu ili tuweze kujitawala wenyewe kutoka kwa dudu la wakoloni nazo zilichangia kutuunganisha. Inaaminika (na ndiyo ilivyo) ya kuwa asilimia kubwa ya Wazanzibari walishiriki kwenye harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Mwingereza ambapo kutokana na nia, ushupavu na nguvu ya pamoja walifanikiwa kupata uhuru wa Tanganyika mnamo Desemba 9, 1961.
Lakini pia licha ya asilimia kubwa ya Wazanzibar kushiriki katika mchakato wa Mapinduzi ya Zanzibar lakini pia kulikuwepo na asilimia kubwa ya mchango wa ushiriki kutoka kwa Watanganyika. Hatimaye matunda yake yalionekana ya mapinduzi matukufu yaliyofikia kilele katika Uwanja wa Gombani Pemba yaliyofanyika Jamhuri 12, 1964, baada ya kuchoshwa na hila na ghiliba za Waarabu uliotamalaki visiwani humo kwa zaidi ya karne mbili na hatimaye waliwaacha wazalendo watwana katika ardhi yao.
Pia tusisahau lengo na nia ya dhati aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere ya kutaka kuiunganisha Afrika mzima kwa hatua lakini jitihada zake zilianza kuzaa matunda ambayo hayatakaa yatokee tena Afrika kwa kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Aprili 22, 1964, marais wa nchi hizi mbili ambazo sasa zinaunda Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (wa Jamhuri ya Tanganyika) na Abeid Aman Karume (wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar ) walitia sahihi mkataba wa kimataifa wa kuunganisha nchi zao, unaojulikana kama “Hati ya Muungano” (Articles of union) na hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ama United Republic of Tanganyika and Zanzibar (URTZ).
Kutokana na kuyapiku majina ya Tangibar na Tanzani yaliyokuwa kwenye mchakato wa ushindano wa jina halisia litakalotumika , mnamo Octoba 1964, lilitangazwa jina la Tanzania mbele ya Baraza la mawaziri wa serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mwalimu Nyerere.
Neno TANZANIA linatokana na muunganiko wa herufi TAN- kuwakilisha Tanganyika, ZAN- kuwakilisha Zanzibar, na herufi IA -zilichukuliwa kutoka kwenye Tanganyika na Zanzibar kama viwakilishi vinavyokamilisha Muungano.
Kama nilivyodokeza kwamba Muungano wa Tanzania ulifikiwa kwa kutiwa sahihi mkataba unaoitwa Hati ya Muungano (Articles of the Union) na wakuu wa nchi hizi mbili, Mwalimu Nyerere (Tanganyika) na Abeid Karume (Zanzibar) Aprili 22,1964 na kuridhiwa na mabunge ya nchi hizo Aprili 25,1964 na hatimaye kuwa sheria ya Muungano ya (Acts of Union) ya mwaka 1964.
Kimsingi sheria ya Muungano ndiyo iliyoanzisha na ndiyo iliyopewa haki ya chombo cha kikatiba kinachodhibiti katiba zote mbili za Serikali ya Muungano.
Mwanzoni kabisa Hati ya Muungano (Articles of Union) iliyomo ndani ya sheria ya Muungano iliorodhesha na hata kudadavua mambo 11 ya Muungano. Mambo hayo ni kama vile: Mambo ya nchi za nje, Ulinzi na usalama (lakini si usalama wa Taifa); Polisi, Uraia, Uhamiaji, mikopo na biashara za nchi za nje, utumishi katika Serikali ya Muungano, kodi ya mapato, usimamizi wa fedha, Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu.
Kwa nia safi na malengo mazuri yanayojitokeza Hati ya Muungano imekuwa ikiboreshwa zaidi kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele kwa malengo kusudi ya kuleta umoja, mshikamano, amani na utulivu wetu ule ule tulioanza nao awali. Ndiyo maana mtu timamu hatoshangaa sana kuona Hati ya Muungano ikiendelea kuboreshwa kila siku (na itaendelea hivyo) ambapo ilianzia na mambo 11 ambapo hii leo yamefikia takriban 23.
Mengineyo ama baadhi ya yale yalioongezeka ni kama vile; Noti; Elimu ya juu, maliasili na mafuta (mafuta) yasiyochujwa, bidhaa za mafuta na gesi asilia, ya mwaka 1968; Baraza la Mitihani ya Taifa; utafiti; utabiri wa hali ya hewa; Takwimu, Mahakama ya Rufaa ya juu ya mwaka 1979; pamoja na uandikishwaji wa vyama vya kisiasa.
Tusisahau mwaka 1965 iliundwa katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The Interim Constitution of The United Republic of Tanzania) mpaka kufikia mwaka 1977 ndipo ilipoundwa Katiba ya kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo inaendesha nchi.
Mwaka huo huo wa 1977 yaani miaka 13 baada ya Muungano kutokea kulikuwa na muungano wa vyama vikubwa viwili kuungana kutoka pande zote mbili (Bara na Visiwani). Vyama hivyo ni TANU (Tanganyika African National Union) pamoja na ASP (Afro Shiraz Party) cha Zanzibar kuungana na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua ama vitendo na mafanikio hayo si tu kwamba yalidumisha bali hata yaliendeleza kukuza Muungano wetu ambao Jahazi lake liligubikwa na misukosuko ya mawimbi makubwa baharini uliojaa uzito wa mambo mbalimbali uliokuja kwa sera ya kero zilizoleta chokochoko mbalimbali katika Muungano wetu., ambao hatutakiwi kamwe kuusahau maishani mwetu.
Tusisahau mchezo mchafu uliojaa rafu za kutisha uliotaka kufanywa na Bunge miaka ya 1990 na 1992 ya kutaka kuyakubali madai yaliyotolewa na kundi la G55 ambalo lilitaka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika, hali hii ingetuvuruga kwani ilihitaji uwepo na serikali tatu yaani Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakika yatupasa tuzishukuru hekima na busara za Mwalimu kwa kutuokoa na chokochoko ya kero hii.
Pia tusiisahau kero ama chokochoko nyingine ya Muungano wetu iliyoibuka Desemba 1, 1992, ambayo Zanzibar ilitaka kujiunga na umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) kama nchi nje ya Muungano.
Tuendelee kukumbuka ni kwa jinsi gani Zanzibar iliyokuwa inasaka ukuu nje ya Muungano kwa kuibua madai ya Bendera ya Taifa lake (Zanzibar), Wimbo wa Taifa, na Nembo yao ya Taifa.
Kwa nyakati tofauti tofauti tumekuwa tukisikia baadhi ya Wazanzibari walio wachache wakiilalamikia hali nzima ya ongezeko la mambo kwenye Hati ya Muungano (Articles of Union) kutoka mambo 11 hadi kufikia 23, ambalo ni sawa na ongezeko la mambo 12 ambao kwa baadhi yao hawaoni umuhimu wa uwepo wake na hata kutishia kujitoa. Ila asilimia kubwa ya Wazanzibari wanayaunga mkono, hali iliyosababisha hoja ya wachache kuzidiwa nguvu.
Pia tumekwisha kusikia jinsi gani Wazanzibari wanavyotaka jambo la maliasili ya mafuta pamoja na mafuta yasiyochujwa na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia iondolewe katika masuala ya Muungano ili Zanzibar kunufaika zaidi na maliasili zake.
Kukuru kakara za Wazanzibari zinatokana na madai yao ya kuwa Tanganyika (Bara) imeimeza Zanzibar (Visiwani) katika masuala mazima yahusuyo Muungano. Ikumbukwe ubaguzi wa dhana ya Tanganyika umeimeza Zanzibar si ya kweli na hii imebainishwa katika Katiba ya Muungano kuwa kuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano na seerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayani mapenzi ya dhati waliyoonyesha kwa Wazanzibari kwa kuwaruhusu wawe na serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ikumbukwe Serikali ya Muungano inaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaongozwa na Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar na chombo chao cha kutunga sheria kinaitwa Baraza la Wawakilishi.
Ndugu zangu hali ya kupuuzia na hata kuuchezea Muungano wetu ni hatari sana tena ni dhambi iliyotukuka. Mathalani Wazanzibari wakiamua kujiengua kwenye huu Muungano ili wawe kivyao vyao, hawatabaki salama. Mwalimu Nyerere alishawahi kusema ya kuwa “wakifika kwenye hatua hiyo watagundua kuwa ndani yao kuna Wazanzibari na Wazanzibara.”
Nao wataamua kuwafukuza wale wa Wazanzibara, lakini hiyo haitakuwa mwisho. Punde si punde watajigundua kuwa nao (Wazanzibari) wamegawanyika kwani kuna Wapemba na Waunguja, na wakifikia hapo pia hawatakuwa salama ni lazima machafuko yatatokea.
Daima Wazanzibari watambue ya kuwa dhambi ya kutokutamalaki kwa dhana ya Unguja na Pemba unatoka na kufunikwa na kivuli cha mwamvuli cha Muungano. Hivyo umoja, mshikamano, amani na utulivu wao unategemea sana uwepo wa nguzo hii imara ya Muungano huu tulionao.
Vivyo hivyo kwa watu wa Bara (Tanganyika) ni rahisi kwao kutafunwa na dhambi ile ile ya ubaguzi watakayo ianzisha nje ya uwepo wa Muungano ni rahisi sana kwa ukabila, udini, ukanda na hata U-rangi kutamalaki ndani ya jamii wakishafikia hapo, hawatabaki salama kwani watachafuana tu.
Muungano huu tulionao unawafanya wale wageni, mataifa ya nje na watu wote wenye hila, donge, roho ya korosho kuogopa kutugusa na kutuvuruga kutokana na kuwepo kwa nguvu kubwa ya umoja, ushirikiano na mshikamano baina yetu.
Muungano huu wetu unatupatia fursa kubwa ya uhuru wa kusafiri kwa pande zote iwe ni bara ama ni visiwani. Leo hii ni rahisi sana kwa mtu wa bara kwenda Visiwani na hata wale wa Visiwani kuja Bara kwa uhuru zaidi kwani Uhuru huo wa uwepo wa nafasi hiyo umeshalipiwa na huu Muungano wetu tulionao.
Kutokana na uwepo wa uhuru wa kusafiri usio na mipaka baina yetu, pia Muungano wetu tulionao unazidi kutuongezea fursa na nafasi zaidi ya uwanja mpana wa ufanyaji biashara. Hali hii imesababisha uwepo wa mzunguuko mkubwa wa pesa ndani yetu kwani si jambo la ajabu kuona pesa zikitoka Visiwani (Zanzibar) kuja Bara (Tanganyika) kupitia mabadilishano ya bidhaa kama vile nafaka, kahawa, matunda, vipuri vya magari na kadhalika.
Pia si jambo geni tena kwa sasa kuona pesa zikivuka bahari na kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya ufanyaji ama ununuzi wa biashara kama vile magari, nazi, karafuu, tende na kadhalika.
Ndugu zangu, mpaka sasa natafuta jibu na bado sijalipata la huu Muungano wetu una ubaya gani kwetu? Muungano huu tulionao ni nguzo ya uwepo wa umoja, mshikamano, amani na utulivu hapa nchini Muungano wetu hautunyimi fursa ya kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, ama kutoka himaya moja kwenda himaya nyingine; Muungano huu hautukatazi kabisa nafasi ya mwingiliano baina ya tamaduni moja na tamaduni nyingine bila kujali ni wa Bara ama Visiwani.
Muungano huu unatuzidishia fursa ya mianya ya uwanja mpana tena usio na kikomo wa ufanyaji biashara, Muungano huu hautubagui au kuwa na upendeleo wa upatikanaji wa elimu bora, huduma za kijamii bora, Muungano hautugawi wala kuwa na upendeleo, bali umejaa uwiano sahihi wa upatikanaji wa mambo yote ya msingi yaliyomo ndani ya “Hati ya Muungano” (Articles of union). Muungano huu ni nguzo imara katika muktadha mzima wa nyanja za kimaisha yetu. Tatizo la huu Muungano wetu ni lipi hasa?
Ni ukweli uliodhahiri kuwa haitatokea Muungano kama huu (wa Tanganyika na Zanzibar) hapa barani Afrika, umoja ushirikiano, amani na utulivu ni sehemu mojawapo ya manufaa ya Muungano huu. Chini ya tawala za serikali zilizopo madarakani, yaani chini ya mwamvuli wa chama tawala CCM, Muungano wetu umeendelea kuwa imara na wenye tija kwa manufaa ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.
Njia mojawapo ya kuwaenzi vyema waasisi wetu ni kwa kuudumisha Muungano wetu. Watanzania yatupasa tuenzi Muungano wetu kwa kuulinda na kuudumisha kwa vitendo, kwani ni nguzo na fahari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika. Naomba kutoa hoja.

h.sep3.gif

0717-488 622
 
h.sep7.gif
master.gif

Kamba ya Muungano imebaki uzi
ban.nasema.jpg

Christopher Nyenyembe​

amka2.gif
SIKU mbili kabla ya maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, niliandika makala ikiwajengea hofu mafisadi walioifaidi nchi hii kwa muda huo ambao sasa wameanza kuumbuana.
Jana ilikuwa kilele cha maadhimisho hayo yaliyofanyika Zanzibar huku upande mmoja ukiendelea kutajwa kuwa ni upande wa Tanzania Bara na kulifanya jina la Tanganyika kutoweka katika kipindi hicho na kuacha muundo wa serikali mbili chini ya mwamvuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wapo wanaothubutu kuita upande wa Zanzibar kwa jina jingine la Tanzania visiwani na Tanganyika ambako jina lake limemezwa ndani ya Muungano wao wanaitwa Watanzania Bara, lakini katika Muungano huo uasili wa jina la Zanzibar haujaweza kupoteza hadhi yake kama ilivyo upande wa Bara.
Jambo la msingi ambalo kwa maana halisi linatia mashaka hapo ni kule kujaribu kwa kila namna kuzika jina la nchi moja na kulikweza jina la nchi nyingine kwenye ramani ya dunia na mara kadhaa nimejaribu kuthubutu kusema kuwa tunapotosha historia na uasili wa Watanganyika, nikiamini fika siku uzi wa Muungano utakapokatika Watanganyika watarudi kwenye jina lao.
Historia haiwezi kuishia hapo au kuyeyushwa ndani ya vichwa vya waasisi wa nchi hii waliokuwepo wakati nchi mbili hizo zilipoungana kwa kuwa yalikuwepo makundi mawili yaliyokuwa yakishuhudia Aprili 22 mwaka 1964, Rais Julius Kambarage wa Tanganyika na Rais Abeid Aman Karume wa Zanzibar (wote hayati) walipotia sahihi maafikiano ya kuwepo kwa Muungano wa nchi hizo mbili.
Kwa mkataba huo wa muungano ambao kadhia yao ilifanyika rasmi aprili 26 mwaka 1964 ndipo ulipoasisiwa rasmi,watanganyika na wazanzibar kwa pamoja walifurahia kuungana na kuanzishwa kwa Jamhuri mpya ya Muungano na kuzaliwa kwa Taifa jipya la Tanzania.
Muungano huo ulioasisiwa na Rais wa Tanganyika, Nyerere na Rais wa Zanzibar Karume uliwafanya watanzania sasa kuwa nchi mbili ndani ya Muungano mmoja, Wazanzibari wanaendelea kuwa na serikali yao na rais wao lakini Watanganyika hawana rais wao wala hawana nchi yao ndani ya Muungano, hiyo naweza kuiita kuwa ni moja ya dosari kubwa za Muungano.
Ukiangalia kwa umakini ndani ya serikali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaye rais wa mungano lakini hatuna rais wa Tanganyika kwa maana ya upande wa bara na hofu kubwa inahojengeka hapo ni kule kuruhusu wimbi la mafisadi wakubwa wa bara kushambuliwa mali za muungano wakidhani kuwa wanaifilisi Tanzania Bara kwa upande mmoja.
Kitendo cha ufisadi kukomaa zaidi upande wa bara na kuwa na dalili ndogo upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari kunaonyesha wazi namna ubovu wa viongozi na uadilifu wa kiutawala ulivyotofautiana pia kwa bara na visiwani na bila shaka kamba ya muungano itakuwa imebaki uzi katikati.
Wakati maadhimisho hayo yakifanyika hakuna mtanzania yoyote anayeweza kukubali akishuhudia genge la mafisadi wachache wa bara wakiuchezea muungano kwa kuiba mabilioni ya fedha ambazo kama si wao kila mtanzania angeweza kupunguziwa adha ya maisha magumu na kuhakikisha kuwa miradi yote ya maendeleo ya jamii inaboreshwa kwa kiwango cha chini.
Kipimo cha ukomeshwaji wa hayo yote ndani ya muungano kunahitaji historia ya nchi hizo mbili zilizoungana ikarejeshwa kwa maana ya kuwepo kwa mfumo mpya wa kuzitambua serikali zote ndani ya muungano, Zanzibar na Tanganyika na kuwa na sura zenye uwiano wa kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali ukubwa wa nchi na idadi ya watu.
Kwa kuwa tumeridhia muungano kuna haki ya kila mtanzania kuweza kufaidi kwa haki sawa rasilimali za nchi zote mbili lakini kunatia mashaka kama hawa wakisema haya mafuta ni yetu na hawa wakisema haya madini ni yetu mwisho wake kila upande utataka kuwa na vitu vyake na mwisho wake, Wazanzibari watasema huyu rais ni wetu lakini Watanganyika hawatasema hivyo, watabaki katikati.
Hapo ndipo ninaposema kuwa kamba ya muungano iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na Karume ndipo inapoweza kukatikia kwa kuwa dalili zinaonyesha kuwa katikati umebaki uzi na endapo busara halisi hazitatumika kuangalia kwa kina dosari za Muungano huko tuendako kamba inaweza kukatika kutokana na wimbi la mfumo wa kiutawala na sura za mafisadi kujichimbia zaidi upande wa Bara.
Ili kuweza kuondoa dalili hizo mbaya zinazosemwa kila wakati ambazo zinaonekana kama volcano iliyolala suala la mapendekezo ya kuwepo ka mfumo mpya wa sura ya Muungano linapaswa kuangaliwa katika Katiba mpya ambayo watanzania wote wanaokodolea macho.
Katika mpya inayotegemewa kuwepo ndiyo itakayoweza kuuimarisha muungano na pengine kuja na wazo jipya la ushauri wa kuwepo kwa serikali tatu yaani,serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano wa Tanganyika.
Hilo limekuwa wazo la muda mrefu na likiwasigina vichwa watu mbalimbali,lakini vile vile unaweza kuwa wakati wa kupokea wazo ambalo sio la kale la kuwepo kwa serikali moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maana ya kuwa na rais mmoja, baraza moja la mawaziri na Bunge moja, bendera moja, wimbo mmoja wa taifa na namna moja ya umilikaji wa raslimali za nchi.
Hiyo inaweza kuwa hatua kubwa na ya mafanikio makubwa kwa kuwa ikitazamwa ndani yake kutakuwa kumepunguza mzigo mkubwa wa uendeshaji wa serikali mbili ndani ya muungano na kuwepo kwa utitiri wa watendaji ndani yake, madaraka na mfumo wa vyeo vilivyopo katika Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari.
Ipo sababu kubwa ya kuuangalia upya Muungano kwa maana ya kufikiri zaidi kuhusu maisha ya watanzania wote wa bara na visiwani kuliko kuwa na uchu wa madaraka ambao hatma yake unaonyesha dhahiri unawanufaisha zaidi watawala na kuwaacha mamilioni ya Watanzania Bara na visiwani wakiwa masikini.
Mfumo wa kuwa na utitiri wa watendaji kwenye serikali mbili zilizopo ndio chanzo cha limbuko la mafisadi na dalili za wazi za viongozi wa serikali kuwa na tamaa ya kuwarithisha madaraka watoto wao ili ile dhana ya utawala wa kiimla usiweze kupotea ndani yao na hilo nalo ni ombwe kubwa la Muungano.
Nyerere na Karume hawakuwa hivyo, hawakuunda Muungano kwa ajili ya kuvinufaisha vizazi vyao na kama wangekuwepo naamini kabisa sasa tungekuwa tunazungumzia serikali moja baada ya matazamio ya miaka inayokaribia kufikia nusu karne ya muungano ambao bila shaka umekomaa lakini bila kuondoa hayo niliyoyasema kamba ya muungano imebakia uzi katikati.
Sipendi tufikie huko lakini mashaka makubwa yanajengwa na sura mbaya za mafisadi ndani ya Muungano ambao bila ya kuwaonea aibu wanapaswa kutengwa na ili watengwe serikali zote mbili zinapaswa kushirikiana na kuwakana bila kuwaonea aibu, bila hivyo huu ninaousema si utabiri bali yanaweza kutokea. Heri ya Muungano.
 
Askofu aonya katiba mpya

*Asema isiandikwe kama ilani za vyama
*Ataka kila jambo lijadiliwe kwa kina

Na Tumaini Makene

WAKATI mchakato wa namna ya kuratibu maoni ya uandikwaji wa katiba mpya ukisubiri sheria ya bunge, wanasiasa walioko
madarakani na wale wa upinzani wametakiwa kuacha kuutaifisha kwa kuufanya sawa na uandishi wa ilani za vyama vyao vya siasa.

Imeelezwa kuwa katiba, ambayo ni sheria mama ya nchi haiwezi kuwa mali ya chama chochote kile cha siasa, pia haipaswi kuandikwa kwa ajili ya kuwasaidia wapinzani kuingia madarakani wala si kwa ajili ya kuwalinda walioko madarakani kuwazuia wapinzani wasiingie kuongoza nchi.

Pia imeelezwa kuwa katika kufikia mchakato huo, haitakuwa sahihi kuitupa katiba ya sasa, kwani 'haikuwa kitabu cha shetani', kwani ina mambo mengi mazuri ambayo Watanzania hawana budi kuyabakiza na kuyaendeleza katika katiba mpya.

Hayo yamesemwa jana katika ibada ya kitaifa ya Sikukuu ya Pasaka, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, ambapo katika ujumbe wake Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Eusebius Nzigilwa, aliwataka Watanzania kuwa na nia njema na umakini katika mchakato wa kuipata katiba mpya.

"Nchi yetu sasa hivi iko katika wakati muhimu sana katika historia na ustawi wa nchi yetu, tunataka kuandika katiba mpya, katiba ni sheria mama ya nchi yeyote ile. Wito wangu kwetu sisi sote, maana ni kitu ambacho kinamgusa kila mtu.

"Mimi kitanigusa katika uhuru wa kuhubiri haya ninayohubiri, pia kitanigusa kama raia na kila kitu, hivyo kila mmoja anahusika. Wito wangu ni kwamba, kitu ambacho...dalili za mwanzoni zilizojitokeza, tunataka kuandika katiba ya nchi kana kwamba tunaandika ilani za vyama vyetu vya siasa.

"Hili limeshaanza kuonekana, katiba sio mali ya chama chochote cha siasa, katiba ni sheria mama ya sisi sote, tukianza kuvutana kwa tofauti zetu za kisiasa kana kwamba tunaandika ilani za vyama vyetu vya kisiasa tunaanza kwa msingi uliokuwa mbovu katika kupata sheria mama ya nchi yetu," alisema Askofu Nzigilwa.

Aliwataka wanasiasa kuacha kuuteka mjadala wa uratibu na hatimaye mchakato wa uandikaji katiba mpya, kwa maslahi ya vyama vyao vya kisiasa, akisema kuwa katiba ya nchi haipaswi kuandikwa katika misingi ya kulinda kundi fulani na kugandamiza jingine.

Alisema kuwa hali hiyo ilianza kujionesha wakati wa utoaji maoni ya wadau katika muswada wa sheria ya kusimamia uratibu wa uandikwaji katiba mpya, akisema kuwa kama mchakato huo muhimu kwa maslahi ya nchi utachukua mwelekeo huo utakuwa 'mguu si sahihi'.

"Ukiwa wewe ni kiongozi ambaye uko kwenye kambi ya upinzani unasema unaandika katiba ili umtoe aliyeko madarakani tayari unaanza na mguu ambao si sahihi. Lengo la katiba si wewe mpinzani ikusaidie kumtoa aliye madarakani.

"Na wewe uliyeko madarakani ukisema tunaandika katiba ili sisi tuendelee kubaki madarakani na yule jamaa wa pembeni asiweze kufaulu hata siku moja kuingia hapa, umeshatuingiza kwenye matatizo makubwa tayari. Katiba haitakiwi kumgandamiza mtu mmoja na kumsaidia mwingine.

"Tunashukuru kuwa mswada sasa umerudishwa. Tunaomba tunaohusika tuutengeneze kwa nia njema, uadilifu, umakini na kwa maslahi mapana ya taifa letu. Tukitaka kutengeneza mswada kwa ajili ya kulinda maslahi ya vikundi au matabaka fulani ya watu, historia haitatusamehe," alisema Askofu Nzigilwa.

Aliongeza kuwa si vyema wote wanaohusika wakaingiza hila na udanganyifu katika mchakato muhimu kama huo kwa taifa taifa, akisihi Watanzania wote washiriki katika shughuli hiyo wakiongozwa na uadilifu, nia safi kwa maslahi ya taifa zima.

Askofu Nzigilwa alisema pia kuwa si vyema kuachana na kila kitu kilichoko katika katiba ya sasa, akisema kuwa haikuwa kitabu cha shetani, wala si mbaya kiasi inavyosemwa, kwani bado baadhi ya vitu vilivyomo ni vizuri, akiwataka Watanzania kuamua kuyabakiza na kuyaendeleza.

Kisha akaonekana kuzungumzia kwa lugha ya kifasihi kwa kutoa mfano kutoka katika biblia alisema si vyema katika mchakato wa utoaji wa maoni ya katiba mpya, watu wakazuiwa kuzungumzia baadhi ya mambo, akisema kuwa Watanzania waachwe waguse kila sehemu, almuradi waendelee kuishi kwa furaha, amani na mshikamano.

"Katika mjadala huu wa kupata katiba mpya tusiwekewe mti wa katikati, katika biblia katika ile Bustani ya Edeni, Mungu aliwaambia Adam na Eva, Mungu aliwaruhusu guseni kila mahali lakini isipokuwa ule mti wa katikati, kwa maana kwamba ule mti ulikuwa mbaya, pana hatari.

"Katiba yetu ya sasa ina mambo mema mengi tu, ambayo Watanzania tunaweza kugusa kila sehemu, popote na bado tukaendelea kuishi kwa amani, furaha na mshikamano, ilimuradi tuongozwe na nia njema, kwa usafi, tukiomba neema na baraka za Mwenyezi Mungu zituongoze katika hilo, sina wasiwasi katiba mpya nzuri tutaipata".

Mambo hayo ambayo Askofu Nzigilwa alionekana kuyazungumzia yalitajwa katika kipengele cha 9(2) cha muswada wa sheria ya marejeo ya katiba uliowasilishwa hivi bungeni kabla haujarudishwa serikalini kubadilishwa.

Kifungu hicho katika sehemu ya tatu ya muswada huo, kinataja mambo manane ambayo yalielezwa kuwa ni marufuku watu kuyahoji au kuyazungumzia wakati tume ya kukusanya maoni ya watu juu ya katiba mpya itakapokuwa ikitekeleza majukumu yake.

Masuala hayo yanayoitwa kuwa ya 'heshima na utukufu', hivyo hayapaswi kuguswa kwa maslahi ya taifa, yalikuwa yameainishwa katika muswada huo kama ifuatavyo; Kuwepo kwa Muungano wa Tanzania na Zanzibar, kuwepo kwa mihimili mitatu ya dola (bunge, serikali na mahakama), nafasi ya urais, mshikamano wa kitaifa na amani ya nchi.

Mengine ni; kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuwepo kwa mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia, haki za binadamu, dhana ya utu wa mtu, usawa mbele ya sheria na mfumo unaoweka utaratibu wa kufuata sheria, dhana ya Serikali ya Tanzania kutokuwa na dini na uhuru wa mahakama.
 
6 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... BRAVOO ASKOFU HAYO NDIO MANENO YA BUSARA TUNAYO YATAKA. WANASIASA WASITEKE HILI LA KATIBA KWANI WAO SIASA WAMEIGEUZA KUWA BIASHARA NA HULKA YA MFANYABIASHARA NI KUPATA FAIDA NA BIASHARA YAKE
April 25, 2011 2:07 AM
blank.gif

Anonymous said... Safi sana,vijibwa vya Slaa viko kimya,umewapenya? au hamjalipwa posho?
April 26, 2011 12:30 AM
franco said... ANONYMOUS SAID,CHANGIA HOJA SIO KUSEMA MANENO YASIYO MAZURI KWA JAMII,IKIWA KILA MTU ANA HAKI YA KUTOA MAONI YAKE NDUGU YANGU USIFANYE HIVYO TENA,TUBADILIKE CHANGIA HOJA
April 26, 2011 1:05 AM
blank.gif

Anonymous said... Pamoja na uhuru wa kutoa maoni, lakini hatuna budi kuwa na mipaka. Ukiwa mtu wa kukurupuka ni aibu, posho gani inayosema mchangiaji wa 2 hapo juu?
April 26, 2011 2:08 AM
blank.gif

Anonymous said... EWE MUUMBA MWENYEEZI MUNGU TUNAKUOMBA UWAJAALIE HAO WASIO NA KIPATO WAPATE, NA WASIO NA BUSARA UWAPE BUSARA NA PIA WABADILIKE WAWE WEMA KTK JAMII,HAKIKA INASIKITISHA MTU BADALA YA KUTOA MAONI AU MCHANGO WENYE FAIDA KWA JAMII ANAONYESHA WEREVU WAKE ILIMRADI AWEKE UOVU WAKE TUWE WASTAARABU
April 26, 2011 10:47 PM
blank.gif

Anonymous said... NIA NA MADHUMUNI YA KUWAOMBEA DUA HAO WATU NI KUKOSA AJIRA NA SHUGHULI YA KUWASHUGHULISHA MATOKEO YAKE NI KUTOA MCHANGO AU MAONI YASIYO NA TIJA HAYA YOTE NI KUKOSA KAZI YA KUFANYA NA KUFUKIRI
April 26, 2011 10:50 PM

Post a Comment
 
Back
Top Bottom