Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

`Constitutional review bill violates Union pact`




By The guardian team



9th April 2011



Comments




headline_bullet.jpg
Makinda says politicians�behind chaos at hearings



Main%20E%282%29.jpg

Youths doze off during the second day of a public hearing on the planned review of Tanzania`s Constitution in Dar es Salaam yesterday. The reason for the nap was not immediately established. (Photo: Selemani Mpochi)



Public hearings on the constitutional review bill entered the second day yesterday with more people questioning the motive behind the rush some saying the move has violated the Union pact.
In Zanzibar where the hearings started yesterday, some government leaders, political parties' representatives as well as House of Representatives members expressed indication that the constitutional review bill cannot be taken wholly as it stands.
Isles Constitutional Affairs and Justice Minister Abubakar Khamis Bakari said the bill has violated the basic agreement of the Union and called on the Speaker of the National Assembly to remove it from the table.
He said according to the Union pact anything warranting to be added or removed from ‘matters of the Union' must be discussed by both parties.
Under the prevailing circumstances, he observed Zanzibar has been sidelined right from the start because discussions have started without Zanzibaris being involved from the very beginning.
For his part, Zanzibar Attorney General Othman Masoud Othman said the bill needed minor reworking before being tabled.
Isles Agriculture and Natural Resources minister Mansour Yussuf Himid said the Zanzibar government has not been involved in the process as from the start, observing that asking the Islanders to air their views now amounted to ‘duping' them.
In Dar es Salaam, those who turned out to air their views at the Karimjee Hall said they did not want to be rushed on the issue and were opposed to the idea of taking the bill to Parliament under certificate of urgency.
"What is so urgent in the constitutional review that calls for all this rush? asked Leonard Lupilia, who identified himself as a student.
The hostile atmosphere experienced on Thursday when a group of rowdy youths booed at speakers who appeared not to agree with the review bill, was repeated yesterday prompting Singida East MP Tundu Lissu to walk out of the debating hall.
Addressing an impromptu press conference at the sidelines of the public hearings, Lissu said it is wrong to have only three debating stations namely, Dar es Salaam, Dodoma and Zanzibar and conclude that the views of over 40 million Tanzanians have been taken on board.
"Unfortunately, there are people who are bent on turning the Parliament into a rubber stamp. That is why they are out to manipulate the constitutional reform process by not listening to the public outcry that the entire work requires time," Lissu said.
The constitutional review is intended to examine consistency and compatibility of the existing constitution with regard to sovereignty, the polity, democracy and good governance in the United Republic.
Meanwhile Speaker of the National Assembly Anne Makinda yesterday accused politicians of creating chaos and disrupting on-going public hearings of the constitutional review, to advance their personal interests.
Makinda's intervention comes in the wake of the fierce confrontations during the hearings in Dodoma and Dar es Salaam on Thursday, forcing armed police to use live bullets and tear gas to disperse thousands of residents who were denied chance to contribute their views.
"These are important forums allowing the public to have their inputs on the draft constitutional Bill-2011, but some politicians are misusing this opportunity," the Speaker clarified as she adjourned the House in Dodoma yesterday.
"These politicians are using the forums as tools to gain political popularity by inciting people to disrupt public debate," Makinda added.
She criticised the politicians instigating members of the public to object the contents of the draft bill by embarking on confrontation instead of contributing their views decently through the public hearings or submitting written comments to the House committee coordinating public opinions collection.
The Parliament, one of the three state pillars, tasked its Commission on Constitution, Justice and Good Governance to collect public views on the Constitutional Review Bill, she said, insisting that politicians and members of the public are required to contribute their views instead of disrupting the entire process.
"This has been done in accordance with the legal powers vested on the Parliament…but if they make their comments through the right channels, members of the public can completely change the contents of the draft document," said the Speaker.
"This is just the draft constitutional review document, which is meant to lay down grounds for the constitutional review process-composition of the commission that would facilitate collection of public views on the new constitution, commission's terms of reference and other related aspects. We are not debating the content of the country's constitution," she clarified.
Without mentioning specific individuals, Makinda blamed politicians for being behind the reported chaos during public hearings on constitutional bill review in Dodoma and Dar es Salaam, saying: "These people and their acts must be condemned."
Speaking to reporters outside the House debate chamber, Leader of the Opposition camp in Parliament and Chadema National Chairman Freeman Mbowe, said his party plans to conduct demonstrations countrywide to press the government to halt what it called fast tracking approach to the constitutional review process.
Already, he said, the opposition had informed their leaders and members across the nation on the planned demonstration, noting that "if the government suspends endorsement of the draft next week, Chadema will also suspend the planned demonstrations."
"The fate of over 44 million Tanzanians cannot be decided by few Tanzanians in Zanzibar, Dodoma and Dar es Salaam," he said.
The draft Bill, according to a clarification issued recently in the august House by Justice and Constitutional Affairs minister Celina Kombani, seeks to kick-start the constitutional review process and not to enact the country's constitution.



SOURCE: THE GUARDIAN
 
Redraft constitutional review bill - stakeholders




By Florian Kaijage



9th April 2011



Comments





Public opinion on the Constitutional Review Act, 2011 debate, which kicked off here yesterday, hinged on major changes to ensure the nation was managed according to good governance principles.
It was proposed that the Bill be rewritten starting with the Bill's title, which did not reflect the need to have a new constitution, as expressed by President Jakaya Kikwete and Constitutional Affairs and Justice Minister Celina Kombani.
University of Dar es Salaam (UDSM) senior lecturer Dr Ezaveli Lwaitama told the gathering that the Bill title ‘The Constitutional Review Bill 2011' did not mean that the process would result in the new Constitution.
He proposed that the title should read: ‘The preparation of the new Constitution Bill 2011'.
Dr Lwaitama also said it was wrong to stipulate in the Bill that the president was empowered to appoint members of Constituent Assembly, who would pass the proposed new Constitution.
"The president should not appoint members of the Constituent Assembly because this is a very special assembly with a special task and, therefore, it has to be elected by people," said the university don.
Jane Magigita from the civil society criticised politicising the constitutional making process and defeating the good intended purpose.
She argued the proposal that the president should have powers to convert the current ordinary Parliament into a Constituent Assembly was extremely dangerous.
"Let the Constituent Assembly be separate from the current one because if that is allowed the Parliament will lean on party inclination," she said.
Magigita added that the Bill should also state clearly what would follow if it happened that after the referendum, members of the public voted no to the new Constitution as the proposed Bill was silent on the matter.
Bernard Mg'ong'o proposed that the local authorities should not be involved at all, saying they had been the root cause of unnecessary chaos during past elections.
He noted that there must be a free electoral Commission to oversee the referendum instead of using the current one, which leaned on the ruling party, which led the government.
Activist Deus Kibamba said the Bill had at least 105 deficiencies and one of them was lack of a timeframe and deadline of various activities.
Kibamba noted that it was evident that the proposed date (June 1, 2011) for the commencement of the coming Act was not realistic because of the short time provided and, therefore, there was a need for revisiting that.
Retired Justice John Mkwawa said the most important thing in the process was the diligence of the people to be appointed for the purpose.
He added that the current electoral Commission had capacity to execute the duties related to elections although there was a certain level of mistrust from the public and he proposed the Commission be overhauled if necessary to save public interests.
In general, a number of people were critical of excessive presidential powers or any other single body.
They also proposed that it was not wise to exclude political party leaders from taking part in the process.
The public hearing is under the parliamentary standing Committee on Constitution, Justice and Administration.



SOURCE: THE GUARDIAN
 
Waziri:Waliochana Muswada wahuni

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 12th April 2011 @ 23:58 Imesomwa na watu: 352; Jumla ya maoni: 0






WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan amesema, watu waliochana muswada wa sheria itakayosimamia mchakato wa kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Tanzania ni wahuni.

Waziri Samia amesema, kitendo kilichofanywa Zanzibar si tabia ya Wazanzibari na kwamba, waliofanya hivyo ni kundi la wahuni.

"Kwa hiyo wamejumuika, wamekuja kufanya uhuni wao pale" amesema Waziri huyo wakati anazungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge mjini Dodoma.

"Ile isichukuliwe kuwa ni tabia ya Wazanzibari kwa kuwa wamesema vile" amesema na akabainisha kuwa, kilichotokea ni tofauti ya mawazo na mitazamo miongoni mwa wananchi.

Waziri Samia ameyasema hayo wakati anazungumzia mafanikio na changamoto za muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati huu unapokaribia kutimiza miaka 47.

Amesema, Muungano huo ni imara lakini kuna vikwazo katika utekelezaji wa Sheria ya Muungano.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, viongozi wa Zanzibar na Tanzania Bara wamekubaliana kuwasilisha miswada Katika Bunge na Baraza la Wawakilishi Oktoba mwaka huu ili kuondoa utata wa kisheria uliopo kati ya pande hizo.

"Kuwa na mfumo tofauti wa sheria kwa pande mbili za muungano hukwamisha utekelezaj i wa baadhi ya maamuzi yanayofikiwa katika kutatua vikwazo vya muungano, mfano katika masuala ya usajili wa magari n.k" amesema.

Amesema, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa zikishirikiana kuondoa vikwazo ili muungano uendelee kuwa imara na uwe na faida kwa wananchi wa pande zote.

Amewaeleza waandishi wa habari kuwa, tangu mwaka 2006 vimefanyika vikao sita vya kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano na SMZ, na kwamba, vikao hivyo vilitanguliwa na vikao vya mawaziri, makatibu wakuu na wataalamu wa kisekta kutoka serikali zote mbili.

Amesema, hoja 13 ziliwasilishwa na kujadiliwa, mbili zimetatuliwa, zikaandaliwa hati za makubaliano, mawaziri wa serikali zote mbili walizisaini Juni 2 mwaka jana mjini Zanzibar.

Samia amesema, hoja nne zimepatiwa ufumbuzi ambazo ni mgawanyo wa mapato yanayotokana na misaada kutoka nje, misamaha ya mikopo ya fedha kutoka IMF, uwezo wa Zanzibar kukopa ndani na nje ya nchi, na malalamiko ya wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili.

Amezitaja hoja zilizo katika hatua mbalimbali za kutafutiwa ufumbuzi kuwa ni ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili, uvuvi kwenye ukanda wa uchumi wa Bahari Kuu, ushirikiano wa Zanzibar na taasisi za nje, na ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za Muungano.

Hoja nyingine ni mgawanyo wa mapato yanayotokana na faida Benki Kuu na hisa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizokuwa katika bodi ya sarafu ya Afrika Mashariki.

Amesema, hoja nyingine inayotafutiwa ufumbuzi ni kodi nyinginezo ikiwemo Kodi ya Mapato, Kodi ya mapato inayozuiwa na usajili wa vyombo vya moto yakiwemo magari na pikipiki.
 
Rasimu Muswada wa Katiba bado Send to a friend Tuesday, 12 April 2011 22:28

f.mboye.jpg
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Waandishi Wetu
RASIMU ya Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba wa mwaka 2011 imeendelea kupata upinzani mkali huku Chadema kikijipanga kuandamana katika mikoa kumi na NCCR-Mageuzi ikiamua kutinga bungeni mjini Dodoma leo kuwashawishi wabunge kuukataa muswada huo.Tayari mjadala wa rasimu hiyo umeibua hali ya wasiwasi nchini, huku Rais Jakaya Kikwete akitumia mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliomalizika mjini Dodoma juzi, kueleza kuwa muswada huo siyo Katiba bali ni njia kuelekea uundwaji katiba.
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia, alisema jana kuwa ameandaa tamko la chama hicho kuhusu sababu za msingi za kupinga muswada huo na nakala zake zitakwenda kwa Rais Kikwete, Waziri Mkuu na Jaji Mkuu.
Kwa mujibu wa Mbatia, nakala ya tamko hilo litafikishwa pia kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, huku akitahadharisha, Muswada huo utaivuruga nchi bila sababu za msingi.
Mbatia Alisema: "Kesho (leo) tutapiga kambi mjini Dodoma, kutakuwa na timu maalumu ya NCCR Mageuzi kuwashawishi wabunge kuukataa muswada huo." Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi alisema muswada huo umezuia mambo nyeti na msingi kwa taifa ikiwamo Muungano na mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, wakati tayari Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 imeyapindua.
Akipitia baadhi ya vifungu nyeti vya muungano katika katiba hiyo ya Zanzibar na ya Muungano, Mbatia alisema mabadiliko yaliyofanyika visiwani yamegusa mpaka mamlaka ya Rais wa Muungano na kunyang'anya mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 24 (3) cha Katiba hiyo.
"Leo muswada unasema tusiguse mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, wakati Katiba ya Zanzibar imekwishayapindua, wanasema tusiguse muungano wakati tayari Zanzibar kuna nchi mbili," alisisitiza.
"Kwa katiba ya sasa ya Zanzibar, Kikwete siyo Rais wa Jamhuri ya Muungano bali ni Rais wa Shirikisho. Kule Zanzibar pia hakuna tena Serikali ya Mapinduzi bali kuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa,"aliongeza.
Alifafanua kwamba ili kupata katiba mpya ni vyema mchakato ukaanzia kwenye marekebisho ya Ibara ya 98 ya katiba iliyopo ambayo itakuwa mhimili wa msingi wa harakati zote za kupata Katiba mpya.

Chadema
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wabunge wa chama hicho wataongoza maandamano yatakayofanyika Aprili 16 mwaka huu katika mikoa 10.
Mkuu wa Operesheni hiyo ya Chadema Benson Kigaila, alisema maandamano hayo yamelenga kuishinikiza Serikali kutekeleza mambo matatu kabla ya kufikia hatua ya kuandikwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Chadema imeona Serikali ya CCM haitaki kutekeleza jukumu la kuandika Katiba mpya, tunakwenda kuandamana katika mikoa kumi ili kuwaunganisha Watanzania na kushinikiza mambo makuu matatu," alifafanua Kigaila.
Alitaja mambo hayo kuwa ni kuitaka Serikali kubadili rasimu ya muswada huo kwa kuzingatia maoni ya wadau badala ya timu ya watu wachache kwa maslahi yao, kutoa muda kwa wananchi kushauriana na kujadiliana kabla ya kufika bungeni na muswada kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili kuwezesha Watanzania kuelewa na kuujadili kwa kina.
Kigaila aliweka bayana kwamba, rasimu hiyo ambayo tayari imekwishawasilishwa bungeni ina upungufu mkubwa likiwamo la kuvunja katiba iliyopo kwa kuwanyima Watanzania fursa ya kudai haki yao mahakamani kama wajumbe wa tume watakiuka haki katika utendaji wao.
Aliongeza kwamba rasimu hiyo pia imewapora haki wananchi wa Tanzania mamlaka ya kuamua utawala wanaoutaka kwa kuwanyima fursa ya kuandika katiba mpya ambayo kwa sasa imeachiwa kwa wanachama watatu wa CCM.
Kigaila alitaja timu za viongozi wa maandamano hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe (Mbeya), Dk Willbrod Slaa ataongoza Mkoa wa Tabora, Arusha yataongozwa na Naibu Katibu wa Chadema Tanzania Bara, Zitto Kabwe akiongozana na Profesa Abdallah Safari aliyejiunga na chama hicho hivi karibuni.

Sahringon yajitosa
Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania (Sahringon), umeitaka Serikali kuongeza siku za kutoa maoni kuhusu Muswada mpya wa Sheria wa marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011 badala ya siku tatu za sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Taifa wa mtandao huo, Martina Kabisama, alisema siku tatu ni chache kwa wananchi kupata fursa ya kutoa maoni yao na kwamba wananchi wengi watashindwa kufikiwa.
Kabisama aliweka bayana kuwa, Serikali kutoa siku tatu za kukusanya maoni kuhusu marekebisho hayo, ambazo tayari zimekwisha ni uonevu kwa wananchi.
Wataka Werema, Kombani wajiuzulu
Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema wametakiwa kujiuzulu baada ya kutofautiana na Rais Kikwete kuhusu kuwapo kwa Katiba mpya.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na washiriki wa Mdahalo wa kujadili Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Chriss Maina, alisema kwa nchi zinazofuata utawala bora, viongozi hao wangekwishajiuzulu baaada ya Rais kutoa muswada wa sheria hiyo. Viongozi hao kwa nyakati tofauti waliwahi kusema kwamba Katiba mpya haitatengenezwa kwa sababu ya gharama kubwa na kuwa iliyopo hivi sasa bado inafaa.
Profesa Maina ambaye alikuwa akitoa maada ya ‘Je ,mchakato unaopendekezwa utazaa Katiba inayotokana na matakwa ya wananchi', alisema hayo baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu viongozi hao kuendelea na nyadhifa zao licha ya kutofautiana na Rais.
 
Comments




0 #13 Bakari 2011-04-13 11:04 Quoting LULU:
Mnapowaambia tu wapinge mnataka wapinge nini na hawaelewi. Tuelimishwe kwanza ili tuwe na katiba madhubuti vinginevyo tutatunga mpya kila mwaka.​
@Lulu, CCM imewachapa wananchi kwa umasikini na u[NENO BAYA], hata wao (CCM) wanalijua hilo ndio maana wakaandika muswada kwa kizungu.

Hao wananchi walishanyimwa elimu, huwezi kuwaelimisha kwa muda wa siku tatu wakakuelewa! Bila kuwahamasisha watufuate tunaoelewa basi CCM itamaliza wote, tunaolewa na wasioelewa! Bila nguvu ya maandamano CCM itasimika katiba ya hovyo!
Quote









0 #12 walimu 2011-04-13 10:54 RAISI HII YA NAMNA YA KUPATA KITÎBA NI MBOVU SANA: huwezi kusema uraisi ni safi usijadiliwe: KTK KATIBA YA SASA URAISI NI ENEO LENYE MATATITZO MAKUBWA. RAIS ANAMADARAKA MAKUBWA SANA- NI KAMA MFALME. SASA UKISEMA USIJADILIWE- SI NI UHANI?
ushauri wangu: Wapinzani wote watoke nje siku mswada unapitishwa bungeni ili tujie kuwa huo ni mswada wa CCM. Tutaendesha kampeni nchi kuukataa
Quote









0 #11 Bakari 2011-04-13 10:53 Quoting LULU:
Chadema badala ya kuchapa lapa nchi nzima milele mngeishawishi serikali kwanza itoe elimu kwa nchi nzima kuhusu katiba...​
@Lulu, inaonekana uhijui vizuri Serikali ya CCM, HAWASHAWISHIKI mpaka utumie nguvu!

Mfano mzuri ni pale umma ulipolia na bei ya sukari, waliziba masikio mpaka CHADEMA walipoandamana!
Quote









0 #10 zabron simon 2011-04-13 10:39 Lulu, fikiria dada tunapopinga mswada huo tunaangalia mbele,kwani watoto wako nafamilia yako kwa ujumla wataishi maisha ya shida hivyo basi focus mbele,huo mswaada ni wa wachache na sio wa watanzania. Zanzibar vyama vyenye nguvu ni CCM na CUF, mbona hata huko wameupinga huo mswaada? Tena sio kupinga tu, wameuchana hadharani kuonyesha msisitizo,halo hii ni dharau kubwa sana, hapo ndio utajua wananchi wamechoka na kuonewa.Elimika na tambua kuwa wanawake wengi ndio huwa wanakipigia kura CCM,ukiwauliza kwanin wameipigia CCm, hawana cha kusema. Nyie wanawake ndio mnaotufanya tuishi maisha magumu, badilikeni nyie.
Quote









0 #9 zabron simon 2011-04-13 10:29 Wewe huna uelewa ndio maana unapinga hayo maandamano,kama ndio hivyo unavyosema kwanini JK na serikali yake wamezuia baadhi ya vipengele kama muungano visijadiliwe? Kama wewe ni mtanzania mwenye kufikiri basi basi huo mswaada ni batili utawanufaisha watu wachache. jitahidi usome na kuelewa vizuri.
Quote









0 #8 LULU 2011-04-13 09:37 Mi nashangaa mnavyomtukana rais na huu mswada kama atatatawala milele. Chadema badala ya kuchapa lapa nchi nzima milele mngeishawishi serikali kwanza itoe elimu kwa nchi nzima kuhusu katiba. Asilimia kubwa ya Watanzania hawajui hata katiba ya sasa ina rangi gani, ina faida gani na imeandikwa nini. Hawajui faida wala hasara yake, hawajui maana ya mswada wala umeandikwa nini wala ni hatua ya ngapi kuelekea kuundwa kwa katiba. Mnapowaambia tu wapinge mnataka wapinge nini na hawaelewi. Tuelimishwe kwanza ili tuwe na katiba madhubuti vinginevyo tutatunga mpya kila mwaka.
Quote









0 #7 CAROLINE 2011-04-13 08:48 KWA HIYO WEWE LAIZA UMEKUBALI KIKWETE AITWE
RAIS WA SHIRIKISHO LA TANZANIA NA ZANZIBAR?. NENDA KANYWE KLORITI UBONGO WAKO UFUNGUKE.HAO CCM WANAHARAKISHA MSWADA UPITISHWE KWA SIKU TATU TU ILI VIFUNGU VYA KUWABANA MAFISADI VISIINGIZWE KWENYE MSWADA. CHADEMA NA NCCR MAGEUZI WAMELIONA HILO. JK PIA AMEJIPA MADARAKA MAKUBWA SANA KWENYE HUU MSWADA WAKATI HAWEZI KUONGOZA NCHI.KAMA MPAKA LEO ANABAKIA KUWATISHIA MAFISADI NA KUWAPA SIKU 90 UNADHANI KUNA KITU ATAWAFANYA. HIZO SIKU AMETOA NA KUWAPIGIA SIMU WAFICHE MALI ZAO.HAFAI!
Quote









+1 #6 yusuf 2011-04-13 08:36 CHADEMA safi sana.Wafafanulieni wananchi maana ya huu mswada na madhara yake kwa Taifa.KATIBA ni mali ya waTZ wote bila kujali chama.Serikali imekuja na mwendo wa zima moto kuhusu huu mswada,sijui wanaficha nini.Kiongozi moja wa dini katukataza wazi tushiriki mjumuiko wa CHADEMA!Namshau ri aende mwenyewe kuwasikiliza wanachotetea,as isubiri kuletewa habari na watu wake.Zaidi ya yote asiingilie uhuru wangu wa KISIASA.
Quote









+1 #5 mhogo mchungu 2011-04-13 08:32 wewe laiza kweli unafikiria pafupi sana au ni mvivu wa kufikiri.kinachopingwa ni rasimu iliyo wakilishwa bungeni kuelezea namna au utatatibu wa kufuata wakati wa kuandika katiba mpya.kwani raisi kapewa mamlaka makubwa sana pamoja na mambo memngine.so fikiri kabla ya kuandika.
Quote









+1 #4 CCM Kapakatwa 2011-04-13 08:28 Quoting laiza:
Cahdema msiptupotoshe wananchi na msitafute umaarufu kwa maandamano. sote tunaelewa hiyo si rasimu ya muswada wa marekebisho ya katiba, viongozi wameeleza hivyo, hiyo ni rasimu ya mchakato wa kuunda chombo na kukusanya maoni ya wananchi. Sas mnapita huku na kule ati muswada umeletwa upingwe mnafikiri kila kitu mtatudanganya tu...hebu chapeni kazi shirikini kwenye kuwatumikia wananchi, pitisheni bajeti za halmashauri ili shughuli zifanyike kwani tukiona hakuna mabadiliko tunayotarajia, msitegemee kitu kwetu ifikapo 2015. Namaanisha Arusha mnakosusa vikao.​

Sikio lako la kufa kama viongozi wako, na mtatoka madarakani kwa aibu zenu, kila kitu mnafanya kiuhuni uhuni, utajiri mnajirimbikizia kwenye matumbo yenu. Ni ukweli usiofichika na unaoeleweka kwa mtu asiye na mtindio wa ubongo kwamba mswada haifai.
Wewe kwa kuwa una maslahi binafsi na CCM unajifanya oooh Chadema mnatudanganya, pumbaff, na mtaelewa sana kama mnadanganya au mnadanganyana! siasa zenyu za uhuni uhuni sasa mwisho!
Quote









+1 #3 OT Kaseka 2011-04-13 08:22 Mimi sioni sababu ya kuwa na haraka sana katika suala zito na nyeti la kuunda katiba mpya. Nyinyi viongozi mtakuwa hapo kwa muda tu. Mfano rais wa sasa amebakisha miaka isiyodhidi minne ya kuwa madarakani... Huu ni wakati wa kuacha historia iliyo njema na ya kutukuka. Tanzania si ya CCM wala CHADEMA. Uadilifu, hekima, maarifa, uvumilivu vinahitajika hapa. Hii si katiba ya chama fulani cha siasa ni ya watanzania wote katika hali zao zote za kiimani, siasa, uchumi, kabila, jamii. Huu ni msaafu kama ilivyo biblia kwa wakristo. Tuache haraka na jazba
Quote









-2 #2 laiza 2011-04-13 08:15 Cahdema msiptupotoshe wananchi na msitafute umaarufu kwa maandamano. sote tunaelewa hiyo si rasimu ya muswada wa marekebisho ya katiba, viongozi wameeleza hivyo, hiyo ni rasimu ya mchakato wa kuunda chombo na kukusanya maoni ya wananchi. Sas mnapita huku na kule ati muswada umeletwa upingwe mnafikiri kila kitu mtatudanganya tu...hebu chapeni kazi shirikini kwenye kuwatumikia wananchi, pitisheni bajeti za halmashauri ili shughuli zifanyike kwani tukiona hakuna mabadiliko tunayotarajia, msitegemee kitu kwetu ifikapo 2015. Namaanisha Arusha mnakosusa vikao.
Quote









0 #1 mtu kwao 2011-04-13 07:40 wacha moto uwake si waliyataka wenyewe!!1
Quote







Refresh comments list
 
'Waliotaka wabunge wajiondoe Bungeni ni kundi la wahuni' Send to a friend Tuesday, 12 April 2011 20:32

Midraji Ibrahim,
Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, amesema vijana waliotaka wabunge wa Zanzibar wajiondoe bungeni ni kundi la wahuni.
Akizungumza kwenye ofisi za Bunge jana, Suluhu alisema vijana hao ni wahuni na kwamba waliamua kufanya hivyo kwa utashi wao na sio kwa utashi wa watu wa Zanzibar.

Suluhu alisema masuala mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa Kamati ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala wakati ikikusanya maoni kuhusu muswada wa kuundwa kwa tume ya marekebisho ya katiba yalikuwa ni mawazo tofauti ya wananchi.

"Wanapokusanyika watu lazima watakuwa na mawazo tofauti, siamini kama kuna Mtanzania hataki amani na usalama wa nchi yetu," alisema.Alisema kifungu cha tisa katika muswada huo, kinabainisha vitu muhimu kwa taifa ambavyo vinatakiwa kuzingatiwa kwenye katiba mpya na kwamba wananchi hawakatazwi kujadili jinsi ya kuviboresha.

Kuhusu kero za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi wakati wa serikali ya awamu ya nne, Suluhu alisema wamefanikiwa kuondoa vikwazo kwenye mgawanyo wa mapato."Serikali ya Zanzibar inapata asilimia 4.5 ya misaada ya kibajeti. Kuanzia mwaka wa fedha 2009/10, SMZ imeanza kunufaika na asilimia 4.5 ya mikopo ya kibajeti," alisema.

Katika hatua nyingine, Serikali SMZ imeanza kupata misamaha ya fedha ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na kwamba dola 15.12 milioni za Marekani zilitumika kununulia magari, vifaa vya kilimo na vifaa vya Hospitali ya Mnazi Mmoja.

"Imekubalika kuwa SMZ inaweza kukopa ndani na nje ya nchi, chini ya udhamini wa Serikali ya muungano wa Tanzania," alisema Suluhu.Kuhusu wafanyabiashara kutozwa kodi mara mbili, Waziri huyo alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imetengeneza mfumo mpya wa usawa wa kutathimini Tanzania bara na visiwani na kwamba umeanza kutumika Februari 25, mwaka huu.
 
Comments




+1 #1 mkilima 2011-04-13 07:33 Mh. kutoka nje ya bunge si uhuni,hata mke na mume wakiktofau[NENO BAYA] jambo basi yule asiye pendezwa na hilo hutoka na kukaa mbali ili kuepusha shari au kuonyesha ama kupeleka ujumbe wakutopendezwa na jambo hilo, kwa hiyo kinacho hitajika ni Elimu na si kejeli,kiongozi safi huwa mvumilivu. kuwampole Mh jipange uonyeshe ukomavu wako kisiasa
Quote







Refresh comments list
 
Mabadiliko ya Katiba yasivuruge amani yetu​
pic_happy3.jpg

blank.gif
bullet3.gif
bullet3.gif
bullet3.gif
blank.gif
blank.gif
h.sep1.gif
Wasiliana na Mwandishi
phone2.gif
0716-774494
Tuma barua-pepe
Happiness Katabazi​

amka2.gif
BABA wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, alisema: "Uhuru bila nidhamu ni sawa uendawazimu na nidhamu bila uhuru ni sawa na utumwa."
Nimelazimika kuyatumia matamshi hayo kwasababu kwa wale ambao ni wafuatiliaji wa masuala yahusiyo mustakabali wa taifa hususan hili la taifa liandike Katiba, mtakubaliana nami kwamba baadhi ya wananchi wanatumia uhuru bila nidhamu.
Matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Aprili 7, mwaka huu yalitokea katika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam wakati wa mjadala wa mabadiliko ya Katiba na kusababisha mjadala huo kuvunjika.
Tukio jingine lilitokea siku hiyo hiyo katika viwanja vya Bunge Dodoma na kusababisha wanausalama kutumia mabomu ya machozi, risasi, virungu na mabango ya kuikebehi serikali baada ya wananchuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kudaiwa kutishia hali ya usalama katika eneo hilo.
Pia matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea katika Ukumbi wa Shule ya Haile Selassie mjini Zanzibar.
Inaelezwa kuwa polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) na wanausalama walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya wanachuo hao waliotaka kutumia nguvu kuingia katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa kushiriki mjadala huo.
Amri ya kupiga mabomu ilitolewa na Mkuu wa Mkoa, Dk. James Msekela baada ya wanachuo hao kuanza kurusha mawe na kumjeruhi mpiga picha wa gazeti la Mwananchi, Edwin Mjwahuzi na askari mmoja.
Wanachuo hao waliokuwa wakiimba nyimbo na mabango ya kuikebehi serikali kwa zaidi ya saa tatu, waliamua kuvurumisha mvua ya mawe ndani ya eneo la Bunge, wakipinga wadau wengine kuendelea na mjadala wakati wao wako nje.
Kwa upande wake Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, alilaani vurugu hizo na kusema wanachuo hao walikuja kwa shari maana hata kukaguliwa walikataa.
Kama maelezo ya viongozi hao ni sahihi basi yale matamshi ya Mwalimu Nyerere kwamba: "Uhuru bila nidhamu ni sawa na wendawazimu," ni sahihi kabisa.
Nchi yetu imeridhia taifa linaloongozwa na Katiba, kanuni mbalimbali za serikali, taratibu na mazoea ya serikali; hivyo kila mwananchi anatakiwa kufuata sheria hizo anapodai dai lake.
Aidha kitendo cha mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Tambwe Hizza na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wakitoa maoni yao kuzomewa na kupigiwa makelele wasiendelee kutoa maoni yao, ni wazi miongoni mwetu tunaohitaji hitaji hilo la katiba, tuna ajenda zetu za siri ambazo tumezivika kilemba cha dai la Katiba mpya.
Aiingii akilini kwa mtu mwenye akili timamu anayeelewa nini maana ya demokrasia na Ibara ya 18(a) ya Katiba ya mwaka 1977 inayosema: "Kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake," kufanya uhuni kama uliofanywa na baadhi ya wanachuo hao na wale washiriki wa mdahalo wa Karimjee uliosababisha uhairishwe kwa ajili ya wananchi kumkatiza kwa makusudi Hizza asiendelee kutoa maoni aliyotumwa na chama chake.
Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake bila kuvunja sheria na ana haki ya kusikilizwa hata kama maoni yake yanatofautiana na mawazo ya watu wengine na hiyo ndiyo demokrasia.
Kitendo cha baadhi ya washiriki kushindwa kumvumilia Hizza amalize kutoa mawazo yake, wamekosa nidhamu, hawajakomaa kidemokrasia na wana ajenda yao binafsi.
Katika mdahalo wa Karimjee imeelezwa kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wastaafu wa serikali na waliopo serikalini kwa sasa na wasomi walikuwepo na kudiriki kuleta fujo za kutupiana maneno ndani ya ukumbi huo.
Siku nyingine wanaoandaa mdahalo huo, kama hawatawaita vyombo vya usalama, ipo siku washiriki wataingia na silaha za jadi kama fimbo, wembe na nyinginezo.
Suala la mjadala wa mabadiliko ya Katiba ni suala nyeti sana kwani ni la ustawi wa taifa letu sasa kama serikali na vyombo vyetu vya dola kama havitakaa imara katika mijadalo hiyo ni wazi kabisa uvunjifu wa amani utakuwa ukitokea mara kwa mara.
Katiba haijaundwa mmeishaanza kuleta vurugu je, huko mbele ya safari ikaundwa halafu hao washiriki wakorofi wakabaini maoni yao hayakuingizwa kwenye Katiba hiyo, si watatuletea vurugu hapa nchini?
Ieleweke kwamba kila sehemu kuna viongozi na sheria na taratibu zake. Sasa kitendo kilichofanywa na wanachuo wa UDOM eti kwa sababu wamezuiliwa kuingia ndani ya ukumbi huo, kimeshusha heshima ya wasomi hao na kimetushangaza na kuona huenda wasomi hao walikuwa na ajenda nyingine zaidi ya kuruhusiwa kuingia kwenye mdahalo huo.
Siku zote jamii inaamini wasomi ni watu waliostaarabika na wawe mfano kwa jamii.
Haiingii akilini kabisa wanafunzi hao kuelezwa kwamba ukumbi huo ni mdogo hauwezi kubeba tena idadi hiyo ya wanafunzi ambao wanakisiwa kuwa ni zaidi ya 9,000 na badala yake wakaruhusu wanafunzi wachache waingie lakini wanafunzi hao wakaamua kuzua tafrani hilo eti kwa kigezo cha kuzuiiliwa kuingia ukumbini.
Watanzania tukumbuke ni hawa hawa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamekuwa wakilalamika kuwa madarasa na mabweni wanayosemea na kulala yameelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi na kuishinikiza serikali itanue vyuo hivyo kwa kujenga majengo zaidi, lakini ghafla wiki iliyopita wanafunzi hao wakakengeuka na kutaka waruhusiwe kujazana kwenye ukumbi huo licha ya kuambiwa umejaa.
Tuwahoji wanafunzi hawa endapo Dk. Msekela na uongozi wa ukumbi wa Msekwa wangekuwa legelege na wangewaruhusu wanachuo hao wote wakajazane kwenye ukumbi huo na kwa bahati mbaya hewa ingekosekana na watu kupoteza maisha kutokana na kukosekana kwa hewa, wangemlaumu nani?
Na ambao wangenusurika kifo hicho ndiyo wangekuwa wa kwanza kuishutumu serikali kuwa ilishindwa kudhibiti mapema idadi ya watu kuingia ukumbini humo?
Tuwaulize wasomi hawa hadi walifikia hatua ya kushupalia kuingia kwa nguvu kwenye ukumbi huo, hivi wanafikiri huyo aliyekuwa anaendesha mdahalo huo angeweza kutoa nafasi kwa kila mwanachuo wa UDOM kutoa maoni yake?
Sasa swali ni je hivi kama wanafunzi hao walikuwa na lengo moja la kushiriki mdahalo huo, yale mabango waliyobeba waliyapata wapi katika kipindi kifupi namna ile?
Huko ni kukosa ni dhamu mbele ya viongozi waliowazidi umri waliokuwa ndani ya ukumbi na jamii kwa ujumla.
Ni kweli wanafunzi hao walikuwa na haki ya kushiriki na kutoa maoni yao kwenye mdahalo huo na midahalo mingine itakayokuja, lakini haki hiyo iligeuka kuwa ghasia kwa wapita njia na wakazi wa maeneo hayo kutokana na vurugu walizozifanya.
Tunaamini wao ni wasomi na wengine wanasomeshwa na kodi za wananchi kama waliona haki yao imeporwa si vyombo vya dola vipo wangeenda kulalamika.
Mkae mkijua mlichokifanya kimeishajengeka vichwani mwa watu kwamba wanafunzi wa UDOM ni wakorofi wanatumiwa na wanasiasa kirahisi na mwisho wa siku sifa hiyo mbaya hata kama mtakuwa mmefaulu vizuri itawawia vigumu kupata ajira kwenye soko la ajira.
Tunafahamu si wanafunzi wote ni wakorofi ila kuna baadhi yao wamesahau dhiki za majumbani kwao na matokeo yao wamejisahau kilichowapelekea chuoni hapo ni kupata elimu na si huo mdahalo wa mabadiliko ya Katiba ambao haupo hata katika mtahala wa masomo yanayotolewa na Chuo hicho.
Lakini wasomi hao busara hiyo hawakuichukua wakaamua kutumia njia ovu ya kurusha mawe na kutoa maneno ya kashfa dhidi ya serikali na CCM.
Tuwaulize wanafunzi hao hivi ndani ya ukumbi ule ulihudhuriwa na wana CCM peke yao?
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema, alisema yeye ndiye aliyekwenda katika Chuo Kikuu cha Dodoma kuwahamasisha wanafunzi hao waje kwa wingi katika mdahalo huo.
Kwanza kabisa wanafunzi hao kabla ya kufika katika viwanja hivyo walipaswa kumuuliza Lema kwamba yeye ndiye mratibu wa mdahalo huo?
Na je, ameweka utaratibu upi ambao ungewawezesha mamia ya wanafunzi hao kuweza kushiriki katika mdahalo huo?
Kama maswali hayo yote wangemuuliza mapema mbunge huyo ni wazi wasingekubali kuswagwa namna ile ambapo mwisho wa siku wakajikuta yule aliyewaalika (Lema) amepata nafasi ya kuingia ukumbini na wao kuishia nje na kupata mkong'oto toka kwa Jeshi la Polisi.
Kama wangeondokana na mawazo mgando baada ya kupata mwaliko wa mdomo toka kwa mbunge huyo ambaye naye alikuwa ni mwaliko kama walivyokuwa waalikwa wengine, serikali ya wanafunzi wa chuo hicho ingeteua wawakilishi wachache waende kushiriki kwa niaba ya wanafunzi wote.
Mwanachuo yoyote aliyekuwa ana mawazo yake angeandika wazo lake na kuwapatia wawakilishi hao ambao wangelifikisha kwenye mdahalo huo ama kwa mdomo au kwa maandishi.
Hivyo idadi kubwa ya wanafunzi wangebaki chuoni na kuendelea kujisomea kwani sisi tunachojua kilichowapeleka wanafunzi hao pale UDOM ni masomo na si ujuha kama ule.
Wanafunzi na wananchi wengine wanaoleta vurugu kwenye midahalo hiyo wajue kwamba wao si waamuzi wa kuruhusu muswada wa mabadiliko ya Katiba upite au usipite.
Waamuzi ni wabunge wetu wanaotuwakilisha bungeni ambapo Alhamisi na Ijumaa wiki hii wataujadili muswaada huo na kuupigia kura za muswada huo upite au usipite.
Hivyo kazi yetu sisi ni kutoa maoni kwa njia ya amani na kazi ya kuamua kuamua mswaada huo upite au usipite ni ya Bunge.
Hivyo msituvurugie amani kwaajili ya ajenda zenu za siri.
Fukuto la Jamii linawaasa wafuasi wa vyama vya siasa hapa nchini vinavyodaiwa vimekuwa vikiwatumia wanachama wao kuleta vurugu kwenye midahalo hiyo, viache tabia hiyo, kwani muswada huo hauna vyama bali unawahusu Watanzania.
Desemba 31 mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete wakati akizungumza na wananchi kupitia hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi, alisema anakubali hoja ya kuundwa kwa Katiba mpya.
Kila mmoja wetu amelichukulia hilo kivyake, na hii ndiyo tabia ya Watanzania ambo hawajajenga mila, desturi na utamaduni wa kushiriki katika mjadala wa kitaifa.
Mjadala wa kitaifa ni mchakato wa kujenga hoja kwa masilahi ya taifa. Kamwe hauendeshwi kwa kila mtu kujenga hoja kutetea tumbo lake.
Kwa hiyo wengi wanaojenga hoja ya kutaka kuundwa kwa Katiba mpya, wanafikiri matumbo yao, masilahi binafsi na umaarufu binafsi.
Vipo vyama na wapo watu na vikundi ambavyo bila kujali umaarufu binafsi wameendeleza hoja hii hadi leo.
Wapo baadhi ya wanasiasa watakaojaribu kuibinafsisha hoja hiyo ili waonekane ni waasisi wa hiyo hoja.
Wanaamini kwamba kumbukumbu za Watanzania ni duni hawawezie kukumbuka hoja hii ilianza lini na waasisi ni kina nani.
Tena katika hali ya kushangaza kama sio kustaajabisha wanachama wa vyama vya siasa na baadhi ya viongozi wao hawajui katiba za vyama vyao ambazo zimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili na wala hawafahamu zimeandikwa nini ndani yake.
Sasa iweje leo hii wawe na ukereketwa wa kudai Katiba mpya ikiwa tu ibara za katiba ya vyama vyao hawazijui zinasema nini?
Wengine hata gamba la Katiba ya Jamhuri hawajawahi kuliona na duka la vitabu vya serikali ambapo ndipo sheria zote za Katiba ya nchi zipo yapo wapi?
Rais Kikwete katika hotuba yake ile pia alitamka kwamba mwaka huu ni wa Watanzania kujadili hoja ya Katiba mpya na yeye ataunda tume ya kuongoza mchakato wa kupata Katiba mpya.
Na kweli ahadi hiyo ya rais imetimia katika kipindi kifupi, kwani tayari muswada umeshaandaliwa na kupelekwa bungeni tayari kwa kuanza kujadiliwa.
Ni vema tukampongeza Rais Kikwete kwa kutekeleza ahadi hiyo katika hatua hii ya awali kwa kuzingatia kwamba hatua hiyo ni ya kijasiri sana kwani ukweli ni kwamba kundi kubwa la wanaopinga hoja hiyo wapo katika chama anachokiongoza cha CCM na serikali anayoingoza.
Sasa Watanzania tuko wapi? Je, tunaelewa kilichomsibu rais hadi akubali hoja ya Katiba mpya?
Kabla ya kupinga na kuona nia ya rais wetu ni mbaya eti kama ana jaribu kuteka hoja au kupora hoja ya wapinzani, tujiulize ni wangapi wanaelewa maana kamili ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka 2010?
Ni wangapi miongoni mwetu wameishaisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977?
Nimalizie kwa kuwakumbusha wale wote wanaoleta vurugu kwenye mijadala hiyo kwamba utawala wa serikali yetu ni utawala unaoongozwa na sheria na Katiba na kamwe utawala huo haufanani na ule utawala wa samaki aina ya kambale ambao baba, mama na mtoto wote wana ndevu.
Hivyo sote tunapaswa tufuate sauti moja ya misingi tuliyojiwekea.
Hakuna ubishi, yale matamshi ya Mwalimu Nyerere kuwa "Uhuru bila nidhamu ni sawa uendawazimu," yametimia kutokana na matukio hayo niliyoyataja na mengine sijayataja ambayo yametokea na yanaoendelea kutokea chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne.
Sasa unapokuwa na taifa lenye wananchi wanaotumia vibaya uhuru wa kutoa maoni ni wazi kabisa muda si mrefu taifa hilo litajikuta linafuga na kuwalinda wananchi wengi ambao ni wendawazimu.
Navyo vyombo vya habari visifanye ushabiki katika suala hili la mchakato wa mabadiliko ya Katiba.
Kwa sababu hoja hiyo si mali binafsi ya Rais Kikwete, CCM, CHADEMA, NCCR-Mageuzi wala vyama vingine vya upinzani bali ni hoja ya Watanzania wote kwa masilahi yao.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.
 
Majukumu ya NEC, ZEC yajadiliwa bungeni
JIBU LA SWALI LA MBUNGE Viti Maalum

na Bakari Kimwanga na Danson Kaijage, Dodoma


amka2.gif
MBUNGE wa Viti Maalumu, Riziki Omar Juma (CUF), amehoji sababu za serikali kutotumia sheria mbili tofauti kwa uchaguzi mmoja wa Jamhuri ya Muungano kwa madai ya kuwanyima fursa wananchi wengi ambao wanatakiwa kupiga kura.
Mbunge huyo alidai kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ambayo ni wakala wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Taifa ya (NEC) inatumia sheria inayohitaji vitambulisho vya ukaazi katika wapiga kura jambo ambalo ni tofauti na NEC.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) William Lukuvi, alisema kuwa siyo kweli kwamba ZEC ni wakala wa NEC.
Alisema ZEC na NEC ni vyombo viwili tofauti vyenye majukumu na kila chombo kina Mamlaka kamili juu ya majukumu yaliyoainishwa kwenye Sheria Husika.
Lukuvi alisema kuwa Tume ya Uchaguzi ya NEC ilianzishwa chini ya Ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na majukumu ya NEC yameainishwa katika ibara hiyo kuwa pamoja na mambo mengine itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Aidha, alisema kwa upande wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC), imeanzishwa chini ya Katiba ya Zanzibar na majukumu yake yameainishwa katika katiba hiyo na kuelekeza majukumu yake kuwa ni kusimamia uchaguzi upande wa Zanzibar (Rais wa Zanzibar na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi).
Akiendelea kutoa ufafanuzi wa swali hilo, Lukuvi alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 12A cha Sheria ya Taifa ya uchaguzi, Sura ya 343 kama ilivyorekebishwa mwaka 2010 kinaipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mamlaka ya kutumia daftari la wapiga kura lililoandaliwa na Tume ya Uchaguziya Zanzibar .
Hata hivyo alisema kuwa kifungu hicho kinaipa NEC mamlaka ya kuandikisha wapiga kura watakaopiga kura ya Rais wa Muungano ambao hawakuandikishwa na ZEC.
 
Bomani: Serikali isione aibu kuondoa Muswada wa Katiba Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:05

bomani%20jaji.jpg
Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa Serikali Jaji Mark Bomani

Ramadhan Semtawa na Exuper Kachenje
MWANASHERIA Mkuu Mstaafu wa Serikali Jaji Mark Bomani, ameitaka Serikali, kutoona aibu kuuondoa Muswada wa Marejeo ya Katiba bungeni akionya kwamba kinyume chake, utaivuruga nchi.Jaji Bomani alitoa wito huo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu ofisini kwake, Dar es Salaam.

"Serikali isione aibu kuondoa muswada huo, isije ikafikiri labda kuuondoa itakuwa ni aibu la... Itakuwa imeonyesha usikivu na umakini wa kusikiliza hoja za wananchi walio wengi. Katiba si kitu cha kuchezea hata kidogo," alisema.Jaji Bomani alifafanua kwamba si vizuri kwa muswada juu ya jambo zito kama la Katiba, ukatolewa kwa hati ya dharura na kuhoji: "Hiyo pupa ya nini?Kutokana na uharaka huo ndiyo maana hata muswada wenyewe umejaa makosa na dosari.''

"Kwa hiyo kwa ushauri wangu, muswada uliokwisha chapishwa uondolewe (withdrawn), kwa maelezo kwamba umekwenda nje ya mstari na kwamba utaletwa mwingine utakaokuwa umezingatia maoni mbalimbali yaliyokwishatolewa.''Kwa mujibu wa Jaji Bomani, muswada huo tayari umekiuka taratibu za awali na kusisitiza: "Kama Serikali ikiendelea kushinikiza uendelee, wapo watu wanaoweza kupinga kwa njia hasi na chanya. Kwa maoni yangu, kila kitu lazima kiangaliwe upya."

Mwanasheria huyo alisema muswada huo umetenga mambo nyeti yasijadiliwe, kitu ambacho alisema ni kosa, kwani Katiba mpya inapaswa kugusa kila eneo... "Kwa maneno mengine, masuala kama aina ya Muungano, muundo wa Serikali, kazi na muundo wa Bunge, aina ya madaraka ya Serikali za Mitaa, aina ya Mahakama na kazi zake n.k."
Alisema mambo hayo yote ni lazima yafikiriwe na kufanyiwa mabadiliko au marekebisho itakavyolazimu na kusisitiza: "Kwa mtazamo huu, kila kitu kinastahili kujadiliwa."

Njia za kuanza mchakato
Jaji Bomani alisema kuna njia nyingi za kujadili suala hilo na mambo mawili lazima yazingatiwe; "Kwanza wananchi lazima washirikishwe vya kutosha ili Katiba itakayotokana na mjadala huo waione kuwa ni yao maana walishiriki katika kuijadili."

Pili, alisema ni lazima mchakato wenyewe uendeshwe kwa makini ili kufika mahali ambako itapatikana Katiba mpya yenye tija: "Maana yangu ni kwamba pamoja na kuwashirikisha wananchi, lazima wahusishwe pia wataalamu na watu wenye uzoefu kwani hatuanzii (zero) sifuri."

Alisema haiwezekani kuacha umma wa watu zaidi ya 40 milioni kujadili na kupitisha Katiba.'' Lazima uwepo utaratibu ambao utawezesha kufikia lengo la katiba kihalali,''alisema.
Kwa mujibu wa Jaji Bomani njia ya Tume maalumu kukusanya maoni ya wananchi wa makundi mbalimbali na baadaye kutoa mapendekezo, ni njia mojawapo inayoweza kufanikisha lengo la kupata katiba mpya.

Muundo wa Tume
Akizungumzia muundo wa Tume, Jaji Bomani alisema lazima iwe kubwa ya kutosha ili ijumuishe makundi na rika mbalimbali."Lakini isiwe kubwa mno kiasi cha kuifanya ishindwe kufanya kazi zake kwa tija na kupata muafaka," alisema.Kuhusu muda wa tume hiyo kukamilisha kazi yake, Jaji Bomani alisema: "Nchi yetu ni kubwa. Ili angalau sehemu nyingi zifikiwe muda wa kutosha unahitajika, labda kati ya mwaka mmoja na miwili. Ni lazima pia izingatiwe kwamba wajumbe wa tume hiyo wana shughuli zao, haiwezekani ukapata watu makini ambao watakuwapo wakati wote."

Uandaaji hadidu za rejea
Akizungumzia suala la hadidu za rejea kwa tume hiyo, Jaji Bomani alisema: "Ni mapema mno kwa Serikali kuandaa hadidu za rejea (terms of reference) na kwamba kilichotakiwa kufanyika ilikuwa ni kwa Rais kuchagua kamati ambayo ndiyo ingeandaa hadidu za rejea baada ya kushauriana na vikundi mbalimbali." Alisema kamati hiyo ndiyo ambayo ingemshauri Rais juu ya hadidu za rejea na mambo mengine husika na huo ndiyo ungekuwa msingi wa kuandaa muswada wa kupeleka bungeni: "Kamati ya namna hii yenye wajumbe takriban 30 ingeweza ikapewa, tuseme, miezi mitatu kukamilisha kazi hiyo ya kuandaa hadidu za rejea."

Ushauri wa Dk Salim, Butiku kuhusu muswada
Katika hatua nyingine waasisi wawili wa CCM wamesema kuwa yanayotokea sasa hayaepukiki na kushauri mjadala huo uendelee kwani ni wakati muafaka kuwapo.Waasisi hao, aliyekuwa Katibu Mkuu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Dk Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku walitoa maoni hayo jana kwa nyakati tofauti nje ya ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipohudhuria kongamano la tatu la Kitaaluma la Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere.

"Yanayotokea sasa hayaepukiki, unajua nchi yetu kwa miaka mingi ilikuwa katika mfumo wa chama kimoja cha siasa, lakini sasa tupo katika mfumo wa vyama vingi na haujawa wa miaka mingi, hivyo tunayoyaona yanatokea ni kutokana na mfumo huo na hayaepukiki," alisema Dk Salim.

Hata hivyo, Dk Salim alionya kuwa itakuwa hatari kwa Watanzania kutumia hali hiyo na kuhatarisha amani ya taifa na kuwagawa watu kwa misingi ya dini, rangi, itikadi za kisiasa au kabila na kuwataka wasiwe wepesi kulaumu mataifa ya kigeni, badala yake wajizuie kufanya makosa yanayoweza kutumiwa na nchi hizo kujinufaisha.
Alisema badala yake, katika kujadili hoja au jambo lolote, ni muhimu kila mmoja kufanya hivyo akiweka mbele maslahi ya taifa kwa kuwa Tanzania ni ya Watanzania wote.

Alisema wakati wa uhai wake, Mwalimu Nyerere aliweka misingi bora ya utaifa kwa maslahi ya Watanzania wote, hivyo ni muhimu misingi hiyo ikadumishwa na ndiyo sababu ya uwepo wa tamasha la Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere.

Kwa upande wake, Butiku alisema: "Napenda, nashauri, tuzungumze kuhusu Katiba, maana iliandikwa muda mrefu na watu wengi wapya. Labda misingi imepitwa na wakati au haieleweki kwao."
Alishauri kuwa mazungumzo hayo kuhusu Katiba yafanyike kwa uhuru na kwamba mawazo yatakayotolewa yaonyeshe kama inahitajika mpya au la na kusiwapo kulazimishana.

"Mazungumzo yafanyike kwa uhuru, mawazo yaonyeshe kweli tunahitaji Katiba au la, yatuonyeshe kwa uwazi waliyoamua Watanzania na tusilazimishane," alisema Butiku.Alisema kuwa zipo kauli alizoziita za hapa na pale ambazo si zake, zinazoeleza kuwa huenda mambo hayaendi vizuri kwa sababu ya Katiba iliyopo, huku wengine wakieleza kuwa ingekuwa vizuri kuwapo kwa maelewano kuhusu sheria mama, yaani Katiba, lakini akasema haoni kama Katiba yote ina matatizo, bali maeneo machache.

Hata hivyo, alisema ni jukumu la Watanzania wenyewe kuamua iwapo wanataka mabadiliko ya Katiba au vinginevyo."Katiba kama itatuzuia kufikiri, kutenda au kuamua, hapo nafikiri ni sahihi kuangaliwa upya, lakini kama si hivyo, hiyo ni Katiba tu, inaweza kuwa karatasi tu, tatizo likawa utekelezaji wa yaliyoandikwa.
 
CCM: Graft war will be won





From MASATO MASATO in Dodoma, 13th April 2011 @ 20:00, Total Comments: 0, Hits: 155

THE ruling party, Chama Cha Mapinduzi (CCM), on Wednesday reiterated its firm resolve to fight corruption and all corrupt elements within its ranks, saying the war it has started will definitely be won.

"The party will ultimately win this war (against corruption)... we are determined to win, we have started and we will sustain it to the end," said Mr Nape Nnauye, the newly elected publicity secretary.

Addressing a news conference, Mr Nnauye welcomed CCM members who had defected to opposition parties in protest against the ruling party's alleged links with corrupt people.

"The party has taken bold steps to cleanse itself. May I seize this opportunity to welcome back our members who were angry and resolved to protest misdeeds within our party."

Mr Nnauye said the party's dismal performance in last October's general elections stemmed from dissatisfaction among party members.

"It is obvious the party lost many constituencies whose majority voters were CCM members... they voted against the party to express their dissatisfaction of the way the corrupt people were worshipped."

Asked to comment on a story published by a local paper that implicated President Jakaya Kikwete to corruption allegations, Mr Nnauye shrugged off the paper's content saying :
"You all know the owner of the tabloid and the reason behind that story."

He said the main suspects of corruption will attempt to clear their names but warned:

"Let all corrupt elements be informed that this time we are serious... all escape routes are closed."

Mr Nnauye urged Tanzanians to shun media opposed to the crusade against corruption in the country, adding:
"Corruption knows no ideology... we are all affected in one way or the other."

Meanwhile, the new CCM secretariat will, under its Vice-Chairman, mainland, Pius Msekwa, start a four-day tour to the central and eastern zones to introduce itself to party members and supporters.

"We have received many requests from party members and supporters who would like to meet with us," said the party spokesperson, adding that the secretariat will this afternoon be at Nyerere Square in Dodoma.

The secretariat will tomorrow receive congratulatory demonstrations in Morogoro before moving to Chalinze and Dar es Salaam on Saturday.

It will end the first phase tour of the country on Sunday by holding a public rally in Zanzibar. "We will then retreat for plans for the next round of the tour... the intention is to go countrywide," he said.
 
NGOs condemn new constitution debate 'hijackers'





By MASEMBE TAMBWE, 13th April 2011 @ 15:04, Total Comments: 0, Hits: 60

NGOs calling themselves Constitution Forum have condemned politicians trying to hijack the review process, demanding that it should be pro-people.

"The only way this nation can have a good constitution is when people are free to voice their views. During public hearing in Dodoma, Dar es Salaam and Zanzibar people were bulldozed because of the interests of certain parties," said Mr Israel Illunde, the Forum's Deputy Chairman.

Mr lIlunde told a press conference in Dar es Salaam on Wednesday that they were appalled by the organisers of the meetings who chose small venues that could not accommodate people interested in the debate.

He wondered why the Bill was written in English, yet barely 15 per cent of the population speaks the language.

"We have read the Bill, we proposed that Kiswahili, a language spoken by over 80 per cent of the population be used," he said.

Other recommendations proposed change in the glossary that the President and Constitution Assembly are the only organs of the formulation of the new constitution, recommending instead the constitution commission, the National Assembly and public opinions.

The Constitution Forum also called for the removal of Certificate of Urgency in the process, saying there was no cause for urgency when formulating a new constitution. The forum also highlighted gender equality and proposed 50/50 representation in Parliament.

The head of Gender and Children Unit at the Legal and Human Rights Centre, Ms Anna Henga, said it was important the process started from the National Assembly but should be owned by the people.

Ms Henga said it would be wrong to have a replica of the existing constitution, insisting the public had to be involved. A member of the forum said it was high time Tanzanians nurtured a culture of civility when welcomed to give their views and avoid chaos and outbursts.

Meanwhile, the Centre for Good Government and Development in Tanzania (CEGODETA) also added their voice in condemning the way the discussions of the constitution was carried out saying it was despicable to see certain political parties bringing in hooligans to disrupt the meetings.

The CEGODETA Executive Director, Mr Thomas Ngawaiya, said in a statement:

"Let's remember that the country changed to multiparty democracy even when 80 per cent of the population was not in favour of the change. The few percentage only won for the sake of democracy and good governance," he said.
 
Shivji awataka vijana kudai mabadiliko


Na Tumaini Makene

MMOJA wa mabingwa wa sheria, ambaye pia ni Profesa wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Chuo Kikuu Dar es Salaam, Issa Sivji, amesema wananchi, hasa vijana, ndiyo
wanatakiwa kuwa cheche ya kudai mabadiliko na kuikomboa nchi, hasa katika zama hizi ambapo viongozi wanatumia madaraka yao kujitajirisha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa mapumziko ya Kongamano la Wiki ya Mwalimu Nyerere lililoanza juzi katika Ukumbi wa Nkrumah, Prof. Shivji alisema kuwa baada ya 'kuuawa' kwa Azimio la Arusha, viongozi nchini sasa wanatumia nafasi zao kujitajirisha, huku wananchi ambao walipigania uhuru wa nchi, wakiachwa kando.

Prof. Shivji aliyasema hayo alipozungumzia uamuzi wa Kigoda cha Mwalimu kuchapisha Kitabu cha Azimio la Arusha na kuendelea kukigawa bure kwa wananchi licha ya azimio hilo kuuawa miaka ya tisini, baada ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukutana Visiwani Zanzibar.

Alisema kuwa wakati wa kuadhimisha miaka 30 ya CCM, chama ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru, wananchi walisikika wakikumbuka azimio hilo wakisema kuwa liliwajali watu wanyonge, kwa kuwa lilizungumzia utu wa binadamu, miiko ya uongozi na maendeleo ya watu kwa ujumla, hivyo linastahili kurudishwa.

"Kimsingi sisi tunachapisha tu hili azimio na kulisambaza kwa watu, lakini ni wananchi wenyewe, tena ninyi (waandishi wa habari) ndiyo mliwauliza na wakasema kuwa Azimio la Arusha liliwajali wanyonge, lilizungumzia misingi ya utu wa binadamu na maendeleo, lakini sasa viongozi wameliacha na wananchi wamewekwa pembeni.

"Mimi kwa kweli wakati mwingine nasita hata kuwaita hawa ni viongozi...maana kiongozi ni yule anayeona majukumu ya kuwatumikia watu. Hawa wanatumia madaraka ya kisiasa, wanatumia vyeo vyao kujitajirisha, wanapenda madaraka...kiongozi wa kweli ni yule asiyependa kuongoza, asiyekimbilia madaraka, maana anauona uongozi ni majukumu. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hili, kiongozi ni yule asiyeona utamu katika madaraka, anaona majukumu, kiongozi ni yule anayekataa madaraka.

"Wanatumia madaraka kujitajirisha na kuwasahau wananchi. Sasa ni wakati mwafaka kwa wananchi, hasa vijana kuichambua jamii yao, kutafakari, historia ya nchi yao, wapi tulikotoka, tunakwenda wapi, vijana ndiyo wanapaswa kuwa cheche ya kuikomboa nchi yao wenyewe," alisema Prof. Shivji.
 
Comments




0 #1 kushake 2011-04-14 04:15 Nimependa sana maoni ya hawa wazee wetu Bomani, Salim na Butiku. kweli JK na Serikali yako tunakuomba sana watz wenzako rudisha huu mswada jikoni, Waache watu waunde constituency assembly ya katiba. Halafu kama alivyosema mwanadiplomasia Salim akina Membe waache kulaumu nchi za ngambo kusaidia chadema kuleta vurugu. watakutoeni madarakani kama Ghabgo!
Quote
 
CCM waenda mikoani kuukana ufisadi


*Wapeleka ujumbe wa NEC mkoa kwa mkoa
*Nape asema watapambana hadi washinde


Na Edmund Mihale, Dodoma

CHAMA Cha Mpinduzi (CCM) kimeanza ziara mikoani kupeleka ujumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM kwa wanachama kuwa kimedhamiria kupambana na ufisadi ndani na nje ya chama hadi kishinde.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye aliyasema hayo Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma jana, wakati akitangaza ratiba ya mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama na Sekretarieti ya chama hicho mkoani hapa.

Alisema chama hicho kimeandaa ziara kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa Halmashauri Kuu kwa wanachama wake kuanzia leo ambapo watafanya makutano katika Uwanja wa Nyerere Square na kesho Mkoani Morogoro.

Alisema kuwa mapokezi hayo yataendelea katika Mkoa wa Pwani Wilaya ya Kibaha ambapo yatapokelewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Alisema kuwa siku hiyo hiyo yataendelea katika Mkoa Dar es Salaam na Aprili 17 mwaka huu yatakuwa Zanzibar.

"Tutapambana na ufisadi hadi tushinde," alisema Bw. Nnauye.

Alisema kuwa CCM haitavumilia kuona inachafuliwa na watu wachache na kuwataka wanachama waliohama kwa hasira kutokana na kashfa ya ufisadi kurudi kundini.

Alisema uamuzi uliofikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa utafanyiwa kazi.Alisema uamuzi wa kuwachukulia hatua wanaojihusisha na ufisadi uko pale pale, hivyo wasidhani kuwa chama kimeishia hapo.

"Ndugu zangu Halmashauri Kuu iliamua kuwa tutapambana na ufisadi hadi tushinde, hivyo kama alivyozungumza mwenyekiti, wanaotuhumiwa wajiandae, tumefunga milango na madirisha yote, ili kuhakikisha tunashinda," alisema Bw. Nnauye.



1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... hata mkipita nchi nzima hamna lolote hamuwezi kushinda tena!!!!!!!!!!!!
April 13, 2011 10:34 PM
 
Mabadiliko CCM yaibua mjadala


*Wengine wadai yalichelewa, uchafu umeganda
*Baadhi wasema ni ndio mwarobani wa ufisadi
*Yusuf Makamba afurahia kuondoka na wengi


Na John Daniel na Chales Masyeba

SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutangaza rasmi mabadiliko makubwa
katika safu yake ya uongozi, kwa kujiuzulu sekretarieti na Kamati Kuu yake, wananchi wametoa maoni tofauti huku wengi wakitaka mabadiliko hayo yaendelee hadi serikalini.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti jana, wananchi hao walisema licha ya mabadiliko hayo kulenga kuleta mabadiliko ndani ya CCM lakini hatua hiyo imechelewa kuchukuliwa, hadi kukifanya chama hicho kukosa mvuta kwa wananchi.

Miongoni mwa walitoa maoni ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuph Makamba ambaye amewataka Watanzania na wanachama wa CCM wasifadhaike kwa kujiuzulu kwao kwani 'wanarudi kwa baba ambaye amewaletea mtume mwingine'.

Mbali na hilo, Bw. Makamba alionesha furaha yake kwa kutowajibika peke yape, bali ukawa ni mkumbo wa wengi.

"Nashukuru tumetoka wote, kama tulivyoingia pamoja na tunatoka pamoja tukiwa wamoja. Haiwezekani mmoja anyoshewe kidole. Hata baadhi ya wajumbe wa mkutano huu walisema atoke Makamba, mimi nikasema tutoke wote".

Bw. Makamba aliyasema hayo alipopewa fulsa ya kuaga kwa niaba ya wajumbe wenzake wa sekretarieti iliyojiuzulu majuzi, huku akishangiliwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa katika ukumbi wa NEC maarufu mjini Dodoma.

Kutokana hatua hiyo, Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho imewateau Bw. Wilson Mukama amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Makamba, akisaidiwa na Naibu Makatibu Wakuu (Bara na Visiwani), Bw. John Chiligati na Bw. Vuai Ali Vuai. Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi ni Bw. Nape Nnauye, huku, Bw. Mwigulu Mchemba akichaguliwa kuongoza Idara ya Fedha na Uchumi. Mkuu wa Oganaizesheni ni Bi. Asha Abdallah Juma na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Bw. Januari Makamba.

Kwa kutumia misemo ya biblia, Bw. Makamba alisema wanarudi kwa baba yao kutayarisha makao mapya na hata wenzao waliokuja na kukalia viti walivyoviacha watawakuta huko.

"Baba ameleta mfariji mwingine ambaye ni Wilson Mukama na wajumbe wengine. Wanachama tuendelee kuvumiliana na kujipanga ili kupata ushindi mkubwa mwaka 2015.

"Tulipoteuliwa tuliaminiwa kufanya kazi za chama na tukafanya kazi hizo kikamilifu na chama kikapata ushindi. Ndiyo, tulishinda hata kama ni kwa namna gani, lakini tulishinda, alisema.

Alisema wao wamekubali kumwaga damu kuokoa chama, kwani hawana tofauti sana na waliobaki na kwamba amefurahi kuona wengine nao wakichukua nafasi zao na kuwaasa kwamba wakitaka kutumia fagio la zamani wao wako tayari wakati wote, lakini wasipolihitaji wakiharibu watawasema.

Akizungumzia hulka ya yake ya kauli za kuudhi, alisema kwa mifano na kusisitiza kuwa kama unatukanwa na mtu mdogo aliyetumwa na mtu mzima ili kuweka mambo sawa, na yeye anamtukana kwa lengo la kusawazisha ili iwe sare.

Mkazi mwingine wa Dar es Salaam alisema, "Chama ni watu na watu ndio wanakuwa na mapungufu, kama mapungufu yao yameonekana ni vizuri waondoke kabisa, alisema akifurahia uamuzi huo wa CCM.

Aliongeza: "Suala la ufisadi upo na siyo siri, fisadi si lazima yeye achukue hela, lakini anaweza kumsaidia mtu mwingine kupata hizo hela, huo pia ni ufiasadi, kama wamepewa muda wa kuondoka wenyewe wafanye haraka wasije wakaahibishwa," alisema Bw, Ashrif Khan, aliyejitaja kama kada wa CCM.

Alisema kumekuwepo na malalamiko mbalimbali ndani ya chama hicho na kwamba hatua ya kuwaondoa watendaji hao na kupanga upya safu ni moja kati ya taratibu za CCM.

"Hatua iliyochukuliwa ni sawa kabisa na kuheshimu maoni ya wananchi, kama chama kikiona kinakwenda vibaya ni lazima irudi kwenye kati na kanuni zake," alisema.

Alisema hatu hiyo inatoa nafasi kwa walioteuliwa kuwa makini na kutothubutu kurudia makosa huku akisisitiza umuhimu wa wana-CCM kurejea itikadi za chama hicho.

Kwa upande wake Bw. Raymond Talawa, mkazi wa Kinyerezi Dar es Salaam licha ya kupongeza mabadiliko hayo alisema yamechelewa kufanywa kwa kuwa mapungufu ya kiutenaji ndani ya CCM yalianza mapema mwaka 20067/2008

"Kama hao akina Makamba wameondolewa na mafisadi wengine wamepewa muda kujiondoa wenyewe, basi hata wale wafanyakazi wazembe serikalini nao waondolewe haraka," alisma.

Alisema kumekuwa na wizi wa fedha za umma zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali lakini wahusika wanahamishwa badala ya kuondolewa kama ilivyofanywa na CCM.

Naye Bi. Rehema Abdala, wa Kimara alisema amefarijika kwa mabadiliko hayo japo hatua hiyo imechelewa kufikiwa na kusababisha madhara makubwa kwa CCM.

"Itabidi CCM ifanye kazi kubwa kurudisha imani iliyopotea, lakini wamefanya vizuri," alisema Bi. Abdallah bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Wananchi wengi walionyesha wazi kufurahishwa na hatu ya mabadiliko hayo huku wakisisitiza umuhimu wa Rais Jakaya Kikwete, kuelekeza nguvu kama hizo kwa baadhi ya watendaji wa serikali wazembe na wala rushwa badala ya kuishia kwenye chama.

"Ujenzi wa shule, barabara na huduma za wananchi zinaishia njiani kutokana na watendaji wa serikali wala rushwa na wazembe, rais angefanya kama alivyofanya kwa CCM kuwaondoa,"alisema mmoja wa walimu wa Chuo cha Uongozi wa Fedha IFM na kuomba jina lake kutotajwa.
 
15 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Makamba acha maneno ya kitoto, mlishinda au mliiba kura.??????
April 12, 2011 11:48 PM
blank.gif

Anonymous said... Nyang'au we labda baba yako aliiba kura. mmshindwa kwa wingi mkubwa wa kura lakini baba yenu kwa aibu akaliweka hilo ili aweze kuonekana hajashindwa. mtu ana wabunge 250 na ushee na wewe una 40 unasema umeibiwa,shukuru vipi maalum vimewaokoa vinginevyo saa hizi tungesikia mengine,subirini 2015 uone mambo yatavyokuwa
April 13, 2011 12:38 AM
blank.gif

jonas mtatina said... Nimefurahishwa na kitendo cha kuondoka kwa Mh.Makamba kwa sababu alikuwa amejisahau sana kupita kiasi.Istoshe ndie aliesabisha CCM kushindwa kwenye uchaguzi baadhi maeneo katika majimbo yalioko Bara na Visiwani.
Kuanzia hivi sasa Mh.afunge mdomo wake wala asijihusishe na siasa.
April 13, 2011 12:51 AM
blank.gif

Anonymous said... Tujadili hoja na siyo matusi jamani. Maamuzi yaliyochukuliwa na Mwenyekiti pamoja na NEC ni mazuri kwa uhai chama hususani kama hao waliopewa siku 90 kufanya uamuzi watafanya hivyo. Vinginevyo wasije wakaleta mfarakano kwa ukwasi wao.
April 13, 2011 1:00 AM
blank.gif

Anonymous said... Miradi mingi iliyokuja kwa kishindo na kasi mpya wakati awamu hii inaanza kipindi chake cha kwanza imegubikwa na sura ya kifisadi na mingi imeonesha kutoleta tija. Pamoja na kujiuzuru kwa viongozi wa kifisadi huko awali, tunaomba watumishi waliopandikizwa wakati huo kuwezesha ufisadi katika ngazi ya kitaifa hadi huko wilayani waondolewe haraka.

Tunampongeza mwenyekiti, lakini, tunamwomba anapovaa kofia ya pili ajue kuwa huko pia kuna hali mbaya zaidi. mwenyewe si anaona miradi ya kifisadi isivyokamilika na jinsi wananchi wanavyoteseka?? Au mpaka watu wazima waandamane kwa machoziii????
April 13, 2011 1:16 AM
blank.gif

Anonymous said... Sijaona mabadiliko yoyote hapo, bali ni danganya toto, ccm haijashindwa kwa sababu ya makamba bali ni kutokana na jina lake kwani watu wamelichoka jina pamoja na watu wake, wapi omary ramadhani mapuri, yule jamaa ndio alikuwa hamnazo kabisa lakini sasa analiwakilisha taifa huko mashariki ya mbali, so msishangae kusikia makamba balozi ulaya au amerika, kikwete awezi kuwatosa masela wake Membe, mkuchika rostam na wengineo kiivyo, kwani wao ndio wamemuweka hapo, hata hizo siku tisini walizo toa wabongo mtakuwa mmesahau, ww tangu lini m2 umpe nafasi ajitoe mwenyewe eti yeye fisadi which means baada ya hapo ni mahakamani kwani atakuwa kakili yeye mwenyewe kuwa fisadi, believe me no one atakaefanya hivyo and they know that, bt they try to look our mind, since watanzania wengi ni wasahaulifu siku tisini nyingi mmnoooo
April 13, 2011 1:25 AM
blank.gif

Anonymous said... Mnachofurahia hapa cha mabadiliko ni nini? Labda nambieni, Chiligati aliyetajwa hapa hakuwepo kwenye timu ya Makamba au amefanyiwa upasuaji wa ubongo na fikra zake? January anaesemwa hapa ni huyu huyu tunaemfahamu mwana wa Makamba au mwingine? kilichofanyika hapa wadanganyika ni suala la muda tu mtaanza kulalama sasa hivi. HAPA NI ZAIDI YA KIINIMACHO. Huu ni msiba wa taifa tulionao. Eti, iigwe tabia ya nyoka kujivua gamba?(labda kwa hili nampongeza mwenyekiti kwa kueleza ukweli nyoka ni nyoka hata akivua gamba hawezi kuwa mjusi). Kwani akivua gamba uhalisia wake nao atauvua, hatakuwa na sumu? MAFISADI NDANI CCM hawawezi kwisha hata siku moja. Ukweli ni kwamba atakaeuweza ufisadi wa ccm ni yule atakaeuvunja mfumo mzima wa utawala na uongozi wa ccm ambaye kwa sasa simuoni ndani ya chama hicho. MUNGU INUSURU NCHI YANGU PENDWA TANZANIA.
April 13, 2011 2:12 AM
blank.gif

Anonymous said... Huu ni usanii, hakuna kujivua gamba wala ngozi. Mafisadi wanaheshimika sana nchi hii, kwenye EPA mh. alielewana nao warudishe fedha taratibu, kwenye CHAMA wanabembelezwa wajiuzulu. Halafu mbona gamba hili halijavuliwa kichwani (MWENYEKITI NAE ANGEJIUZULU).
April 13, 2011 2:16 AM
blank.gif

Anonymous said... Mimi nadhani CCM wamebadili shati au suti toka ile iliyochafuka na kuvaa safi. Hawajajivua gamba bali wamebadili gamba. Jihadharini na chama cha ukoo. Ina maana hao akina Nape,January, na Nchimbi ndio vijana peke wa CCM au ni kutokana na majina ya baba zao. Kwa Nape, na January sioni jipya kwanza si makada wazoefu na sidhani kama watahimili mikikimikiki ya makada wazoefu ambao ndio chanzo cha vurugu ndani ya CCM. Kumbuka Nnauye bado anakumbukwa kwa utovu wa nidhamu akiwa UVCCM. Nawatakia kila la heri lakini mtu wa maana ninayemuona hapa ni Mukama pekee ingawa sina uhakika na ukada wake maana amefanya kazi serikalini kwa muda mrefu.
April 13, 2011 3:15 AM
blank.gif

Anonymous said... Siasa za CCM ni za ubabe, sikio la lao halisikii dawa kwa sababu ni wapenda madaraka mno. hali ya CCM imeharibu hata hali ya utawala sehemu mbali mbali zimekuwa ni mzigo kwa viongozi.

Tatizo la hawa wajamaa wanajipa uhuru kupita kiasi na kujisahau kutumia sheria sijui ni kwa sababu ni chama cha mjomba shangazi watoto wa mafisadi hakuna wa kumkemea mwingine. Hapa hakuna kilichobadilika bado ni sumu ile ile tu. Hawajaweza kuwashawishi watanzania kubadilisha mawazo yao.
April 13, 2011 3:49 AM
blank.gif

Anonymous said... Nahisi kama ni kituko hicho, Yaani mtoto atafanya mambo mazuri ya kuonesha baba yake alikuwa wrong? bado sijawasoma C.C.M, Makamba mtoto atakuwa pale kama boya tu bila kufanya jambo lolote la maana kwani akifanya mazuri atakuwa anamdhalilisha baba yake kwani tutauliza mbona mzazi wake hakufanya hivyo? na labda afanye mambo ya hovyo ambayo kwa siasa za sasa hawezi kuzifanya wakati anapenda kuendelea na cheo cha Mh. Mbunge wakati waTz wakisikia umeharibu tu hawana tena mpango na wewe, mimi naona waendelee kubadili staili ya kutembea ila sio urefu wa hatua zao wala uwezo wa kukimbia badala ya kutembea kama walivyozoea. Nawapa Big Up sana ccm kwa staili yenu yakututeka sisi wananchi naona mnadhani bado tumelala ila mwisho wenu upo kama wa Laurent Bagbo. Kiulaini kama kuvua gamba
April 13, 2011 5:38 AM
blank.gif

Anonymous said... Hiyo safu mpya ni danganya tupu, maana ilishapangwa kiaina kabla ya kuvunjwa.walishajipanga na mapemwa,na mafisadi wakashauriwa watulie wakiachwa ili kupunguza jazba lakin wako pamoja,hivi rostam au lowasa waachane na jakaya,kwa akl ya haraka itawezekana?hiyo ni namna ya kutuliza mukari!wao ndo wamemwezesha urais kama hujui!hawezi kuwatosa kwa aina ya kijinga.
Hivi anaachwa mtu makin kama sita,kisa hapendi mafisad.huyo January kapachikwa ili babake awe anamtuma kwenye kikao akaseme nini, na awe anaenda kumpa babake taarifa kikao kimeendaje,jakaya ameona asimtose Makamba kabisa,hivyo wanaridhishana chama cha ukoo.Bado chama tete,hakuna cha gamba wala nguo chakavu,inataka moyo kubadilika.hawawezi walishazoea,na watakufa jumla,maana mpasuko ktk chama ni mkubwa,na makundi yana nguvu!
April 13, 2011 6:12 AM
blank.gif

Anonymous said... Hivi JK atakuwa na ujasiri lini? Kama angekuwa jasiri wa kuleta mabadiliko bila shaka Januari Makamba asingekuwa katika safu ya uongozi. Ni yaleyale tu - URAFIKI. Uozo ni ule ule tu wa ufisadi na kulindana. JK umepata nafasi ya kuleta mabadiliko ya kweli katika CCM na nchi lakini kwa UDHAIFU umeshindwa. Hakuna la kushabikia hapo wala kupongeza.
April 13, 2011 7:07 AM
blank.gif

Anonymous said... kama ulizoea kulala na njaa basi hata aje nani hiyo njaa haitakutoka hayo mambo ya kushindwa na kushinda mnapoteza muda wenu bure umasikini ulionao usitegemee ccm au chadema watauondoa nawasikitikia sana watu mnaopoteza muda wenu kwenda kuwasikiliza wanasiasa wanaotaka kujiridhisha wenyewe na familia zao eti aje akusaidie ww tusijidanganye kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe hayo maneno nakumbuka aliwahi kuyasema mzee msuya alipokuwa waziri wa fedha miaka hiyo kwa watu ambao hamkuwepo na ameyarudia tena mzee mkulo hiyo ndiyo hali halisi hakuna mtu atakae kuokota ukianguka ndugu yangu mtanzania mwenzangu sifa na elimu mungu aliotujalia watanzania na elimu tuliyopewa na mungu ni kuongea saaaaaana na uongo ulio tawala maishani mwetu umasikini hautaondoka ng;ooooooooooo kwa mtaji huo watu wanachokitumia ni kauli ya kula na kipofu usimshike mkono mwaka wa komomonyoka unakuja na haupo mbali vita wala vurugu haitatokea mungu ni mwema tunaliomba hilo wenye nchi wapo sio nyie mnaopiga kelele
April 13, 2011 11:40 AM
blank.gif

Anonymous said... Huo wimbo wa CCM yaani ubeti wa kwanza Ufisadi, ubeti wa pili Tatizo ni MFUMO ubeti kuropoka na wa nne ni hue sasa wa Mukama nitawaondoa Mafisadi. Tutaona wamuulize mwigizaji mwanasheria Shitambala yaliyompata kwao Mbeya uyole. Watu wakipata nyadhifa hupenda kutamba hooooo nitafanya hike, nitafanya kile, utadhani mkolon aliyekuwa anasema nimevumbua mlima Kilimanjaro.
April 13, 2011 7:05 PM
 
Zanzibar wataka Serikali ndogo

Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 140; Jumla ya maoni: 0






CHAMA cha Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) kimeonesha wasiwasi juu ya ukubwa wa muundo wa Serikali na kutopangiliwa kwa idara zake na kumwomba Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein, kuupitia upya muundo huo.

Pia kimemwomba aangalie uwezekano wa kupunguza pengo kubwa la mshahara kati ya watendaji waandamizi na watumishi wa umma wanaoanza kazi, ili kuongeza ufanisi.

"Tunamwomba Rais aangalie ukubwa wa serikali yake, mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi kwa kuwa ni mzigo kwa walipa kodi. Tunahitaji kuwa na Serikali ndogo na kuokoa fedha kwa ajili ya mishahara bora kwa wote," alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Khamis Mwinyi Mohamed.

Khamis alitoa ombi hilo kwa Rais Shein wakati akizungumza Jumatano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, inayofanyika kila mwaka Mei Mosi huku akidai kuwa Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa idara zake zimekaa vibaya.

"Mahakama ya Kazi iko chini ya Mahakama Kuu, idara zinazohusika na ajira kwa watoto, usalama kazini na malipo kwa wafanyakazi zipo chini ya Wizara ya Ustawi wa Jamii, hii si sawa, idara hizi zinapaswa kuwa chini ya Wizara ya Kazi kwa ufanisi zaidi," alisema.

Alisema kutopangiliwa ipasavyo kwa idara zinazohusiana na ajira, pia kunawavunja moyo wafadhili kama vile Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika kusaidia maendeleo ya ajira kwa kuwa wanadhani Serikali haiko makini.

Aidha, chama hicho pia kilionesha wasiwasi wake juu ya kupanda kwa bei ya bidhaa kutokana na kukosekana kwa chombo maalumu cha kudhibiti bei ambacho kinatakiwa kuboresha pia maslahi ya wafanyakazi na kuziba pengo la mishahara.

"Haikubaliki kwa mfano, baadhi ya wakurugenzi wanalipwa mshahara wa mwezi unaofikia Sh milioni 1.5 wakati mfanyakazi wa kawaida mwenye shahada, analipwa Sh 150,000 kwa mwezi na mshahara wa kima cha chini wa Serikali ni Sh 100,000," alisema na kushauri kima cha chini kiwe Sh 350,000.
 
Zanzibar wataka Serikali ndogo

Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 140; Jumla ya maoni: 0


CHAMA cha Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) kimeonesha wasiwasi juu ya ukubwa wa muundo wa Serikali na kutopangiliwa kwa idara zake na kumwomba Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein, kuupitia upya muundo huo.

Pia kimemwomba aangalie uwezekano wa kupunguza pengo kubwa la mshahara kati ya watendaji waandamizi na watumishi wa umma wanaoanza kazi, ili kuongeza ufanisi.


“Tunamwomba Rais aangalie ukubwa wa serikali yake, mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi kwa kuwa ni mzigo kwa walipa kodi. Tunahitaji kuwa na Serikali ndogo na kuokoa fedha kwa ajili ya mishahara bora kwa wote,” alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Khamis Mwinyi Mohamed.


Khamis alitoa ombi hilo kwa Rais Shein wakati akizungumza Jumatano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, inayofanyika kila mwaka Mei Mosi huku akidai kuwa Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa idara zake zimekaa vibaya.


“Mahakama ya Kazi iko chini ya Mahakama Kuu, idara zinazohusika na ajira kwa watoto, usalama kazini na malipo kwa wafanyakazi zipo chini ya Wizara ya Ustawi wa Jamii, hii si sawa, idara hizi zinapaswa kuwa chini ya Wizara ya Kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema.


Alisema kutopangiliwa ipasavyo kwa idara zinazohusiana na ajira, pia kunawavunja moyo wafadhili kama vile Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika kusaidia maendeleo ya ajira kwa kuwa wanadhani Serikali haiko makini.


Aidha, chama hicho pia kilionesha wasiwasi wake juu ya kupanda kwa bei ya bidhaa kutokana na kukosekana kwa chombo maalumu cha kudhibiti bei ambacho kinatakiwa kuboresha pia maslahi ya wafanyakazi na kuziba pengo la mishahara.


“Haikubaliki kwa mfano, baadhi ya wakurugenzi wanalipwa mshahara wa mwezi unaofikia Sh milioni 1.5 wakati mfanyakazi wa kawaida mwenye shahada, analipwa Sh 150,000 kwa mwezi na mshahara wa kima cha chini wa Serikali ni Sh 100,000,” alisema na kushauri kima cha chini kiwe Sh 350,000.
 
Serikali yafyata mkia Bungeni
• Mbowe, Zitto, Mnyika wamtoa jasho Pinda

na Martin Malera, Dodoma


amka2.gif
HATIMAYE serikali imesalimu amri kwa kukubali kuuondoa Bungeni mswada wa sheria utakaosimamia mchakato wa kupatikana kwa Katiba, Tanzania Daima
limebaini.
Mbali ya muswada huo, serikali pia imelazimika kuuondoa muswada wa sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2010 (Public Procurement Act, 2010), kwa madai kuwa una kasoro nyingi zinazoweza kuliingiza taifa kuendelea kufanya manunuzi ya mitambo chakavu.
Taarifa za uchunguzi kutoka bungeni zimethibitisha kwamba Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria na Katiba imeshawasilisha mapendekezo yake kwa ofisi ya spika kuhusu muswada huo ambayo pamoja na mambo mengine yanataka uondolewe bungeni na kwamba serikali inalijua hilo.
Muswada wa mabadiliko ya Katiba Mpya ambao wiki iliyopita uliletwa Bungeni chini ya hati ya dharula umeondolewa kutokana na shinikizo kali la viongozi na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na harakati za wadau mbalimbali hususan asasi zisizo za kiserikali na wasomi ambao tangu uliposomwa mara ya kwanza waliukataa na kuitaka serikali iuchomoe bungeni ili kutoa fursa zaidi kwa wananchi kutoa maoni yao ya kuanzisha utaratibu unaokubalika wa kupata Katiba.
Baadhi ya asasi zisizo za kiserikali ambazo ziliitisha makongamano au kutoa moja kwa moja msimamo hivi karibuni wa kutaka muswada huo uchomolewe bungeni ni Chama cha Mringano wa Dini ya Kiislamu (Istqama), Tanzania Development Initiative (TADIP), Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDASA), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Jukwaa la Katiba na Jukwaa la Sera (Policy Forum).
CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, kesho Jumamosi imepanga kufanya maandamano nchi nzima kuelimisha ubaya wa muswada huo na kuwahamasisha wananchi kushinikiza uandikwaji wa Katiba mpya itakayotokana na ushiriki wao wa moja kwa moja kuanzia mwanzo wa mchakato hadi mwisho.
Miongoni mwa mapungufu makubwa yanayopingwa, ni muswada huo kulenga kurekebisha Katiba iliyopo wakati madai na matarajio ya wananchi ni kuona Katiba inaandikwa upya.
Madaraka makubwa aliyopewa Rais kuanzia kuunda tume hadi kupewa mwanya wa kuamua aina ya rasimu ya katiba ya kupitishwa, pia yamepingwa vikali na wadau ambao wamesisitiza vikali: "Rais ni mtoto wa Katiba na madaraka yake yanaishia ndani ya Katiba iliyopo hivyo hapaswi kupewa mamlaka ya kuamua Katiba, …wananchi wapewe mamlaka yote ya kuamua upya nchi yao ijiendeshe vipi kupitia wajumbe wa makundi mbalimbali."
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa mbali na tishio la CHADEMA kutaka kufanya maandamano nchi nzima, serikali pia imeamua kuuondoa muswada huo kuhofia vurugu zilizotokea katika vituo vya Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma.
Wakati mjini Dodoma wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walitawanywa kwa mabomu wakati wakitaka kuingia kwenye ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa kwa nguvu ili kutoa maoni yao, jijini Dar es Salaam mjadala huo ulivunjika wakati kule Zanzibar muswada huo ulichanwachanwa hadharani kwa madai kuwa Zanzibar hawakushirikishwa kuuandaa.
Kuhusu muswada wa sheria ya manunuzi ya umma, taarifa zinasema serikali imeamua kuondoa muswada huo baada ya kuibuka mjadala mzito kwenye Kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha kutaka baadhi ya vipengele viondolewe.
Moja ya vipengele vilivyobishaniwa ni kile kinachotoa tafsiri ya mzabuni mwenye bei ndogo ndiye atakayepewa kazi kipengele ambacho kitahalalisha serikali kuendelea kufanya manunuzi ya mitambo chakavu.
Kwa hali hiyo basi, shughuli za Bunge hili ambazo zilipaswa kufikia tamati Jumanne ijayo zinatarajiwa kumalizika kesho. Taarifa kamili ya hatua hiyo, inatarajiwa kutangazwa rasmi leo na Spika wa Bunge, Anna Makinda mjini hapa.
Hivi karibuni, Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, alitamka Bungeni kuwa utaratibu wa kukusanya mawazo ya wadau juu ya mapendekezo ya muswaada wa sheria itakayosimamia mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya, utachukua siku tatu.
Baadaye serikali iliongeza siku moja zaidi. Kwa hali hiyo ingefanya mjadala huo uchukue, siku nne, sawa na saa 96. Hii ina maana kuwa baada ya saa 96 za kukusanya maoni ya wadau muswada huo ungerudi tena bungeni na kujadiliwa na wabunge kwa siku mbili, yaani Jumatatu na Jumanne wiki ijayo.
Mbowe, Zitto Mnyika wamtoa jasho Pinda
Awali, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Naibu wake Zitto Kabwe na mbunge wa Ubungo, John Mnyika, jana walimbana kwa maswali Waziri Mkuu Mizengo Pinda kiasi cha kushindwa kuyatolea majibu ya papo hapo.
Mbowe alimbana Waziri Mkuu Pinda kutaka atoe tamko la kutaka mjadala wa muswada wa mabadiliko ya Katiba uliowasilishwa Bungeni uahirishwe ili kutoa fursa zaidi kwa wananchi, huku Zitto akimtaka atoe taarifa kwa nini Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) alinyimwa taarifa muhimu ambazo zingemwezesha kubaini orodha ya watumishi waliokwamua mabilioni ya fedha za serikali.
Hali hiyo ilijitokeza jana Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu ya papo hapo kwa Waziri Mkuu na kusababisha Spika wa Bunge, Anna Makinda kuingilia kati kumnusuru.
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Hai, ndiye alikuwa wa kwanza kumrushia swali Waziri Mkuu.
Katika swali hilo, Mbowe alihoji kwa kuwa Katiba ni roho ya taifa na kwa kuwa Serikali imewasilisha mswada Bungeni kwa hati ya dharura na kwa kuwa yaliyotokea katika kituo cha Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar yameibua hofu kwa wananchi, Serikali haioni umuhimu wa kuahirisha muswada huo ili kutoa fursa zaidi kwa wananchi kutoa maoni yao.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwa kweli Serikali imewasilisha muswada wa mchakato wa kuunda tume itakayoratibu maoni ya kupitia Katiba chini ya hati ya dharula kwa nia njema ili kuharakisha upatikanaji wa kile alichokiita "katiba mpya."
"Nimeambiwa baada ya kazi ya kukusanya maoni katika vituo vya Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma, Kamati ya Katiba na Sheria inaendelea kujadili kazi hiyo na matatizo yaliyojitokeza, maoni yao yataletwa kwa Spika naye atayaleta Serikalini na atayawasilisha Bungeni.
"Hadi sasa bado sijapata taarifa za Kamati hiyo, nikiyapata nitayaona lakini mwisho wa siku Spika ndiye mwenye uamuzi wa kuamua nini kifanyike kwa namna atakavyoshauriwa na Kamati ya Katiba na Sheria," alisema Waziri Pinda.
Pamoja na kutoa majibu hayo, Mbowe aliendelea kumbana Waziri Mkuu akimtaka atoe kauli Bungeni kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa mjadala wa kukusanya maoni katika vituo vya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar.
Alisema vurugu hizo zimeleta hofu kwa wananchi hivyo alimtaka atangaze kuahirisha mswada huo kwa lengo la kutoa muda zaidi kwa wananchi kutoa maoni yao.
Akijibu swali hili, Waziri Mkuu Pinda alisema wananchi hawapaswi kuwa na hofu kwa kazi ya kutoa maoni na kusisitiza kuwa uamuzi wa kuahirisha au kutoahirisha utategemea taarifa ya Kamati ya Sheria na Katiba kwa Spika wa Bunge.
"Mbowe anataka niseme hapa sawa tunaahirisha. Mimi nataka nimtoe hofu kwamba
tusubiri taarifa ya Kamati ya Katiba na Sheria. Kwanza sijui hofu ya wananchi inatoka wapi. Ndugu yangu Mbowe, haraka ya nini, wee poa tu," alisema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, alimwuliza Waziri Mkuu Pinda kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), ametoa taarifa kwamba Serikali imemnyima taarifa muhimu ili kubaini waliofaidika na sh trilioni 1.7 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kuhuhisha uchumi na sh bilioni 48 zilizoyeyuka serikalini katika mazingira ya kutatanisha.
Akijibu swali hilo, Pinda alilishangaza Bunge kwamba hana taarifa hiyo na kwamba hivi sasa amewaagiza wataalam wake kuipitia taarifa za CAG kujua kilichomo ndani. Hata hivyo alisisitiza kuwa Serikali haina sababu ya kunyima taarifa muhimu CAG ili kufanya kazi yake.
Baada ya jibu hilo, Zitto alisimama tena kutaka kuuliza swali la nyongeza kwa kusoma sehemu fupi ya taarifa ya CAG, lakini Spika Makinda aliingilia kati kupinga swali hilo kwa madai kuwa tayari Waziri Pinda alishasema hana taarifa hiyo.
"Waziri Mkuu amesema hajaiona hiyo taarifa ya CAG, wewe unataka kumsomea, sasa atajibu nini wakati amesema ameagiza wataalam wake waipitie," alisema Makinda na kumuamuru Zitto kukaa chini.
Naye Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimbana Waziri Mkuu Pinda kutaka ataje orodha ya mafisadi waliohusika na kashfa ya Meremeta.
Mnyika alisema kwa kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimejivua gamba na kuahidi kupambana na ufisadi, alimtaka Waziri Kuu kuendeleza dhamira iliyotangazwa na mwenyekiti wao Rais Jakaya Kikwete, kwa kutaja orodha ya mafisadi wa kashfa ya Meremeta.
Katika majibu yake, Pinda alimtaka Mnyika kuacha kutumia mgongo wa CCM kuuliza swali hilo kwani yaliyotokea ndani ya chama hicho ni ya chama na yale ya serikali nayo yatashughulikiwa kwa utaratibu wake.
Hata hivyo, baadaye Mnyika alitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kubainisha kuwa majibu hayo ya Pinda yanadhihirisha kuwa sumu ya ufisadi wa CCM itaendelea kufuja raslimali za taifa kama chama hicho hakitang'olewa kwa haraka.
"Majibu ya Waziri Mkuu yamedhihirisha kwamba CCM haiko tayari kuvua magamba ya ufisadi katika serikali ambao ndio wenye kuathiri zaidi wananchi ....na kwamba kauli ya Rais Kikwete ya CCM kujivua gamba kama nyoka ni ushahidi wa kwamba bado hata baada ya kujivua gamba katika chama chao sumu ya ufisadi itaendelea kuua rasilimali za taifa huku meno ya mafisadi yakiendelea kushikilia hatma ya mwelekeo wa serikali,'' alisema Mnyika katika taarifa yake hiyo na kuongeza:
"Pamoja na majibu ya Waziri Mkuu, kwa nafasi yangu ya Uwaziri Kivuli wa Nishati na Madini naitaka serikali itoe kauli ya kuruhusu ukaguzi maalumu kufanyika katika mahesabu ya kampuni ya Meremeta na kueleza hatma ya mgodi wa Buhemba ambao mali zake zinaendelea kuibwa mpaka hivi sasa kutokana na udhaifu katika utawala.''
Kwa upande wake, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, aliomba mwongozo wa Spika na aliposimama alisoma kanuni ya Bunge inayoruhusu swali la nyongeza kwa Waziri Mkuu. Lissu alihoji sababu za Spika kumzuia Zitto kuuliza swali la nyongeza kwa Pinda.
Akitoa mwongozo wake, Makinda alijibu kwa jazba kuwa anapoongoza kiti cha Spika, hafungi kitambaa machoni kwani anaona na kusikiliza.
"Mwongozo wangu ni kwamba, Zitto kauliza swali, Waziri Mkuu kasema hajapata taarifa. Hilo swali la nyongeza la nini sasa. Huo ndio mwongozo wangu," alisema Spika Makinda.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye Bunge lililopita aliuliza swali kwa Waziri Mkuu lililozua utata, naye aliomba mwongozo wa Spika na kuhoji utaratibu anaotumia Spika kupanga watu wa kuuliza msawali kwa Waziri Mkuu.
"Mheshimiwa Spika mimi nimeamka mapema, nimekuwa mtu wa nane kwenye orodha ya kuuliza maswali, Mnyika amekuwa wa 14, lakini yeye amepata nafasi, mimi
sikupata, naomba mwongozo wako," alisema Lema.
Spika ambaye alionekana kukerwa na miongozo ya wabunge wa CHADEMA, alisema: "Nilijua ungeuliza swali hili. Ninapokaa kupanga kuuliza maswali, nazingatia uwiano wa vyama, jinsia, kwa hiyo wewe hukupata nafasi leo."
Mbunge mwingine aliomba mwongozo, lakini Spika Makinda alikasirika na kuukataa huku akisema hataki kuongozwa bali yeye anapaswa kuliongoza Bunge.
 
Back
Top Bottom