Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Wasomi - CCM: Tuna mafisadi 100
• Wataka chama chao kiwatimue haraka

na Hellen Ngoromera na Irene Mark


amka2.gif
UMOJA wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi kutoka vyuo vikuu nchini, umesema hatua ya CCM kujivua gamba kwa kufanya mabadiliko ya kiutendaji haitoshi kwani ndani ya chama hicho na serikali yake kuna magamba (mafisadi) zaidi ya 100 yanayotakiwa kuondoshwa.
Kauli ya wasomi hao imekuja huku Mjumbe wa Mkutano Mkuu UVCCM wilaya ya Moshi Mjini, Paul Makonda, akibainisha kuwa uongozi wa kitaifa wa jumuiya hiyo nao unapaswa kung'olewa kwani nao unafanya ufisadi wa kutumiwa na mafisadi ambao unazidi kukiua chama hicho na jumuiya yake.
Makonda alisema kinachofanyika ni kuhakikisha mafisadi wote ndani ya chama wanaondoka kwa kuunda ‘UVCCM Maadili' na kukiondoa ‘UVCCM Maslahi' chini ya uongozi wa Benno Malisa na ushawishi wa Hussein Bashe.
Umoja huo pia umetangaza kufanya operesheni maalumu nchini kumsaidia Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, kuwaondoa mafisadi ndani ya chama hicho.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Katibu wa Umoja huo Leoni Mboya na Mwenyekiti wake Nestory Chilumba, walimpongeza Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete kwa ujasiri aliouonyesha wa kufanya mabadiliko hayo na kutaka mfumo mzima ndani ya chama hicho kubadilishwa.
"Sisi kama vijana wasomi tunaamini kwamba CCM kujivua gamba si tu kujiuzulu kwa sekretarieti wala kufukuza wanachama wanaokipotezea umaarufu bali kufanya mabadiliko ya mfumo mzima wa chama kuanzia mwenyekiti taifa hadi shina pamoja na katiba ya chama.
"CCM kuna magamba zaidi ya 100 hivyo kuna haja ya kutoa gamba moja hadi jingine, wembe uliotumika kwa sekretarieti utumike kwa watu wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya chama …tumechoshwa na kelele za wapinzani," alisema Chilumba.
Alisema wao kama wana CCM wapenda maendeleo wanamwakikishia mwenyekiti wao kuwa watakuwa bega kwa bega naye kwa kila hatua anazochukua ndani ya chama hicho ili kukiwezesha kuwa na wanachama wenye maadili, uadilifu na nidhamu.
Aliishauri sekretarieti kuu ya chama hicho kutekeleza ahadi yake ya kuwashughulikia wanachama mafisadi na kusema wana matumaini nayo katika kukiletea chama hicho mabadiliko makubwa.
Kuhusu kutaka uongozi wa umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM) kujiuzulu kutokana na kushindwa kazi, Chilumba alisema kwa kuwa kuna sekretarieti mpya wameona ni busara wakaonane nayo ili kuona njia za busara zinazofaa katika kuhakikisha UVCCM inajisafisha.
Wanachama hao hai wa CCM walisema kwa sauti moja kuwa hawaogopi nguvu yoyote ya mafisadi na kama wana pesa nyingi waanzishe chama chao.
Akizungumzia kuhusu operesheni kokoro ambayo wamepanga kuifanya hivi karibuni Katibu, Leoni Mboya, alisema itakuwa na lengo la kuwaondoa mafisadi wote.
"Tunataka umma uelewe kuwa kuna operesheni kokoro inakuja, hii itakuwa maalumu kwa ajili ya kumsaidia mwenyekiti wetu kuyaondoa mayai na ‘mapapa' ndani ya CCM ikiwa hawatafanya hivyo wenyewe," alisema Mboya.
Kwa upande wake Makonda alisema mfumo mbovu wa utawala na kusubiri vikao ndani ya chama hutoa mwanya kwa matajiri wachache wenye maslahi binafsi kukiharibu chama na jumuiya zake.
Katika hilo alipongeza uamuzi wa mwenyekiti wao Kikwete kubadili uongozi wa sekretarieti na kutoa changamoto kwa viongozi wapya chini ya Katibu Mkuu Wilson Mukama kuunda mfumo bora wa uongozi ili kukiimarisha chama na kurejesha imani ya wananchi kwa chama hicho.
"Inahitaji utashi na uamuzi mgumu kubadili uongozi katikati ya safari… haijawahi kutokea tangu kuanza kwa CCM, baada ya mabadiliko hayo naamini sasa changamoto kubwa ipo kwa hiyo sekretarieti mpya ihakikishe inabadili mfumo, itoke kwenye sera za kitamaduni tulizorithi ikipeleke chama kwenye sera za kisasa.
"…Sekretarieti iliyopita ilikuwa inasubiri vikao na taratibu bila kujali madhara yanayokikumba chama kwa kuchelewa kutoa maamuzi kwa wakati. Ilifika kipindi chama kinafanya mabadiliko kutokana na kauli ya wapinzani.
"Naishauri sekretarieti mpya kurejesha heshma na imani ya chama… tunategemea mabadiliko makubwa sasa," alisema Makonda huku akiongeza kwamba kinachotakiwa ni kubadili mfumo.
Alisema UVCCM maadili ipo kwenye mchakato wa kuunda umoja mpya utakaosaidia kukuza na kukiimarisha chama huku akibainisha kwamba wanaruhusiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.
 
Muswada wa Katiba hatihati kuondolewa Send to a friend Thursday, 14 April 2011 21:44

aamsitta.jpg
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika kikao cha sita cha mkutano wa tatu bungeni Dodoma

Midraji Ibrahim, Dodoma
MUSWADA wa Marejeo ya Katiba uliokuwa umewasilishwa katika hati ya dharura kwenye Mkutano wa Tatu wa Bunge unaoendelea mjini hapa kuna kila dalili kuwa huenda ukaondolewa.Habari zilizopatikana jana zimeeleza kwamba mbali ya muswada huo ambao sasa taarifa zinasema utawasilishwa Oktoba mwaka huu, hata ule wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ambao ulipangwa kupitishwa katika mkutano huu pia umeahirishwa mpaka Bunge lijalo.Lengo la kuondoa miswada hiyo linaelezwa kuwa ni kutoa nafasi zaidi ya kuiboresha, huku habari zikieleza kwamba Muswada wa Marejeo ya Katiba unahitaji kuandikwa upya kwa kujumuisha maoni yaliyotolewa na wadau mbalimbali ambao walionyesha hofu ya namna ulivyoandikwa.
Spika wa Bunge, Anne Makinda alipotakiwa kuzungumzia suala hilo alisema: " Sijui ‘source' (chanzo cha habari) yenu ni reliable (ya kuaminika) kiasi gani lakini mimi siwezi kuzungumzia hilo sasa. Utaratibu wangu wa kufanya kazi hauko hivyo, ila kama tutauondoa tutasema na kama hatutauondoa tutasema."

Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani naye alisema hakuwa na taarifa za kuondolewa kwa muswada huo huku akisisitiza kuwa upo mikononi mwa Bunge.
"Lengo letu ni kuunda Katiba itakayoshirikisha watu, Kamati ya Bunge imekusanya maoni kutoka kwa umma ambayo yatahusishwa kwenye muswada huo," alisema Kombani.
Taarifa za kuondolewa kwa muswada huo bungeni zimekuja wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema kuwa nia ya Serikali kuendelea au kuuondoa bungeni muswada huo itategemea ushauri itakaoupata kutoka kwa Spika wa Bunge, baada ya kupitia mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.

Akijibu maswali ya wabunge ya papo kwa hapo bungeni jana, Pinda alisema taarifa alizonazo ni kwamba kamati hiyo imeshakamilisha mchakato wa kukusanya maoni ya wadau na imewasilisha mapendekezo yake kwa Spika wa Bunge.
Alisema baada ya kamati hiyo kuwasilisha mapendekezo yake, Spika kwa kutumia wataalamu wake, atashauri iwapo muswada huo uendelee au usitishwe.Pinda alisema Serikali iliwasilisha muswada huo kwa hati ya dharura ikiwa na nia njema kwa sababu iliamini kwamba wananchi wana shauku kubwa ya kupata Katiba mpya haraka.

"Sasa baada ya kuwasilishwa bungeni, kilichopo ni utaratibu wa Bunge. Nimearifiwa kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, ilikwishakutana kuzungumzia yaliyojitokeza wakati wa public hearing (maoni ya wadau) walipokuwa wanakutana na Watanzania," alisema.
Pinda alisema kwa utaratibu, inapaswa mapendekezo hayo kwenda kwa Spika, ambaye akishayapata na kuchambua, akiona inafaa kushauriana na Serikali, atafanya hivyo.

"Niliposimama hapa bado sijapata taarifa yoyote ya wamefikia wapi kwenye hatua hiyo. Kwa hiyo tumejipanga tukiamini kama tulivyoleta jambo hili bungeni, kama hakutakuwa na maoni tofauti tutaendelea nalo," alisema Pinda na kuongeza:
"Lakini kama tukipata maoni hayo mengine kwa uzito stahiki, kama Serikali tutaridhia kwa kuwa nia ni njema. Nia ni kutaka tusonge mbele kwa namna ambayo Watanzania wote tutaridhia kwamba jambo hilo limekwenda vizuri."

Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali juu ya maoni ya wadau waliyoyatoa kwenye Kamati ya Bunge.
"Katiba ni roho ya Taifa na kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya mabadiliko ya Katiba au kuandikwa upya kutoka kwa wananchi, jambo ambalo Serikali imeridhia kupitia kwa Rais, kwa sababu Serikali imeleta muswada katika utaratibu wa haraka, muswada wa constitutional review," alisema Mbowe na kuongeza:
"Je, baada ya Serikali kuona 'reaction' ya wadau mbalimbali wakiwamo wanazuoni, vyama vya siasa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao wanaona mchakato huu ulikuwa unakwenda kwenye kasi ambayo badala ya kujenga inaweza ikatia nyufa katika nyumba yetu. Ni kwa nini Serikali kupitia Waziri Mkuu isitoe tamko rasmi pengine la kukubaliana na utashi wa wadau?"
Mbowe pia alimtaka Waziri Mkuu kutumia fursa hiyo kulieleza taifa kukubaliana na mawazo ya wadau na kuondoa muswada huo kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo limezua hofu kubwa kwa taifa kutokana na uzito wake.

Akijibu swali hilo, Pinda alisema: "Na mimi ni Mtanzania kama wewe na kwa dhamira nzuri tuliyonayo nitaonekana mtu wa ajabu sana iwapo ushauri nitakaopata kutoka kwa Spika niupuuze, niseme naendelea. Siwezi kufanya hivyo."
Katika kipindi hicho cha maswali, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alitaka kujua iwapo Waziri Mkuu yuko tayari kuzungumzia kashfa ya Meremeta na Tangold, baada ya Rais Jakaya Kikwete kutamka kuwa CCM imeamua kujivua gamba la ufisadi.
"Baada ya kauli hii ya Rais na dhamira hii ya kujivua gamba masuala ya ufisadi, uko tayari kutaja wahusika wa Makampuni ya Meremeta na Serikali kuchukua hatua zinazostahili?" aliuliza.

Hata hivyo, Pinda alikataa kuwataja wahusika hao kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo limejengwa kwenye misingi tofauti.
"...Hapo umepandia rafiki yangu, yaliyofanyika ndani ya Chama Cha Mapinduzi, kinashughulika na wanachama wake...chama kizuri lazima muwe na utaratibu wa kujikosoa, kama ulisikia vizuri mwenyekiti wetu alisema tutaendeleza hizo juhudi kwa lengo la kujenga chama kilicho imara kinachokubalika, ili tukifika 2015 tuweze kuwashinda kwa mara nyingine," alisema Pinda na kuongeza:
"Suala la Meremeta ni jambo tofauti kabisa, pengine sipo katika nafasi ya kuweza kulizungumzia kama unavyotaka nizungumzie kwa sababu ni jambo jingine ambalo lina misingi tofauti sana."

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Regia Mtema aliyetaka kujua kutotekelezwa kwa tamko la Serikali kuhusu bei ya sukari, Pinda alisema wameelekeza halmashauri kusimamia agizo la Serikali kuwadhibiti wauzaji wadogo wadogo, ambao wameonekana kuwa chanzo cha kupanda kwa bei hiyo... "Tumelazimika kuomba halmashauri zetu zijaribu kuwabana hawa wauzaji wadogo," alisema
 
Comments

123



+2 #43 Samson 2011-04-15 23:44 Yani kuna viongozi ambao wanaongea u[NENO BAYA] amabye kwa mtu amabye umeenda shule inasikitisha.Mimi ni mwananfunzi nchi moja huku ulaya kila siku nikifikiria Tanzania huwanalia machozi. Sisi tutakufa tu tukiwa maskini. Kuna nchi amabazo hazikuwa na raslimali kama tulizo nazo sisi watanzania. But ilifika sehemu wakabadili jinsi ya kufikiria, serikali na ikabadili maisha yao hadi leo. Sisi bado tunachagua viongozi amabao wanaiba pesa za walipa kodi kuingia kwenye mikataba ambayo hainufaishi nchi na kunufaissha familia na wao wenyewe. Kwa jinsi hii ndugu watanzania tutatoka?
Quote









+1 #42 blandes 2011-04-15 23:20 Mh Pinda wewe ni mmojawapo uliyekuwa unatupatia imani ya utendaji.lakini umegeuka kuvaa ngozi ya kondoo,lakini siku za ccm zinaesabika tu.NAJIULIZA ILI SWALI KILA SIKU KWANINI TANZANIA MASKINI wakiti rasilimali tunazo za kutosha?PONGEZI GAZETI PENDWA MWANANCHI
Quote









+2 #41 kero 2011-04-15 22:49 Pinda kapinda si kidogo,huyo ni kibaraka na msaliti aliyejaa unafiki wa kuliangamiza Taifa letu kwa kuhakikisha analinda kwa hali na mali au kudhibiti kwa kadiri anavyoweza au atakavyowezeshw a na Wahaini wanao operate nyuma ya pazia kuhakikisha haki ya mnyonge haipatikani kamwe.Amekuwa mwaminifu hata kufa kulinda uoza wote unaoendelea Serikalini akisaidiwa na mwanamke aliyejaliwa sura mbaya kuliko maelezo(Anna Makinda) kulinda maslahi ya Mafisadi.Yote haya yana mwisho mchungu sana kwao.It's just a matter of time & the time will tell.
Quote









0 #40 fisadi 2011-04-15 21:43 Quoting makwa:
hivi ni kweli wabunge wa CCM hawaoni kasoro za kitaratibu za Bunge? au wamelogwa. Kila kitu mpaka tu wapinzani ndio waseme. Hata sisi huku nnje ya mjengo tunaona
Mheshimiwa Pinda naona mambo mazito, achana na lichama letu hili (CCM) LINAKUHARIBIA CV. We tunajua ni mwadirifu sana​
Quoting Emmanuel:
Kwa kadri ninavyoelewa kilichowasilish wa si Mswada wa Katiba bali Mswada wa Sheria itakayoongoza upatikanaji wa katiba mpya...Come on PEOPLE!!!​
Tuchukue hatua za haraka!!! wabunge hasa wa upinzani wamecharuka na watatupeperushi a ndege wetu,lazima tuwapatie mikopo mikubwa,mishaha ra mikubwa,posho kubwa etc LASIVYO WATANDELEA KUPIGA KELELE
Quote









+3 #39 Jackson Kembe 2011-04-15 19:54 Hongera sana gazeti la mwananchi,Kila mnaloandika ni kweli tupu hakuna hata chembe ya shaka.Mfano mlisema CCM inataka kijivua gamba,na ni kweli ikawa hivyo.Leo mmesema muswada wa katiba hatihati kuondolewa na kweli umeondolewa.Hongereni sana.
Quote









+2 #38 cardil 2011-04-15 19:46 Enough is enough guys,"to get something u never had, u have to do something u never did"nchi ya kwanza kwa utajiri na nchi ya kwanza kwa umaskini,raslim ali zetu zinazidi kututesa tulio wengi angali wachache wanafaidi.enz za mwalimu nyerere alishawah kuwaulza watu wa geita huwa mnakula wali au ugali na dhahabu wakamjibu hapana,huwa tunakula wali na maharage akawaambia basi nafunga mgodi wa geita kwa sababu ni hasara kwa nchi na watanzania kwa ujumla.leo hii kuna kiongozi anaweza simama km nyerere akaifokea barrick wanaoua ndg zetu huko north mara na kutuaribia mazingira buzwagi na kwingineko,ggm imedhulumu watu kwa tathmn za mashamba wkt serikali inachekelea!tun ataka maoni kwa level zote za wananchi maana katiba ni ya wananchi...hii yenu ya kulinda matumbo na familia zenu itakuja kuwatokea puan km ya ben ali,mubaraki na gbabo.somen alama za nyakati.tumechokaaaaa.
Quote









+4 #37 CAROLINE 2011-04-15 19:23 WAMILIKI WA MEREMETA GOLD MINE NA MAFISADI WOTE WATAJULIKANA TU NI SIKU HAIJAFIKA.
Quote









+3 #36 mzalendo 2011-04-15 18:08 UADIOLIFU WA KIONGOZI HUONEKANA PALE MWENENDO WAKE NA MATENDO YAKE YANAPOLETA FARAJA, MABADILIKO CHANYA NA UFANISI KATIKA KAZI AU TAASISI. LAKINI KWA NAFASI YA PINDA KAMA PM INAONEKANA KUMPWAYA KWANI AMEKUWA MTU WA KUPOZA MIJADALA INAYOLENGA KUSSAFISHA UCHAFU NDANI YA SERIKALI. KAMA MASUALA YA MEREMETA, KAGODA ETC.
Quote









+4 #35 nemio 2011-04-15 15:10 Mh Pinda kaza buti kwani taifa hili ni letu sote nafasi inaonekana inazidi kupwaya
toa misimamo isiyoacha maswali kwa wananchi.Gamba imejivua serikali ipi sasa mh?hivi kwanini wasiwajibishwe wahusika?
Quote









+5 #34 makwa 2011-04-15 14:40 hivi ni kweli wabunge wa CCM hawaoni kasoro za kitaratibu za Bunge? au wamelogwa. Kila kitu mpaka tu wapinzani ndio waseme. Hata sisi huku nnje ya mjengo tunaona
Mheshimiwa Pinda naona mambo mazito, achana na lichama letu hili (CCM) LINAKUHARIBIA CV. We tunajua ni mwadirifu sana
Quote









+2 #33 Beatus 2011-04-15 14:31 Naungana na mchambuzi mmoja aliyepata kusema waziri mkuu PINDA ni SHOK UP SOBA ya serikali hajui hata hasara ya mabilioni ya pesa yanayopotea serikalini? wakati CAG anapeleka taarifa kwake? kweli tunaongozwa na viongozi mambumbumbu EE MUNGU TUSAIDIE.
Quote









+7 #32 Mwana-CCM Makini 2011-04-15 12:39 Ni jambo la aibu na KUSIKITISHA SAAA...ANA mwanachama wa chama changu(CCM) na MKUU WA MAWAZIRI (Waziri Mkuu)anaposema WAMEJIVUA GAMBA LA UFISADI lakini wakati huo huo akifanya yafuatayo:

Akishindwa kuwataja MAFISADI WANAOFAHAMIKA NA KILA MTANZANIA HADHARANI. JE HAJIAMINI AU ANATUONA WATANZANIA [NENO BAYA].

Akishindwa kuchukua HATUA PAMOJA NA CHAMA CHANGU(ccm) ZA KUWAFIKISHA MAFISADI WA Meremeta, TanGold, Kagoda, Dowans, Rada, Ndege la Raisi nk MAHAKAMANI.

MH. PINDA HUJAFANYA LOLOTE TANGU UMEINGIA HAPO OFISINI; HUNA LA KUKUMBUKWA NALO HADI LEO. ACHA USANII KWANI HAUKUFAI.

MWISHO NAOMBA UTUJALI WATANZANIA KWA KUPAMBANA NA UFISADI KI-UKWELI
Quote









+1 #31 abel 2011-04-15 12:33 Katika maandiko matakatifu wageni kuwatawala wenye nchi kwa kushika njia kuu za uchumi ni moja ya laana kwa Taifa. Si kwamba kina Kikwete hawajui sababu za umasikini wetu ila hawataki kusema kwa sababu wao ndiyo sababu za umasikini uliokithiri hasa kwa kuendekeza uroho na ubinafsi. Kiongozi wa umma na mzalendo hawezi kununua magari ya fahari ya kutembelea kwa kutumia fedha za walipa kodi wakati raia wanakufa njaa,dawa Hospitalini hakuna,vituoni wazee wanshindia mlo moja. Epukeni hizi laana kwa kutenda haki ndugu zangu kwani haya yote yatawarudia nyinyi!!!!!!!!
Quote









+9 #30 Shonde 2011-04-15 11:28 Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa kuwa wachambuzi wazuri wa masuala haya ya Siasa, hasa kwa wale wanaoelewa na kulitakia taifa letyu mema.

Kutaka Katiba ya Watanzania na si ya CCM wala CHADEMA ndilo jambo la Msingi kabisa,Hatma ya Tanzania ipo mikononi mwa Mchakato mzima wa Kuunda Katiba mpya kwa maslahi ya sasa na vizazi vijavyo.

Serikali ya sasa imelewa madaraka, Viongozi wake wapo tayari kukiokoa Chama na kuiangamiza Nchi na watu wake, Wageni wanafaidi matunda ta Taifa kushinda wananchi, MIfano ipo mingi sana.

Ardhi ya Watanzania inauzwa kwa wageni eti kisingizio ni wawekezaji, ni jambo la hatari sana, Rasilimali za Nchi zinapotea kila sekunde. Tujiuliuze hao wawekezaji wametusaidia nini tangu wamekuja? MEREMETA, TANGOLD, BARRICK,IPTL, KIWIRA, LIGANGA,KAGODA MCHUCHUMA ,BUZWAGI,DOWANS ,RICHMOND SONGAS,NBC 1997 LTD, 5 GROUP, CELTEL, ZAIN, AIR TELL na mangine mengi,ni wizi wa mchana huku wakilindwa na viongozi waliopo madarakani.

Enough is enough, mmetuonea vya kutosha.Halafu eti mnajivua gamba, huu ni uhuni.
Quote









+4 #29 minja marco evarist 2011-04-15 10:50 shida moja ni kwamba ccm wamezidi kuiba sera sasa suala la katiba mpya halikuwa la ccm ila waliiba sera za wapinzani ambao ni chadema ili kuwafurahisha wananchi, matokeo ya wizi huu sasa ni kwamba wameshindwa kutekeleza vyema mchakato huu, huu ni wizi na kuwahadaa wananchi, sifa mioja zuri ni kwammba chadema wameweza kuteka hisia za vijana waliochoshwa na ngojera za kila uchao na ahadi za ajira zisizotekelezek a.
Quote







123
Refresh comments list
 
Makinda awakuna Watanzania

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 15th April 2011 @ 16:15 Imesomwa na watu: 473; Jumla ya maoni: 0








SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, ameutoa muswada wa sheria ya mapitio ya Katiba kwenye ratiba ya Mkutano wa Tatu wa Bunge unaoendelea Dodoma ili kutoa fursa kwa wananchi kuendele kutoa maoni kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.

Baada ya Makinda kutangaza uamuzi wake bungeni mjini Dodoma, wabunge walishangilia na wengine kupiga vigelegele wakimaanisha kuwa wamefurahia uamuzi huo wa Spika wa Bunge.

Spika amekubali maombi ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kwamba kamati ipewe muda zaidi ili na wananchi wapate muda wa kuufikiria zaidi muswada huo na kutoa maoni yao.

Kamati hiyo hiyo pia imemuomba Spika iandae muswada huo kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi waweze kuusoma wenyewe badala ya kupewa tafsiri tu, na pia ikaomba muswada huo uchapishwe kwenye magazeti na kutangazwa kwenye vyombo vya habari ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi wengi wauelewe na watoe maoni.

Iliomba pia utangulizi wa muswada huo uwekwe vizuri zaidi ili wananchi waelewe madhumuni ya muswada huo kwa kuwa baadhi yao wanadhani kuwa tayari Bunge limeanza kuandika Katiba.

Makinda amewataka watakaochangia muswada huo wajadili mapendekezo badala ya kulumbana, na pia wanasiasa waache kushindana majukwaani.

"Wanasiasa tuache kushindana majukwaani, tujadili muswada. Maoni, ushauri na mapendekezo ndiyo yatasababisha kutungwa kwa sheria nzuri" amesema Makinda na kuwataka watakaotoa maoni waache malumbano na amewaomba Watanzania kudumisha mila zao za utulivu na amani.

Kiongozi huyo wa Bunge amesema, muswada huo si mali ya chama chochote cha siasa na kwamba, huu si wakati wa kulaumiana ila kutoa hoja zenye uzito zinazoweza kusaidia kuandika muswada vizuri.

"Nasisitiza utulivu wakati wote wa kazi hii. Kila mwanakamati ajue kwamba shughuli hii inatawaliwa na Kanuni za Bunge na itaratibiwa na kusimamiwa na kamati husika na siyo vyama vya siasa" amesema.

Spika amewaomba wananchi waiamini kamati yake kwa kuwa imejaa watu wenye uzoefu mkubwa na waliobobea katika taaluma mbalimbali ikiwemo ya sheria.

Makinda amesema, wahusika kwenye vyama vya siasa wanapaswa kutumia busara kutoa mawazo yao na wakisema hili liondolewe wawe pia tayari kusema kiwekwe nini badala yake.

"Waheshimiwa wabunge, kupitia kwenu nawaomba wananchi waepuke uandikaji wa muswada kwa kuleta fujo ya aina yoyote ile" amesema Makinda leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Spika wa Bunge ameitaka Serikali iuwasilishe muswada huo kwa lugha ya Kiswahili na uandikwe kwenye magazeti mbalimbali ili wananchi wausome, waulize maswali na waondoe jazba ambazo hazina mantiki.

"Muswada kwa hatua tuliyofikia si wakati wa kulaumu au kulaumiana bali ni kutoa hoja zenye uzito zinazoweza kusaidia muswada mzuri" amesema na kusisitiza kwamba, uandikaji wa Katiba mpya ya nchi uwe chanzo cha kuwaunganisha Watanzania na kuimarisha utaifa wetu kwa kuwa lengo letu ni ni kuwa na Tanzania moja yenye amani na utulivu.

"Aidha ninaiagiza kamati iniletee ratiba na utaratibu wa kukamilisha kazi hii ili muswada huu uweze kusomwa mara ya pili katika mkutano ujao wa Bunge" amesema Makinda na kuwaomba wananchi watoe maoni yao kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kupitia Ofisi za Bunge zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, na Zanzibar.
 
Serikali iwe sikivu, muswada huu wa Katiba uondolewe Send to a friend Thursday, 14 April 2011 21:05

katiba.jpg
TUNALAZIMIKA kwa mara nyingine katika kipindi kifupi kilichopita kuitahadhalisha Serikali kuhusu maafa yanayoweza kuikumba nchi yetu iwapo suala la kuandika Katiba mpya litaendelea kufanyiwa mzaha na kupewa mwelekeo wa kisiasa kwa kile kinachoonekana kama kukidhi matakwa na manufaa ya watu wachache.

Tangu Serikali iandae Muswada wa Marejeo ya Katiba na kuuwakilisha bungeni ili ujadiliwe chini ya hati ya dharura, matukio mengi ya kusikitisha yametokea na kuashiria kwamba mustakabali wa taifa letu hivi sasa uko katika mashaka makubwa.

Tumeshuhudia jinsi muswada huo ulivyojadiliwa kwa hisia kali na makundi mbalimbali katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar kiasi cha polisi wenye silaha kuingilia kati ili kuzima purukushani zilizotokea kufuatia washiriki wengi kuukataa muswada huo kwa kusema kuwa, mbali na kuwa na makosa na kasoro nyingi za kiufundi, ulikuwa haukidhi matakwa ya Watanzania wote bali watu wachache walio serikalini na chama tawala. Baadhi ya washiriki walichana na kuchoma nakala za muswada huo mbele ya viongozi wa ngazi ya kitaifa wa serikali zote mbili, yaani ya Zanzibar na Muungano.

Mtafaruku huo ulipata nguvu kutokana na wananchi kwa ujumla wao kuupinga na kusema kuwa maudhui yaliyomo katika muswada huo yanaonyesha kuwa Serikali haikuwa na nia njema bali ilikuwa na ajenda ya siri ya kuwalaghai. Wananchi walichukizwa sio tu na kitendo cha Serikali kuupeleka muswada huo bungeni kwa hati ya dharura, bali pia muswada huo kusheheni vifungu vyenye vitisho kwa lengo la kuwafumba midomo wananchi na vyenye kumpatia rais madaraka makubwa katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.

Lakini pamoja na kelele hizo na msimamo wa wananchi kutaka Serikali iuondoe muswada huo bungeni hadi makosa yaliyomo yatakaporekebishwa na wananchi wote kupewa fursa ya kuujadili ukiwa katika lugha ya Kiswahili, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alithibitisha kuwa serikali yake sio sikivu, baada ya kuliambia Bunge wakati akijibu maswali ya hapo kwa hapo, kuwa Serikali haijauondoa muswada huo kwa sababu Kamati ya Sheria na Katiba haijaishauri kufanya hivyo.

Hii ni ishara tosha kuwa ukaidi huo utatuletea madhara makubwa na kusambaratisha umoja wetu. Tayari baadhi ya wananchi wa Zanzibar wametumia mtafaruku huo kutaka Muungano uvunjwe na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar wameshabikia kauli hizo waziwazi, pengine kutokana na wao kutoshirikishwa katika uandaaji wa muswada huo.

Wataalamu wa masuala ya katiba, wanazuoni na makundi mbalimbali katika jamii yetu wametoa ushauri kuwa muswada huo uondolewe lakini Serikali bado imetia pamba masikioni. Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani ambaye anaheshimika sana katika Bara la Afrika kama mshauri katika masuala ya kutunga katiba, naye ameshauri muswada huo uondolewe kutokana na kasoro nyingi zilizomo na pia ameishauri Serikali isione aibu kufanya hivyo. Huo pia ndio ushauri waliotoa wataalamu na wasomi wengine wengi, akiwamo gwiji la sheria na masuala ya katiba, Profesa Issa Shivji.

Sisi tunasema Tanzania bila katiba yenye kasoro na mizengwe inawezekana iwapo kila mtu ataweka mbele maslahi ya Taifa na ya vizazi vya sasa na vijavyo. Tunawasihi viongozi walio serikalini na katika chama tawala ambacho kimeunda serikali hiyo, waone umuhimu wa nchi yetu kuwa na katiba yenye kukidhi matakwa, maono na matazamio ya wananchi wote ili tuweze kuishi kwa amani pasipo uwezekano wa kuingia katika vita na umwagaji damu.

Ni imani yetu kuwa hekima na busara vitatumika katika suala hili la kupata Katiba mpya. Iwapo Serikali itauondoa muswada huo, itakuwa imeonyesha usikivu na umakini wa kusikiliza hoja za wananchi wengi. Ni imani yetu pia kuwa Serikali haitaleta tena bungeni miswada inayohusu masuala nyeti kwa hati ya dharura.
 
Muswada huu wa Katiba utavuruga umoja wetu Send to a friend Monday, 11 April 2011 21:55

katiba.jpg
SASA ni dhahiri kwamba muswada wa marekebisho ya Katiba mpya unachukua mwelekeo wa kuvuruga umoja wetu na kutusambaratisha kama taifa. Tangu muswada huo uanze kujadiliwa na wadau mbalimbali takribani wiki moja iliyopita, jambo lililojitokeza waziwazi ni kuwa Watanzania wengi, pasipo kujali tofauti ya itikadi na imani zao, wameghadhabishwa na muswada huo kutokana na ukweli kwamba unabeba maudhui yenye lengo la kukidhi matakwa na maslahi ya watu wachache katika nchi yetu.
Pamoja na kuwapo mwangwi mkubwa utokanao na sauti za wananchi katika kila kona ya nchi yetu wanaoendelea kuupinga muswada huo, kikundi hicho kidogo cha watawala kinaendelea kuweka pamba masikioni na kusema kuwa wananchi watake wasitake, muswada huo ndio pekee utakaokuwa msingi wa mchakato utakaozaa Katiba mpya na Rais anafanywa kuwa alpha na omega.

Wananchi kwa ujumla wanasema kuwa hawakushirikishwa katika mchakato mzima wa kuandaa muswada huo, kwa maana ya kutoa mawazo yao ili yazingatiwe katika kutayarisha muswada huo. Huko Zanzibar, mijadala ya muswada huo imejaa vitimbi, ghadhabu na jazba kwa kiwango cha kutisha kiasi cha baadhi ya wananchi kuchana na kuchoma moto nakala za muswada huo mbele ya viongozi wa kitaifa wa Serikali ya Mapinduzi na ya Muungano.

Viongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na vyama vya CCM na CUF vinavyounda serikali hiyo wamekaa kimya. Kama tulivyosema hapo juu, bila shaka hali hii inachochewa na ukaidi wa kikundi kidogo cha viongozi wa Serikali ya Muungano – hasa kutoka Tanzania Bara – ambao wanaweka mbele maslahi binafsi kwa kuhakikisha kuwa Katiba mpya itakayotungwa inakuwa hati miliki yao.
Tumeshuhudia Wazanzibari wengine wakienda mbele zaidi kwa kusema kuwa hawautaki Muungano, kwa maelezo kuwa Zanzibar inaendelea kuburuzwa na kwamba mustakabali wa nchi yao bado unaamuliwa kutoka Tanzania Bara. Kwa vyovyote vile, haya ni madai mazito na ya msingi ambayo lazima yafanyiwe kazi iwapo tunataka Muungano uendelee kuwapo kwa utashi wa wananchi wa pande zote mbili.
Itakumbukwa kuwa madai hayo mazito yamepewa nguvu zaidi katika kujadili muswada huo wa Katiba mpya kutokana na kauli ya hivi karibuni ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kwamba serikali hiyo ilipeleka mapendekezo 14 katika Serikali ya Muungano kuhusu muswada huo wa Katiba mpya lakini ni mawili tu yaliyokubaliwa na hakuna sababu zilizotolewa kuhusu mapendekezo 12 yaliyokataliwa. Tukizingatia pia ukweli kuwa idadi ya mambo ya Muungano iliongezwa kinyemela kutoka 11 hadi 22 pasipo ridhaa ya Wazanzibari, ndio sababu mijadala ya muswada wa Katiba mpya imekuwa na mwelekeo huo.

Tangu mwanzo tulionya kuhusu uwezekano wa kusambaratika kwa taifa letu iwapo Serikali ya Muungano, chini ya Rais Kikwete, isingehakikisha kuwa mchakato wa kuwapatia Watanzania Katiba mpya haufanyiki kwa mizengwe na ujanjaujanja wa kutanguliza mbele maslahi na matakwa ya wachache. Tunashuhudia sasa jinsi serikali hiyo inavyofanya juhudi za makusudi kutisha wananchi wasijadili na kutoa mapendekezo kuhusu Katiba wanayoitaka.

Ndio maana mijadala hiyo inafanyika Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar peke yake, tena katika mazingira ya vitisho vya vyombo vya dola vilivyosheheni silaha za kivita, zikiwamo mabomu ya machozi na risasi za moto. Badala ya kuruhusu wananchi katika mikoa yote wajadili muswada huo kwa uhuru, Serikali imeona ikifanya hivyo ajenda yake ya siri itashindwa kwa sababu wananchi watapata muda wa kuuelewa muswada huo kwa upana zaidi na mwishowe wataukataa.
Na ndio hasa siri ya muswada huo kuletwa katika lugha ya Kiingereza badala ya lugha yetu ya taifa ya Kiswahili. Na ndio maana vyama vya siasa ambavyo ni wadau muhimu katika mchakato huo vimepigwa marufuku kuhamasisha wafuasi wake.
 
Wataka muda wa kujadili muswada uongezwe Send to a friend Thursday, 14 April 2011 21:12

Patricia Kimelemeta
TAASISI ya Kimataifa ya Jopa Foundation (JPF), imeitaka serikali kuongeza siku kwa wananchi kutoa maoni yao juu ya muswada wa mapitio ya katiba mpya, uliowasilishwa Bunge hivi karibuni.

Rai hiyo imekuja baada ya serikali kutoa muda wa siku tatu kwa wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar, kutoa maoni yao kuhusu muswada huo unaopingwa na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Praygod Mmasy, alisema muda uliotolewa na serikali haukidhi matakwa ya wananchi wenye kiu ya kutaka kutoa maoni yao.
Alisema kwa hali hiyo,serikali inapasa kuongeza muda ili kutoa fursa kwa kima mmoja kushiriki katika kutoa maoni yake.

Alisema, taasisi yake kwa kushirikiana na wadau wengine wanaopinga muswada huo, watafanya maandamano ya kuishinikiza serikali, iongeze muda ili kuwawezesha wanachi kutoa maoni yao kuhusu muswada huo.

"Kama serikali itashindwa kuongeza muda katika jambo hili, tutafanya maandamano, ya kuishinikiza ifanye hivyo,"alisema Mmasy.Alisema maandamano hayo yatafanyika Aprili 20 mwaka huu na kwamba yataanzia Buguruni na kumalizikia katika Viwanja vya Jangwani.

Aliwataka wananchi wanaopinga muswada huo, wajitokeze kwa wingi kushiriki katika maandamano hayo na kuyapa nguvu zitakazoifanya serikali, ikubali kuongeza muda."Tunashughulikia kibali cha maandamano ya amani kwa ajili ya kupinga muswada huu, kwa sababu muda uliotolewa hautoshi, wananchi wengi wanashindwa kupata haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni," alisema.
 
Comments




+2 #1 Lema W.E 2011-04-15 09:18 Ikiwezekana watoe hata miezi minne mbele na wabunge wote mrudi kwenye majimbo yenu mkaongee na wananchi wenu msikilize maoni yao juu ya muundo huo wa katiba mpya then mrudi tena bungeni kuwasilisha maoni yeo, sio kukaakaa tuu huko bungeni mkisinziasinzia na kula posho ya bure, huku hamjui nini tunachohitaji sisi wananchi wenu tuliowachagua kutuwakilisha huko,sio mnavimbisha mitumbo tu huko.
Quote







Refresh comments list
 
Bunge larudisha muswada wa Katiba kwa umma Send to a friend Saturday, 16 April 2011 08:46

aliseifiddbalozi.jpg
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Kitope, Balozi Ali Seif Idd (kulia) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu wakifuatilia kikao cha bunge jana mjini Dodoma walipohudhuria kikao cha nane cha mkutano wa tatu wa bunge. Picha na Edwin Mjwahuzi

Midraji Ibrahim, Dodoma
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amesema baada ya kupitia maelezo na ushauri wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, ameridhika na kuona ni busara kutoa muda zaidi kwa kamati kuendelea na kazi ya kuchambua muswada wa Marejeo ya Katiba.

Akitoa uamuzi wake kuhusu muswada huo bungeni jana, Makinda alisema kamati itaendelea kuchambua maoni ambayo tayari yametolewa na wadau na itakusanya mengine, kwa lengo la kuboresha zaidi muswada huo ili kuwa na manufaa zaidi.

"Naomba Watanzania kudumisha mila zetu za utulivu na amani, muswada kwa lugha ya kibunge ni mapendekezo tu, safari hii ni mapendekezo ya Serikali kuhusu namna ya kuanzisha zoezi la kuandika Katiba ya nchi," alisema.

Alisema Bunge linawaomba wananchi, wasomi, wafanyakazi, wanawake, wanafunzi, wana vyuo, mashirika yasiyo ya kiserikali, walemavu, wakulima, madhehebu ya dini, vyama vya siasa na makundi mengine ya jamii, wajadili mapendekezo ya muswada.

"Tuache malumbano, kuzomeana na maandamano. Wanasiasa tuache kushindana majukwaani, tujadili muswada. Maoni, ushauri na mapendekezo ndiyo yatasababisha kutungwa kwa sheria nzuri," alisema Makinda.

Spika aliwataka wananchi kuiamini Kamati ya Bunge, kwa sababu imejaa watu wenye uzoefu mkubwa na waliobobea kwenye taaluma mbalimbali ikiwamo sheria.Alisema muswada huo siyo mali ya chama chochote cha siasa na kwamba, busara zaidi zitumike na mtu anayebainisha lisilofaa awe tayari kutaja linalostahili kuwapo.

"Tunaitaka Serikali ilete muswada kwa Kiswahili na uandikwe kwenye magazeti mbalimbali, ili watu wote wasome wenyewe, waulize maswali, waondoe jazba ambazo hazina mantiki," alisema Makinda na kuongeza:

"Uandikaji wa Katiba mpya iwe chanzo cha kutuunganisha Watanzania wote na kuimarisha utaifa wetu. Lengo letu ni kuwa na Tanzania moja yenye amani na utulivu."

Makinda alisema wananchi wanatakiwa kupeleka maoni yao kwa Kamati ya Bunge kupitia ofisi za Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar, huku akiagiza kamati hiyo kumpelekea ratiba na utaratibu wa kukamilisha kazi ya muswada, ili uweze kusomwa mara ya pili mkutano ujao wa Bunge.

"Nasisitiza utulivu wakati wote wa kazi hii. Kila mwana kamati ajue kwamba shughuli hii inatawaliwa na Kanuni za Bunge na itaratibiwa na kusimamiwa na kamati husika na siyo vyama vya siasa," alisema Makinda.

Akizungumzia hatua hiyo ya Bunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema Chadema kimesitisha maandamano yake ambayo yalikuwa yafanyike leo nchi nzima kupinga upitishaji wa muswada huo kuwa sheria.

"Chadema tunasema tumesitisha maandamano yetu, tunataka Watanzania watuelewe. Tunasubiri Serikali ili tuone hiyo nia njema inayotaka kuonyesha inakuja kwa njia gani," alisema Mbowe.Mbowe alilaumu hatua ya Serikali kupeleka muswada huo kuwa umesababisha hofu, malumbano na migongano mikubwa kwa taifa.

"Ule muswada unaweza ukaandikwa na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria, Serikali inaleta muswada kama ule na upungufu wote huo. Taarifa za uhakika ni kwamba wenzetu wa Zanzibar hawakushirikishwa wakati wao ni sehemu ya Serikali ya Muungano," alisema Mbowe na kuongeza:

"Vikao vya Chama Cha Mapinduzi ambacho ndicho kinachoongoza Serikali, vikao vya maamuzi ya kisera kama Nec (Halmashauri Kuu ya CCM), havikuwa na taarifa ya mabadiliko ya Katiba.

Ukweli ni kwamba kilikurupuka kikundi kidogo cha watu kikapata baraka za Rais, kikaleta muswada bungeni ambao ulikuwa haujapata hata baraka za chama chake."Alisema mabadiliko ya Katiba ni makubwa kwenye taifa hivyo kitendo cha Serikali kupeleka mabadiliko hayo kwenye Bunge bila kushirikisha hata vikao vya chama ni aibu.

"Hii haikuwa sera ya CCM, ingekuwa Serikali inatekeleza sera ya chama chake ingekuwa haina tatizo. Hii haikuwa sera ya CCM, haikuwa sehemu ya vipaumbele vya chama hicho kwenye ilani ya uchaguzi uliopita, ilinyofoa kipengele hiki cha hoja ya mabadiliko ya Katiba baada ya shinikizo kubwa la kitaifa na pekee shinikizo kubwa la Chadema," alisema Mbowe na kuongeza;

"Mpaka tukaenda bungeni tukadai Serikali ifanye mabadiliko, lakini kwa utaratibu wa kawaida wa utawala bora, vyama vya siasa na vyombo vyake vya kufanya maamuzi ya kisera hasa yanapokuwa makubwa kama haya, vishirikishwe kama wadau."Mbowe alidai kuwa CCM wana tabia ya kubeba hoja bila kuangalia undani wake na kwamba hilo lilijidhihirisha jana wakati Spika akitoa uamuzi, wabunge wa CCM walishangilia ilhali Serikali yao ndiyo iliyopeleka hoja isiyo sahihi.

Akizungumzia hatua hiyo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema Singo Bensoni aliielezea hatua hiyo kuwa ni ."Ushindi wa nguvu ya umma dhidi ya mafisadi wa Katiba."
Alisema maandamano ya chama hicho yalikuwa na malengo matatu ambayo kutokana na uamuzi wa Spika, mawili yameshapatiwa ufumbuzi ambayo ni kuondoa muswada bungeni pamoja na muswada huo kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
 
Comments




0 #15 mtaisoma 2011-04-16 22:03 nyie chadema acheni longolongo zenu, eti ni ushindi wa nguvu ya umma, hamna lolote warongo wakubwa nyie, hiyo ni busara ya serikali iliyopo madarakani, inaangalia zaidi maslahi ya watu kuliko hizo kelele zenu za majukwaani, mmekuwa kama wanawake wenye nyege za kutombwa, tulieni tuachieni nchi yetu iliyotulia sio kutuletea fujo. si vibaya mkiitwa mavuvuzela.
Quote









0 #14 Gamba Beshubeo 2011-04-16 18:13 Kwa kweli watu wameamka. Wamechoshwa na uozo.Kufukia mambo kwa upande wa spika na wenzake ni kukaribisha mapambano, zogo zaidi kutoka upinzani. Bora wafuate dhamira zao, waseme ukweli ili wawe na uwanja mzuri wa kujitetea. Ukweli utapeta na utawapunguzia mzigo spika na wasaidizi wake.
Quote









0 #13 fr.baptiste mapunda 2011-04-16 16:50 Hongrereni Chadema kwa kuwa na msmamo, maandamano ni silaha kubwa ya kudai haiki, na ni haki ya chama cha upinzani au chochote kile/ Nawaunga mkono 300%. Mimi mtanzania mzalendo, Padre baptiste Mapunda, nairobi, kenya
Quote









+3 #12 Najaribu 2011-04-16 14:35 Vuvuzela, ni kweli ndivyo inavyoonekana kuwa CCM inataka mtu wao wa 2015 aendelee kuiba kura. Na inaanza kutia shaka wanamwaandaa Mtoto wa Mkulima. Naye bila soni, anaana kutetea uvunjifu wa sheria (tazama ile ya bomoa bomoa). Ndiyo sababu wameamua kuwatosa Maghufuli na akina Lowassa and company mapema.

Ila kuhusu katiba nzuri, wananchi wakishirikiana na chama makini kama CHADEMA, katiba nzuri ni MUST. Shime tu sote tutoe maoni ya kweli na kwa kudhamiria. Na pale pa kushikamana bega kwa bega na wana-mapinduzi wa kweli, basi nguvu ya umma ituongoze. Wenzetu wameweza, kwa nini sisi tushindwe?. Wakati ni huu wa kuionyesha CCM Kuwa waTanzania wale-e-e-e si hawa wa SASA
Quote









0 #11 Najaribu 2011-04-16 14:31 Vuvuvzela, ni kweli ndivyo inavyoonekana kuwa CCM inaaka mtu wao wa 2015 aendelee kuiba kura. Na inaanza kutia shaka ni Mtoto wanamwandaa Mtoto wa Mkulima. Ndiyo sababu wameamua kumtosa Lowassa and company mapema. Ila kuhusu katiba nzuri, wananchi wakishirikiana na chama makini kama CHADEMA, katiba nzuri ni MUST. Shiem tu sote tutoe maoni y akweli na kwa kudhamiria. Na pale pa kushikana bega kwa bega na wanamapinduzi wa kweli, basi nguvu ya umma ituongoze. Wenzetu wameweza, kwa nini sisi tushindwe. Wakati ni huu wa kuionyesha CCM Kuwa waTanzania wale-e-e-e si hawa wa SASA
Quote









+4 #10 Bakari 2011-04-16 13:33 Pongezi za dhati kwa CHADEMA na VYOMBO VYA HABARI. Tumeshuhudia CCM ikiingiza wanafunzi wa sekondari kujaza nafasi za wachangiaji wa mijadala ya katiba, aibuuuu!!!
Quote









+4 #9 vuvulzela 2011-04-16 13:17 Hakuna muswada mzuri wa katiba utakaokuja kama Pinda, C Komani na Werema bado wapo madarakani. Hawa vijiongozi waliutunga kwa kujipendekeza kwa JK na wanadhani kuwa Pinda is next 2015
CDM hongera sana maana maandamano ya Nguvu ya Umma mliyoyatangaza week end hii yamewatisha serikali ya CCM. Huu ni upinzani wa kweli serikali ya CCM inaupata na haijauzoea tangu ianzishwe.
CDM sasa ibueni madudu mengine ya serikali ya CCM, jamii ipo nyuma yenu ili tusonge mbele
Quote









+6 #8 CAROLINE 2011-04-16 11:58 WATANZANIA WOTE WENYE BUSARA NA MAPENZI MEMA NA TAIFA HILI LA TANZANIA TUWAPE MOYO NDUGU ZETU WA CHADEMA. KWA KWELI MIMI NADIRIKI KUSEMA KAMA SIO HAWA CHADEMA TANZANIA TUNGESHAWEKWA REHANI. CCM NI MDUDU HATARI SANA(DANGEROUS MOLECULE)
Quote









+5 #7 walimu 2011-04-16 10:51 HONGERA SANA CHADEMA: kidumu chama hiki. CCM IFE KABISA. CHADEMA ENDELEENI NA MAPAMBANO kwa kuwa ccm watakuja na u[NENO BAYA] na ujanja mwengine. MAKINDA NI ZIZO KABISA: eti tuamina kamati ya bunge la ccm, uwendawazimu huu.
Quote









+6 #6 mtu kwao 2011-04-16 10:44 Ngumu ya ummaaaaaaaaaaaa a..CHADEMA BABA LAO ..WAMEWAPIGISHA JAMBA JAMBA CCM HADI WAKACHIA NA BADO MAANDAMANO YA MWEZI UJAO NYANDA ZA JUU KUSINI..LAZIMA MOTO UWAKE ,,KAMA SI CHADEMA HAWA JAMA WASINGEACHIA ..HEKO VIONGOZI MAKINI MNAOANGALIA MASILAHI YA TIF AMBELE..
Quote









0 #5 Zacharia 2011-04-16 10:35 Nawasihi watanzania wote tuwe na mazoea ya kusoma alama za nyakati. Na tuende bega kwa bega katika kutoa maoni ya kuutengeneza muswada utakaofaa kutengeneza sheria ya kusaidia kubadilisha katiba yetu ya jamhuri ya muungano.
Na wadau wote wa siasa tupunguzeni malumbano cha msingi ni kuyaendesha kwa busara na utashi kama zawadi tulizopewa na Mungu.
Tujiangalie haya maandamano yasije yakaleta Ulibya na ucorde viore hapa kwetu.
Cha msingi kuna mifano mizuri ya nchi jirani ambao wameweza kubadilisha katiba bila malumbano tuige nchi hizo kama Kenya.
" Mungu ibariki Tanzania"
Quote









+2 #4 alex marung 2011-04-16 10:34 Mswada uandikwe magazetini, utangazwe redioni na kwenye television. Kuwe na vipindi vya majadiliano na sehemu za kutolea maoni hasa magazetini (blank part/page) kwa ajili ya wananchi,vikund i mbalimbali kwa jinsi alivyotaja spika, kuandika maoni yao, waikate sehemu hiyo na kupeleka patakapoelekezw a.Hii itakuwa njia mojawapo rahisi kwani magazeti yanasambaa nchi nzima na ndiyo kumbukumbu ya habari ambayo mwananchi anaweza kuihifadhi kwa urahisi bila kupotea.
Quote









+4 #3 cardil 2011-04-16 10:18 Chadema mzidi kufumbua macho ya serikali pamoja na wananchi kwa ujumla.zama za bora liende lilikuwa enzi ya chama kimoja,umma upo nyuma yenu na si nyuma ya mafisadi maana nchi hii ishauzwa na inahtaji ukombozi toka kwa wtu wachache km wa chadema walvyo.mtoto wa mkulima nae ni walewale shock up ya ccm na serikali kwa ujumla.mijadala ipelekwe kwa wananchi watoe maoni yao tanzania tunayoitaka na si tanzania tuliopo mwisho wa siku taasis,wafanyak az,wakulima,waz ururaji,walemav u na wengneo waweze kurdhka na kilchopo.uchakachuaji mpk kwenye muswada?kweli serikali imechoka na nchi hii pamoja na wananchi wake."chadema big up"
Quote









+6 #2 Najaribu 2011-04-16 09:19 Hakuna cha hekima na busara kwa CCM ila wamesoma alama za nyakati. Ukweli wananchi wameamka sana kisiasa na wanataka maendeleo ya kweli. Tunashukuru vyama vya upinzani kwa kuwapa wananchi elimu ya uraia kwa maneno na kwa vitendo.

Kamati pamoja na Spika wameangalia upepo ulivyovuma wakati wa mijadala na wamegundua ngoma itakuwa nzito endapo wataleta maamuzi tofauti na haya.

Ila ninalaani sana matumizi makubwa ya fedha yaliyotumika kutayarisha mswada mbovu kwa makusudi. Waandaaji wananpaswa kujua siasa za sasa si zile za "kidumu chama cha mapinduzi; zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi" hapana, ni fikra za mageuzi yatakayoleta maendeleo kwa wananchi.
Quote









+4 #1 Edijoe 2011-04-16 09:00 Hiyo ndio hekima na busara tunayoitaka sio kulazimisha bora iende nawapongeza watanzania kuwa na uelewa sasa na kutokubali kuburuzwa na wachache na naomba tuujadili mswada huu na kuutolea maoni. Na asitokee mwanasiasa, kiongozi yeyote kuwasemea wananchi au kuwalazimisha. Inabidi uwekwe kwenye magazeti, upelekwe kwa njia ya sanaa na vilvile muswada huu uwe na vipindi kwenye radio na tv ili hata kwa bibi nao waupate na watoe maoni yao.
Quote







Refresh comments list
 
Muswada wa katiba kuandikwa Kiswahili

Saturday, 16 April 2011 10:48 newsroom




* CCM yaipongeza serikali
Na Joseph Damas, Dodoma
BUNGE limesimamisha mjadala wa muswada wa marejeo ya mabadiliko ya katiba mpya, na kuiagiza serikali kuuandaa upya ukiwa katika lugha ya Kiswahili. Serikali pia imeagizwa muswada huo uchapishwe na kutangazwa kwenye vyombo vya habari ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi kuusoma na kuuelewa kabla ya kutoa maoni. Kutokana na uamuzi huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeipongeza serikali kwa kuwa imedhihirisha jinsi ilivyo sikivu. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, alisema Chama kina imani Watanzania walio katika pembe zote za nchi watapata fursa ya kutoa maoni kwa uhuru na kwa uelewa mpana zaidi. Alisema CCM iko bega kwa bega na serikali na wananchi katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya kupata tume na hatimaye mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya utakapoanza yanafikiwa.
Uamuzi wa kusimamisha mjadala ulitangazwa bungeni jana na Spika Anne Makinda, baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, iliyosimamia uratibu wa maoni ya wananchi. Muswada huo uliwasilishwa bungeni kwa hati ya dharura na baada ya kusomwa Bunge liliandaa utaratibu wa wananchi kutoa maoni katika vituo vya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar. Hata hivyo, kinyume cha matarajio, kazi ya utoaji maoni ilizusha vurugu na watu kurushiana maneno, huku baadhi ya wanasiasa wakidaiwa kuhusika kupotosha wananchi. Spika Anne alisema Aprili 13, mwaka huu, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti Pindi Chana, iliwasilisha taarifa ya maelekezo ya awali juu ya muswada ulivyofanyiwa kazi na kutoa mapendekezo. Alisema kanuni 2(2) ya Kanuni za Bunge toleo la 2007, inatoa mamlaka kwa spika kuamua utaratibu wa kufuata iwapo kamati iliyopelekewa muswada haitakuwa imekamilisha kazi kwa muda husika.
Spika Anne alisema kutokana na ushauri huo, iliamuliwa muda zaidi utolewe kwa kamati na wananchi kuufikiria muswada huo, ambao unatakiwa kuwekwa vizuri ili wananchi waelewe madhumuni yake. Anne alisema imeonekana wazi kuwa wananchi wengi wamedhani tayari serikali imeanza kuandika katiba, wakati kilichofanyika ni kutunga sheria ya kuunda tume ya kukusanya maoni. "Nimeridhika na mapendekezo yaliyotolewa, nimeona ni busara kutoa muda zaidi ili kazi ya kuuchambua muswada huu iendelee. Pia kuendelea kukusanya maoni ya wadau na kuyachambua ili kuuboresha zaidi, uwe na manufaa kwa taifa," alisema. Hata hivyo, Spika Anne alionya kuwa muswada huo si mali ya chama chochote cha siasa, na watatumia busara ya kutoa mawazo kikamilifu. Alisema iwapo mtu ataona kuna haja ya kuondoa kifungu au neno basi awe tayari kupendekeza kitu kingine cha kuingizwa ili kusaidia kuandikwa muswada mzuri.
"Muswada utakuja kwa Kiswahili na utatangazwa ili watu wasome, tutumie fursa hiyo kuuliza maswali bila kuwa na jazba zisizo na mantiki," alisema. Aliwaasa Watanzania kuwa, uandikaji wa katiba mpya uwe chanzo cha kuwaunganisha wote na kuimarisha utaifa, kwani lengo ni kuijenga Tanzania moja yenye amani. Spika Anne alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kutoa maoni kwa kamati kupitia ofisi za Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar. Kutokana na hatua hiyo, muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa bungeni kusomwa kwa mara ya pili katika mkutano ujao wa Bunge.
Katika hatua nyingine, taarifa ya Nape ilisema CCM inaipongeza serikali kwa kuongeza muda wa majadiliano ya muswada huo, kwani Chama kina imani kuongezwa muda kutawezesha wananchi na wadau wengine kujitokeza kuchangia muswada huo kwa njia ya kidemokrasia na kwa mapana zaidi. Alisema Chama kina imani kuwa maoni yatakayotokana na mjadala huo yatapewa kipaumbele na serikali, hususan katika kufanikisha mchakato wa mabadiliko ya katiba.
Nape alisema Chama kinatoa wito kwa wananchi kujitokeza katika maeneo ambayo yameandaliwa na kamati ya bunge kutoa maoni. Naye Anne Kilango Malecela (Same Mashariki -CCM), amepongeza hatua ya serikali kuridhia kusogezwa mbele kwa muswada huo. Alisema kitendo hicho kinadhihirisha usikivu wa serikali ya CCM na inafanya mambo kwa maslahi ya Watanzania na ni jambo la kupigiwa mfano.
"Jamani siku zote nasema serikali ya CCM ni sikivu kwa wananchi, sasa tumesimamisha muswada huu kwa maslahi ya Watanzania wote," alisema. Wakati huo huo, CHADEMA imesema inasitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike nchini kupinga muswada huo.
Akizungumza jana, Mkuu wa Operesheni wa chama hicho, Benson Singo, alisema baada ya uamuzi wa serikali wameamua kusitisha maandamano hayo.
ìMaandamano yetu kwa mikoa 10 tumeyasitisha kwa muda baada ya serikali kuonekana kutoa ufumbuzi wa baadhi ya mambo,íí alisema.
Kwa mujibu wa Singo maandamano yalikuwa yafanyike Arusha, Mbeya, Kigoma, Kilimanjaro, Ruvuma, Dodoma, Pwani, Mtwara, Tabora na Morogoro.
Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, alisema leo atataja orodha mpya ya watuhumiwa wa ufisadi akiwa mkoani Tabora.
 
Pinda aifagilia Katiba, aponda maandamano

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 16th April 2011 @ 15:43 Imesomwa na watu: 212; Jumla ya maoni: 0








WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema, Tanzania inabadili Katiba si kwa sababu iliyopo haifai.

Pinda pia amelieleza Bunge kuwa, Tanzania inatunga Katiba mpya si kwa sababu haina Katiba, au imetoka katika ukoloni.

Kwa mujibu wa Pinda, Tanzania inatunga Katiba mpya kwa ajili ya kukidhi mazingira mapya ya leo na matakwa ya wananchi wa leo baada ya miaka 50 ya uhuru.

"Napenda kutoa wito kwa Watanzania wenzangu kuwa, tushirikiane katika hatua zote zinazofuata katika mchakato wa kuelekea kutungwa kwa Katiba mpya" amesema bungeni mjini Dodoma wakati anahutubia Bunge kuahirisha Mkutano wa Tatu wa Bunge na amesema si sahihi kulinganisha marekebisho ya Katiba na viraka.

"Baadhi ya Watanzania wanabeza Katiba zetu kwa msingi tu kuwa zimerekebishwa mara nyingi na hivyo kuzifananisha na viraka. Kama ilivyo sheria, Katiba nazo hufanyiwa marekebisho kila inapobidi ili kuzingatia hali mpya inayojitokeza katika taifa ambayo inaonekana kuwa na uzito wa kulazimika kurekebisha Katiba ili kutambua hali hiyo kikatiba" amesema.

Pinda amesema, Serikali imekubali uamuzi wa Spika wa Bunge, Anne Makinda, wa kuongeza muda wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu muswada wa sheria itakayosimamia mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Makinda jana aliutoa muswada huo kwenye ratiba ya Mkutano wa Tatu wa Bunge unaoendelea Dodoma ili kutoa fursa kwa wananchi kuendele kutoa maoni kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amempongeza Makinda na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kwa kuona umuhimu wa kuongeza muda wa kupokea maoni kwa wananchi na wadau ili kuuboresha muswada huo kwa manufaa ya taifa.

"Wakati muafaka utakapowadia, Serikali itatoa ushirikiano thabiti kwa kamati ili kuwasilisha muswada bungeni utakaozingatia mambo ya msingi yatakayotolewa na wananchi kuanzia sasa" amesema Pinda wakati anahutubia Bunge kuahirisha Mkutano wa Tatu wa Bunge.

"Sasa tunayo fursa nyingine ya kutazama upya Katiba yetu. Basi sote tushirikiane kwa dhamira moja ya kutoa maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali ili kwa pamoja tuweze kupata Katiba itakayowanufaisha Watanzania wote. Katiba itakayotokana na michango yetu mbalimbali na kumilikiwa na Wananchi wenyewe, haina budi kutokana na Watanzania wote wenye nia ya kulitakia taifa hili na wananchi amani, upendo na utulivu" amesema Pinda na kuongeza kuwa, Serikali itahakikisha kuwa muswada huo unachapishwa kwa lugha ya Kiswahili na kuusambaza kwa wananchi.

Waziri Mkuu amelieza Bunge kuwa, maandamano yasiyo na tija, fujo, vurugu na migomo havina tija wala manufaa kwa Watanzania na si busara kubeza mafanikio ya Watanzania yaliyopatikana hadi sasa.

Spika amekubali maombi ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kwamba kamati ipewe muda zaidi ili na wananchi wapate muda wa kuufikiria zaidi muswada huo na kutoa maoni yao.

Kamati hiyo hiyo pia imemuomba Spika iandae muswada huo kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi waweze kuusoma wenyewe badala ya kupewa tafsiri tu, na pia ikaomba muswada huo uchapishwe kwenye magazeti na kutangazwa kwenye vyombo vya habari ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi wengi wauelewe na watoe maoni.

Iliomba pia utangulizi wa muswada huo uwekwe vizuri zaidi ili wananchi waelewe madhumuni ya muswada huo kwa kuwa baadhi yao wanadhani kuwa tayari Bunge limeanza kuandika Katiba.

Makinda amewataka watakaochangia muswada huo wajadili mapendekezo badala ya kulumbana, na pia wanasiasa waache kushindana majukwaani.

"Wanasiasa tuache kushindana majukwaani, tujadili muswada. Maoni, ushauri na mapendekezo ndiyo yatasababisha kutungwa kwa sheria nzuri" amesema Makinda na kuwataka watakaotoa maoni waache malumbano na amewaomba Watanzania kudumisha mila zao za utulivu na amani.

Kiongozi huyo wa Bunge amesema, muswada huo si mali ya chama chochote cha siasa na kwamba, huu si wakati wa kulaumiana ila kutoa hoja zenye uzito zinazoweza kusaidia kuandika muswada vizuri.

"Nasisitiza utulivu wakati wote wa kazi hii. Kila mwanakamati ajue kwamba shughuli hii inatawaliwa na Kanuni za Bunge na itaratibiwa na kusimamiwa na kamati husika na siyo vyama vya siasa" amesema. Spika amewaomba wananchi waiamini kamati yake kwa kuwa imejaa watu wenye uzoefu mkubwa na waliobobea katika taaluma mbalimbali ikiwemo ya sheria.

Makinda amesema, wahusika kwenye vyama vya siasa wanapaswa kutumia busara kutoa mawazo yao na wakisema hili liondolewe wawe pia tayari kusema kiwekwe nini badala yake.

"Waheshimiwa wabunge, kupitia kwenu nawaomba wananchi waepuke uandikaji wa muswada kwa kuleta fujo ya aina yoyote ile" amesema Makinda.
Spika wa Bunge ameitaka Serikali iuwasilishe muswada huo kwa lugha ya Kiswahili na uandikwe kwenye magazeti mbalimbali ili wananchi wausome, waulize maswali na waondoe jazba ambazo hazina mantiki.

"Muswada kwa hatua tuliyofikia si wakati wa kulaumu au kulaumiana bali ni kutoa hoja zenye uzito zinazoweza kusaidia muswada mzuri" amesema na kusisitiza kwamba, uandikaji wa Katiba mpya ya nchi uwe chanzo cha kuwaunganisha Watanzania na kuimarisha utaifa wetu kwa kuwa lengo letu ni ni kuwa na Tanzania moja yenye amani na utulivu.
 
Pinda afafanua muswada wa katiba

Thursday, 14 April 2011 19:09 newsroom



Na Joseph Damas, Dodoma
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali imewasilisha bungeni muswada wa marejeo ya mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura ili kukidhi matakwa ya Watanzania. Amesema serikali ina nia njema na wananchi na kwamba, taarifa ya yaliyotokea wakati wa utoaji maoni itawasilishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na baadae atakabidhiwa.
mizengo%20pinda%20good.jpg

Pinda alisema hayo bungeni jana wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu, baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA kuweka bayana kuwa watapinga muswada huo kwa nguvu zote.
Mbowe aliposimama bungeni alipongeza hatua ya serikali ya kuwa sikivu kwa Watanzania kwa kuridhia mabadiliko ya katiba.
Hata hivyo, alisema serikali ilileta muswada huo bungeni kwa hati ya dharura, lakini kumekuwa na malalamiko makubwa, hivyo kuitaka kuuondoa muswada huo.
"Kwa kuwa muswada huu umezua malalamiko mengi kwa wadau na wananchi wamekuwa na hofu, ni kwa nini waziri mkuu usitoe msimamo wa kuridhia kuuondoa muswada huu?" alihoji Mbowe.
Wakati Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ikikusanya maoni ya wananchi kuhusu muswada huo wiki iliyopita mjini Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar, kulizuka vurugu, baadhi ya watu wakizomewa ili kuwazuia wasitoe maoni.
Waziri Mkuu Pinda akijibu hoja ya Mbowe, alisema bado hajapata taarifa kuhusu vurugu hizo.
"Bado sijapata taarifa kwa kuwa kamati itaiwasilisha kwa spika kwanza lakini kama wananchi watataka hivyo, serikali itaangalia na itaridhia. Nia yetu ni njema na hili ni jambo linalotuhusu wote," alisema.
Kuhusu madai ya Mbowe kuwa Watanzania wengi wana hofu, Pinda alisema hakuna mtu mwenye hofu.
"Sioni hofu ya Watanzania iko wapi, hatua tuliyofikia katika kutimiza matakwa ya wananchi ni kubwa na haijengi hofu," alisema.
Wakati huo huo, Regia Mtema (Viti Maalumu-CHADEMA), alihoji ni kwa nini bei ya sukari haijashuka licha ya serikali kutoa tamko kwa wafanyabiashara kuishusha.
Waziri Mkuu Pinda alikiri katika baadhi ya maeneo bei bado haijashuka. Hata hivyo, alisema hilo linatokana na ubinafsi wa wafanyabiashara, ambao hawajali kusaidia wengine na kuweka mbele maslahi binafsi.
Pinda alisema serikali itahakikisha inapambana hadi bei halali ya sukari ya sh. 1,700 kwa kilo iliyopangwa itakapotumika katika maeneo yote nchini.
Awali, sukari ilipanda kwa kasi hadi kufikia kati ya sh. 2,000 na sh. 2,200 katika baadhi ya maeneo. Tangu serikali ilipotoa tamko kwamba bei ishuke, katika baadhi ya maeneo inauzwa kati ya sh. 1,800 na sh. 1,700 kwa kilo.
"Watu ni wabinafsi, kuliko kusaidia wengine wanataka kujinufaisha kwa kupata senti kupitia tatizo hili. Ni changamoto kwa serikali lakini tutaendelea kulipatia ufumbuzi wa kina kwa maslahi ya wananchi," alisema.

Last Updated ( Thursday, 14 April 2011 19:41 )
 
Profesa Maina: Wanasheria wanaokiuka taratibu wanyang'anywe shahada


na Ananilea Nkya


amka2.gif
MWANASHERIA mashuhuri nchini, Profesa Chris Maina, amesema umefika wakati Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanza kufikiria kukopesha shahada kwa wahitimu wake wa fani ya sheria ili atakayejihusisha na jambo la kukivunjia heshima chuo hicho haweze kunyang'anywa.
Kauli hiyo aliitoa wiki hii chuoni hapo katika mhadhara uliojadili hali na mtazamo wa baadaye wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Taaluma ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Profesa Maina alisema katika miaka ya nyuma wahitimu wa sheria kutoka chuo kikuu waliheshimika kwenye jamii ndani na nje ya nchi kutokana na kutumia taaluma yao vyema na kutetea maslahi ya wananchi.
Alisema heshima hiyo imeanza kupungua kutokana na wahitimu hao wa sheria kushiriki katika vitendo visivyozingatia maslahi ya umma.
Alitoa mfano kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya ambaye alihitimu chuoni hapo, Kivuitu, alishindwa kusema ukweli juu ya matokeo ya uchaguzi uliosababisha umwagaji damu wa raia wengi wasio na hatia.
Alisema hata mikataba mingi iliyoigharimu nchi ukiwemo ule wa Dowans, IPTL, Meremeta, Buzwagi na mingine mingi ina saini za wahitimu wa sheria wa chuo kikuu hicho.
"Sitashangaa kusikia kuwa hata huu Muswada wa Marejeo ya Katiba mwaka 2011 unaopingwa na wananchi umetengenezwa na mhitimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," alisema Profesa Maina.
Alisema hata Ujerumani wana utaratibu wa kukopesha shahada na anayeitumia vibaya ananyang'anywa.
 
Mbowe, Lissu walitesa Bunge muswada wa Mahakama


na Bakari Kimwanga


amka2.gif
KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ameitaka serikali kutambua haki na wajibu wake na kukemea kitendo cha mahabusu wa kesi za kawaida kusota rumande huku kesi za vigogo zikisikilizwa hadi siku za mapumziko.
Alisema katika kutenda haki ni lazima wajibu wa mahakama uende sambamba na mtiririko wa haki, ingawa kuna upungufu mkubwa wa majaji, hali iliyosababishwa na serikali kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri.
Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai (CHADEMA), alisema mwaka 2010/2011, Mahakama ya Rufani nchini ilitakiwa kusikiliza mashauri 30 lakini kutokana na ufinyu wa bajeti ilifanikiwa kusikiliza mashauri 18 pekee.
Alisema kutokana na hali hiyo kuwepo na malalamiko mengi hasa kwa kesi wanazotuhumiwa vigogo wa serikali ndizo zilipewa kipaembele.
"Hali ya idara hii ni mbaya lakini kwa Mahakama Kuu walitakiwa kusikiliza kesi 432 , kutokana na ufinyu wa bajeti wamesikiliza mashauri 214, sawa na asilimia 51, ya matarajio na ratiba zao, huku kesi za vigogo zikisikilizwa kwa wakati haki iko wapi nchini," alisema Mbowe.
Kiongozi huyo wa Upinzani bungeni alisema ipo haja kwa serikali kuangalia makusanyo yake ya kodi na kutenga fungu la kutosha kwa Idara ya Mahakama.
Hata hivyo hatua hiyo ya Mbowe, ilimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kusimama na kumtaka kiongozi huyo wa upinzani kuacha kuzungumzia masuala ya maandamano na kesi iliyofunguliwa ambayo inaendelea mahakamani.
Kauli hiyo ya Spika haikumzuia Mbowe ambaye alisema msukumo wa kufanya maandamano huisababisha serikali kusikiliza na kutekeleza wajibu wake kwa wakati.
Katika kujadili muswada huo wa sheria ya utawala wa mahakama, ulichukua sura nyingine baada ya Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, kutoa mapendekezo katika kifungu cha 50 cha sheria ya utawala wa mahakama na kuitaka serikali kuondoa kufungu cha kuwataka wakuu wa mikoa kuwa wenyeviti wa kamati za maadili za mahakimu, hali iliyolifanya Bunge kupiga kura kwa majina.
Spika wa Bunge, alipaza sauti kuita majina, alimwita Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye alipiga kura ya ndiyo kuunga mkono hoja ya Lissu lakini mpaka mwisho hoja hiyo ilishindwa kwa kura za ndiyo 69, huku za siyo zikiwa 152, zilizopigwa na wabunge wa CCM.
 
Tujadili Katiba mpya kwa amani, utulivu

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
JUZI Spika wa Bunge, Anne Makinda, alitangaza kunyofoa kwenye ratiba ya shughuli za Bunge muswada wa sheria ya mapitio ya Katiba ambao kwa kiasi kikubwa ulipata upinzani mkali ndani na nje ya Bunge.
Kwa mujibu wa Spika Makinda, ni kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilitoa maombi ya kupewa muda zaidi kwa lengo la wananchi kupatiwa fursa kubwa zaidi ili watoe maoni yao yatakayosaidia uundwaji wa Katiba mpya.
Kabla ya Bunge kufikia uamuzi huo muswada huo ulipata upinzani mkali na kudaiwa kuwa na kasoro lukuki, ikiwemo kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza ambayo idadi kubwa ya Watanzania hawaielewi hivyo kuwakosesha fursa ya kujua nini kilichomo ndani yake.
Tunapenda kuichukua fursa hii kulipongeza Bunge kwa hatua yake hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa itatoa fursa kwa wananchi wengi kushiriki kwenye mchakato huo muhimu kwa masilahi ya taifa, hasa katika kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi.
Tunaamini kuwa kuahirishwa huko hakutatumiwa na wataalamu wa serikali kufinyanga finyanga muswada huo kama ilivyokuwa awali ambapo kasoro zilizorodheshwa zilionyesha kuwa serikali haikuwa na nia ya kuanzisha mcahakato wa uundwaji wa katiba mpya kama ilivyosema bali ilikuwa na lengo la kufanyia marekebisho.
Tunaliomba Bunge pia libatilishe kanuni inayoainisha maeneo ya wananchi kutoa maoni yao ambayo hivi sasa ni mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar, tunaamini uundwaji wa katiba ni mchakato muhimu zaidi, hivyo ni vema maeneo yote nchini yaruhusiwe kuwa vituo vya kupokea maoni.
Tunaamini wananchi, wanasiasa na wadau wengine wataitumia fursa hii vizuri na kuachana na vurugu, matusi na vitendo visivyofaa mbavyo vilionekana wakati wa utaoji wa maoni kabla ya muswada kutositishwa kujadiliwa bungeni.
Wananchi ni vema wajenge utaratibu wa kuvumiliana, hasa wa kusikiliza mawazo wasiyopenda kuyasikia kwa kuwa kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake ambayo yatachukuliwa na watu waliopewa jukumu la kuratibu.
Tunaungana na kauli ya Spika Makinda kuwa huu si wakati wa kulaumu au kulaumiana, bali ni wa kutoa hoja zenye uzito zinazoweza kusaidia muswada utakaokuwa na masilahi kwa wananchi pamoja na kudumisha muungano ambao tayari kuna watu wameanza kuudodosa kwa madai kuwa Zanzibar walikwisha kubadilisha katiba yao.
Tusingependa kundi la watu fulani wajione wao ndio Watanzania zaidi kuliko wengine, kwa kupanga na kuamua wanchi wafanye nini na waache kipi, taifa hili ni letu sote, hivyo ni vema kila mtu akapewa nafasi ya kutoa mawazo yake kwa namna anayoona inafaa.
Tunaamini kuwa watendaji wa serikali watakuwa wamejifunza matatizo yaliyoonekana wakati wa mjadala wa muswada uliositishwa, hivyo watachukua hatua za kurekebisha kasoro hizo ambazo zilitishia amani, utulivu na mshikamano uliojengeka kwa muda mrefu.
Lengo la uundwaji wa Katiba mpya si kuvuruga amani na mshikamano uliojengeka kwa kipindi kirefu bali ni kutatua upungufu wote unaonekana kuwapo hivi sasa ambapo mambo mengi yamebadilika ikiwemo mfumo wa siasa, ambao sasa ni wa vyama vingi.
Tuna kila sababu ya kuendesha mchakato huu kwa amani na utulivu kwani tukifanya kinyume chake hatutaweza kutimiza lengo letu na kuna hatari nchi ikaingia kwenye vurugu na kupoteza sifa ya kuwa kisiwa cha amani duniani.
 
Warioba wants tolerance in Bill debate

By ABDULWAKIL SAIBOKO, 16th April 2011 @ 14:00, Total Comments: 0, Hits: 95

A former Prime Minister, Justice Joseph Warioba, has called upon political parties to promote tolerance among their members and other Tanzanians, if the country is to achieve a smooth transition in the process of writing a new Constitution.

"Last week's incidents that were characterized by chaos in Dar es Salaam and Dodoma when public debates on the Constitutional Review Bill 2011 were being held, is a clear indication that there was serious intolerance among certain people," he said.


Mr Warioba, who was delivering his keynote address at a public debate on the Constitution organised by the Tanzania Centre for Democracy (TCD) in Dar es Salaam on Saturday said that people should be ready to accommodate divergent views and show tolerance.


"I am not supporting the view that politicians have no role to play in the process. My view is that politicians should play a constructive role by telling their supporters to make constructive contributions in the ongoing debates as the future of this country lies in their hands," he said.


Mr Warioba further hailed the move by the National Assembly to extend the public deliberations on the Bill by giving the Parliamentary Committee on Justice, Constitutional Affairs and Administration more time to work on the Bill.


"The recommendation that the Bill should be translated into Kiswahili language is equally important but it should also go an extra mile to rewrite some of the sections which hinder the public from discussing issues of national interest," he said.


Mr Warioba also explained further that section 9 (10) limits public deliberations on sensitive issues such as the Union, the structure of the government and human rights matters among others.


"We cannot deny members of the public their right to discuss these issues since it is their democratic right, he said.


He added that Sections 19 (4) and 28 (2) give a lot of powers to the Constitutional Review Commission over and above the deliberation of the public and denies politicians and their parties' participation in campaigning for the new Constitution.


In another development, an NCCR-Mageuzi cadre, Dr Sengondo Mvungi, pointed out that the Bill should state clearly that it aims at forming a roadmap in the formation of a new Constitution and not constitution review as it is the case now.


He pointed out further that, the procedures should begin with an amendment of Section 98 of the current Constitution to allow the formation of a Constitutional Parliament and Constitutional Council.


"The amendment will allow fairness in the process of getting a new Constitution as the current parliament, which is formed mainly by members from the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) cannot represent the views of the public objectively," he said.


The Civic United Front (CUF) Secretary General (Mainland), Mr Julius Mtatiro, said his party was against the power of the President in the process indicated in the Bill.


In the debate CCM did not send a representative. The session, which also brought representatives from NGOs, started with uncertainty in the morning as some people were denied entrance with police officers claiming that the gathering was illegal.


The move to table the Bill in the august House for the second reading was postponed on Friday until the next assembly.
 
ni kweli kabisa mkutano wa katiba ndio suluisho la yote kwan selikari wanazan ichi ni kizaz cha analogy,ichi ni kizazi cha digital ambacho kinapambanua mambo na kufuatilia.Tanzania inapoendea cjui kwan kwa sasa vyombo vya habar kama vile radio,television na maghazeti yanaharibu sana habar,mfano tbc ambacho ndio chombo cha umma kionyesha habar za ccm tu ata kama mtu ameludisha kadi yupo lindi ataonyeshwa tu,sasa tunaelekea wap kama taifa?nchi hii sio ya serikali jaman bal ni ya kila mtanzania mwenye cheti cha kuzaliwa,mswada wa katiba ulivyoletwa hakuna chombo ata kimoja kilicho andaa mwanasheria kuja kutoa mapungufu yaliyopo kasolo channel ten ndio kidogo tumeona wameleta mtu ambae alijalibu kuelimisha watanzania waliobahaatika kuona,ivi waandishi wa habar na vyombo ivi vinaishi ktk jamii gan?kwa sasa mchele kilo ni elfu1 na mia6,sukali ni elfu2,maharage ni elfu moja mia5,mafuta ya taa lita ni elfu1 na 800,ivi wenyewe hawaguswi na hili kwel?mm naumia kwan nakumbuka wakat natumwa na mama yangu dukan miaka michache ilyopita bizaa zilikuani mchele na maharage kilo ni 400,sukal500,mafuta lita mia400,ivi tunakwenda wapi?
 
Msekwa: Yafaa spika kuwa mwanasheria, Spika Makinda asema si lazima Send to a friend Wednesday, 20 April 2011 08:03

msekwawetu.jpg
Pius Msekwa

Elias Msuya
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa amesema ni vigumu kwa mtu asiye na taaluma ya sheria kuliongoza Bunge akiwa Spika.Msekwa ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 2000 hadi 2005, aliyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), hivi karibuni akizungumzia utendaji wake akiwa na wadhifa huo. Pia alizungumzia miaka 50 ya Uhuru.

Katika mahojiano hayo, Msekwa alisema alilazimika kurudi shule, kusomea shahada ya sheria ili aweze kuliendesha vyema Bunge.

Kauli hiyo ya Msekwa imekuja wakati Bunge la sasa likishuhudia mivutano ya kisheria baina ya wabunge na Spika wa Bunge hilo la 10, Anne Makinda.

Katika mkutano wa tatu wa Bunge hilo uliomalizika Jumamosi ya wiki iliyopita, Mbunge wa Singida Kusini (Chadema), Tundu Lissu ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba alionekana kuipa wakati mgumu Serikali alipokuwa akipinga kifungu cha sheria kinachowaruhusu wanasiasa kuingilia uhuru wa mahakama.

Katika mvutano huo ambao pia ulimhusisha, Spika Makinda, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alimuunga mkono Lissu licha ya muswada huo kupitishwa.

Katika Bunge la 10 pia kumekuwepo malumbano yanayoashiria wabunge wengi kutozijua vyema Kanuni za Bunge na sheria mbalimbali hivyo kujikuta wakivutana wao kwa wao, wakati mwingine na Spika Makinda.

Hata hivyo, baadaye akizungumza na Mwananchi, Msekwa alirejea kauli hiyo akisema: "Bunge ni la kutunga sheria, kwa hiyo ni muhimu kwa Spika kuwa na taaluma ya sheria."

"Ni kweli walinihoji TBC, ilikuwa ni kuhusu miaka 50 ya Uhuru. Ndiyo lile ni Bunge la kutunga sheria, kwa hiyo ni muhimu kwa Spika kuwa na taaluma ya sheria."

Msekwa ambaye aliwahi pia kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1962-1970, Katibu Msaidizi wa Bunge kati ya mwaka 1960-1962 na Spika wa Bunge kati ya mwaka 2000-2005 alisema suala la Spika kusoma sheria ni la uamuzi binafsi siyo lazima.

"Huwezi kulilinganisha Bunge la wakati wangu na Bunge la sasa. Ni kweli kazi za Bunge ni zilezile, lakini wabunge wa sasa ni wengine. Siyo lazima kwa Spika kusoma sheria, ni uamuzi wa mtu binafsi," alisema na kufafanua:

"Adam Sapi Mkwawa hakuwa mwanasheria, Chifu Mang'enya hakuwa mwanasheria. Hata mimi nilipoanza sikuwa mwanasheria, lakini baadaye niliona umuhimu wa kusoma sheria."

Bunge aliloongoza Msekwa lilishuhudia mawaziri wakilazimika kujiuzulu kutokana na kashfa. Hao ni pamoja na Profesa Simon Mbilinyi, Dk Juma Ngasongwa na baadaye Idi Simba wote hao kutokana na nguvu ya Bunge.
Akizungumzia kauli hiyo ya Msemwa, Spika Makinda licha ya kukiri kutosomea sheria moja kwa moja, alisema uzoefu alioupata Bungeni tangu alipotoka shule ndiyo unaomwezesha kuliendesha kwa ufanisi.

"Nimekulia na kuzeekea bungeni, taaluma yangu ni uhasibu, lakini mimi ni kati ya wabunge wakongwe. Tangu nimetoka shule niko bungeni," alisema.

Alipoulizwa iwapo ana mpango wa kusomea sheria ili kumudu vyema zaidi uendeshaji wa Bunge, Makinda alisema kuwa amesomea sheria katika taaluma yake ya uhasibu ambayo inamsaidia pia kuzielewa Kanuni za Bunge.

"Kwani mimi sijasoma sheria? Mimi ni ‘accountant by professional', (mhasibu kitaaluma) na huko nimesomea sheria. Ni kweli sina ‘bachelor' (shahada) ya sheria, lakini, nina uelewa wa sheria," alisema.
Makinda alijigamba: " Nimekuwa mbunge, 'chief whip' (mnadhimu) kwa muda wa miaka minane, nimekuwa mwenyekiti wa Bunge, yote hayo yamenipa uwezo."

Kuhusu changamoto anazokabiliana nazo katika nafasi hiyo, Spika Makinda alisema kuwa hilo jambo la kawaida kwake, lakini akasema tatizo na jambo kubwa ni wabunge kutokuelewa kanuni.

Hata hivyo, alisema anajitahidi kuwafundisha Kanuni za Bunge ili waendane na mwenendo wake.

"Unajua kipindi hiki wabunge ndiyo wamekuja, wengi wao hawajui Kanuni za Bunge, wanafanya makosa na utundu mwingi. Lakini tutawafundisha kanuni, naamini, Bunge litakuwa ‘smart' siku zijazo," alisema na kuongeza:

"Kwa mfano, sasa kuna kitu kinachoitwa ‘adjoin motion' ambapo mbunge anamtaarifu Spika pale anapokuwa akiahirisha Bunge kuwa ana hoja ya kulitaarifu Bunge, basi Mbunge anapewa dakika 15 za kujieleza. Yote hayo tutawafundisha na wengi wameshaleta maoni ya kufanya hivyo."

Akizungumzia tukio la hivi karibuni ambalo Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje alitoa kauli iliyosababisha wabunge kurushiana maneno, Spika Makinda alisema kuwa tukio hilo lilikuwa ni kinyume cha Kanuni za Bunge.

"Kanuni zinakataza wabunge ku-shout hovyo (Kupayuka). Ile ilikuwa ni makosa. Unajua wabunge bado wanajifunza na tutafanya ‘amendments' (marekebisho) ya kanuni ili kuwawezesha wabunge kuzoea Bunge. Kwa mfano, sasa kuna kitu kinaitwa "Committee of supply," yaani wakati wa mbunge kutoa shilingi Bungeni. Hilo nalo tutawafundisha ili waelewe," alisema.
 
Miaka 47, Muungano wetu unaumwa mno!
ban.blank.jpg


Joseph Sabinus​

amka2.gif
ILIKUWA Aprili 26, 1964, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kwa sasa hayati), akachukua udongo wa Tanganyika na ule wa Zanzibar; akachanganya pamoja ishara ya Muungano.
Sote tukawa kitu kimoja kama kidole na pete. Wote tukamuomba Mungu tukisema, "Muungano udumu Tanzania iende mbele".
Ndipo sasa ikazaliwa Tanzania ambayo ni tunda la Muungano wa Tanganyika (Tanzania Bara) na Zanzibar (Tanzania Visiwani). Wanaopenda kuiga, wakaiga, lakini wengi kama sio wote; wakashindwa maana sio jambo la mchezo kuunganisha nchi mbili kuwa moja.
Hili likaashiria hata kwa asiyetaka kuona ukweli kuwa Watanzania ni wamoja na watu wa amani kwa asili yao, maana hata tausi hahitaji mapambo ili urembo wake uonekanae.
Kuungana kwa nchi tu, hakukutosha, busara za viongozi na Watanzania wakati huo, zikawasukuma kuunganisha hata vyama vya Afro Shiraz Party (ASP) cha Visiwani Zanzibar na Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika na ndipo zao la muungano wa vyama hivyo vya siasa likawa kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Februari 5, 1977.
Zimepita siku, miezi miaka na sasa tunazungumzia miongo; kelele na manung'uniko ya kichinichini zinapenya masikioni.
Baadhi ya watu toka kila upande wanaona upande fulani unanufaika kuliko mwingine. Watanzania si haba; wa Visiwani na wa Bara; wanalitazama kinyume Lengo la Nane la Milenia linalozungumzia ushirikiano kama sio ubia (partinership) duniani.
Watanzania hao kwa kazi ya mikono na midomo yao, wamehakikisha "wanaubemenda" Muungano na sasa Muungano wetu unaumwa kwelikweli; uko mahututi ingawa najua wasiotaka ukweli watasema huo sio ukweli.
Muungano wetu unaolifanya taifa hili kuitwa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania; uko hoi katika chumba cha wagonjwa mahututi wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU). Muungano umesulibishwa hadi sasa unafikia hatua ya kukaribia ‘kukata kamba' japo bado wengi wanautaka huku mataifa mengine yakiutamani.
Ugonjwa wa Muungano huu ulianza kuonekana pale ambapo baadhi ya watu ama kwa nia mbaya au kwa nia njema, walipoanza kuhoji uhalali wa kuwa na serikali mbili ndani ya Muungano yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayohusisha Tanzania Bara na Tanzania Visiwani; pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inayohusu Tanzania Visiwani pekee.
Miongoni mwa Watanzania ambao wamekuwa wakipinga suala hilo la kuwa na Serikali mbili badala ya moja au tatu, ni Mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila ambaye amekuwa akidai na kupigania suala la kuwapo Serikali ya Tanganyika; kwa maana kuwa Tanganyika iwe nchi inayojitegemea.
Watu wengine wamekuwa wakisema kwa vile Tanganyika na Zanzibar zimeungana, hakuna sababu ya kuwa na utitiri wa serikali, bali serikali moja tu, inatosha yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ingawa umuhimu wa Muungano unajulikana kila mahali hasa kwa nchi changa kama Tanzania ambayo inahitaji nguvu ya pamoja na kukimbia huku wengine wakitembea, Muungano huu wa Tanzania sasa umekuwa mithili ya mkia wa ng'ombe ambao ng'ombe mwenyewe hajui umuhimu wake hadi unapokatika.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, mwanzoni mwa mwezi Aprili 2011 alizungumza na waandishi wa habari na kusema, "Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yanafanya hoja ya kuwa na Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ya muhimu na ya lazima kujadiliwa sasa."
Mbatia anaongeza, "Kwa kuzingatia kwamba Zanzibar imekwishajitangaza kuwa ni nchi na imekwishamchagua Mkuu wa nchi (Dk. Ali Mohamed Shein) lazima sasa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itambue mabadiliko hayo makubwa ambayo yatapelekea Tanganyika kutangazwa rasmi kuwa ni nchi."
Kwangu mimi binafsi, vikao vya kutafuta mwafaka vilivyokuwa vikifanywa kwa faragha baina ya viongozi (baadhi) wakuu wa vyama vya CCM na CUF, vimechangia kuujeruhi na hata kukaribia kuua Muuungano wetu jambo linalotufanya Watanzania wa sasa tusibanduke katika kizimba cha mahakama ya vizazi vijavyo vitakavyotuhukumu kwa historia.
Huu ni Muungano uliotuunganisha kwa historia; Muungano ambao mataifa mengine yanautamani lakini yasijue namna ya kuupata maana wakati wewe unasema wa kazi gani, wengine wanasema wataupataje.
Katiba ya Zanzibar, Ibara ya Kwanza, imecharuka na kusema bayana ikisisitiza kuwa, Zanzibar ni nchi. Katiba hiyo siyo siri, ‘imeibaka' Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuizidi nguvu hali inayoilazimisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema Tanzania ni eneo lote la maji na nchi kavu la Tanganyika na Visiwa Unguja na Pemba (Zanzibar), ifuate matakwa ya Katiba ya Zanzibar, badala ya Katiba ya Zanzibar kufuatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mabadiliko hayo ya Katiba ya Zanzibar yameufanya Muungano wetu ambao Jumanne ijayo (Aprili 26, 2011) unatimiza umri wa miaka 47, uwe mithili ya ‘maiti anayetembea'; upo lakini umechoka na kujeruhiwa kwelikweli.
Watanzania wenzetu wameuua Muungano na imebidi ufe ukiwaangalia kwa macho ya huruma kama kifo cha dagaa kinavyohitaji huruma wa mvuvi na mlaji.
Kwangu mimi binafsi, naona huenda mabadiliko hayo ya Katiba hayakuwa yakilenga kutafuta mwafaka wa kisiasa Visiwani humo kama ilivyokuwa ikifahamika, bali kwamba kumbe yalikuwa yanatumia mwafaka wa kisiasa kuficha makucha ya kuurarua Muungano huo wenye tija kwa Watanzania wote na hata usio na kosa kwa mtu, nchi wala mbele ya Mungu.
Inauma mno maana viongozi niliowategemea kuunganisha nguvu na kuufanya Muungano wa Tanzania kuwa imara na wenye kudumu, wametumia akili na mikono yao wenyewe kuujeruhi huku moja kwa moja wakijua mabadiliko wanayoyafanya yanakwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sijui na ninasisitiza kwamba sijui kama kweli labda hata baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulibaini hilo, ndiyo maana hakuwa na lingine la kufanya bali tu, kutangaza kuwa huu ni mwaka wa Katiba maana tayati mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ‘yamelikoroga' hivyo, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ama inapenda, au la, lazima itii matakwa ya katiba ya Zanzibar ambayo tayari imetangaza kuwa Zanzibar ni nchi.
Kama hivyo ndivyo kwamba Zanzibar ni nchi, Tanzania ni nini sasa? Tanganyika nayo iitweje? Ndiyo maana ninasema, Muungano wetu unaumwa mno.
Muungano unaumwa hata hakuna ajuaye Maadhimisho ya Siku ya Muungano mwaka huu yatakuwa yanatafakari na kuakisi kitu gani, kuzaliwa kwa Muungano au kuuawa kwa Muungano!
Siyo siri, kwa Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi na hata kumchagua Mkuu wa nchi, tayari Katiba ya Zanzibar imeyapora madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndiyo maana Mtaalamu wa Katiba na Mambo ya Sheria, Dk. Sengondo Mvungi anasema, "Huu ni uhaini wa waziwazi."
Anaongeza kuwa, "Ni uhaini, lakini uhaini mtakatifu maana umewawezesha Watanzania wa Bara kurejesha Tanganyika yao bila jasho; yaani wamerudishiwa Tanganyika yao."
Inauma maana sasa ni vigumu kujua Rais wa Tanzania (Mfano, Jakaya Kikwete) akienda katika sherehe huko Zanzibar, nani anatangulia kuingia au kutoka uwanjani, au la! Ikifika hatua kwa mfano, Dk. Shein akatangulia kuondoka uwanjani au ukumbini huku Kikwete akitangulia kuingia ukumbini au kuwasili uwanjani, vipi tuseme bado tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, badala ya kusema kuna shirikisho? Bado yangu macho kutafuta jibu la kitendawili hiki.
Ingawa inauma; tena inauma kwelikweli, hakuna ujanja, tutake tusitake, tukubali au tusikubali tayari Muungano wetu unaumwa na uko chumba cha wagonjwa mahututi! Chenye afya njema kwa sasa ni Tanzania kuitwa shirikisho la Tanzania, badala ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tangu lini nchi zilizoungana zikawa na marais wawili, serikali mbili, mabunge mawili na katiba mbili zinazotofautiana kauli?
Mungu ibariku Tanzania



h.sep3.gif

sabinus55@yahoo.com na 0788 007070
 
Back
Top Bottom