Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Tundu Lisu asusia mkutano Dar Send to a friend Saturday, 09 April 2011 09:06

Geofrey Nyang'oro
MJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Tundu Lisu, jana alitoka ndani ya ukumbi wa mkutano kuhusu mjadala wa maoni wa muswada wa sheria ya mapitio ya katiba, kwa madai kuwa kulikuwa na kundi la watu waliokodiwa kuvuruga mchakato huo.

Lisu alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutoka nje ya kumbi wa mikutano wa Karimjee, kufuatia kuwapo kwa kundi la watu waliokuwa wakuzomea wachangiaji wa mjadala.Akiwa nje ya ukumbi huo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kundi hilo lilikodiwa na CCM kwa lengo la kuvuruga mchakato huo, ili usifanikiwe.

Tundi pia aliwatupia lawama polisi katika Kanda Maalamu ya Dar es Salaam, kuwa wamekuwa katika katika eneo hilo, kwa lengo la kulinda kikundi hicho kilichokuwa kinafanya kazi ya kuzomea wachangiaji, waliokuwa wakikosoa muswada.
"Jana (juzi)tulikubalina kwenye kikao cha kamati kuwa ulinzi katika mkutano wa leo (jana) ungeimarishwa na mtu yeyote atakayebainika kuwa anazomea au kuzuia maoni ya watu wengine kutolewa, polisi wangemtoa nje ya ukumbi, lakini kinchofanyika leo ni tofauti kwa sababu polisi wanawalinda wanaofanya vurugu," alisema.

Lisu pia alipinga muswada huo kwa maelezo kuwa una mapungufu mengi na kwamba hakuna
sababu ya kuupeleka bungeni kujadiliwa, kwa utumia hati ya dhararu.

Kwa mujibu wa Lisu, muswada huo ulipaswa kufuata njia ya kawaida ya kutunga sheria na si kwa hati ya dharura.
Alisema haiwezekani kwa muswada ambao ni mali ya wananchi na roho ya taifa, kujadiliwa ndani ya siku tatu na kupitishwa.

Alisema sababu nyingine ya kupinga muswada huo, ni vipengele vilivyopo ndani yake ambavyo alisema kwa maoni yake, vinakandamamiza uhuru wa watu kushiriki katika kutunga katiba.Alisema kwa hali ilivyo, mjadala huo ulioandaliwa kwa siku chache hautakuwa na manufaa kwa wananchi na kwamba badala yake, utatengeneza manung'uniko kwa wananchi.

Alipoulizwa kuhusu hatua ya Lisu kutoka nje ya ukumbi, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Pindi Chana, alisema hawezi kulizungumzia hadi kwanza apate sababu zilizomfanya kufikia uamuzi huo."Mimi muda huu siwezi kuzungumza chochote mpaka niwe na ushahidi wa kile kilichomfanya atoke ndani ya ukumbi wa mikutano,"alisema Chana.
Katika mjadala huo wadau mbalimbali waliochangia walipinga baadhi ya vipengele vya muswada kwa maelezo kuwa vinavunja katiba ya sasa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanznaia.
 
Zanzibari wachana muswada wa katiba Send to a friend Sunday, 10 April 2011 07:50

Waandishi Wetu, Dar na Mikoani
MJADALA wa Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba wa mwaka 2011 umeendelea kuibua mambo mazito, baada ya wananchi Zanzibar kuchana nakala za muswada huo mbele ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na kudai kuwa wapewe katiba ya Tanganyika kwanza.

Kitendo hicho kilichokuwa kifanyika mitihili ya filamu, kilitokea wakati wa mkutano wa kujadili muswada huo katika ukumbi wa Shule ya Haile Sellasie, mjini Zanzibar.

Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed alianza kuichana na baadaye wananchi wengine walifuatia huku wakidai waonyeshwe kwanza Katiba ya Tanganyika na kufanyika kura ya maoni kuhusu uhalali wa Muungano.

Kabla ya kuchana muswada huo, Sheikh Faridi alisema hauna faida kwa Wazanzibari na kwamba haukuzingatia hadhi ya Zanzibar.

Kabla ya kuuchana Sheikh huyo aliwauliza wananchi waliohudhuria mkutano huo akisema, "Huu mswaada mnautaka?."

Wananchi wakajibu kwa sauti kubwa," Hatuutaki huu mswaada". Akawauliza tena nao wakajibu kuwa hawautaki.

Baada ya kuwahoji na kupata majibu hayo akamgeukia, Mwenyekiti wa kikao hicho, Jadi Simai Jadi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano aliyekuwa meza kuu na viongozi wengine akiwemo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na kusema:

"Waheshimiwa mnasubiri nini tena, kama mnataka tuonyeshe kivitendo hatuutaki, basi ndio hivi…"

Baada ya maneno hayo Sheikh Farid alichanachana nakala yake ya muswada aliyokuwa nayo mkononi, huku wananchi wengine waliokuwa katika ukumbi huo nao wakichama nakala zao.

Mkutano huo ulipangwa kumalizika saa nane mchana, lakini ilipofika saa saba Sheikh Farid alisema hakuna haja ya kuendelea na mkutano huo, huku baadhi ya wananchi wakiwataka wenzao waondoke katika mkutano huo wakidai kuwa hakuna faida kwao.

Awali, akiochangia mjadala huo, Sheikh Farid alisema alijaribu kufutalia mchakato wote wa muswada huo, akabaini kuwa taratibu nyingi hazikufuatwa, hivyo hakuna sababu ya kuendelea kuujadili kwa vile hauna maana kwao.

"Hapa tumesikia kelele nyingi sana, kwa hivyo ilikuwa inatosha tutawanyike. Sasa tunakwenda katika kujadili marekebisho ya Katiba ya Tanzania, lakini swali ni je, Katiba ya Tanganyika mnayo hapa? Huo muungano uko wapi hapa na kipi cha kipi cha kutangulizwa? Kwanza kafanyeni Katiba ya Tanganyika," alisema Sheikh Farid na kushangiliwa na wananchi waliohudhuria, huku Waziri Sitta na viongozi wenzake wakimwangilia.

Sheikh Farid alisema lazima uamuzi wa wananchi uchukuliwe na kwamba, hakuna sababu ya kuwalazimisha kitu wasichokitaka.

"Natoa wasia wangu kwa Serikali ya MapinduziZanzibar na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuwa, tunataka kura ya maoni na tuulizwe kama Muungano tunautaka au hatuutaki?" alisema huku akishangiliwa kwa na kuongeza, " Muungano huu hatuutaki."

Baada ya wananchi kuonyesha kutoheshimu utaratibu wa kikoa kwa kupiga makelele ya kuwa hataki muswada, Mwenyekiti Jadi aliamua kuuvunja na kuwataka wananchi waondoke kwa usalama.

"Sasa mkutano wetu utakuwa umemalizikia hapa maana naona hali ya usalama inaweza kutoweka. Kwa hivyo nasema kwamba, tunafunga mkutano huu," alisema Jadi, huku wananchi wakitoka na kuimba kwa sauti za hadi nje ya ukumbi akisema hawautaki Muungano.

"Muungano hatuutaki..., muungano hatuutaki..., tunataka kura ya maoni... tunataka kura ya maoni…," walisikika wakiimba baadhi ya wananchi huku wengine wakiwa wamebeba mabango ya karatasi yaliyokuwa yameandikwa, "hatutaki muungano, Saya na wabunge wenzako rudini Zanzibar tudai takala".

Nassor Moyo

Akiongea katika mjadala huo juzi jioni, Muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo, ambaye alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba wakati wa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, alisema kuwa amekuwa shahidi wa makubaliano hayo muungano na hakuna asichokifahamu.

Hata hivyo, alisema suala la wananchi kupewa uhuru wa kujadili muungano wao lipewe nafasi kubwa.

"Mnatuambia tusizungumze suala la Muungano, mnataka tuzungumze nini hapa wakati hilo ndio jambo la msingi, mnataka tuzungumze nini? Hili ndio jambo tutakalolizuingumza," alisema Nassor Moyo.

Alisisitiza kuwa kosa walilofanya wakati wa kupitisha uamuzi kuzinganisha nchi hizo bila ya kuwashirikisha wananchi lisirudiwe tena, ikizingatiwa kua hivi sasa vijana wamesoma siyo wajinga kama walivyokuwa wakati wao.
"Nilikuwa Waziri wa Sheria wakati huo, mambo haya ni 11, lakini hivi sasa yameongezeka, naambiwa yamefikia mpaka 30. Haya yote yaliongezwa na wenzetu Bara," alisema Moyo huku akionyesha nakala ya makubaliano hayo ya muungano.

Alionya kwamba watafanya makosa kuzuia mambo ya Muungano yasijadiliwe na Wazanzibari katika katiba mpya.

" Wananchi wapewe nafasi waseme kwani hili nalisema kutoka ndani ya moyo wangu. Nyerere alikuja Zanzibar na karatasi ina mambo 11, mimi nilikuwa Waziri wa Sheria alinipa faili na hakuna hata sentesi moja iliyotolewa, leo tunaambiwa kuna mambo 22, sasa mnaposema tusizungumze mambo ya Muungano maana yake nini, mnawaambia nini Wazanzibari," alisema Moyo.

Mzee Moyo ambaye alifika na nakala ya hati ya makubaliano ya Muungano alisema mambo waliyokuwa wameafikiana Nyerere na Mzee Abeid Karume wakati huo yameweza kuheshimiwa na viongozi wengine kulingana na wakati, lakini kwa sasa vijana hawawezi kupangiwa mambo kama ilivyokuwa huko nyuma.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari, alisema utaratibu uliotumiwa kuandaa muswada huo na Serikali si sahihi kwa kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar haikushirikishwa wakati wa kuandaa wa rasimu hiyo.

Alisema licha ya kutowashirikishwa, Serikali ya Zanzibar kupitia Mwanasheria Mkuu wake iliandika barua kupeleka Serikali ya Muungano kuhusiana na suala hilo, mpaka sasa haikujibiwa licha ya kupokelewa.

Alisema walipeleka mapendekezo yao 14, lakini ni mambo mawili pekee ndio yaliyoingizwa katika rasimu hiyo na mambo mengine manane yameongezwa kinyume na makubaliano.

Chama cha wanasheria

Wakati hayo yakitokea Zanzibar, Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara (TLS), kikimtaka Rais Jakaya Kikwete kuondoa hati ya dharura katika muswada huo wakidai uma kasoro nyingi mno.

TLS iliyofanya mkutano wake jana jijini Dar es Salaam ilisema haikubalina na muswada huo.

Rais wake Francis Stolla alisema, "Kwa maudhui yake tu, huu muswada ni mzuri kwa kuwa unazungumzia kuwa na Katiba mpya, hii inaonyesha kuwa nchi ina utashi wa kisiasa. Lakini muswada huu una upungufu mwingi sana, unaoufanya usiwe tayari kupelekwa bungeni," alisema Stolla na kuongeza:

"Sisi hata hiyo hati ya dharura hatujaiona, kwa hiyo bado tunajiuliza kuwa ni kwa nini Rais ameamua kuupeleka muswada huu bungeni kwa hati ya dharura.

Tunamshauri Rais Kikwete kuondoa hati ya dharura iliyoambatanishwa na muswada huu, ili ufuate utaratibu wa kawaida kuufikisha bungeni na wadau wengine wapate fursa ya kuuchambua.

Aliongeza kuwa, licha ya TLS kutoa maoni yake kwa kamati inayokusanya maoni ya wadau juu ya muswada huo na jana kuweka wazi msimamo wao, watakutana na Rais Kikwete kumshauri mambo mbalimbali ya kisheria ikiwa pamoja na suala hilo la muswada wa sheria uliopewa jina la Muswada wa Mapitio ya Katiba 2011.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu muswada unaopelekwa bungeni kwa njia za kawaida, baada kutungwa hujadiliwa na wadau kwa muda wa miezi sita, kisha huwasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge.

Lakini tofauti na hali hiyo muswada huo wa Sheria ya Mapitio ya Katiba 2011, ulitangazwa na Serikali Machi 11 mwaka huu na kuwasilishwa kwa Kamati ya Bunge ya Sheria isivyo rasmi Machi 29 na kusomwa bungeni kwa mara ya kwanza Aprili 5 mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Aprili 7 na 8 kamati ilianza kukusanya maoni ya wadau.

Stolla alisema TLS inaitaka Serikali kutoharakisha mchakato wa muswada huo, badala yake watu wapate nafasi ya kuujadili, pia kuiga mambo mazuri kutoka kwa nchi ambazo zimepata katiba mpya hivi karibuni kama vile Kenya na Uganda.

Edwin Mtei

Wakati hayo yakiendelea, muasisi wa Chadema, Edwin Mtei ameibuka na kuiponda Serikali ya CCM kuwa inalipeleka kwa haraka suala la muswada wa katiba mpya ili kulinda maslahi yake binafsi na si ya umma.
Ê
Mtei aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu (BoT), alisistiza kuwa chama chake kitaidai katiba mpya kwa gharama yoyote

Mjini Dodoma mwitikio wa wananchi kuhudhuria mkutano kutoa maoni ya muswada huo umekuwa hafifu katika ukumbi wa zamani wa Bunge wa Pius Msekwa.

Wakitoa maoni yao kuhusu muswada huo, watu hao walishari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), isihusishwe katika ukusanyaji na upigaji wa kura za maoni wakidai kwa kuwa imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya vyama vya siasa kuwa hatendi haki

Fredy Azzah, Dar, Salma Said, Zanzibar, Moses Mashala, Arusha, Israel Mgusi, Dodoma
mwisho
 
Comments

#4 rutashubanyuma 2011-04-10 19:25 What I see are the last days of CCM and like KANU among others it will try to regroup, reconfigure and rediscover.........but the truth remains CCM has outlived its mission statement which waa ..............Kuwahadaa watanganyika or should I reveal wadanganyika kujitawala.................
Quote

0 #3 Babu 2011-04-10 19:19 nawapongeza wale wote waliochangia kabla yangu, ndugu watanzania wenzangu tukumbuke kuwa, Tanzania ni muungano wa nchi mbili TANGANYIKA NA ZANZIBAR, sasa iweje leo mapendekezo ya kitu muhimu kama katiba kijadiliwe upande mmoja tu? hawa wengine matahira au? au mazuzu? au tuseme hakuna kinacho wakera?, kuchanwa kwa mswada mbele ya mh. sita ni ishara tosha kwamba wazanzibari wako tayari kupinga ukandamizi unaofanywa na serekali ya ccm, tusipo ziba ufa tutajenga ukuta..............
Quote

0 #2 shaban kashingo 2011-04-10 16:50 hivi kweli hii serikali yetu ni sikivu kama ni sikivu kweli basi ikubali tu kwamba huu muswada haukubaliki kwa wananchi waliowengi kwani mapungufu yake ni makubwa mno
Quote

+2 #1 simon john 2011-04-10 10:10 Katiba ndio dira ya Taifa lolote duniani. Katiba inalinda maslahi ya Taifa na watu wake wote na sii chama ama [NENO BAYA] fulani. Katiba inatoa mwelekeo wa namna raslimali za nchi zitakavyotumika kwa manufaa ya Taifa. Sasa katiba inachukuliwa kama chombo cha kulinda maslahi ya kundi chache la jamii ama watu. Nashauri tuvue tofauti za kiitikadi tuingie kwenye mchakato ulio wazi wa kuandaa katiba kwa manufaa ya Watanzania. Katiba isije ikawa ni chanzo cha vurugu. Mungu ibariki Tanzania, kemea viongozi wanafiki.
Quote
 
Udini wapenyezwa madai ya katiba

Na Heckton Chuwa, Moshi

SIKU chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) kutangaza maandamano ya nchi nzima kupinga mchakato unaoendelea wa muswada wa
katiba nchini, kundi moja la wasilamu limeonya uamuzi huo usifanyike Dar es Salaam kwa madai ya kwamba una agenda ya kumng'oa Rais Jakaya Kikwete ikulu.

Onyo hilo limetolewa na Amir wa Vijana wa Kiislamu, Shekhe Shaban Mapeyo, wakati akihutubia kongamano la waislamu lililofanyika mjini Moshi, mkoani
Kilimanjaro, jana.

"CHADEMA wamekuja na agenda mbalimbali wakidai ni za kisiasa na wengi tumeamini hivyo, ukweli ni kwamba wana agenda ya siri wao na maajenti wao tangu mwanzo kwa
njia mbaalimbali kama vile Dowans na sasa wameikomalia hii ya katiba mpya, hili waislamu tusilikubali wakija huko mikoani wakataeni.

"Sisi Dar es Salaam tunawasubiri watakutana na nguvu za wenye historia ya Tanzania," alisema Shekhe Mapeyo huku akishangiliwa na umati wa waliohudhuria kongamano hilo.

Alisema agenda ya katiba inayotumiwa na CHADEMA kwa madai ya kutumia nguvu za umma ni danganya toto, lengo halisi ni kumng'o Rais Kikwete ikulu na kwamba waislamu watapambana kwa hali na mali kuzuia uovu huo kwa niaba ya Watanzania wote.

Shekhe Mapeyo alisema kuwa waislamu wamekuwa wakinyamaza kwa kila jambo wakati ajenda zikiibuliwa na vyama mbalimbali vya siasa lakini kwa sasa wameamua kusimama
kidete baada ya kuona CHADEMA wamekuja na ajenda ya kutaka 'kuhatarisha amani ya nchi'.

Sheikh Mapeyo alisema, "Meseji zimesambazwa zinazohamasisha watu wajiandae kumng'oa Mujahidina Ikulu na sisi tunajiuliza Rais Kikwete ni Mujahidina tangu lini? Maana sisi tunachojua ni kiongozi wa wananchi wa Tanzania anayefanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa," alisema Sheikh Mapeyo.

Kuhusu madai ya CHADEMA kuwa wanahangaikia katiba mpya kwa niaba ya Watanzania wote, Sheikh Mapeyo alisema kuwa huo ni uzushi kutokana na jinsi viongozi wa chama hicho
wanavyotaka katiba hiyo ipatikane kwa haraka tena ndani ya miezi sita tu.

"Jamani mchakato wa kutafuta katiba mpya si mwepesi na wa haraka tena kwa miezi sita tu kama wanavyotaka wenzetu hawa, nia yao hii ni hatari kutokana na umuhimu wa katiba ya nchi; katiba inayopatikana kwa muda wa miezi sita ni ya nchi ya watu waliochanganyikiwa, kunahitajika umakini wa hali ya juu kwenye swala kama hili," alisema.

Kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya CHADEMA iliyonadiwa na mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa mwaka jana, chama hicho kilipanga kuanzisha mchakato wa kuandaa katiba mpya ndani ya siku 100 (siku 100).

18 Maoni:
 
18 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... UZUSHI WA MWANDISHI. JE HUJAMUONA IMAMU WA ZANZIBAR AKIICHANA RASIMU YA KATIBA? WAISLAMU TUNATAKA KATIBA MPYA NA ITAYOANDIKWA NA WANANCHI NA SI WANASIASA. CCM NA CHADEMA HAWANA TOFAUTI WANAGOMBEA UONGOZI KUWEZA KUNUFAISHA BIASHARA ZAO IKULU. WAANDISHI KAMA NYIE MLIOEGEMEA UPANDE MMOJA NDIO HATARI KWA NCHI NA SIO WAISLAMU. MTAYARISHAJI WA RASIMU YA KATIBA NI MWANASHERIA MKUU AMBAYE NI WEREMA AKISHIRIKIANA NA WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA KOMBANI WOTE HAWA NI WAKIRISTO. WEWE MUANDISHI USILETE MAMBO YA KIJINGA HAPA,WAACHENI MASHEIKH,MAPADRI,MAASKOFU NA MADHEHEBU MENGINE WASEME,HICHI NDICHO TUNACHOKATAA KWENYE RASIMU YA KATIBA KUPANGIWA YA KUSEMA.HIYO KATIBA NDANI YA SIKU MIA NI YA WANANCHI AU YA MBOWE,SLAA,NDESA NA MTEI? HATUTAKI WANASIASA WATUTUNGIE KATIBA. TAYARI NYUSO ZAO ZIMEISHAONDOKANA NA UBINAADAMU KUTOKANA NA TAMAA YA MADARAKA NA UTAJIRI NDANI YA SIASA. TUNAPENDA MTU MUADILIFU,MCHA MUNGU NA ANAYEISHI MAISHA YA KAWAIDA SANA NA FAMILIA YAKE KAMA ILIVYOKUWA ENZI ZA KINA NYERERE. AHSANTE SANA MBATIA NA NCCR MAGEUZI KWA KULITAKA BUNGE LIBADILISHE KIPENGERE CHA KUANDIKWA KATIBA ILI KATIBA ITUNGWE NJE YA CHOMBO HICHO ILI TUWEZE KUWADHIBITI.
April 10, 2011 11:29 PM
blank.gif

Anonymous said... Hawa CDM wao wanajifanya kila jambo wanalivalia njuga, na kulifahamu fika na kujifanya wana uchungu sana na nchi hii lakini hizi ni sera maalumu za kuwarubuni watu na ni waongo na wazandiki. Ninakubaliana na maneno ya Ngawaia wkt wa NCCR akiwa na Mrema kuwa hata wao walikutana na huo mtandao wa kufanya vurugu ili wananchi waichukie Serikali iliyo madarakani na wanalipwa hela nyingi sana maana hao ni wenye pesa chafu hazina kazi wao starehe yao ni kuona watu wakipigana wenyewe kwa wenyewe na kukuuana, Sera zao inakuwa maandamano na kupinga hata likiwa jema ndio kazi yao tuwe makini na tuamke hawa ni wanafiki na hawafiki mbali.Angalieni Tunisia,Somalia,Egypy Yemen,Syria na hata huko Libya ni haohao kuuondoa uongozi halali uliopo madarakani,na hapa utaona leo wamedai katiba,inataka kuanza mchakato wanaandamana,ikiteuliwa hiyo kamati pia wataipinga na kuandamana ikija kujadiliwa pia wataandamana na ikicheleweshwa kupitishwa pia wataandamana na mwisho lengo lao litimie TUWE MAKINI NA HAWA WENYE UCHU NA TAMAA YA MBWA MWITU
April 10, 2011 11:46 PM
blank.gif

Anonymous said... Kama hali ndiyo hii ya dini kuingia kwenye siasa tanzania tunakwenda wapi? waislam kama huyu sheik wao wametuchosha sana na hawafai katika jamii ya usasa, tunajua kuwa wanatumiwa na CCM ili kumlinda mwislam mwenzao ambaye amedhihirisha wazi kuwa hana uwezo wa kuongoza nchi. Labda hili hawalijui, Hapa hatuna Rais bali tuna Mkaazi wa IKULU TU.
April 11, 2011 12:30 AM
blank.gif

Miyango said... Kwan wanayoyalalamikia chadema uongo?sasa ule muswada gan acha uchanwe..kuhusu kupewa pesa na wamerekan ni bora waongezewe kabisa hata wangepewa na shetan ilimradi wanayoyapigia kelele ni mazur kwa wananch its okey..ccm wasipopelekwa puta wanajisahau sana na kutuona watz *******.hata sio ishu ya kikwete hapa ni ccm hao waislam nao siwaamin watakuwa ccm na sio waislam..mana 2po waislam lkn ha2na wawazo hayo..kwanza watanzania ADUI YETU MKUBWA SI DINI FULANI WALA KABILA FULAN BALI ADUI YETU NI UFISADI. Saa ya ukomboz ni sasa 2sikubali kugawanywa.
April 11, 2011 12:52 AM
blank.gif

Anonymous said... Mwenye macho haambiwi tazama na ukiwa ndio unaamka basi hujachelewa osha uso wako kuwa tayari kwa chai,hii hali ni mpango maalumu wa kutaka kumng`oa kikwete kwa njia ya maandamano,kinachosubiriwa hapo ni kupitishwa katiba haraka haraka ili aweze kushtakiwa,ikiwa mmeamka basi hongereni la ikiwa bado mpo katika ndoto oh poleni sana.hapo yoyote yule mwenye jina la kiswahili basi ni adui tu ila akikaa mwenye jina la kizungu huyo ni mzuri hata afanye baya kiasi gani!hebu tazameni mfano hai kwa rais mstaafu wa awamu ya pili au mmesahau nyie wadanganyika!amkeni sasa sio kulala tu na kulalamika.Mungu tuepushe na vyama vyenye mtazamo wa UDINI kama hivi vya chaga na vingine.
April 11, 2011 1:54 AM
blank.gif

Anonymous said... Lakini kwanini hawa jamaa wanakurupuka siku zote? Au hawana vichwa? Mbona inaonesha uwezo wao wa kuchambua mambo ni mdogo? Wao siku zote ni kuchanganya mada tu.Nawashauri wawe wanasoma na vitabu vingine vya kuwasaidia kubrashi bongo zao siyo kun'gan'gana na kile kitabu kimoja tu,hakiwajengi.Hasa wale wanopendelea kutoa mawazo yao hadharani.
April 11, 2011 2:34 AM
blank.gif

Anonymous said... oh!!! poleni sana watanzania wenzangu kwani binafsi nimeona bora niseme kwa sababu naona hali si nzuri kwa nini tunapenda kuamini kila kitu bila kukifanyia uchunguzi kama hili suala la UDINI hili suala lilikuja tena kupitia viongozi wetu wa juu serikalini bila uchunguzi wowote kwamba ni kweli au si kweli tumeanza kukurupuka nalo oh dini oh mara kabila tunakwenda wapi bila hata aibu vijana nao wamejikita wakisema kile ambacho mkuu wa nchi alisema jamani vijana hapa tukisema tuende kidini itakuwa hatari maana tukisema upande wa shule kuna shule za wakristo nyingi hata waislamu wanasoma upande wa hosipitali hivyhivyo kwa hiyo hapa vijana wenzangu cha msingi nikuangalia jinsi ya kujitoa ktk huu umaskini ulio ikumba nchi yetu na si malumbano ya UDINI
April 11, 2011 3:02 AM
blank.gif

Anonymous said... Kuna watu wanauchafua Uislam. Wanautumia kama Idara ya CCM. Wameangukia kwenye propoganda ya CCM dhidi ya CHADEMA. Wanadanganywa kuwa mtu hawezi kuwa dhaifu ila kwa sababu ya dini yake. Tuseme basi hata Makamba anaandamwa kwa sababu ya Uislamu wake? au Lowasa alijiuzulu kwa ajili ya kuandamwa na waislamu? Tuache kufanywa wajinga, tufikiri kwa vichwa vyetu na tusihusishe dini zetu na propaganda za CCM
April 11, 2011 3:11 AM
blank.gif

Anonymous said... Kwa kweli mwelekeo wa taifa letu juu ya propaganda za udini sio nzuri. Watanzania tumekubali kugawanywa na kuchochewa kuaanza kutazamana kwa misingi ya udini. Hebu fungua na sikiliza link hii hapa chini uone mwenyewe:

Muungano wa Tanzania uvunjike usivunjike? Sikiliza kauli ya Maalim Bassaleh - Wavuti
April 11, 2011 4:20 AM
blank.gif

Anonymous said... Tunawauliza washenzi nyie pale maaskofu wanapotoa maoni yao kuhusu katiba wanapenyeza udini kwa ajili ya kuisapoti chadema? Washenzi ni washenzi tu hata ukiwafanyeje,Katiba sio ya Kikwete,ccm si ya waislamu wala Kikwete na wala haitungwi na Kikwete,kwanza yeye ana muda mfupi sana umebaki kuwaachia balaa lenu. Kila mtu ana haki ya kuzungumzia katiba,si mmeona Zanzibar Waislamu wameichana,hatuna unafiki sisi,nyie mlimuangalia Mkapa akiisulubu nchi mkamuangalia tu sasa mnataka Kikwete amfanye nini? Tunataka katiba mpya hatutaki udini,ukabila katika nchi yetu. Kuna pointi nzuri tu Sheikh kaitoa hapo ya kuwa katiba si kitu cha kufumba na kufumbua ni kitu cha kuchukua muda,ya wa kenya ilikuwa ya dharura na mpaka leo ni mashaka matupu huko Kenya. Washenzi nyie katiba haijaanzwa na Chadema Waislam walianza siku nyingi na Nerere akawatimua bungeni,Mtikila,Mapalala nao pia wamedai siku nyingi tu.
April 11, 2011 4:45 AM
blank.gif

Anonymous said... Ndugu yangu uliyenitangulia hapo juu acha lugha chafu kuwaita wengine washenzi! Dini gani ile inajiona inafaa machoni pa Mungu? acha hayo, fuata dini yako kama unataka kwenda mbinguni/peponi! Tatizo lako nahisi una shida ya elimu kwani aliyesoma anapinga hoja si kutoa matusi na kuwaita wengine washenzi! Nenda shule kwanza!
April 11, 2011 5:33 AM
blank.gif

Anonymous said... Mshenz ww usiyejitambua..umeusoma mswada kwanza nna uhakika ujauelewa sasa watu wakipinga madudu yale mnasema wadin..sa wa2 wasikemee maovu mnaanza ooh mnamsema kikwete kwa sababu ya din yake..viongoz wa din hawajaanza leo kukemea..mshenz ww unaye2mia din kuficha ufisad wenu na walaaniwe wote wanaotumia udin kuficha uovu..mkapa na kikwete walewale,wapinzan wkt wanamshadadia mkapa kikwete c alimtetea eti aachwe.. Sasa ndo ujiulize wale din moja kwanza din zenyewe za wakolon..na mtakoma mwaka huu mafisad ha2danganyik..
April 11, 2011 5:41 AM
blank.gif

Anonymous said... nyie wote mnanjaa nendeni mkale kwa mboe na slaa ndio muongee hamna maana hata kidogo hamjui mlifanyalo misioni sababu ya kuzozana hapa simuandamane tu tatizo lipo wapi?ingieni tu mtaani iwe historia kwenu nyie ndio vijana mliosoma na mnauchungu na hiyo nchi wengine hawana wengine hatutaki hata kuongozwa na mtu mtatuweka kundi gani?kama hujasoma unategemea utaletewa chakula mdomoni mwako na kusoma kwenyewe uangalie sio unasoma kozi za midomo kuchonga utamaliza viatu kutafuta kazi mbona wenye fani zenye akili hatuwasikii kukosa kazi?tatizo la vijana wengi mmesoma na kuhudhuria kozi za fani yenu
April 11, 2011 7:27 AM
blank.gif

Anonymous said... Ukitukanwa na wewe ukarudishia ma2c inamaanisha yamekuingia hayo ma2c, Mie ni mkristo ila nilifurahi kuona Waiclam wa Zanzibar wamekataa mswada wa katiba mpyaa kwani wao maoni yao wameona umeegemea upande mmoja tu wa Tanganyika na wala si udini kama mnavyotukanana sasa, pia bungeni kuna mbunge leo asubuhi alikua anatoa maoni baadhi ya vipengele viondolewe hasa vya kumuwekea kinga rais asishitakiwe afanyapo makosa, sasa naomba mtambue tatizo ni kikwete anataka kuharakisha hiyo katiba atakayoisimamia hadi ikamilike ila ki2 muhimu kwake aweke vipengele vitakavyomlinda atakapotoka madarakani nyie hamuoni hilo tatizo? kumbukeni ameshirikiana na mafisadi wengi wakiwamo wakristo tena ndio wengi sasa mmepandikizwa chuki mmekubali kununuliwa, Chadema wanaongelea watz na co wakristo je Zitto kaondolewa na wanachama wote ambao ni waiclam ndani ya Chadema ili tuamini ni chama cha Kidini? Think Twice Guy's msikulupuke kuanza kunununiana kisa udini kumbukeni wote ni watanzania.
April 11, 2011 7:59 AM
blank.gif

Anonymous said... Inashangaza kuona kiongozi wa dini anatumia nafasi yake ya uongozi kutoa matamshi ya kutishia jamii kua watatumia wafusi wa dhehebu lao kulinda maslahi ya kiongozi wa serikali tuliwahi kusikia eti kiongozi wa serekali atapewa ulinzi wa majini hapa kuna agenda isiojulikana lakini wa Tanzania wanatakiwa kua makini siku zote wajinga hutumiwa wakajikuta wana ua hata ndugu zao kutokana na ujinga wao, Ni nani asie jua kua utawala ni mbovu? Anaepinga ni kwa sababu anafaidika na utawala huo kwa namna fulani na hao ndio tusio wataka hivyo mabadiliko ya kweli ni ya lazma kwani wanao teseka ni wengi.
April 11, 2011 8:00 AM
blank.gif

Anonymous said... Eti suala la DOWANS na Katiba ni agenda ya siri ya CHADEMA? Nina mashaka na uelewa wa Waislamu hawa. Katiba imeanza kudaiwa toka enzi za Mwalimu, Suala la Dowans hadi Waziri mkuu kaziuzuru halafu eti ni janja ya kumuondoa JK madarakani? Uislamu sasa kama alivyosema Makamba unakuwa kama chama cha siasa.

Ebu angalia kila mwaka wanaandamana wakihamasishana Ijumaa siku ya Swala.Eti wanapinga GADAFI kuondolewa madarakani. Mbona hawaandamani kupinga Ufaransa kumsaidia Quatara kumg'oa Laurent GABO? Ujinga huu watauacha lini?
April 11, 2011 8:21 AM
blank.gif

Anonymous said... Unajua ni kitu cha kushangaza mtu anaposema eti watz ha2fanyi kaz ndomana ni masikin nasema hapana kaz 2nafanya lkn hatul mafisad wanakula jasho le2..afu naudhika nnapoona eti viongoz wa din wanapotetea viongoz dhaifu eti tu kwa sababu ya din zao utafikir wao sio watz na hawapat shda kama wenzao..narudia tena adui ya mtanzania ni FISADI NA WALA SI DINI NYINGINE WALA KABILA LINGINE. Ful stop
April 11, 2011 8:30 AM
blank.gif

Anonymous said... HIVI NYIE WAKRISTO MNACHEKESHA SANA. NYIE MMESOMA SANA HATUKATAI MMESOMA LAKINI UWAJIBIKAJI HAMNA. SASA KISOMO CHENU KINA FAIDA GANI KUJIVUNIA? MMEONGOZA NCHI HII WENGI WENU MKIWA VIONGOZI NA NI NYIENYIE MNAOSEMA NCHI HAINA MAENDELEO TOKA UHURU SASA TUWAELEWEJE? KISOMO CHENU SI CHA KUJIVUNIA AU VIPI? MMESOMA LAKINI HAMKUELEWA? TUNAWAAMBIA CCM INA NAFUU MARA MILLIONI KULIKO HIYO CHADEMA YENU,CCM HAINA UKABILA WALA UDINI,HUO UDINI SIKU ZOTE HUPANDIKIZWA NA MAASKOFU WENU AKISHIKA KIONGOZI MUISLAMU. NA WEWE MUANDISHI WA HABARI HIZI UTUAMBIE MAPADRI NA MAASKOFU WANAPOTOA MAONI YAO KUHUSU KATIBA WANAPENYEZA UDINI? SWINE
April 11, 2011 9:32 AM
 
Mbowe ataka waliojiuzulu waondoke pia serikalini Send to a friend Sunday, 10 April 2011 21:38

f.mboye.jpg
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Habel Chidawali, Dodoma
SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya CCM (CC) na Sekretarieti yake kujiuzulu, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka wajumbe wote waliojiuzulu ambao wana nyadhifa serikalini kuondoka madarakani pia.Mbowe alisema hayo jana katika kongamano la wasomi wa vyuo vikuu lililoandaliwa na chama hicho Mjini Dodoma.
Alisema utamaduni wa kujiuzulu kwa viongozi wa CCM kwa kupisha wenye uwezo kufanya kazi, ungekuwa na maana zaidi kama ungefika katika nafasi za Serikali ambako nako alisema kuwa kunatakiwa kuvuliwa gamba.
Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema kama ilivyo kwa kila mtu muungwana kueleza ukweli pale anapoona kuwa kazi imemshinda, ndivyo inavyotakiwa hata kwa Serikali kwani kwa mujibu wa maelezo yake kuna watu wengi ambao hawajui wajibu wao na kwamba wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea kwa ajili ya kuwafurahisha wakubwa wao.
"Tunawashukuru CCM kwa kuelewa kuwa kutokuwajibika dawa yake ni kujiuzulu, tunataka utamaduni huu waupeleke serikalini na siyo ndani ya chama kwani hilo halitasaidia kitu," alisema Mbowe na kuongeza;
"Tunawaona wanajiuzulu ndani ya chama lakini hawajiuzulu serikalini na serikalini ndiko wanakowakosea wananchi siyo kwenye chama kwa nini wanakataa kujiuzulu serikalini?"
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kitendo cha Kamati Kuu ya CCM (CC) na sekretarieti yake kujiuzulu ni ishara ya kuweweseka na kukiri udhaifu akisema sasa yamewafika (CCM) shingoni ndipo wanaweka mambo hadharani.
"Kama Kamati Kuu na sekretarieti vimeonekana ni legelege na dhaifu ni wazi kuwa hata fikra zinazoongoza taifa nazo ni dhaifu na legelege," alisema.
Alisema kama wanaCCM watavuana madaraka haitasaidia kitu kwa kuwa watu bado ni walewale wasiowajibika katika ngazi zote na siyo kwa kamati kuu peke yake.Kwa mujibu wa Mbowe, tatizo la CCM halipo kwenye gamba, bali ndani ya damu hata kama wakijivua gamba bado damu yao imejaa 'saratani,' akahoji kujivua gamba kama ndiyo suluhisho la matatizo.Alisema hatua ya kamati kuu na sekretarieti ya CCM ya kujiuzulu imewapa wao ari na nguvu zaidi wa kujiimarisha.

Chadema na vyombo vyake vya habari
Akizungumza na wasomi katika kongamano hilo, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema kutokana na changamoto kubwa wanayoiona hivi sasa ndani ya CCM ni wazi kuwa kunahitajika maandalizi ya kutosha na kwamba wana uhakika kuwa wataibuka washindi 2015.
Mnyika alisema baada ya kuona CCM wanataka kuamka, Chadema kinapanga kuanzisha vyombo vya habari kwa ajili ya kuwapasha habari wananchi."Pamoja na mambo mengine, Baraza Kuu litapitisha mpango kabambe wa miaka mitano katika kuanzisha vyombo vya habari. Tunaamini kuwa wananchi wengi wanakosa kusikia mambo mazuri yanayozungumzwa na viongozi wao.
 
Mbowe kuongoza maandamano Mbeya Send to a friend Sunday, 10 April 2011 21:25

Brandy Nelson, Mbeya
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anatarajiwa kuongoza maandamano ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya, yenye lengo la kushinikiza mswada kupinga muswada wa mapitio ya katiba mpya.Maandamano hayo yanayotarajiwa Jumamosi ijayo, yamendaliwa na chama hicho cha upinzani.

Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya Mbowe, kila mbunge wa chama hicho, atakwenda katika mkoa mmoja kuongoza maandamano.Habari kuhusu kiongozi huyo kuongoza maandamano hayo mkoani Mbeya, zilitangazwa jana na Katibu wa Chadema wa mkoa huo, Eddo Makatta, alipokuwa akizungumza na waandishi habari.

Alisema chama hicho kinatarajia kufanya maandamano makubwa ya kupinga muswada na kwamba tayari maandalizi yameanza."Imeonekana kuna ujanja ujanja ambao serikali inataka kuufanya kwa kuwatumia watu wachache,kutoa maoni kuhusu katiba kwa manufaa ya wachache na kuwakandamiza wananchi walio wengi,"alisema.

Alisema maandamano hayo yatafuatiwa na mkutano mkubwa utakaohutubiwa na Mbowe.Kuhusu hatua ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Mbeya,Sambwee Shitambala, kuhamia CCM alisema chama chake hakina taarifa rasmi na kwamba habari hizo kimezipata kupitia vyombo vya habari.

Alisema hata hivyo kama kweli Shitambala amemua kuhamia CCM, hajafanya kosa kwa sababu hiyo ni haki yake ya kikatiba."Chama chetu hakiwezi kulumbana naye, kwanza ni mchanga kisiasa na tunamuonea uhuruma kwa hatua hiyo ya kwenda katika chama kinachoendelea kupasuka na kukiacha chama kinachozidi kuimarika," alisema Makatta.

Katibu huyo amemtaka Shitambala asitumie vifaa mbalimbali vya Chadema.
 
Comments

12

0 #21 mtu kwao 2011-04-11 18:41 sabweeee kweli,,ulikuja kugombea u-makamu mwenyekiti cahdema taifa ili usambaratishe chamaaaaaaaa!! ni kweli watu pale kiramuu hall, mbezi beach walikumbamba kweli..ulimwagamaelimu yako yotee.. Mzee Arfi akaesma sisi tusio na elimu tuchaguane wenyewe,,akakub waga vibaya ukapata kura 99 tuu..na Dr. feki wako Kapwani naye maruwe ruwe tuu yuko CCM leo duu...nyambafu.
Quote

0 #20 jumbe 2011-04-11 16:23 huyo anaye sema chadema ni chama cha watu wa moshi na arusha tunamuomba afunge domo lake,sisi hatuna ukabila.CHADEMA nguvu ya ummaa tunaenderea kuikimbiza ccm hadi kieleweke.
Quote

0 #19 Chachandu Motto 2011-04-11 16:17 kuna watu akili zao matope badala ya kujadili hoja wamekalia kusema kanisa mara ukabila sijui nini, [NENO BAYA] zenu, hayo waliyofanya CCM kwa nchi hii hadi tunaliwa raslimali zetu kama kondoo hamuyaoni, kama kusoma hujui hata kuangalia picha huwezi! we MTENDA umerogwa kaa fikiria kabla ya kuandika na kama hujui ukabila udini ameanzisha JK na nyie [NENO BAYA] mnafuata tu bila kufikiri, natamani ungekuwa karibu yangu nikunyonge upotee ktk nchi yetu ya wastaarabu. Na Shitambala hajui alitendalo na atajuta kufanya hivi siku hazigandi tunajua ulichotufanyia Mbeya tangu uliposhiriki uchaguzi wa awali na una haki ya kuamia popote, na sisi hatukutaki. Peoples power .......
Quote

+1 #18 m s mtenda 2011-04-11 13:52 Quoting thadeus mbani:
wake up all Tanzanias,this is show time,dont sleep do somethig good to your country Tanzania like CHADEMA do now.​
chadema ni chama cha watu wa moshi na Arusha ndio maana Kafulila akafukuzwa na Wangwe mwana harakati
Quote

-2 #17 m s mtenda 2011-04-11 13:43 chadema ni chama kichanga siasa za kitoto kumbukeni kiongozi wake mkuu alivyopiga binti mdogo kwenye uchaguzi uliopita leo akipewa idhini ya kusaini kifo si atamaliza watu? msitarajie kabisa siasa kanisani ziwapeleke mbali
Quote

+1 #16 frenando 2011-04-11 13:01 mapambano yanaendelea makamanda wote tanzania tukae tayari kwa kuwateka MAFISADI CCM,chitamballa kapoteza dira... na huu ndio wakati wa maji kutengana na mafuta. nguvu ya umma itashinda na kudumu daima
Quote

+2 #15 BOMU SHITAMBALA 2011-04-11 10:44 My friend Shitambala, wewe ni ndumila kuwili tangu mapema tukiwa Chuoni, sijawahi kukuamini hata kidogo; kwanza umebembelezwa mno ulipojiuzulu Uenyekiti Mbeya, ukaombwa ukarudi, sasa umehama kabisa. Kweli sikio la kufa halisikiii dawa, Umejimaliza kisiasa while you still too young brother. Umeombwa ukamtetee Mgombea Ubunge Chadema Sumbawanga, ukauweka usiku kwasababu ulijua wewe ni kibaraka wa CCM. Lo,Kimjazacho mtu ndo kimtokacho. Kwa heri Shitambala, Umepoteza *Puristiji* hata katika maisha yako binafsi, hakuna mtu atakayekuheshim u labda wanafiki kama wewe mwenyewe.
Quote

+1 #14 shida 2011-04-11 10:24 Nakushangaa unaejiita J.Mtatina huna hoja ya msingi wala hayo maneno ya maana kazi yako kujifanya ni mchambuzi ya habari za watu walizoandika angalia hapo chini huna hata hoja kz yk wajifanya mchacha mbuzi, naona wewe ndio akili zako mbofumbofu pole sana
Quote

+1 #13 thadeus mbani 2011-04-11 10:17 wake up all Tanzanias,this is show time,dont sleep do somethig good to your country Tanzania like CHADEMA do now.
Quote

0 #12 ambilikile mwasapile 2011-04-11 10:11 mmh mbombo ngafu ikyisu kimalike kyala atutule
Quote

+1 #11 jonas mtatina 2011-04-11 10:01 Quoting mtu kwao:
shitambala si aliuza jimbo la mbeya vijijini kwa sh.miloni 600? amedhirisha unafiki wake na usaliti mkubwa dhidi ya wanambeya..hatumtaki tena achaneni naye..​
Mtu Kwao ninakupongeza kwa tamko lako dhidi ya hayawani Shitambala.Usiwe na wasiwasi amekwisha kujimaliza kisasa bila kujijua,Kama ukonae karibu mpe pole sana.
Quote

+1 #10 jonas mtatina 2011-04-11 09:51 Quoting joshua n. salehe:
SHITAMBALA NI KWELI UMEHAMA CHAMA CHA KUTETEA WATANZANIA?WEWE HUONI HALI ILIVYO NGUMU UMEWASALITI WAPIGAKURA WAKO WA MBEYA VIJIJINI MUNGU ATAKUONA​
Bw.Joshua ninakuunga mkono kwa hoja yako.Kabla mungu hajaanza kumwangalia tayari amekwisha kujimaliza kisiasa.Zile tuhuma za kuuza Chama zilkuwa ni za kweli ndio matunda yake hayo ya kukimbilia CCM.Na asinge fanya hivyo ingebidi arudishe pesa za CCM alizokula.
Quote

-1 #9 jonas mtatina 2011-04-11 09:43 Quoting shida:
Ninaamini maneno ya Ndugu Ngawaia kuwa kuna mtandao wa kuwahamasisha wananchi waandae vurugu na kuna fungu kubwa sana wanalopa[NENO BAYA] kwa masharti!!Iweje uanda e maandamano ya kupinga rasimu ya katiba wakati ni mwanzo tuu wa mchakato wa kujadiliwa hiyo Katiba ambayo itachukuwa hata zaidi ya miezi 6 ili kila kijiji na kila wilaya na mikoa iweze kupata haki ya kuijadili na kutoa maoni yao wanapinga eti haraka mno maana huo ni mwanzo, halafu ije iteuliwe kamati ya kuratibu maoni nayo itafanyiwa maandamno kupingwa mwisho ni vurugu uwe makini [NENO BAYA]oweeee!!​
Shida kumbe ww una akili mbovu kama za Ngawaia?kama ulikuwa unataka Umaarufu kupitia gazeti hili usingetaja jina la huyo hawaini mwenzio Ngawaia.Mh.Mrema alimbeba akamleta bungeni,je?shukrani yake ulioona?Dalili za vurugu ni kuipinga serkali ya CCM.Je?kuinga mkono serikali ya CCM ndio kuleta Amani?
Shida ninaomba uwe unachagua maneno ya kuandika kwenye Gazeti kama hili.
Quote

0 #8 mkereketwa 2011-04-11 09:26 kumbe mikoa mingine haiko tanzania,mikoa mitatu tu inajadili katiba,this is crazy dision please mswada wa katiba wananchi mikoa yote wahusishwe.
Quote

0 #7 shida 2011-04-11 09:07 Ninaamini maneno ya Ndugu Ngawaia kuwa kuna mtandao wa kuwahamasisha wananchi waandae vurugu na kuna fungu kubwa sana wanalopa[NENO BAYA] kwa masharti!!Iweje uanda e maandamano ya kupinga rasimu ya katiba wakati ni mwanzo tuu wa mchakato wa kujadiliwa hiyo Katiba ambayo itachukuwa hata zaidi ya miezi 6 ili kila kijiji na kila wilaya na mikoa iweze kupata haki ya kuijadili na kutoa maoni yao wanapinga eti haraka mno maana huo ni mwanzo, halafu ije iteuliwe kamati ya kuratibu maoni nayo itafanyiwa maandamno kupingwa mwisho ni vurugu uwe makini [NENO BAYA]oweeee!!
Quote

12
Refresh comments list
 
Mukama Katibu Mkuu CCM

*Nape, Megji, Kinana wateuliwa Sekretarieti

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya Chama Chama Mapinduzi (CCM)na Sekretarieti kujiuzulu, taarifa zilizovuja jana
kutoka kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma zilisema kuwa Bw. Wilson Mukana ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kushika nafasi iliyoachwa na Bw. Yusuf Makamba.

Wengine waliotajwa kuwamo kwenye sekretarieti hiyo ni Bw. Abdulahaman Kinana (Naibu Katibu Mkuu (Bara), Bw. Nape Nnauye (Katibu wa Itikadi na Uenezi), Bi. Zakia Megji (Fedha za Uchumi) na Bi. Rehema Nchimbi (Organazesheni).

Chanzo chetu ndani ya NEC kilisema kuwa wajumbe walikuwa tayari wametangaziwa uteuzi huo, lakini chanzo chetu kingine, kikadokeza kuwa pia kulikuwa na uwezekano wa kuteuliwa Jaka Mwambi, Balozi wa tanzania nchini Russia na aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM katika sekretarieti ya kwanza ya Rais Kikwete.

Bw. Mukama alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na baadaye Katibu Mkuu Wizara ya Afya. Kwa sasa ni mstaafu, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magazeti ya TSN.

Bw. Makamba, aliyekuwa akiongoza sekretarieti hiyo amelazimika kujiuzulu kabla ya mwaka 2012 aliokuwa ametangaza kutoka na tuhuma mbalimbali dhidi yake, zikiwamo za kukigawa chama na kushindwa kumsaidia mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Kutokana na tuhuma hizo, juzi usiku, kiongozi huyo, sekretarieti nzima iliyo chini yake, pamoja na Kamati Kuu, isipokuwa Mwenyekiti na Makamu wake wawili, Bw. Pius Msekwa (Bara) na Aman Abeid Karume (Zanzibar) walilazimika kujiuzulu, katika kile kinachotajwa kama chama hicho kujivua gamba.

Wengine waliojiuzulu katika secretarieti ni manaibu makatibu wakuu wa CCM Bara na Visiwani, Bw. George Mkuchika, Bw. Saleh Ramadhan Feruzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, Katibu wa Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala, Katibu wa Mipango, Bi. Kidawa Saleh na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mambo ya Nje, Bw. Bernard Membe.

Kwa maamuzi hayo, Rais Kikwete amepata fursa nyingine ya kuteua sekretarieti mpya na Kamati Kuu nyingine ikiwa ni takriban mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa chama hicho kufanyika mwakani, ikiwa ni njia ya kukinusuru chama hicho kilionesha kupauka mbele ya macho ya umma, kutokana na tuhuma mbalimbali, kubwa ikiwa ni kukumbatia ufisadi.

Waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu iliyoondolewa ni Bw. Makamba (Katibu Mkuu), Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Z'bar), Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe, Edward Lowassa na Shamsi Vuai Nahodha.

Pia walikuwamo marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dkt. Salmin Amour. Wengine ni John Malecela, John Chiligati, Amos Makala, Bernard Membe, Kidawa Hamid Salehe, Samuel Sitta, Pandu Ameir Kificho na Anna Abdallah.

Wajumbe wengine ni Rostam Aziz, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Pindi Chana, Andrew Chenge, Dkt. Maua Daftari, Samia Suluhu Hassan, Mohamed Seif Khatib, Haji Omar Kheri, Dkt. Abdallah Kigoda, Abdurahman Kinana, Anne Makinda, Fatuma Said Ali, Zakia Meghji, Omar Yussuf Mzee, Dkt. Emmanuel Nchimbi, Ali Ameir Mohamed na Yussuf Mohamed Yussuf.

Habari kutoka Dodoma zilisema kuwa kulikuwa na juhudi za wajumbe mbalimbali, hasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kutaka uamuzi wa kuitema sekretarieti ushindikane, lakini baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu wakawa mbogo na kutoa uamuzi huo, huku wakimweleza mwenyekiti kuwa kamati hiyo wanaiacha mikononi mwaka kwa kuwa baadhi ya wajumbe ni marafiki zake.

Kwa mujibu wa habari hizo, mmoja wa watuhumiwa hao alijitetea akitaka tuhuma za ufisadi ambazo hazijathibitishwa na mahakama yoyote zisiwe kigezo cha kufanya maamuzi hayo, kwa madai kuwa hazikuwa sabau ya kupunguza kura za CCM katika uchaguzi mkuu uliopita wala kukichafua chama.

Inasemekana kuwa kigogo huyo alijitetea kuwa hata wao (watuhumiwa) walichaguliwa kwa kura nyingi kuwa wabunge, na Rais Kikwete alipata kura nyingi kwenye majimbo yao.
 
13 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Mabadiliko yamefanyika lakini hayakidhi uhitaji uliopo sasa. Ni Changa la Macho tu. Katika hao waliochaguliwa sioni mwenye ujasiri wa kuwakabili mafisadi. HAYUPO.
April 10, 2011 10:28 PM
blank.gif

Anonymous said... ni sawa na chupa mpya "wine" ile ile!
April 10, 2011 10:53 PM
blank.gif

Anonymous said... Lakini mbona waandishi mna kiherehere mnaandika maneno yanayokisiwa kusikia radio mbao si mngojee itangazwe rasmi? Maana mpk saa 6 za usiku kikao kiliisha bila kutangazwa chochote sasa hii haraka ya nini?
April 10, 2011 11:32 PM
blank.gif

Anonymous said... CCM WOTE MAFISADI, ANZIA NA HUYO KIWETE MWENYEWE, AVULIWE GAMBA KWANZA YEYE, NDIYE ANALO GUMU KABISA, ASIJITOE HAPO. AACHIE NAE NGAZI.
April 11, 2011 12:45 AM
blank.gif

Anonymous said... mwaka wa shetani?makamba anaenda kukuna nazi Lushoto....teh eh./..teh..eh...
April 11, 2011 1:15 AM
blank.gif

Anonymous said... Mabadiliko yaliyofanywa na CCM ni mwanzo wa madiliko makubwa ktk safari ndefu ya kujisafisha na kukidhi mahitaji ya wanaccm
April 11, 2011 1:33 AM
blank.gif

Anonymous said... Tulitegemea sura mpya lakini wapi!punda ni yule yule ila sogi tu....
April 11, 2011 1:39 AM
blank.gif

mikwaju said... halafu ninyi vyama vya upinzani mlivyo na akili mbovu wakihamia kwenye chama chenu mnawapokea.
Tunajua kansa haiponi lakini subiri utasikia wameingia chadema mnawapigia makofi, paimbafu senu.
ACHENI HISO TAKA SIISIE HOKO MBORINI HIHIHIII!
April 11, 2011 1:47 AM
blank.gif

Anonymous said... bado hakuna matumaini kabisaaaa! Hata mnaowapatia madaraka ni mafisadi ili waendelee kuwalinda! Kama kweli mnaitakia Tanzania hii mema na hao mawaziri wote waliojipiga chini kwenye sekretarieti na pia wajiuluzu! Acheni danganya toto!
April 11, 2011 5:43 AM
blank.gif

Anonymous said... ni utaratibu tu wa uongozi bora na huru, haijaanzia na ccm, its a way forward. thanks
April 11, 2011 6:02 AM
blank.gif

Anonymous said... kamati ya sekratarieti hamujafanya vibaya kwani hiyo ndio siasa,ukiona maji yamezidi unga hauna budi kuachia ngazi,na kuwaachia wengine.ni mimi masumbuko mussa nachuchi wa mtwara mjini.
April 11, 2011 6:11 AM
blank.gif

Anonymous said... Udini tu unawasumbua!
April 11, 2011 8:03 AM
blank.gif

Anonymous said... KIKWETE AANZE YEYE KUJIVUA GAMBA LA UDINI

WIZI MTUPU HATULALI MPAKA KIELEWEKE
April 11, 2011 10:15 AM

Post a Comment
 
UDOM watawanywa kwa mabomu bungeni

Na Edmund Mihale, Dodoma

ASKARI wa Kikosi cha Kuzia Fujo (FFU) jana, walilazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi kuwatawanya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na
wanaharakati wengine baada ya kufunga barabara kuu ya kutoka Morogoro ili kulishinikiza waruhusiwe kuingia kwenye eneo la kushiriki mjadala Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Wakizungumza katika lango kuu la Ofisi za Bunge majini Dodoma jana kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walisema kuwa ni jambo la kushangaza kwa ofisi hiyo kuwaalika wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya City na kukiacha chuo hicho bila ya kuwa na uwakilishi.

"Muswada huo umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza wamealika wanafunzi wa Shule ya Sekondari City ambao hawajui Kiingereza shule yenye matokeo mabovu kila mwaka, huku ni kuwachezea wananchi, alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Mmoja ya wanafunzi hao ambaye alijitambulisha kwa jina la moja la Denis, alisema iwapo wabunge watapitisha muswada huo wako radhi kuingia mtaani kupinga tume hiyo kwa kuwa haiwezekani kufanya majadiliano katika mikoa mitatu ya Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma, ilihali kuna mikoa mingi inatakiwa kuwasilisha maoni yake.

"Hawa wabunge wakipitisha mambo hayo tutashtaki kwa wananchi na kisha tunahamia mtaani tunafanya kama ilivyo Tunisia, Libya na Misri lazima kieleweke," alisema mmoja wa wanafunzi hao kwa kipaza sauti.Alisema kuwa muswada uliowasilishwa bungeni na serikali chini ya hati ya dharura haukidhi mahitaji ya Watanzania.

"Watanzania wa leo sio wa juzi au jana, hatutaki kijitabu chenye maandishi kinachoitwa katiba bali makubaliano ya utaratibu wa jinsi ya kuendesha maisha yetu katika nchi hii kwa kujadiliana kila kitu jambo linalohusu kwa manufaa ya wote, kwa haki na usawa ulioandikwa katika kitabu kitakachokuwa na kumbukumbu ya makubaliano.

"Kwa matiki hii rasmu ya serikali inaonesha kuzidisha matatizo badala ya kuyapunguza kwa kuwa inaonesha kuwepo kwa kikundi cha watu wachache wanaotugilibu na kujitengenezea katiba ya kujilinda wao na mambo yao kwa manufaa yao. Tena wanaonesha kuwa wananufaika kwa sisi kupata shida, kwa kuwa ukisoma utagundua katika yale matatizo yetu makubwa hawataki tujadili kwa pamoja na kuyatatua," alisema.

Hata hivyo, hotuba hizo zilikatishwa baada ya kujitokeza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. James Msekela ambaye alijikuta katika wakati mgumu kwa kuzomewa na wanafunzi hao.

"Mtoe huyo mtoe huyo mtoe huyo alitupiga mabomu, hatumtaki anaongea pumba, pumba, pumbaaaa pumbaaaa," walisikika wanafunzi hao wakisema kwa jaziba.

Dkt. Msekela alishindwa kutuliza fujo hizo hadi alipojitokeza Mbunge wa Arusha mjini, Bw. Godbless Lema ambaye alipokewa kwa shangwe na vigelegele, 'jembee, jembee, jembee zilisikika sauti za wanafunzi hao.

Baada ya kuwashusha munkari, Bw. Lema aliwataka wanafunzi hao kuacha jazba, lakini aliulaumu utaratibu uliowekwa na bunge kwa kuwa haukuwatendea haki wananchi wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma na migine kwa kutumia ukumbi mdogo wakati wakijua kuwa wananchi wana shauku ya kutoa maoni yao kwenye muswada huo.

"Nimewaita wanafunzi wa chuo kikuu ili kuja kujadili muswada huu kwa kuwa umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza, hivi muuza mchicha, bagia anaweza kujadili muswada huu? Kuna watu wangapi wanapenda kuja hapa kujadili mustakabali nchi yao, hamuwezi kuita watu 300 ambao ni sawa na idadi ya wabunge wote," alisema Bw. Bw. Lema.

Alisema kuwa bora ofisi hiyo ikatafuta sehemu nyingine kubwa itakayoshirikisha watu wengi kujadili muswaada huo na kutoa maoni yao kwa uhuru kuliko kufanya katika chumba kidogo na kuwanyima haki watu wengine.

Mazungumzo hayo yalikatishwa na vurugu za wanafunzi hao waliotaka majadiliano hao yafanyike katika Uwanja wa Jamhuri, jambo lilopingwa na Dkt. Msekela ambaye alitaka kufanyika katika ukumbi wa Chimwaga.

Wanafunzi hao walipiga kelele kushinikiza kufanyika katika uwanja huo huku wakirusha mawe na kumzomea ndipo, Dkt. Msekela alipoamru Jeshi la Polisi kuwatanya, jambo lilozua kizazaaa katika mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya vurugu hizo, Dkt. Msekela alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kushindwa kuelewana na wanafunzi hao, huku akimrushia lawama, Bw. Lema kuwa ndiye chanzo cha vurugu hizo.

"Ninatoa onyo kwa wanasiasa wanaojihusisha na siasa katika Chuo Kikuu cha Dodoma nimeambiwa kuwa jana kuna mwanasiasa mmoja alikwenda kule kuwahamasisha wanafunzi hawa," alisema Dkt Msekela.

Baada ya kusikia hivyo, Bw. Lema, alisema kuwa hakuna haja kuuma maneno, bali yeye ndiye aliyekwenda katika chuo hicho na kuzungumza na wanachama chama chake na atarudi tena Jumamosi.

"Mie ndiyo nilikwenda huko na kuzungumza na wanachama wangu na Jumamosi nitakwenda tena, njoo tutakutana tusitishane, si muda wa kutishana. Nimekwenda nikafanya siasa nje ya maeneo ya chuo sasa tatizo langu nini," alisema Bw. Lema. Baada ya kauli hiyo, Dkt. Msekela alionekana kunywea.
 
10 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Ya.mimi sishangai kuona hali hii ya wasomi kuzuiwa kwani watanzania mmesahau ni serikali hii hii iliyowanyima wanachuo haki ya kupiga kura kwa kudai anayetaka apande gari aende alipojiandikishia...mi nadhani mfumo wa wanasiasa wa kiafrika kuhofia wasomi ndio huo unatufikisha hapo.Udom tuakilisheni nyie mlio karibu na mjengoni...Mungu wabariki wote wenye mawazo mema na TZ
April 7, 2011 11:53 PM
blank.gif

Anonymous said... by grace;
kama uchangiaji wa mawzo ya katibani huru na wazi, kwa nini wanavyuo wanazuiwa? kila mmoja anatakiwa kuchangia bila kutumia uwakilishi uliobuniwa kwa makusudi ili kuharibu taswira halisi iliyokusudiwa.
kwa mustakabali huo, wanaozuia wana vyuo wasiingie inaonesha walikuwa na watu maalum waliowaandaa ili kuwakilisha kilichoandaliwa, na kuna habari ambazo wapo wa2 maalum waliochomekwa ili kuwakilisha majumuisho yasiyo na lengo halisi.maandalio hayo ya kundi dogo,baada ya habari kuvuja na kugundulika, ndiyo yamesababisha wanavyuo kutotulia na wao kuhitaji nafasi. hivyo ndivyo ilivyo, tusidanganyane.
April 8, 2011 1:02 AM
blank.gif

Anonymous said... Kwa kweli nchi hii viongozi wa chama tawala wanataka kuleta vurugu.Kwani wanahofu nini uundwaji wa katiba mpya. Ninachofahamu ni kuwa katiba ya nchi ndiyo sheria mama ya kila kitu.Hawa watu wasitengeneze hati ya dharula kutaka kutufisha ambako siko wabunge wa chama tawala naomba mjadiliane kwa kuangalia maslahi ya wananchi waliowatuma kuwakilsha katika bunge mjue mkifanya haya mambo kwa ushabiki wa chama mkaye mkijua 2015 hata kwa katiba hiyo mbovu hamtapita labda mchakachue sana.kitu ambacho kitakuwa ni kigumu watu watalinda masanduku ya kura.Chondechonde wabunge wa chama tawala jadilini huu mswada kwa manaufaa ya watanzania na si vinginevyo.
April 8, 2011 1:36 AM
blank.gif

Anonymous said... Kwa vile kumbi zilizoandaliwa ni ndogo kulingana na jumla ya watu wanaotaka kushiriki na umuhimu wa kazi yenyewe, basi mijadala ifanyike katika maeneo mengi na wawakilishi wachaguliwe kati yao ili kuwakilisha maoni yao. Mchango wa wasomi, wafanyakazi, na idara nyingi ni muhimu, hivyo kuwepo na vituo mabali mbali vya kukusanya maoni na baadye yawekwe pamoja na tume huru. Huwezi kuweka mijadala ya namna hii katika sehemu wazi na kwenye watu wengi kwani muda utatuminka mwingi na mawazo yanapishana. Kwa mfano, Walimu wa vyou vikuu wangejipanga pamoja na wanafunzi wao wajadili mswada na wachague wawakilishi wa maoni katika tume huru. Sioni sababu ya watu kuvamia ukumbi. Wabunge tumieni busara kupanga namna ya kuongoza mijadala. Mbona ktk kujadili mishahara yenu hatusikii fujo?
April 8, 2011 5:58 AM
blank.gif

Anonymous said... wasomi gani uchwara chuo hakina hata hadhi za kimataifa?vitanda dabodeka utafikiri sekondari du mue na aibu tatizo vyuo vya kuongea vimezidi hapo bongo mbona muhimbili hao wanasiasa hawaendi?nani ataacha kusoma akamsikilize mwana siasa?hatuwasikii hata maprofesa wa kweli ambao wote wapo muhimbili kujihusisha na vyama?lkn hao maprofesa wa kozi za kuongea ndio wenyewe kila kitu wanajua wenyewe nchi hiyo umasikini utaisha kweli? ama kweli inasikitisha maana kwa sisi tulio ughaibuni tunaona maprofesa wanavyo fanya kazi zao za kitaaluma sio siasa wana tunga vitabu na ndio vinavyotumika mashuleni lkn sio kwetu vitabu hakuna mpaka tupewe msaada maprofesa tunao wanafanya kazi gani?
April 8, 2011 9:32 AM
blank.gif

Anonymous said... Viongozi wa ccm wote ni mbumbumbu. Yaani mnashindwa kusoma alama za nyakati.. nawasikitikiea sana. Mnatafuta mchawi wa vurugu za kujadili katiba na mnadhani kuwa mchawi ni chadema au mbunge G. lema. Huu uhuru na haki wa kila mtanzania kutoa maoni yake umetoka wapi? Mswaada wenyewe umeandikwa kwa kiingereza kwa makusudi ili kuwaondoa kwenye majadiliano asilimia kubwa ya Watanzania ambao mnajua hawajui klugha hiyo. majadiliana yanafanyika katika kumbi ambazo hazimudu idadi kubwa ya watu. Huu uhuru wa watanzania wengi kujadili mswada huu utafanyika vichakani au kwenye vilabu vya pombe ikiwa hakuna mazingira mazuri ya kuchangia mswada huu. Tunaomba usituletee kichefuchefu.
gazeti lako siku zote linabezi kutetea CCM tu ambao sasa wanataka kuchakachua mswada wa katiba mpya. Na ndiyo maana akina Prince Bagenda, Tambwe Hizza .. na mzee warioba walizomewa hovyo! Someni alama za nyakati.. watanzania wamechoka na uchakachuaji wenu! Mnakwenda kwenye mijadala wa mswada wa hamsemila maana ila mnamjadili rais ambaye ameonyesha wazi nia ya kuchakachua kupatikana kwa katiba...bohhh! Msizomewe!!
April 8, 2011 12:05 PM
blank.gif

Anonymous said... wewe uliyechangia maoni muda 9.32 ndiye uchwara! nchi ambayo hata baada ya miaka 50 ya uhuru haina umeme na maji unataka iwe na vyuo vyenye vitanda vya vioo! Nchi itaendeleakuw maskini kam wasomi hawatajihusisha na siasa.Na si kweli vitabu havitungwi, tatizo hata vile vichache vianvyotungwa havipati sapoti ya serikali.DAWA YA MATATIZO YETU SI KUWAACHIA WATU MBUMBUMBU WAENDELEE KUTUONGOZA BALI NI KILA MMOJA (HASA WASOMI)N KUJIHUSISHA NA SIASA KWANI HATA DAKTARI, PROFESA WA MUHIMBILI UFANISI WAKE UNAATHIRIWA NA SERA ZA WANASIASA
April 8, 2011 1:04 PM
blank.gif

Anonymous said... Mswada huu utakuwa na maaana kama watu wote watachangia kwa naman ambalimbali. Vitolewe vipeperushi mbalimbali vya kudondoa vipengere kimojakimoja visambazwe, machapisho pia kwenye magazeti juu ya mswada huo yawekwe, watu wasome na watoe mawazo yao, vipindi vya redio na television virushwe kueleza mambo muhimu kwenye mswada ili kila mtanzania aelewe. Zaidi uwekwe kwa lugha ya taifa, mbona kampeni na mabango ya uchaguzi mkuu yaliandikwa kiswahili? hili la mswada liweje kiingereza ambapo wengi hawajui?
April 8, 2011 6:34 PM
blank.gif

Anonymous said... CCM na serekali yake msiwafanye watanzania wajinga kuwaendesha mtakavyo. Muda umefika mkubali utawala wazi na haki vinatakiwa si kudanganya watu. Mswada huu ufike kwa wote hadi vijijini, kama mlivyoweza kufikisha kampeni za uchaguzi mkuu. Kufanya manvyofanya mnachochoa vurugu na kuhatarisha amani. Sasa siyo CHADEMA tena wanaochochea vurugu ni ccm na serekali yake. Mswada huu usiwe wa kundi dogo la watu hiyo siyo Demokrasia.Tafadhari wapeni watanzania haki yao ya kutoa maoni na kunda katiba mpya. Msifanye siri maana hata ile katiba ya zamani watu wengi hawaijui maana haipatikani kwa urahisi. Hizi ni mbinu za kutawala maana mtu kama hajui katiba ambayo ndo sheria mama atadai vipi haki yake? Watanzania wamekuwa wanaburuzwa miaka mingi na hawajui wadai haki vipi kwa vile hata katiba haiwaijui tokana na kuwa ni kitu cha wachache. Utaratibu au mfumo huu usiendelezwe katika msikabali mzima wa mswada. Mambo yawekwe wazi na huru na watu wafaffanuliwe nchi nzima, siyo ilivyowekwa sasa hivi kujadiliwa kumbi za Dom na Dar ni kuwakosea haki watanzania. Kama Kikwete ulivyotumia lugha ya kumuonya Magufuli asitumie "ubabe", basi ccm na serekali msitumie ubabe kuwalazimisha watanzania maamuzi ya wachache kujadili mswada. Wapeni watanzania fursa kuchangia mswada.
April 8, 2011 6:54 PM
blank.gif

Anonymous said... KUNA KUPITISHA MSWADA WA KUTUNGA KATIBA NA KUCHANGIA MJADALA NA KUTOA MAONI KUHUSU MFUMO WA KATIBA MPYA,HAPA KUNA KIKUNDI CHA WANASIASA WANAOJIPANDIKIZA KUJIFANYA KATIBA NI HAKI YAO PEKEYAO NA NDIO WANAWARUBUNI BAADHI YA WANACHUO KUSHIRIKI KTK KUANZISHA VURUGU,MAANA SASA IMEKUWA NI NJIA YA KUJIFANYA WAO WANASIKILIZWA SANA NA BAADHI YA HAO WASOMI,NA PIA NDIO AKISIMAMA MCHANGIAJI YYT WA CHAMA TAWALA AZOMEWE NK KWA MWENDO HUU HATUTAPATA UFUMBUZI MAANA KILA KITU WANADAI NGUVU YA UMMA MARA MAANDAMANO MPK KIELEWEKE HV SHIDA NA MATAKWA YAKO YAKULAZIMISHA FUJO NDIO UFUMBUZI?AU KUSEMA MPK KIELEWEKE IWE KAMA MISRI,TUNISIA AU SYRIA HIVI MPK SASA HUKO MNAKOTOLEA MIFANO KIMEELEWEKA AU NDIO WAMEKUWA WAKIMBIZI KTK NCHI ZAO? TUWE MAKINI MTANDAO HUO WA FUJO HAO VIONGOZI WANAOWARUBUNI WANALIPWA HELA NYINGI SANA NYINYI MNAAMBULIA MABOMU YA MACHOZI HAYA JITAHIDINI KWA MWENDO HUO MTAFIKA..!!
April 11, 2011 2:17 AM
 
'Serikali inataka kulinda maslahi ya CCM' Send to a friend Sunday, 10 April 2011 21:22

Moses Mashalla,Arusha
MUAASISI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei, amesema hatua ya serikali kuharakisha muswada wa mapitio ya katiba, inalenga katika kulinda maslahi ya CCM badala ya umma.

Kauli hiyo ya Mtei, imekuja wakati Chadema ikiwa amiazimia kuwatumia wabunge wake kwenda mikoani na kuendesha maandamano ya kupingwa muswada huo.Alisema madai ya wananchi kutaka katiba mpya, yamewafanya viongozi wa CCM kuchanganyikiwa na matokeo yake sasa wanataka kupeleka mambo hararaka haraka, ili wapate katika itakayoendelea kuilinda CCM.

Mwasiasa huyo ambaye alikuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizo juzi mjini Arusha, alisema kitendo cha Rais Jakaya Kikwete, kupeleka muswada huo bungeni chini ya hati ya dharura, kinalenga katika maslahi ya chama tawala.

"Serikali ya CCM inataka kuhakikisha kuwa maslahi ya chama hicho ynaendelea kulindwa na inafanya hivyo bila kujasli maslahi ya umma," alisema.Alisema kwa vyovyote vile, serikali inapaswa iwape wananchi, fursa na muda wa kutosha kujadili muswada wa katiba mpya kwa muda wa kutosha itakayolinda maslahi yao.

Mkongwe huyo alisema "halitakuwa jambo la busara kwa serikali kutaka kuwafunga midomo wananchi ili wasijadili jambo linalohusu maisha yao.""Tunataka kujadili kila kitu katika muswada huo, kwa hiyo lazima tupate muda wa kutosha," alisisitiza Mtei.
 
Comments

0 #7 Mdaho Gwalihenzi 2011-04-11 18:37 Quoting Israa:
Quoting CAROLINE:
TUMESHALIONA HILO NDUGU YETU MTEI NA HAPAPITISHWI KITU TANZANIA BILA WATANZANI KUJADILI NA KUKUBALIANA VINGINEVYO TUNAINGIA IKULU KUMTOA JK. AMEZOEA KUTUFANYA WATANZANIA KUWA HATUJUI TUNALOFANYA. YEYE ANARINGIA POLISI SISI TUNARINGIA NGUVU YA UMMA. HAKUNA MSWADA WA CCM UTAPITA MIFANO HAI AMEIONA KULE ZANZIBAR NA DODOMA. AMA ZAKE AMA ZETU!​

KAFIE MBALI WE MAKENGEZA,HATUT AKI CHADEMA WALA CCM KATIKA MCHAKATO WA KATIBA NYIE WOTE WEZI. SIO CHAMA CHAKO KILOSEMA KIKIPATA UONGOZI WA NCHI NDANI YA MWEZI MMOJA NCHI ITAPATA KATIBA MPYA? HII KATIBA MPYA MLIITAYARISHA NYIE WEZI KAMA WALIVYO CCM. PIA HATUTAKI WAFANYABIASHARA KATIKA UONGOZI WA NCHI HII KWQA SABABU KWA MUAFRIKA SI RAHISI KUTENGANISHA MASLAHI YAKE BINAFSI NA UONGOZI. KATIBA NI YA WANANCHI MKIWEMO NYIE LAKINI MKO KIDOGO MLIOJIBEBESHA JUKUMU HILO. HATUTAKI TUNATAKA KATIBA ITAKAYOANDALIWA NA WANANCHI ITAKAYOWADHIBIT I KUJIPA MARUPURUPU MAKUBWA​
Israa, ninawasiwasi sana na uwezo wako wa akili. Kuhamaki kwako na kutoa mitusi kwenye hii hoja kunanifanya nikuone kuwa wewe ndiye m[NENO BAYA] usie maana. Unaposema "hatutaki", unamjumuisha nani? Wacha ujuha wako. Acha kila mtu atumie haki yake ya kutoa mawazo yake.
Quote

+1 #6 wa ukweli 2011-04-11 15:45 rimaro nahisi sio mzima wewe watanzania wanalalamika utaratibu wa rais na ukusanyaji wa maoni ya katiba elewa mada ndo ulopoke sio kwa sababu hatulupii hizi coment ndo ukaleta u[NENO BAYA] wa kukusanya watoto wachangie mswada wa katiba muulize mzee wako atakwambia unachotakiwa kufanya kama kijana
Quote

+1 #5 Edijoe 2011-04-11 14:43 Ni kweli huu mswada inabidi uende taratibu si umeona zanzibar washauchoma moto yaani hawukubali wala hawutaki kabisa ni yale yale hivi unadhani rais atatenda haki kuchagua watu wa tume ambao si marafiki zake wenye kulinda maslahi ya ccm. Inabidi wananchi ndio waamue na si rais.
Quote

-1 #4 kadio 2011-04-11 11:51 NASEMA HIVI,KATIBA NI YAWANCHI..WENGINE MNAANDIKA TU KWASABABU SAFU HII IMEANDALIWA BILA KUFIKIRI,...SAWA NAPENDA KUKUBALI NA KUHESHIMU MAONI YA MTU..LAKINI NAUNGA MKONO HUYO HAPO JUU ALIYESEMA KATIBA SI YA CHADEMA WALA CCM NI YA WANANCHI...,WANANCHI WA TZ SIO WAJANA....WANAUTASI NA FIKRA HAI..!
Quote

-2 #3 rimamo 2011-04-11 10:58 nyie CHADEMA ni mavuvuzera. maana naona hamueleweki. mara mlisema makipata madaraka utaipatia nchi katiba mpya ndani ya siku 100, mara mkampa rais kuhakikisha katiba mpya ndani ya miezi sita, leo tena mnalalamika rais anaharakisha mchakato,sasa lipi jema kwenu? au ni lazima tuu muongee? hamueleweki kama sigara kali. nyie nao ndio wale wale tuu siyo chama cha siasa bali ni wanaharakati, maana kila kitu kwenu kibaya. duh kweli ukistaajabu ya mussa utakutana ya firauni.tumewachoka na kelele zenu. kila kitu kikifanyika kwenu kibaya tuu. unapoteza muda mwingi wa watanzania badala ya kufanya kazi kushiriki maandamano kila kukicha,sasa nyinyi mngefanyaje kuleta hiyo katiba mpya ndani ya siku 100 au miezi 6? hayo maoni ya wananchi mngekusnya vipi kwa nchi mzima?
Quote

-2 #2 Israa 2011-04-11 09:09 Quoting CAROLINE:

KAFIE MBALI WE MAKENGEZA,HATUT AKI CHADEMA WALA CCM KATIKA MCHAKATO WA KATIBA NYIE WOTE WEZI. SIO CHAMA CHAKO KILOSEMA KIKIPATA UONGOZI WA NCHI NDANI YA MWEZI MMOJA NCHI ITAPATA KATIBA MPYA? HII KATIBA MPYA MLIITAYARISHA NYIE WEZI KAMA WALIVYO CCM. PIA HATUTAKI WAFANYABIASHARA KATIKA UONGOZI WA NCHI HII KWQA SABABU KWA MUAFRIKA SI RAHISI KUTENGANISHA MASLAHI YAKE BINAFSI NA UONGOZI. KATIBA NI YA WANANCHI MKIWEMO NYIE LAKINI MKO KIDOGO MLIOJIBEBESHA JUKUMU HILO. HATUTAKI TUNATAKA KATIBA ITAKAYOANDALIWA NA WANANCHI ITAKAYOWADHIBIT I KUJIPA MARUPURUPU MAKUBWA
Quote

+2 #1 CAROLINE 2011-04-11 05:46 TUMESHALIONA HILO NDUGU YETU MTEI NA HAPAPITISHWI KITU TANZANIA BILA WATANZANI KUJADILI NA KUKUBALIANA VINGINEVYO TUNAINGIA IKULU KUMTOA JK. AMEZOEA KUTUFANYA WATANZANIA KUWA HATUJUI TUNALOFANYA. YEYE ANARINGIA POLISI SISI TUNARINGIA NGUVU YA UMMA. HAKUNA MSWADA WA CCM UTAPITA MIFANO HAI AMEIONA KULE ZANZIBAR NA DODOMA. AMA ZAKE AMA ZETU!
Quote

Refresh comments list

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!
 
Katibu Mkuu CCM atajwa

na Mwandishi wetu, Dodoma

amka2.gif
WAKATI wa macho na masikio ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), yakielekezwa mjini Dodoma kutaka kujua nani atakayeteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, jina la Abdulhaman Kinana na Willison Mkama, yametajwa kurithi mikopa ya Yussuf Makamba.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa Mkama ambaye amepata kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya anadaiwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu na Naibu wake Bara ni Kinana.
Mbali ya kuwa Katibu Mkuu, Mkama pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.
Wengine wanaotajwa na nafasi zao kwenye mabano ni pamoja na Mkuu Wilaya ya Masasi, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi), Zakhia Meghji (Fedha na Uchumi) na Rehema Nchimbi (Organisation na Uchunguzi).
Hata hivyo, majina hayo hayajatangazwa rasmi wala kuthibitishwa na NEC, kwani walikuwa wakiendelea na kikao kwa ajenda ya kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita.
Akizungumza wakati akifungua kikao cha NEC mjini hapa, Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa chama chake kimejipanga kufanya mabadiliko makubwa, ili kikabiliane na hali ya kisiasa ilivyo sasa nchini.
"Katika kipindi hiki cha mazongo mazongo yetu, wananchi wamekata tamaa na ninyi ndio wenye mamlaka ya kubadilisha hali hiyo," alisema Rais Kikwete na kufungua kikao.
Awali akizungumza na waandishi wa habari jana,aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, alisema kuwa CCM imeamua kufanya mabadiliko makubwa ili chama hicho kiweze kwenda na kasi ya wakati wa sasa.
Alisema hana kinyongo na hatua iliyofikia ndani ya chama chake kwa madai kuwa huo ni utaratibu wa kawaida kwa chama chochote duniani.
Kwa upande wake, aliyekuwa Naibu Katibu Bara, George Mkuchika, alisema kuwa muundo wa chama kwa sasa utahakikisha kuwa wajumbe wote wanaoingia kwenye sekretarieti wasiwe wabunge wala mawaziri, ili waweze kufanyakazi za chama kwa ukamilifu.
"Safari hii hatutakuwa na kofia mbili. Awali wajumbe wengi walikuwa mawaziri na wabunge, hali ambayo ilisababisha shughuli za chama kusimama," alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wanachama walikaririwa wakisema kama lengo la chama ni kutenganisha kofia ili kuleta ufanisi, utaratibu huo uwekwe hata kwa rais ili abaki na kofia moja ya urais.
 
Mbatia: Mjadala wa Katiba usitishwe

na Datus Boniface

amka2.gif
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ametaka kusikitishwa mara moja kuendelea na zoezi la kuratibu pamoja na kuwasilishwa katika kikao cha Bunge mjini Dodoma kwa Muswada wa Marejeo ya Katiba kutokana na muswada huo kuvunja Katiba ya nchi.
Mbatia alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mjadala wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbele ya waandishi wa habari.
"Serikali inazungumzia Marejeo ya Katiba wakati sisi tunazungumzia Katiba Mpya, tangu kuanzishwa kwa chama chetu hatujawahi kuomba marejeo bali tulikuwa tukipigania kupatikana kwa Katiba Mpya iliyotungwa na wananchi wenyewe.
"NCCR-Mageuzi tunatoa msimamo wa kupigwa ‘stop' haraka iwezekanavyo kuendelea na mchakato huu kwa maslahi ya taifa, kama wananchi wa Tanzania Visiwani (Zanzibar), wamepinga juu ya mchakato wenyewe, kuna maana gani ya kuuwasilisha katika kikao cha Bunge Dodoma?" alihoji Mbatia.
Katika maelezo yake Mbatia alisema taratibu zinazofanyika katika kuratibu maoni ya muswada ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri inayotakiwa kurekebishwa.
Mbatia alisema endapo marekebisho ya ibara hiyo yakishafanyika kama wanavyopendekeza, ni wazi kwamba katiba iliyopo itakuwa ndiyo mhimili wa msingi wa harakati zote za kupata katiba mpya, kutokana na kwamba yote yatakayofanyika yatakuwa na ridhaa ya Katiba.
Ingawa Mbatia hakueleza sababu wanazotarajia kuchukua endapo serikali na mamlaka husika zitashindwa kusitisha zoezi hilo, alisema msimamo wao ni wa nia njema, wenye kuzingatia masilahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.
 
JPF: Wananchi kataeni muswada wa Katiba

na Mwandishi wetu

amka2.gif
TAASISI ya kimataifa inayojishughulisha na tafiti za Utawala Bora, Jopa (JPF), imewataka Watanzania kuungana na kupinga muswada wa Katiba, kwani haukuzingatia matakwa ya wadau mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Praygod Mmasi, alieleza hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia muswada huo.
Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa iwapo muswada huo utafikishwa bungeni na kupitishwa, watakuwa wamejiingiza kwenye kitanzi.
Mmasi alisema kuna kipengele ambacho kitawazuia wananchi kujadili suala lolote litakalomhusu rais ama Muungano ambapo atakayejaribu kufanya hivyo ataweza kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Aidha, Mmasi aliwataka Watanzania kufahamu Katiba hii ya Tanzania ndiyo Katiba ya Tanganyika, kuwa katiba mpya inayotakiwa kuandikwa ni ya Tanznia Bara na si Katiba ya Tanzania.
Alisema Zanzibar wamekwishaandika yao, baada ya katiba hiyo, ndipo itungwe Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
"Hivyo kimsingi zoezi hili la kuandikwa Katiba ya Tanzania haliwahusu Wazanzibari hadi pale tutakapokamilisha Katiba ya Tanzania Bara ndipo Rais ataitisha baraza la muungano la kutunga Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na hii ya Tanzania Bara," alisema Mmasi.
 
Rais asiteue Mtendaji wa Mahakama - Wadau

Imeandikwa na Na Gloria Tesha, Dodoma; Tarehe: 11th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 27; Jumla ya maoni: 0

WADAU wa masuala ya sheria nchini wametaka mamlaka ya Rais kumteua Mtendaji Mkuu wa
Mahakama iliyopo katika Muswada wa Sheria ya Utumishi wa Mahakama iondolewe kwani ni kuingilia uhuru wa mahakama, na badala yake wamependekeza ateuliwe na Tume ya Mahakama.

Aidha, wametaka Rais aondolewe Mamlaka ya Nidhamu iliyoainishwa katika Kifungu cha 9 cha Muswada huo na kuipa Tume iliyopendekezwa katika Muswada huo na yeye (Rais) apelekewe taarifa ya hatua za kinidhamu zilizochukuliwa.

Wadau hao walitoa maoni ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), mjini hapa Jumapili katika mkutano wa kukusanya
maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Utawala wa Mahakama chini ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo.

Mwakilishi wa asasi hizo kutoka LHRC jijini Dar es Salaam, Merick Luvinga alisema muswada huo umempa Rais mamlaka makubwa mno, hivyo wamependekeza mamlaka ya Rais inayoainishwa katika muswada huo ni dalili ya kuingilia uhuru wa mahakama hasa kumteua
Mtendaji Mkuu wa Mahakama.

Alitaka Sheria ijayo iangalie mamlaka hiyo pamoja na uwezekano wa kuweka fungu la kutosha la ujenzi wa Mahakama za Wilaya na za Mwanzo na nyumba za mahakimu. Katika mkutano huo chini ya Mwenyekiti wa Kamati, Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, (CCM) ulikuwa na mahudhurio hafifu ya watu wasiozidi 25 wakati ukumbi unachukua watu 540, suala
lililoelezwa na washiriki wa mkutano huo kuwa suala la mahakama halina mvuto na ushawishi kama Katiba.

Wiki iliyopita, wakati wa mkutano wa maoni kuhusu Muswada wa Katiba, watu walikuwa wengi kiasi cha ukumbi kuwa mdogo hali iliyosababisha baadhi yao wakiwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma waliozuiwa kuingia, walifanya fujo nje ya Jengo la Bunge na kusababisha Polisi kutumia nguvu ya mabomu na risasi kuwatawanya.
 
Back
Top Bottom