Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

'Tanzania ina vilema vitatu'


*Paroko ahimiza ujasiri kukemea maovu

Grace Michael, Dar na Heckton Chuwa, Moshi

WAKATI mwaka huu Tanzania inaadhimisha Jubilei ya miaka 50 tangu kupata uhuru wake, imeelezwa kuwa itaendelea kuwa nchi ya chini kimaendeleo
ikilinganishwa na nchi nyingine duniani kutokana na watu wake kutopenda kufanya kazi na kuathiriwa na 'vilema vitatu'.

Tahadhari hiyo imetolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, mkoani Kilimanjaro, Mhashamu Isaac Amani, wakati akitoa salamu zake za Pasaka katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme, mjini Moshi, jana.

Alivitaja vilema hivyo kuwa ni ulevi wa kupindukia, kuishi kinyumba na utandawazi.

Alisema wengi wa Watanzania bado wako vijiweni, hawataki kufanya kazi na kwamba tabia hiyo imesababisha kidogo kinachopatikana kutokana na wachache wanaojituma, kitumiwe kwa taabu na watu wengi, wengi wao wakiwa ni wale wasiotaka kujituma.

Askofu Amani alisema suala hilo na mambo mengine yamekuwa yakirudisha nyuma maendeleo ya nchi, na kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ulevi wa kupindukia ambao alisema ni moja ya vilema vitatu ambavyo vimelikumba Taifa la Tanzania katika wakati huu linapoadhimisha miaka 50 ya Uhuru wake.

"Kuna vilema vinavyopatikana kwa ajali, kuzaliwa na vingine vya kujitakia, hivi vya kujitakia ni pamoja na ulevi wa kupindukia, kuishi kinyumba na utandawazi, kwa kweli hivi vitatu vinaelekea kuipeleka nchi yetu pabaya," alisema.

Alisema ulevi wa kupindukia umewamaliza na unaendelea kuwamaliza watu wengi haswa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa ambapo alisema kuna baadhi ya viongozi na wananchi ambao si waaminifu na ambao wamekuwa wakiyaona haya na kuyafungia macho.

"Pombe hizi zinauzwa katika maeneo tunayokaa, baadhi ya viongozi wanayajua haya na kuyaona lakini wanayafumbia macho hii imesababisha watu wengi kutokufanya kazi kutokana na nguvu kazi ya Taifa kumalizwa na ulevi wa gongo tena katika kipindi hiki ambapo Taifa linaadhimisha Jubilei muhimu ya Uhuru wake," alisema.

Kuhusu kuishi kinyumba, askofu huyo alisema kuwa tabia hiyo imekithiri miongoni mwa wakristu wengi na kwamba umepora haki na uhalali wa ndoa kama alivyoelekeza Mwenyezi Mungu, ambapo alisema kitendo hicho kimekuwa mfano mbaya katika maisha ya kila siku, kiasi cha hata watoto na vijana kuona ya kuwa ni jambo la kawaida katika maisha.

Aidha Askofu Amani alisema utandawazi ni kilema kingine ambacho kinaiweka nchi mahali pabaya na kwamba tayari umeshaanza kuwadhuru Watanzania wengi wakiwemo watoto wadogo.

"Mfano mzuri ni matumizi ya simu za mkononi ambazo kwa sasa zinatumika vibaya, ambapo watu wanazitumia kwa kutumiana ujumbe wa matusi, vitisho, uchochezi, kupanga ujambazi na mambo ya fitina, hivyo kupoteza maana halisi ya matumizi ya vyombo hivi muhimu ambayo vililengwa kurahisisha mawasiliano," alisema.

Aliagiza ya kuwa wakati Taifa likiendelea kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kuwe kunafanyika sala maalumu ya kuliombea taifa kila siku kila baada ya ibada, katika Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristu na mashirika yote
ya kikatoliki jimboni humo hadi kilele cha sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, zinazotarajiwa kufanyika Desemba, mwaka huu.

Ujasiri wa kukemea maovu

Waumini wa Kanisa Katoliki na Watanzania kwa ujumla wametakiwa kuiombea nchi ili ipate watu wenye ujasiri wa kukemea maovu nchini, ukiwemo ufisadi, kwa kuwa watu wengi wameshindwa kusimamia haki kutokana na kufungwa midomo yao kwa kununuliwa.

Kutokana na baadhi ya watu kushindwa kusimamia haki kumewafanya kushindwa kutofautisha dhambi na isiyo dhambi hatua inayokwamisha hata kumwogopa Mungu.

Alikwenda mbali zaidi na kuwakumbusha waumini utendaji kazi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage, ambapo alisema kuwa kutokana na kuwa na moyo wa kuwatumikia kwa dhati Watanzania ilifika mahali hata akaisahau familia yake na ikabaki ya kawaida sana ambayo haina tofauti na familia za wananchi wa kawaida.

"Baba wa Taifa ilifika mahali akawashangaa hata wanaogombania kwenda Ikulu, alihoji sana na ndio maana familia yake ni ya kawaida tofauti na watoto wa viongozi wa siku hizi ambao wana fedha kibao na sijui wanazitoa wapi, hivyo kama waumini tunatakiwa kuiombea nchi yetu amani," alisema.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam kwenye mkesha wa pasaka na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kitunda, Padri Maximilian Wambura wakati akitoa mahubiri katika ibada hiyo.

"Katika kipindi hiki tuna kila haja ya kuliombea taifa letu amani...viongozi wetu wanatakiwa kuombewa sana kwa kuwa hata magamba wanayodai kujivua hakuna kitu chochote, imefika mahali watu wameshindwa hata kutofautisha dhambi na neema kwa kuwa muda wote wako ndani ya dhambi na wengine wameshindwa kusimamia ukweli kutokana na midomo yao kufungwa na plasta," alisema Paroko Wambura.

Ibada hiyo ya pasaka pia ilikuwa na matukio mbalimbali yakiwemo ya baadhi ya waumini kuokea sakaramenti za ndoa, ubatizo na kipaimara ambao nao aliwataka kudumu katika imani yao na kuachana na tabia ya kuhama hama makanisa kwa kuwa kufanya hivyo ni kukwepa kubeba misalaba yao.

Alisema kuwa ukwepaji wa kila mmoja kubeba msalaba wake umewafanya baadhi ya wananchi kudanganyika kutokana na matatizo yanayowakabili yakiwemo maradhi, kufarakana kwa ndoa, tamaa ya mali yanayofanya kujikuta wakihangaika na kubadili makanisa kwa kukimbilia mengine ambayo yameanzishwa kwa tamaa za kifedha.

"Kuna wimbi la watu kuhama hama makanisa lakini wengi ukiwachunguza utabaini wamekata tamaa, wapo wanaotaka watajirike kwa kuombewa, wapo wanaokwenda kwa kusumbuliwa na maradhi lakini Mungu wetu anasema kama unaumwa nenda hospitali na ndio maana kawaweka madaktari na kama unahitaji mali unatakiwa ufanye kazi sana...pamoja na kuwepo kwa watu ambao wamepewa nguvu za kiroho lakini kama muumini unatakiwa kuubeba msalaba wako," alisema.

Akiwaasa wanandoa aliwataka kuwa wavumilivu na kutokuwa na makuu kwa wenza wao kwa kuwa siri ya ndoa ni uvumilivu.

"Ndoa nyingi zinasambaratika kwa kuwa wengi wanataka makuu, wanataka kulipiza visasi kwa wenzao wao na matokeo yake huwa ni mabaya zaidi, hivyo kama ndani ya ndoa mmetofautiana mnatakiwa kuwaona hata wazazi na mkishindwa zipo taratibu hata za kumwona padri ili awasaidie kumaliza tatizo lenu," alisema.
 
Mapitio ya Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba 2011
ban.sheria.jpg


Allan Kajembe​

amka2.gif
KWA kuzingatia umuhimu katika kutunga katiba ya wananchi wa nchi hii, na itakayozingatia matakwa ya wanachi, nimeona ni muhimu kufanya mapitio ya Muswada wa Sheria ambao wananchi wengi hawajapata nafasi ya kuusoma.
Na kwa wale waliousoma, baadhi yao wameshindwa kuuelewa na kwa wale waliouona inawezekana kuwa lugha iliyotumika imewanyima fursa, kwa kiasi fulani kujua mantiki na maudhui yake.
Kwa kuzingatia unyeti wa suala lenyewe, nimeona ni vizuri nikapitia kifungu baada ya kifungu cha muswada huu.
Kwanza, ningependa niwafahamishe wananchi kwamba, huu si muswada wa katiba kama wengi wanavyoelewa, bali ni muswada wa kutunga sheria itakayoleta /kusababisha marejeo ya katiba.
Maana yake ni kwamba, muswada huu ukipita kama ulivyopangwa, utakuwa sheria, ambayo kwao ndiyo marejeo ya katiba yatafanyika.
Kwanza muswada huu umegawanyika katika sehemu sita, kuna sehemu ya kwanza ambayo ni ya utangulizi, sehemu ya pili inahusu masharti, madhumuni ya muswada huu, uthibitisho na viapo vya wajumbe wa tume na sekretarieti ya kuratibu marejeo ya katiba.
Sehemu ya tatu inahusu masharti ya kuanzishwa kwa tume ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi kwa minajili ya ‘kutunga katiba mpya.'
Sehemu hii pia inahusu sifa za wajumbe wa tume hiyo, hadidu za rejea ambazo zitatolewa na rais, mamlaka ya vyombo vitakavyoundwa kwa ajili ya kuratibu mchakato mzima wa marejeo ya katiba na kadhalika.
Katika sehemu ya nne, inahusu utaratibu wa utendaji wa tume pamoja na mamlaka na utaratibu wa kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba tarajiwa.
Sehemu ya tano inahusu mamlaka ya rais kuunda Bunge la Katiba, mamlaka ya Bunge hilo liliundwa na rais na kadhalika.
Katika sehemu hii, muswada huu pia unaelekeza utaratibu wa utekelezaji wa Bunge la katiba.
Sehemu ya mwisho inahusu uhalalishaji wa katiba kwa kura ya maoni kama ambavyo itasimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kwa kuanza sehemu ya kwanza ya muswada huu ni yale madhumuni ya muswada huu, ambayo yameanishwa katika utangulizi kuwa ni kutoa muongozo wa kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba na pia kuanzisha mchakato na utaratibu wa kuanzisha taasisi kwa ajili ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba ikienda sambamba na kuweka uwanja kwa marejeo ya katiba na uhalalishwaji wake.
Pia kuweka utaratibu wa kuandaa na kuwasilisha taarifa ya maoni ya wananchi juu ya vyombo mbalimbali za kikatiba, taratibu za kuweka Bunge la Katiba, kura ya maoni na masuala yote yanayohusiana na hayo.
Haya yote ni madhumuni ya muswada huu kama yanavyoelezewa na dibaji (long title) ya muswada huu.
Jina la sheria hii limeanishwa chini ya kifungu cha 1(1) cha muswada huu, na itaanza kutumika kuanzia Juni mosi, mwaka huu, kama ambavyo kifungu cha 1(2) cha muswada huu kinavyoeleza.
Kwa mujibu wa kifungu cha 2, sheria hii itatumika sehemu zote za nchi yetu kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Madhumuni ya sheria hii yameainishwa katika kifungu cha 4 kuanzia herufi (a) mpaka (l) cha sheria hii, na kimsingi yanafanana na maudhui ya muswada kama niliyoyaeleza hapo juu, kama yanavyosemeka katika utangulizi wa muswada huo.
Rais (ambaye kutokana na tafsiri ya muswada huu, ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar na baada ya kupokea ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na baada ya kuzingatia taarifa yeyote au muktadha/mazingira ya wakati huo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ndani ya Jamhuri ya Muungano, anaweza kuanzisha tume kwa ajili ya kuupitia, kuuchambua na kushauri utungwaji wa katiba au katiba iliyopo kuongeza wigo, na kuhamasisha utawala wa sheria na utawala bora.
Atafanya hivi, muda wowote baada ya kuchapisha amri hiyo katika gazeti la serikali.
Tume hii, kwa mujibu wa kifungu cha 6(1) cha muswada huu, itakuwa na wajumbe ambao watachaguliwa na rais, na idadi yao ni lazima iwe sawa kutoka Tanzania Bara na wale wa kutoka Zanzibar.
Vigezo ambavyo rais atatakiwa kuzingatia vimeainishwa na kifungu cha 6(2) cha muswada huu, kuwa ni pamoja na uzoefu na utaalamu wa wajumbe wa tume hiyo, ushiriki kutoka maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maslahi ya taifa, umri, jinsia na uwakilishi toka katika makundi mbalimbali ya jamii na kigezo chochote ambacho Rais mwenyewe ataona kinafaa kutumika kumchagua mjumbe wa tume hii.
 
Bunge: Muswada wa Katiba haukustahili hati ya dharura


na Irene Mark


amka2.gif
BUNGE limesema Muswada wa Katiba ulioondolewa bungeni kwenye mkutano uliopita, haukuwa na sababu za kuwasilishwa kwa hati ya dharura kama ilivyofanywa na serikali.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akitoa ufafanuzi wa mambo yaliyofanyika wakati wa Mkutano wa tatu wa Bunge, ikiwemo kuondolewa kwa hati ya dharura kwenye Muswada wa Mapitio ya Katiba.
Dk. Kashillilah alisema baada ya serikali kuuandaa muswada huo, waliutangaza kwenye Gazeti la Serikali la Machi 21 mwaka huu hivyo hadi siku ulipofikishwa bungeni ulistahili kupelekwa bila hati ya dharura kwa sababu ulishatimiza siku 21 tangu kutangazwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo alisema hapakuwa na tatizo kuwepo kwa hati ya dharura kwenye muswada ule kwa kuwa kilichotakiwa ni maoni ya wadau ambayo yana uwezo wa kuubadili kabisa muswada huo au kuufanyia marekebisho kabla ya kurudishwa tena bungeni.
"Watu wengi hawakuuelewa ule muswada… wenyewe unasema utaanzisha kamisheni ya kupokea maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya Katiba, hayakuwa maoni ya kufanya marekebisho ya Katiba, kimsingi kuna upungufu kwa sababu kichwa cha habari na maudhui yake ni vitu viwili tofauti.
"Lengo la serikali ni kuunda Katiba mpya, si marekebisho ya Katiba. Wadau wengi wametoa mapendekezo yaliyojikita kwenye kuondoa vipengele kadhaa kikiwamo cha kubadili kabisa jina la muswada huo, kuwaruhusu wadau kujadili Muungano, kumpunguzia madaraka rais, eneo la Mahakama na kipengele cha haki za binadamu.
"Kwa hiyo napenda kuwatoa hofu wananchi kwamba maoni na mapendekezo yao yanafanyiwa kazi, hivyo wategemee mabadiliko kwenye muswada ule," alisema Dk. Kashillilah huku akitoa mifano ya miswada iliyowahi kurejeshwa na kurekebishwa kwenye Bunge ni muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Uchaguzi na Muswada wa kuundwa kwa Baraza la Usalama wa Taifa.
Kadhalika, Katibu huyo wa Bunge alipongeza hatua ya Rais Jakaya Kikwete kuwashirikisha wananchi katika kuandika Katiba mpya tofauti na marais waliotangalia ambao kwa mamlaka waliyonayo kikatiba waliunda kamisheni za kufanyia marekebisho baadhi ya maeneo kwenye Katiba iliyopo.
Mbali na suala la Katiba, katibu huyo alizungumzia utendaji wa Bunge wakati wa vikao rasmi na kueleza kwamba vurugu zinazoonekana hivi sasa ni matokeo ya wabunge wengi wageni kushindwa kuelewa kanuni zinazoongoza vikao vyao.
Alisema si rahisi asilimia 70 ya wabunge wapya kuzielewa Kanuni za Bunge katika kipindi kifupi, hivyo alipongeza busara za Spika Anne Makinda za kuwaelimisha zaidi wabunge hao.
"Tatizo la vurugu mnazoziona ni kwa sababu kuna wabunge wapya asilimia 70, wengi wao ni vijana ambao hawajawahi kufanya kazi serikalini, hivyo hawazifahamu taratibu za vikao kama vile vya Bunge… kama mtakumbuka ofisi hii iliwafanyia semina elekezi mara mbili wabunge wote ili kuwaelimisha kuhusu kanuni na jinsi Bunge linavyoendeshwa, sasa kule wanapewa nadharia, wakiwa bungeni wanafanya vitendo, hivyo si rahisi katika kipindi hiki kifupi wote wakaelewa, ndiyo maana Spika anakwenda nao taratibu.
"Mnachotakiwa kufahamu ni kwamba spika anayo mamlaka ya kumfukuza mbunge kwenye kikao… lakini akiamua kusimamia kanuni hivi sasa atakuwa anawaonea. Ni sawa na watoto wa darasa la kwanza wakizoea wataelewa na haya mnayoyaona yatakwisha.
"Naamini katika mabunge ya Jumuiya za Madola, Bunge letu ni la kistaarabu sana si kama kwingine, huko wanatupiana viatu, kutupiana maneno ya vijembe. Ni mapema mno Spika kuanza kuwaadhibu wabunge, anachofanya ni kwenda nao polepole akiwasaidia kuzielewa kanuni," alisisitiza Dk. Kashillilah na kuongeza kwamba Spika Makinda si dhaifu, bali ni katika uendeshaji wa shughuli za Bunge.
 
Kashilillah amkingia kifua Spika Makinda


*Asema Spika si dhaifu, ana uzoefu mkubwa bungeni
*Amwombea muda kuwafunda wabunge wapya vijana
*Atetea muswada wa serikali wa mabadiliko ya katiba

Na Tumaini Makene

BAADA ya wananchi mbalimbali kuanza kutoa maoni yao juu ya mwenendo wa bunge kama moja ya
mihimili mitatu ya dola, wakikosoa utendaji wa Spika Bi. Anne Makinda, mzigo umesukumiwa kwa wabunge wapya hasa vijana kuwa hawajui taratibu, hivyo spika huyo anahitaji muda wa kuwafunda ili wajue kanuni hadi wakae sawa.

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilillah, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa bunge kuanzia Novemba hadi Machi, utaratibu wa kutunga sheria na matumizi ya hati ya dharura pamoja na nafasi ya spika katika kusimamia mijadala bungeni.

Alisema kuwa mwenendo wa bunge la 10 ambalo lilianza Novemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu, ambao wananchi wengi wameonekana kutoufurahia, ikiwemo kuzomeana na kuzungumza lugha isiyofaa au kutofuatwa kwa kanuni, kunatokana na wabunge wengi kuwa wageni, wakiwa takribani asilimia 69, huku pia wengi wao wakiwa ni vijana.

Dkt. Kashilillah ambaye alitumia muda mwingi wa mkutano huo na waandishi wa habari kuutetea muswada wa kurekebisha katiba, ambao hivi karibuni ulirudishwa serikalini kwa ajili ya kuubadili lugha na kuongeza muda wa kusikiliza maoni ya wadau, alisema kuwa itachukua muda mrefu kwa wabunge wapya kumudu uendeshaji wa bunge kwa kuzingatia weledi wa kanuni.

"Suala jingine ambalo nilitaka kulitolea ufafanuzi na mlielewe vizuri ni juu ya uendeshaji wa bunge, hasa juu ya mambo ambayo yamekuwa yakitokea bungeni, kurushiana maneno, wengine wamefikia hatua ya kulifananisha bunge na shule ya msingi, suala hili linasababishwa na wabunge wengi kuwa wageni.

"Bunge la sasa linatakiwa kuwa na wabunge 357 mpaka sasa wapo wabunge 350 kwa sababau rais hajamaliza kuchagua katika zile nafasi zake 10 alizonazo. Wabunge 239 wanatoka majimboni, watano wanatoka Baraza la Wawakilishi (Zanzibar) mmoja ambaye ni mwanasheria mkuu anaingia kwa nafasi yake, wengine 102 ni viti maalumu wanawake.

"Hivyo zaidi ya asilimia 69 ya wabunge wa sasa ni wapya, wengi wao vijana ambao hawajawahi kufanya kazi serikalini, hawajawahi kushiriki makongamano au mijadala kama ya bunge. Wanahitaji msaada. Tulifanya semina mbili hapa Dar es Salaam, vyama vikuu kwa maana ya Chama Tawala CCM na Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA navyo pia viliwapatia semina wabunge wao," alisema Dkt. Kashililla.

Akimtetea Spika Makinda kuwa si dhaifu, kwani ana uzoefu bungeni akiwa ameshika nafasi mbalimbali, Dkt. Kashililla alisema kuwa mwenendo wa bunge unaonekana kwenda mlama kutokana na wabunge wengi kutokuwa na uelewa juu ya kanuni za bunge ambazo ndizo msingi wa taratibu za uendeshaji wa mhimili huo.

Alisema kuwa itachukua muda kwa spika kuwasaidia wabunge hao wapya ili waweze kuelewa taratibu za bunge na kuendesha shughuli zao kwa weledi wa kanuni.

"Bado hawajapata uelewa mzuri juu ya kanuni, bado wana upungufu, lakini upungufu huu si wa makusudi bali wa kutoelewa kanuni. Bunge letu ni la kistaarabu sana kati ya mabunge machache katika Jumuiya ya Madola, kuna wenzetu hata kutupiana viti ukumbini wanasema ni moja ya starehe za bungeni.

"Kwa mfano kuna kitu tunaita kwa lugha ya bunge 'Catching Speaker's eye', yaani kumfanya spika akuone, kuna njia tatu ambazo mbunge anaweza kutumia mojawapo ni kusimama, au kumtumia memo spika au kubonyeza chombo cha kuzungumzia na atasme kama ni taarifa au ni kuhusu utaratibu...lakini pia;

"Kwa mujibu wa kanuni akisimama spika hakuna mtu mwingine mbunge anaruhusiwa kusimama, mbunge yeyote hata kama alikuwa anazungumza akimwona spika kasimama lazima asitishe kuzungumza na anapaswa kukaa, lakini siku hizi mnaona wenyewe spika amesimama lakini kuna wabunge karibu 10 nao wamesimama tena wanazungumza," alisema Dkt. Kashililla.

Dkt. Kashililla aliongeza kuwa Spika Makinda amekuwa akitumia busara ya kutowaadhibu wabunge ili wajifunze pole pole mpaka hapo watakapoelewa na kuwa sawa na wabunge wazoefu waliokaa muda mrefu bungeni, akisema kufukuzana bungeni au kusimamisha shughuli za bunge kwa sababu ya utovu wa nidhamu wa wabunge 'wawili watatu' si vyema.
 
Katibu wa Bunge amtetea Spika Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:29

Exuper Kachenje
KATIBU wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, amemtetea Spika wa Bunge, Anna Makinda, kuwa kurushiana maneno kulikotokea kwenye mkutano wa tatu wa Bunge sio udhaifu wake, bali inatokana na wengi wa wabunge hao kutojua Kanuni za Bunge na Sheria.

Kauli ya Dk Kashilillah inaonekana kumkingia kifua bosi wake, Spika Makinda ambaye baadhi ya watu wameanza kuhoji uwezo wa utendaji wake katika kuliongoza Bunge."La pili, ni maandiko kuhusu uendeshaji Bunge, ninyi pia mmeandika. Katika mkutano wa Bunge uliopita wabunge kurushiana maneno
Ilitokea hivyo hata baadhi ya watu kuita Bunge shule ya msingi," alisema Dk Kashilillah na kuongeza:
"Asilimia 69 ya wabunge wa sasa ni wapya…hawajawahi kufanya kazi serikalini au kuajiriwa, kushiriki mijadala au makongamano."

Kuhusu umakini, Dk Kashilillah alisema kutokana na hali hiyo, uwapo wa wabunge hao unahitaji uvumilivu na msaada ili kuwawezesha kufanya kazi zao za Bunge."Uwapo wao unahitaji uvumilivu na msaada kuwawezesha kufanya kazi zao," alisema.

Alisema ofisi yake ilitoa semina kuelimisha wabunge kuhusu uendeshaji wa Bunge sanjari na vyama vikuu vya siasa nchini; CCM na Chadema kutoa semina kwa wabunge wake kuhusu masuala ya fedha, sheria na utawala zilizogharamiwa na ofisi yake.

Akijibu swali lililotaka kujua iwapo haoni kurushiana maneno kumetokana na Spika kutojua sheria na kanuni, hivyo kushindwa kuliongoza Bunge, Dk Kashilillah alisema madai hayo hayana ukweli.

Alisema Spika Makinda anajua sheria na Kanuni za Bunge, lakini anachofanya ni kuwalea kwa kufahamu kuwa bado wengi wao hawajui kanuni na taratibu za Bunge, ndio sababu hawafukuzi ndani ya Bunge.

Katika mkutano huo uliofanyika ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam, Dk Kashilillah alizungumzia pia Muswada wa Sheria wa Mapitio ya Katiba, ambao ulisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tatu wa Bunge, lakini ulirejeshwa kwa umma kupata fursa ya kuujadili zaidi.

Dk Kashilillah alisema kutopitishwa kwa muswada huo kutachelewesha hatua za kupatikana kwa katiba mpya, ambayo alisema wananchi ndio wataamua iwapo iandikwe katiba mpya au iliyopo ifanyiwe marekebisho.

Alisema ingawa muswada huo ulitambulika kama ni Muswada wa Marekebisho ya Katiba wa 2011, lakini uhalisia utambulike kuwa ni Muswada wa Kuanzisha Kamisheni ya Kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba.

"..Kikubwa najua mngependa kujua kuhusu Muswada wa Katiba. Ulitammbulika kama Muswada wa Mapitio na Marekebisho ya Katiba ya Mwaka 2011, lakini kimsingi utambulike kuwa ni Muswada wa Uundaji Kamisheni ya Ukusanyaji Maoni ya Wananchi kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba," alisema na kuongeza:
"Sisi tunaona muswada huu ungepita, ungesaidia kuipa muda wa kutosha kamisheni, tulitarajia sehemu ya hitaji la gharama zingeingia katika bajeti ijayo."

Alisema ingawa uliwasilishwa kwa hati ya dharura, lakini ulitangazwa katika gazeti la serikali Machi 11, hivyo ulifikia siku 21 na ungeweza kuwasilishwa kwa njia za kawaida.
 
Raza: Muswada wa Katiba upitishwe kwa uwiano


Na Mwajuma Juma, Zanzibar

MFANYABIASHARA Mohammed Raza, amesema mswada wa kuweka utaratibu wa
marekebisho ya katiba lazima upitishwe na wabunge, kwa
kuzingatia theluthi
mbili kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar, Bw. Raza alisema
mswada huo una umuhimu mkubwa katika misingi ya muungano na kulitaka bunge
lisipitishe muswada huo kwa kuangalia wingi wa idadi ya wabunge.

"Muswada wa kuweka utaratibu wa marekebisho ya katiba upitishwe kwa
kuzingatia theluthi mbili za wabunge kutoka bara na Zanzibar na sio wingi wa
kura," alisema.

Alisema kwamba kabla ya muswada huo kupeleka bungeni matayarisho yake
lazima yaangaliwe na pande mbili za muungano, ili kuondosha mivutano kama ilivyojitokeza na kusababisha muswada huo kukwama kuwasilishwa hivi karibuni.

Hata hivyo, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeleta faida kubwa
kwa vile Wazanzibari wengi wanategemea soko la biashara la Tanzania Bara na
umesaidia kuwaunganisha wananchi wa pande mbili za Muungano.

"Asiyetaka muungano sio mwana halali, na bahati mbaya wanaopinga hawafahamu
faida za muungano, ikiwemo kuwa na umoja," alisema Bw. Raza ambae aliwahi
kuwa mshauri wa Rais wa Zanzibar wa awamu ya tano, katika masuala ya michezo.

Aidha alisema kwamba wakati wa kuzungumza maslahi ya nchi mbili ni vizuri
Wazanzibari wakatumia nafasi hiyo kwa kujenga hoja, kuondoa woga na kuwa
wakweli.

Alisema matatizo mengi yaliyomo katika Muungano yalisababishwa na
wazanzibari wenyewe kutokana na kutokuwa wakweli hasa kusimamia maslahi ya
Zanzibar ndani ya Muungano.

Alitoa mfano alisema nafasi ya rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa
Muungano ilifutwa na Wazanzibari wenyewe kuwa mstari wa mbele kupitisha
suala hilo bungeni bila ya kuangalia maslahi ya Zanzibar.

Aidha alisema kwamba wapo Wazanzibari waliokuwa mstari wa mbele kupinga Rais
wa Zanzibar asiwe na uwezo wa kupigiwa mizinga 21 kwa wageni wa kitaifa
wanapotembelea Zanzibar, kwa vile sio Amiri Jeshi Mkuu wa Majenshi ya Ulinzi
na Usalama nchini.
 
Spika Makinda awashambulia wasomi


na Dixon Busagaga, Mwanga


amka2.gif
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ameonyesha kukerwa na baadhi ya wasomi ambao amedai wamekuwa wakiwapotosha wananchi kuhusu muswada wa kuundwa kwa tume itakayoratibu mchakato wa wananchi kutoa maoni kuhusu Katiba mpya.
Akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga waliokwenda kumsalimu alipowasili wilayani humo kwa ajili ya kuendesha harambee ya uchangiaji wa shule ya sekondari ya wasichana ya St Theresa, Makinda alisema baadhi ya wasomi wanalenga kuupotosha umma juu ya muswada huo.
Alisema wasomi hao ambao wamesoma robo ya elimu inayohitajika, wamelenga kufanya upotoshwaji ili wananchi waamini kwamba serikali imeandaa muswada wa Katiba mpya, jambo ambalo halikuwa na ukweli wa aina yoyote.
Alisema mswada ambao ulisababisha baadhi ya wasomi kuzomea bila kujua nini kimeandikwa, ulikusudia kupata maoni ya wananchi juu upatikanaji wa tume hiyo kulingana na mapendekezo ya rais Jakaya Kikwete.
"Hawa wasomi wetu baadhi yao wamepata elimu robo robo, wanashindwa kuelewa muswada unataka nini…wengine wanazomea kiholela tu bila kuusoma
vyema, hawa ni watu wa kuelimisha kweli?" alihoji Makinda.

Alisema muswada huo uliwasilishwa katika mkutano wa tatu wa bunge, kabla haujasomwa mara ya pili wananchi walipata fursa ya kutoa maoni
katika vituo vya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar lakini kuliibuka vurugu zilizosababisha kurejeshwa serikalini.

Hata hivyo, alisema kamati za bunge zilizokuwa zikiratibu maoni hayo zilipata maoni mengi ambayo yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha taifa linapata utaratibu ambao utasaidia upatikanaji wa katiba mpya.
Aidha, akizungumzia Bunge la sasa, Makinda alisema yeye amekuwa ndani ya Bunge kwa takribani miaka 36 hivyo anafahamu vyema kanuni lakini baadhi ya wabunge hufanya makusudi kusababisha malumbano ili yeye achukue sheria ambazo wakati mwingine zitasababisha vurugu.
Spika Makinda alikuwa wilayani humo kwa mwaliko wa Shule ya St Theresa ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki nchini lakini pia lengo la kuchangia
upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kike lilimgusa zaidi na kukubali mwaliko huo.
 
Profesa Shivji: Katiba mpya itambue azimio la Arusha


na Lilian Lihame na Mariana Mathias


amka2.gif
SERIKALI imeshauriwa kuzingatia maadili katika uandaaji wa Katiba mpya kwa kuzingatia maadili yatokanayo na Azimio la Arusha kwa kufuatilia sheria za misingi ya kanuni za ujamaa na kujitegemea.
Hayo yalisemwa jana katika kongamano la kujadili miaka 44 ya Azimio la lililofanyika jana jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na wasomi wa kada mbalimbali nchini.
Akiwasilisha mada katika kongamano hilo la Azimio la Arusha, Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, alisema dhana ya utawala bora ni muhimu kuzingatiwa ili kwenda sambamba na misingi iliyoasisiwa ambapo azimio hilo lilibainisha haki na wajibu katika nchi.
"Ili tuwe na katiba itakayokuwa na manufaa kwa Watanzania wote ni lazima izingatiwe misingi ya maadili ya azimio la Arusha kwa mujibu wa kanuni ya ujamaa na kujitegemea ambayo itatufikisha katika malengo ya Taifa yaliyoazimiwa kufikiwa ya kuleta maendeleo na kutetea maslahi ya Watanzania wote badala ya watu wachache.
"Vijana wamesahaulika katika Taifa hili la Tanzania na kupewa nafasi ndogo katika jamii hivyo kama uandaaji wa katiba utazingatia maadili ya azimio la Arusha ni wazi Katiba mpya itakidhi mahitaji ya vijana hasa wakifahamu kuwa wanatoka wapi na wanaenda wapi," alisema Shivji.
Muadhiri huyo ambaye ni muumini wa Azimio la Arusha, alieleza kuwa miiko ya ilibadilishwa kwa manufaa ya watu wachache ambao hawana uchungu na taifa.
 
Kwanini Dk. Kashililah hajui udhaifu wa Spika Makinda?
ban.blank.jpg

Abdul Juma

amka2.gif
JUMATANO ya wiki hii, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alizungumza na vyombo mbalimbali vya habari akiwa anajaribu kufafanua rabsha na zomeazomea zilizojitokeza katika kikao cha Bunge lililopita hadi kufikia hatua ya mbunge mmoja kudai milango ya ukumbi ifungwe wazichape.
Katika ufafanuzi wake huo, Dk. Kashilila alionesha dhahiri kumkingia kifua, Spika wa Bunge, Anne Makinda, akisema kuwa hatua hiyo haimaanishi kuwa ni dhaifu bali inatokana na wabunge wengi kutokujua kanuni na sheria za Bunge vizuri kwa sababu ya upya wao.
Anasema kuwa asilimia 69 ya wabunge wa sasa ni wapya, hawajawahi kufanya kazi serikalini au kuajiriwa, kushiriki mijadala au makongamano, hivyo wanahitaji uvumilivu na msaada ili kuwawezesha kufanya kazi za Bunge.
Kwa hamasa kubwa, katibu huyo anadiriki kuwaambia waandishi kuwa ukiwachuguza wabunge wengi wapya wa sasa utagundua hawana hata kanuni za Bunge kwenye mikoba yao.
Kwa kifupi huo ndiyo ulikuwa ufafanuzi wa Dk. Kashilila ambaye anaamini kuwa Spika Makinda ni imara na mwenye kuzijua vema kanuni na sheria za Bunge, hivyo lawama zinazotolewa kwake kuwa ni dhaifu si za kweli.
Binafsi nataka nipingane na Katibu huyu kwa kuwa anaamini wabunge wapya ndiyo watovu wa nidhamu bungeni na ambao hawazijui kanuni. Na siamini kama kuzijua kanuni ni lazima utembee nazo kwenye mkoba kama alivyoeleza.
Sijui ni kwanini Dk. Kashilila hataki kukubali ukweli kuwa Spika Makinda anapwaya, na kwa hali jinsi ilivyo huko mbele huenda tukashuhudia maajabu makubwa kuliko sakata la hoja ya kufungwa kwa milango ili wazichape.
Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo aliwahi kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Spika Samuel Sitta katika Bunge la tisa kutokana na hatua ya mbunge huyo kukaidi amri ya kiongozi huyo badala yake akaendelea kubishana na kiti.
Kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge, Spika akisimama ni lazima mbunge anayekuwa akizungumza akae chini hadi pale atakaporuhusiwa kuendelea kuzungumza. Lakini katika uongozi wa Spika Makinda hali ni tofauti.
Spika Makinda anatatizika na kuelemewa na nguvu za uchama wa chama chake cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kushindwa kutumia kanuni ipasavyo kuwashughulikia wabunge wanaochezea hadhi ya Spika.
Kama ni zomeazomea, Makinda anajua wazi na wala haitaji kuangalia tena kwenye luninga ili kuamini kuwa wabunge wa CCM ndio maarufu wa kuzomea wapinzani bungeni, hasa wapinzani wanapoleta hoja ya kuigusa serikali.
Spika Makinda badala ya kutumia kanuni kuwawajibisha wahusika, anaishia kuwabembeleza na kubishana nao ama kungoja hadi akumbushwe na upande uliokereka na jambo fulani lililokuwa linaendelea.
Huyu ni tofauti na alivyokuwa Spika aliyepita Samuel Sitta. Spika Makinda anataka mawaziri na manaibu wao kujibu maswali kwa kifupi sana ili mradi muda ukifika yawe yamemalizika, hivyo hatoi uwanja mpana kwa upande wa serikali kutoa majibu ya kina.
Kila anaposimama mbunge kuuliza swali, basi utamsikia Spika Makinda akiingilia kati akisema naomba uulize kwa kifupi maana hatuna muda na hata waziri au naibu asimamapo kujibu naye anaambiwa hadithi hizo hizo za kwa kifupi.
Ni Spika huyu huyu amekalia hukumu ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), dhidi ya Waziri Mkuu, bila sababu yoyote ya msingi wakati mbunge huyo alikwisha wasilisha vielelezo vya kuthibitisha uongo wa Waziri Mkuu kama alivyotakiwa kufanya na Spika.
Lakini ni katika mgogoro huo tulimwona Spika Makinda alivyobabaika hadi kusahau kutoa utaratibu kwa Lema, wapi awasilishe utetezi wake. Maana alitangaza utaratibu mzima wa siku husika bila kugusia suala hilo wakati alikuwa amempangia mbunge huyo kuwasilisha vilelezo vyake siku hiyo.
Hadi Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alipoomba mwongozo wa Spika na kuhoji jambo hilo ndipo Spika Makinda aligutuka na kusema Lema atawasilisha utetezi wake ofisini kwa Spika kwa maandishi.
Pengine dawa ya tatizo hili ni ndogo na huenda hata kina Dk. Kashilila wanaifahamu ila hawataki kuisema. Kwamba yafaa sasa tuwe na Spika ambaye baada ya kuchaguliwa kwenye wadhifa huo, avivue vyeo vyote ndani ya chama chake na kubakia huru.
Naamini kama Spika Makinda angejivua ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mkutano Mkuu na Kamati Kuu, bila shaka angekuwa mwepesi wa kuwakemea wabunge wa CCM wanaozomea na kuwakejeli wapinzani kwa kuwa tu ni wachache bungeni.
Hatua hii ya kutenganisha majukumu ya uspika na shughuli za chama inafanyika katika mataifa mengi, wakiwamo majirani zate Wakenya.
Sina shaka kuwa wafuasi wa siasa watakuwa wanakumbuka vyema patashika ya siasa za Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Kama si sheria na utaratibu wao unaomtaka spika kujiengua majukumu ya chama, basi huenda wabunge wasingeapishwa kushika majukumu yao hayo kama katiba inavyosema.
Kwenye kiapo cha utii cha ubunge nchini Kenya, mbali na mambo mengine, mbunge anapaswa kutaja kuwa atakuwa mtiifu kwa rais aliyeko madarakani huku akimtamka kwa jina.
Chama cha upinzani cha ODM kinaamini kuwa kilishinda uchaguzi huo lakini kikaporwa madaraka na chama tawala cha PNU, hivyo wakati wa kuapa, wabunge wa ODM walikuwa wamekataa kumtaja Rais Mwai Kibaki kama kiongozi wao na badala yake walimtaja Raila Odinga.
Spika wa Bunge hilo anatoka upande wa ODM lakini kwa mujibu wa kanuni na sheria za Kenya, mara baada ya kuchaguliwa analazimika kujivua vyeo vyake vyote ndani ya chama chake.
Spika Keneth Marende, alikuwa ni mjumbe wa Baraza Kuu la ODM, maarufu kama Pentagon na alikuwa mstari wa mbele kupinga ushindi wa Rais Kibaki, lakini alipochaguliwa kuliongoza Bunge aliwageuka hata wenzake wa ODM.
Siku ya kwanza kutofautiana na wabunge wenzake wa ODM ni pale alipokuwa akiwaapisha. Kila walipomtaja Odinga kama rais badala ya Kibaki, aliwataka warudie kiapo hicho.
Huu bila shaka ni mfano hai kwa siasa za sasa, kuwa kumbe ili kumuepusha Spika Makinda na lawama za chama chake, anapaswa kuachia madaraka ndani ya chama na kubakia huru katika kufanya maamuzi.
Hili ndilo nilitegemea Dk. Kashilila kama msomi alitazame kwa marefu na mapana yake badala ya kuibuka na kauli za jazba kama wanasiasa wetu akiwa na hoja dhaifu kuwa wabunge vijana ndio tatizo wakati Spika ndiye ameelemewa. Tafakari.


h.sep3.gif

Niachie ujumbe: 0788452350 au mpyafikra@yahoo.com
 
Zanzibar imebadilika lakini…..!
ban.tusemezane.jpg

Padri Privatus Karugendo

amka2.gif
SIKU mbili baada ya sherehe za miaka 47 ya Muungano, TEMCO imeandaa warsha ya siku tatu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Bwawani, Zanzibar kujadili ripoti ya uangalizi wa kura ya maoni na uchaguzi mkuu wa 2010. Naandika makala hii baada ya mada nne kuwasilishwa kwenye warsha hii.
Mada zenyewe zilizowasilishwa Aprili 28, 2011 ni usuli wa kura ya maoni ya kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa (2010) iliyowasilishwa na Dk. Mohammed Bakari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Sheria ya kura ya maoni iliyowasilishwa na Dk. Makulilo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ZEC ilivyoendesha zoezi zima la kura ya maoni iliyowasilishwa na Dk. Ambrose Kessy naye wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ile ya mikakati ya kampeni wakati wa kura ya maoni iliyotolewa na Dk. Bernadeta Killiani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mada nyingine nyingi zitatolewa kesho na kesho kutwa.
Mada hii ya kura ya maoni imefafanuliwa vizuri. Usuli wake na historia ya Zanzibar kuanzia miaka ya hamsini hadi leo hii. Chaguzi zote hazikuleta maelewano, kila baada ya uchaguzi ilikuwa ni machafuko.
Jamii ya Zanzibar imegawanyika kwenye matabaka na sera tofauti za vyama viwili vyenye nguvu. Muafaka wa kwanza, wa pili na watatu haukuzaa matunda, hivyo kura ya maoni kuelekea serikali ya umoja wa kitaifa ni jambo lilikokuwa la lazima, na matunda yake yameonyesha jinsi ilivyokuwa ni lazima kufikia hatua hii.
Watoa mada, wamefafanua vizuri kwamba taasisi ya kura ya maoni ni mpya Zanzibar na pia ni mpya katika Serikali ya Muungano wa Tanzania. Tangu tupate uhuru, hakuna kitu kilichopitishwa kwa kura ya maoni.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ilikuwa ni makubaliano ya watu wawili, yaani Marehemu Baba wa Taifa na marehemu Rais Karume.
Kuunganisha vyama vya TANU na ASP, hakuna kura ya maoni iliyopitishwa, kutangaza Azimio la Arusha, hakuna kura ya maoni iliyoitishwa hivyo Zanzibar, imejenga historia na ni mfano wa kuigwa.
Imependekezwa na watoa mada na kuungwa mkono na washiriki kwamba Serikali ya Muungano, ijifunze kutoka Zanzibar, wakati wa mchakato mzima wa kuunda Katiba mpya, kura ya maoni ni muhimu kabla ya kufikia uamuzi wowote ule.
Upepo unavyovuma, na kwa kuona matunda ya kura ya maoni ya Zanzibar, kuna ushawishi wa kutaka hata na kero za Muungano kufuata nyayo hizo.
Kwamba ipigwe kura ya maoni, ili Watanzania waamue; Muungano, kutengana, serikali moja au serikali tatu lakini kilio cha wengi kwenye warsha hii ni kwamba watu wafundishwe kwa kina juu ya kura ya maoni na umuhimu wake.
Ingawa matunda ya kura ya maoni yanaonekana Zanzibar, zoezi zima lilifanyika bila maandalizi ya kutosha; kiasi kwamba watu ambao hawakushiriki zoezi hilo ni wengi zaidi kiasi cha kubadilisha matokeo ya "ndiyo" na "hapana" kama wangeamua kushiriki.
Mpaka leo haijulikani watu hawa walikuwa upande gani, kwa vile hakukuwa na jukwaa zaidi ya hili la TEMCO, ilibaki kuwa siri kubwa.
Ingawa washiriki kutoka vyama vya siasa mbali ya CUF na CCM, walipinga kwa nguvu zote jinsi zoezi zima la kura ya maoni lilivyoendeshwa; kwamba watu waliotaka kusema hapana, hawakupewa nafasi; kwamba pamoja na sheria ya kura ya maoni kuzuia kampeni ya vyama vya siasa, CCM ilitumia ujanja wa kutumia Jukwaa la kuwatangaza wagombea wake kupiga kampeni ya "NDIYO", kwamba runinga, redio na magazeti vilitumika kupiga kampeni ya ndiyo; na kwamba watu waliotoa maoni yao au kuhoji kura ya maoni walifutwa kazi kama mkuu wa wilaya, aliyefukuzwa baada ya kuhoji kura ya maoni ilionyesha kwamba Serikali ilitaka kuwalazimisha watu kupiga kura ya "Ndiyo".
Vipeperushi vilitumika kama kile chenye Picha ya Mzee Mwinyi na vigogo wengine, kikisema hawa wametia kura ya ndiyo, wewe unasubiri nini? Hata hivyo baadhi wanayaona matunda ya maridhiano.
Hoja inayotolewa ni kwamba agenda ya kura ya maoni haikutoka kwa wananchi wenyewe. Agenda ilitokana na mazungumzo ya watu wawili,( Rais mstaafu Karume na Maalim Seif Sharif Hamad) ambao hawakukubali kueleza ni kitu gani walikubaliana huku kesho na keshokutwa yawezekana maridhiano haya yakawa shida kwa Wazanzibari.
Si lengo la makala hii kuelezea mada hizi zilizotolewa kwenye warsha, bali ni kutaka kuwashirikisha wasomaji wangu jinsi Zanzibar ilivyobadilika.
Wazanzibari wenyewe wamesema kwenye warsha hii kwamba sasa Zanzibar kuna amani, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, aliyekuwa mgeni wa rasmi, wakati akifungua warsha hiyo, aliungama wazi kwamba siku za nyuma Zanzibar, hakukuwa na amani na watu walichukiana kiasi cha kuacha hata kuzikana, Serikali ya umoja wa kitaifa, imebadilisha hali hii na sasa kuna amani.
Pamoja na amani na utulivu unaojionyesha kwenye visiwa hivi vya Zanzibar, bado kuna malalamiko ya chini kwa chini ambayo inaelekea hayana jukwaa, TEMCO imefanya jambo zuri la kuendesha warsha hii, ambayo imeonekana kuwa Jukwaa la wasiokuwa na sauti.
Ukitoa vyama vikubwa vya CCM na CUF, vyama vingine vya siasa Kisiwani Zanzibar, vina malalamiko makubwa, swali la kujiuliza ni je vyama hivi vina wanachama wangapi? Je, hoja zao ni hoja wa Wazanzibari wengi au ni hoja za watu wachache tu?, hata hivyo kwenye nchi ya kidemokrasia, hata wachache ni lazima wasikilizwe na kuwakilishwa.
Wasemaji kutoka kwenye vyama hivi wanasema Serikali ya umoja wa Kitaifa, ni Serikali ya CCM na CUF, kwa maana kwamba watu wawili, yaani Rais mstaafu Aman Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, walikutana, bila kuvishirikisha vyama vingine na kufikia maridhiano yaliyozaa kura ya maoni na hatimaye serikali ya umoja wa kitaifa, na baadaye baada ya uchaguzi vyama hivi vimeunda serikali bila kuvishirikisha vyama vingine vya siasa.
Ingawa sheria ya kura ya maoni, inasema kwamba ili chama kishirikishwe kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ni lazima kipate asilimia 15 ya kura wakati wa uchaguzi mkuu, vyama vya siasa ambavyo havikuweza kufikisha asilimia hizo, vinasema busara ingetumika ili kuondoa picha kwamba serikali ni ya vyama viwili.
Wanasema rais ana nafasi 10 za kuteua wawakilishi, basi nafasi hizo angezisambaza kwenye vyama vya siasa ambavyo havikufanikiwa kufikisha asilimia 15 ya kura, ili navyo vishiriki kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.
Hoja kubwa ikiwa kwamba serikali ya CCM na CUF, inadumaza upinzani, maana sasa hakuna kambi ya upinzani kwenye Baraza la Wawakilishi, hakuna mawaziri vivuli kwani hali hii haiwezi kuleta tija, maana hakuna anayeikosoa serikali.
Hoja nyingine ni kwamba inaelekea wizara zote walizopewa CUF, zinayumba, huku wachangiaji wakitoa mfano wa wizara ya Afya, ambayo wakati ikiwa chini ya CCM, hali ilikuwa nzuri.
Lakini eti leo hii hata mashuka hakuna hospitalini na dawa ni shida kupatikana, pia mfano umetolewa wa wizara ya Viwanda na Bishara, ambayo vitu vingi vimepanda bei na upatikanaji wake umeanza kuwa shida.
Wakati majadiliano yakiendelea kwenye warsha hii ya siku tatu na wachangiaji wakitoa hoja zao kwa uchungu, uwakilishi wa CUF na CCM, katika warsha hii unaonekana kuwa mdogo.
Mpaka sasa amejitambulisha mwakilishi wa Katibu Mkuu wa CCM kutoka Dar esSalaam, pamoja na kwamba TEMCO imetoa mwaliko kwa vyama vyote vya siasa, bado hatujasikia mtu akijitambulisha kutoka CUF.
Ina maana CUF na CCM, hawapendi kusikia ripoti ya uangalizi wa TEMCO? au ndio hivyo baada ya amani kupatikana, siasa zimewekwa pembeni na sasa kazi ni ya kuijenga Zanzibar?
Tusubiri hadi mwisho wa warsha tutaupata ukweli na msomaji wangu utashirikishwa!
 
Muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba uandikwe upya
ban.tafakuri.jpg

Deogratius Temba

amka2.gif
KAMA kuna jambo la kushangaza au kuwashangaa, wabunge wetu wanaotuwakilisha katika Bunge ni jinsi walivyoshindwa kuukataa na kuurudisha serikalini muswada wa sheria ya mapitio ya Katiba wa mwaka 2011.
Muswada huo kama ulivyoelezwa na wachambuzi mbalimbali wa sheria na wananchi waliobahatika kutoa maoni, ulitakiwa kuwa muswada wa sheria ya wananchi wote na sio wa wachache na ulitakiwa kuandikwa upya.
Tumelalamika kuwa muswada una upungufu mkubwa, haukuwa shirikishi lakini leo hii tunakubali uendelee kujadiliwa na wananchi, chini ya uongozi wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria. Hivyo ni kuendelea kuukubali muswada huo. Wanaweza kuweka maoni na marekebisho kidogo lakini sio mengi. Lakini kama tungewarudisha serikali wakauandike upya wangefanya kazi nzuri.
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), na mashirika mengine ya kiraia wamepinga suala hilo, wananchi hawajaridhika na muswada ulivyoandikwa. Uamuzi wa Bunge unaoitaka serikali kuufanyia marekebisho muswada huo na kuutafsiri kwa Kiswahili ni wa msingi ingawa una upungufu. Tulitarajia kwamba Bunge lingeishauri waziwazi serikali kuuondoa muswada huo bungeni na kuanzisha mchakato shirikishi wa kutunga muswada mpya.
Kwa jinsi ambavyo maoni ya wananchi na msimamo wa kuitaka serikali kuandaa muswada mpya unaozingatia maoni ya makundi mbalimbali ya wananchi, ilitosha kwa wabunge kuonyesha ushirikiano wa dhati wa kutaka serikali iandae muswada mpya na si kuendelea kuujadili muswada ambao hata wananchi wanafikia hatua ya kuuchana hadharani.
Wananchi hawapaswi kutungiwa sheria ya kuanzisha mchakato na mfumo wa kutunga katiba mpya na chombo chochote kabla hawajajadiliana na kukubaliana juu ya dira, tunu na maadili ya taifa lao. Msingi wa madai yetu ni upungufu mkubwa uliomo kwenye muswada wa marejeo ya katiba wa 2011 uliowasilishwa na serikali bungeni kwa hati ya dharura.
Muswada huu ulitungwa na serikali kabla ya kuanzishwa kwa mjadala wa kitaifa na ndio maana ulikuwa na kasoro nyingi zisizokubalika na watu wengi waliopata fursa ya kuusoma na kutoa maoni yao.
Mjadala wa kujenga muafaka wa kitaifa unapaswa kuutangulia mchakato wa kisheria wa kutunga katiba mpya. Mjadala wa Kitaifa ndio utakaoainisha: wigo wa uwakilishi wa makundi mbalimbali; sifa za wajumbe wa mkutano wa kitaifa wa katiba na kazi zake; sifa za wajumbe wa tume huru ya katiba na hadidu za rejea za tume hiyo; sifa za wajumbe wa Bunge la Katiba, muundo na kazi zake; na utaratibu wa kuandaa na kusimamia kura ya maoni.
Ili mjadala huo uwe na tija, wananchi wanahitaji muda wa kutosha wa kujadiliana na kukubaliana kwanza juu ya dira, misingi ya kisiasa na kiuchumi na maadili ya taifa lao. Vilevile serikali inahitaji muda wa kutosha wa kukusanya maoni ya wananchi na kuyachambua kabla ya kuandaa sheria ya kusimamia mchakato wa kutunga katiba mpya.
Kazi ya kuandaa na kuratibu mjadala wa kitaifa inapaswa kufanywa na chombo huru kinachoundwa na wataalamu wenye misimamo thabiti na sio vyombo au taasisi za dola.
Ningeishauri serikali, kuheshimu maamuzi ya wananchi yatakayotolewa wakati wa mjadala huo.Kwani maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayozaa sheria nzuri ya mchakato na mfumo wa kutunga katiba mpya.
Bunge linapaswa kutimiza wajibu wake wa kikatiba kwa kuishauri Serikali juu ya namna bora ya kuandaa na kuratibu mjadala wa kitaifa ili wananchi wote waweze kushiriki kwa amani, utulivu na kuvumiliana.
Bunge linapaswa pia kushirikiana na serikali katika kuweka mazingira muafaka ya kisiasa na kisheria ili mchakato wa kutunga katiba ukamilike kwa mujibu wa matarajio ya Watanzania wote.
Tunawataka wanasiasa wote kutambua wajibu wao wa kutetea maslahi ya taifa na kuepuke kuweka mbele masilahi ya vyama vyao wanapowasilisha hoja zao ndani na nje ya Bunge.
Ili kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia haki na wajibu wao wa kuunda katiba mpya, mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa na wadau wote wa siasa nchini: Kuafikiana juu ya mfumo wa kuratibu mjadala wa kitaifa utakaoweka misingi ya kisiasa na kisheria ya kutunga katiba mpya.
Kuafikiana juu ya sheria ya kuunda Bunge la katiba na sheria ya kuandaa na kusimamia kura ya maoni. Sheria hizi zitatungwa na Bunge kwa kuzingatia mapendekezo ya wananchi yatakayotokana na mjadala ya kitaifa ulioratibiwa na tume huru ya katiba.
Kushirikiana kuweka mazingira muafaka ya kisiasa yatakayowezesha wananchi wote kushiriki katika mchakato wa kutunga katiba mpya bila hofu au kuburuzwa na kundi la watu au taasisi yoyote. Bunge kutotunga sheria yoyote yenye lengo au mwelekeo wa kuchakachua mchakato wa kutunga katiba mpya katika kipindi chote cha mchakato wa kutunga katiba mpya.
Kuafikiana juu ya muda wa mchakato wa kutunga katiba. Kuafikiana juu ya namna ya kutoa elimu kwa wananchi wote ili waweze kushiriki ipasavyo katika mchakato wa kutunga katiba.


h.sep3.gif

deojkt@yahoo.com/0715 686575
 
Wasomi waikaanga Serikali Send to a friend Sunday, 01 May 2011 07:02
* SHIVJI ASHANGAA CCM KUTAKA KUREJESHA AZIMIO LA ARUSHA
Elias Msuya

shivji.jpg
Profesa Issa Shivji

WASOMI na wanasiasa mbalimbali wameilaumu Serikali ya CCM kwa kuua Azimio la Arusha na kuanzisha Azimio la Zanzibar lililoua mwelekeo wa taifa. Wakizungumza katika Kongamano la kujadili Azimio la Arusha lililoandaliwa na Chama cha Sauti ya Vijana cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kufanyika katika chuo hicho jana, wasomi na wanasiasa hao walionyesha nia ya kutaka azimio hilo lirudishwe na kuwa moja ya misingi ya mabadiliko ya Katiba.

Awali akitoa mada kuhusu Azimio la Arusha, Mwenyekiti wa Kigoda cha Kitaaluma cha Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, alisema kuwa dalili za kufa kwa Azimio la Arusha zilianza kujionyesha kabla ya Azimio la Zanzibar.
Profesa Shivji alizitaja dalili hizo kuwa ni pamoja na utaifishwaji wa rasilimali za umma, operesheni vijiji iliyotokea mwanzoni mwa miaka ya 1970, vuguvugu la wafanyakazi na hatua ya CCM kushika hatamu. Profesa Shvji ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema pamoja na kufa kwa azimio hilo bado mzimu wake utaendelea kusumbua.

"Walijitokeza watu wenye jazba ndani ya chama na kuhoji uhalali wa Serikali kutaifisha hata maduka, vituo vya kuuzia mafuta. Kwa kawaida Serikali haiwezi kumiliki maduka, lakini walitaka kuichanganya tu ili nao wamiliki," alisema Profesa Shivji. Akizungumzia kuhusu CCM kushika hatamu kama hatua mojawapo iliyovunja Azimio la Arusha, Profesa Shivji alisema kuwa chama hicho ndiyo kilichoshika mwongozo huku Bunge likiwa mtendaji tu.
"Chama kiliposhika hatamu, kilikuwa chama dola, Bunge lilikuwa na kazi ya kutekeleza tu, viongozi nao walishika ‘utamu'," alisema.
Kuhusu vyama vya siasa, Profesa Shivji alikumbusha kauli ya Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kusema kuwa angependa nchi iwe na vyama viwili vikubwa vya upinzani vinavyofuata mfumo wa ujamaa, lakini mpaka sasa karibu vyama vyote vinafuata ubepari.
"Hadi sasa hakuna hata chama kimoja kinachofuata ujamaa na kuwajali wananchi, vyama vyote vinafuata mrengo wa kulia. Hata wakipata matatizo wanakimbilia kwenye balozi za nchi za kibepari," alisema.
Kuhusu Azimio la Arusha katika mchakato wa Katiba, Profesa Shivji alisema katiba mpya siyo suluhisho, bali maoni ya wananchi pekee ndiyo yanapaswa kuangaliwa zaidi.
Shivji alitanabaisha: "Katiba mpya siyo mwarobaini au kikombe cha Babu wa Loliondo kinachotibu maradhi yote. Kitu cha muhimu ni mchakato, wananchi watatoa malalamiko yao, manung'uniko kulingana na mahitaji yao."
Akichangia mjadala huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikiri umuhimu wa Azimio la Arusha na kuhimiza vijana kujitokeza na kulirudisha.
"Leo huwezi kuzungumza historia ya nchi yetu bila kutaja Azimio la Arusha. Kwa kuwa Profesa Shivji amesema kuwa haiwezekanai kulirudisha ila tunaweza kuirejesha misingi yake, basi vijana tujifunge mikanda na kufanya hivyo ili tutoke hapa tulipo," alisema Nnauye.
Hata hivyo, akihitimisha kongamano hilo, Profesa Shivji alimkosoa Nape akihoji kuwa CCM itawezaje kulirudisha Azimio la Arusha wakati ilishindwa kulitetea?
"Sijui kama bado Nape yupo, lakini alizungumzia kuhusu kulirudisha azimio. Ni kweli sasa CCM wafikirie kulirudisha azimio. Lakini watalirudishaje wakati walishindwa kulisimamia? Ni swali tu najiuliza," alisema Profesa Shivji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisahihisha dhana iliyojengeka kuwa kulikuwa na Azimio la Zanzibar akisema, "Hakuna Azimio la Zanzibar, ndiyo maana nikasema fanyeni utafiti, siyo mnasimama hapa chuo kikuu na kusema kuwa kulikuwa na Azimio la Zanzibar. Kile kilikuwa ni kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Zanzibar," alisema Butiku.

Alifafanua kuwa kikao hicho kilipokea maombi ya waliokuwa viongozi wa CCM ambao walilalamika kuwa miiko ya Azimio la Arusha ilikuwa inawafanya kuwa ombaomba, ndipo wakaomba masharti yalegezwe.
Hata hivyo, alisema baada ya kuruhusiwa, ndipo matajiri walipopata mwanya wa kujilimbikizia mali.
Butiku alifahamisha kuwa miiko ya Azimio la Arusha ilikuwa migumu mno kuifuata.

"Miiko ya Azimio la Arusha ilikuwa migumu. Nyie tukiwaletea miiko hiyo mtaimudu?" alihoji Butiku.
Naye Balozi Ibrahim Kaduma, aliyewahi kuwa Waziri wakati wa Mwalimu Nyerere, alisisitiza juu ya umuhimu wa maadili ya uongozi kama njia ya kukomesha ufisadi nchini.
Hata hivyo, Kaduma alimkosoa Profesa Shivji katika suala la maadili aliposema kuwa maadili hayafundishwi darasani bali yanaigwa tu.
"Inawezekana kweli miiko ya Azimio la Arusha haikuwa maadili, lakini lengo lake lilikuwa ni kujenga maadili. Kwa hiyo maadili yanafundishika, yakikomaa yanakuwa utamaduni wa nchi. Mmomonyoko wa maadili ndiyo umeleta rushwa, wizi na ufisadi," alisema Kaduma.

Tofauti na makongamano ya kujadili mchakato wa kupata Katiba mpya yanayofanyika katika ukumbi huo na kutawaliwa na vurugu, kongamano hilo lilitawaliwa na utulivu huku watu wakisikiliza hoja kwa makini. Hili ni kongamano la pili kufanyika chuoni hapo siku za hivi karibuni baada ya lile la katiba mpya lililowafanya washiriki kujadili kwa jazba.
 
Comments




0 #15 Yusuph Kutegwa 2011-05-01 10:25 Acheni unafiki,maendel eo ni process na tusifikilie kuwa tulala na kuamka asubuhi tukute Tanzania imeendelea.Nawashangaa mnaotaka tuendelee lakini moyoni mmekumbatia dira za na dhamira za udini na ukabila.Hakika nwaambia Tanzania itaendelea pale tutakapo tambua kuwa kila mtu ni BINADAMU na ana HAKI kama mwingine.THATS IT.
Quote









0 #14 Mtonga 2011-05-01 09:52 Kurudisha azimio la arusha haiwezekani kwani ni sawa kula matapishi ulio tapika kwani hao wenzetu wenye dhamana tayari wameshajirudiki a mali. Mfano mdogo wanashindwa kutoa taarifa idadi ya mali zao kwe tume ya maadili. Je wataitaji azimio la arusha?
Quote









+2 #13 SINA 2011-05-01 09:45 Kurudisha Azimio la Arusha ni sawasawa na kupiga hatua mbili mbele tatu nyuma. Hivi viwanda vilikufa katika kipindi gani? Ulikuwa ubishi wa Rais wa awamu ya kwanza Hayati Kambona alimwambia wachague mkoa mmoja iwe kama Pilot kwanza lakini kutokana na ubishi wake akahamua afanye anavyotaka wakati katika hicho kipindi tulikuwa na wataalam wachache. Hali jaribu kuuwa upinzani wowote uliokuwepo dhidi yake leo watu wanathubutu kusema fulani Fisadi lakini si wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza kwa hiyo watu hawakuweza kumchallenge ni jinsi gani utaendelea kama hakuna changamoto kwako. Naamini kuna mazuri aliyoyafanya kama Rais lakini watanzania walimfanya kama mtu ambaye hana makosa ilo lilikuwa kosa kubwa. Nashangaa leo karibu watu wote wanajaribu kuwin majority kwa kutolea mfano wa Mwalimu (RIP) lakini huku ni kurudi nyuma tunachotakiwa ni kwenda mbele Prof Shivji ndio awa wakulahumiwa kwani wao ndio walikuwa wasomi wa kwanza waliotegemewa lakini wamefanya nini hata kubadilisha mfumo wa elimu Tanzania wameshindwa wapo chuoni many decades. Imefika wakati hata kina Shivji wanatakiwa wawaache vijana wenye fikra mpya.
Quote









0 #12 Kingaaa... 2011-05-01 09:44 Quoting Mangi Lelo:
Quoting LENGAI:
Mangi Lelo Mwalimu Nyerere angeiba angejengewaje nyumba na Jeshi. Mwalimu alivaa pea nane za viatu wakati Mawaziri wake walivaa pea kumi na sita.Mangi Lelo acha kumuonea na kumshuhudia uongo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu alikuwa mwadilifu sana hakuwa Fisadi, Mwizi, Mhujumu uchumi wala mtu wa tamaa.
Mwenyezi Mungu akuangaze na kukupatia ufahamu wa kutosha kumjua Mwalimu na kujua maisha yake. Mimi nadhani sio akili yako imekutuma kumsema vibaya Baba wa Taifa tena marehemu. Nadhani unabuya unga au unavita bangi. Nenda kwa Meshehe, au wachungaji ukaombewe.​
Ni uzembe wake na dangaya toto kukaa kwenye nyumba ya jechi.Nyinyi watoto wa juzi...mshukurini mzee ruksa..mulivaa magunia.Kama si wizi nini kuchukua mali za watu kwa nguvu.Na sasa hizo nyumba za so called mali umma zinauzwa tena kwa bei chee,sisi wachagga tunamtambua aliiba tuu.​
Asilimia tisini ya mafisadi ni wachaga...
Quote









+1 #11 msamaria mwema 2011-05-01 09:28 shida nnayoiona ni kwamba uzalendo umetutoka sana mioyoni mwetu sio wote wasemao "MASLAI YA TAIFA"wataendelea kusimamia hapo daima wengi wanajificha nyuma ya kauli hii.kila mtu amepania akikamata kitengo shida zote kwisha.wazee wote ambao walifanya kazi kwa uadilfu serikalini tena kwenye idara nyeti tu, hawakufanikiwa kua matajiri.KINACHONISIKITI SHA ZAIDI jamii inayowazunguka leo inawaona walikua ma[NENO BAYA]. kama azimio la arusha litaturudishia nchi kutoka kwa MAFISADI [wa elimu au pesa]na kuturejeshea uzalendo[na kuona uadilifu sio u[NENO BAYA]]kila lakheri lije.na kwa kuanzia lianze na hawa hawa [JAMAA WA TATU]rafki zake mobutu
Quote









+1 #10 Mangi Lelo 2011-05-01 09:14 Quoting LENGAI:
Mangi Lelo Mwalimu Nyerere angeiba angejengewaje nyumba na Jeshi. Mwalimu alivaa pea nane za viatu wakati Mawaziri wake walivaa pea kumi na sita.Mangi Lelo acha kumuonea na kumshuhudia uongo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu alikuwa mwadilifu sana hakuwa Fisadi, Mwizi, Mhujumu uchumi wala mtu wa tamaa.
Mwenyezi Mungu akuangaze na kukupatia ufahamu wa kutosha kumjua Mwalimu na kujua maisha yake. Mimi nadhani sio akili yako imekutuma kumsema vibaya Baba wa Taifa tena marehemu. Nadhani unabuya unga au unavita bangi. Nenda kwa Meshehe, au wachungaji ukaombewe.​
Ni uzembe wake na dangaya toto kukaa kwenye nyumba ya jechi.Nyinyi watoto wa juzi...mshukurini mzee ruksa..mulivaa magunia.Kama si wizi nini kuchukua mali za watu kwa nguvu.Na sasa hizo nyumba za so called mali umma zinauzwa tena kwa bei chee,sisi wachagga tunamtambua aliiba tuu.
Quote









+1 #9 Katiba TANGANYIKA 2011-05-01 08:58 KWANINI KILA KITU CHUO KIKUUUUUUUU!!!

Huu ni uzembe kupita kiasi, hao wasomi wa chuo kikuu ndio kina nani? Ndio wanaoteseka vijijini? ndio wanaoshika jembe bila mavuno vijijini????

Kama vyuo na shule zipo nyingi , kwahiyo kama tatizo ni majengo ya mijadala! na hata viwanja na maeneo ya wazi yanapatikana vijijivi na mijini pia.

Mijadala yote ikiwemo kuhusu KATIBA MPYA, Azimio la Arusha nk, ifikishwe kwa wenye nchi mitaani na haswa vijijini, na kuacha kasumba ya kudai wasomi ndio wenye mawazo yenye kujenga nchi wkt walala hoi ndio wenye nchi na walipa kodi.

Vyama vya siasa inabidi kuliangalia hilo swala.

Kingine ni kwamba kizazi kipya kinatawaliwa na mawazo ya mwaka 47, kwanini tujadili AZIMIO LA ARUSHA, badala kujadili ugumu wa maisha na namna ya kutatua na kutawala nchi vyema , bila kuwa na mafisadi? Hilo Azimio la Arusha ni mhimili wa itikadi za CCM. tuliweke kando kama historia na kujadili hali ya sasa na namna ya kusonga mbele.

Tusipumbazike na mawazo ya kizamani, tusafishe mafisadi na kutawala nchi kwa mawazo ya kisasa
Quote









+1 #8 LENGAI 2011-05-01 08:55 Mangi Lelo Mwalimu Nyerere angeiba angejengewaje nyumba na Jeshi. Mwalimu alivaa pea nane za viatu wakati Mawaziri wake walivaa pea kumi na sita.Mangi Lelo acha kumuonea na kumshuhudia uongo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu alikuwa mwadilifu sana hakuwa Fisadi, Mwizi, Mhujumu uchumi wala mtu wa tamaa.
Mwenyezi Mungu akuangaze na kukupatia ufahamu wa kutosha kumjua Mwalimu na kujua maisha yake. Mimi nadhani sio akili yako imekutuma kumsema vibaya Baba wa Taifa tena marehemu. Nadhani unabuya unga au unavita bangi. Nenda kwa Meshehe, au wachungaji ukaombewe.
Quote









-1 #7 Mangi Lelo 2011-05-01 08:08 Quoting MWAYA:
Mangi lelo mawazo yako ya ndoto za kula kuku usingizini kumbe unakula godoro hayana nafasi eneo hili. Mwl. Nyerere alikuwa mtu wa utu si mtu wa kitu! Kama wazee wako walipi[NENO BAYA] na panga lake wape pole nawe ujirekebishe. Azimio la Arusha lazima lirudi tutengeneze nchi yetu!​
Wewe Mshamba hujaliona athari yake ndio unasema hivyo sasa hivi uko shule na unapelekwa kwa gari sisi tumeliona badala ya kusoma tunalimishwa Azimio La Kurushwa watu wamepoteza mali zao.Wewendio unaota wacha lije ule mavi...
Quote









+1 #6 Burton mwakatumbula 2011-05-01 08:05 Aliyoyaongea Shivji ni ukweli mtupu,wasomi tuwe macho kwani haya yanayotokea hivi sasa ni dalili tosha kuonyesha kuwa nchi inaelekea kubaya.
Quote









+1 #5 MWAYA 2011-05-01 08:02 Mangi lelo mawazo yako ya ndoto za kula kuku usingizini kumbe unakula godoro hayana nafasi eneo hili. Mwl. Nyerere alikuwa mtu wa utu si mtu wa kitu! Kama wazee wako walipi[NENO BAYA] na panga lake wape pole nawe ujirekebishe. Azimio la Arusha lazima lirudi tutengeneze nchi yetu!
Quote









+2 #4 Nauliza 2011-05-01 07:32 Mbona sioni anayezungumzia suluhisho?Tufanye nini kujikwamua?
Azimio la Arusha tuchukue kipi na tusikirudishe kipi na kwa sababu gani?
kidogo mzee Kaduma naona ameelekea huko.
Quote









+1 #3 Bajabir 2011-05-01 07:25 AA lina mambo mema tuuu,lakin kulitekeleza mmmmh,lilimuand aa mwanafunz kua na uwezo wa kujitegemea,
ukilisoma mpaka rahaaaaa
Quote









-2 #2 Mangi Lelo 2011-05-01 07:14 Liletwa tena hilo Azimio la WIZi kama nchi haikufa mara ya pili.Azimio ambalo Nrere aliiba mali za watu kwa kuimia nguvu angekua yuko hai tungempeleka Hague....Mwiziiiii
Quote









+1 #1 rahby4real 2011-05-01 07:10 Mungu ibariki nchi yetu waangamize wote wanaoitafuna nchi kwa njia yeyote,,,
Quote







Refresh comments list

Add comment
 
Makinda: sitishiki, natumia busara

Imeandikwa na Nakajumo James, Mwanga; Tarehe: 1st May 2011 @ 07:45 Imesomwa na watu: 284; Jumla ya maoni: 1








SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amesema hatishiki na yale yanayotokea ndani ya Bunge kwa baadhi ya wabunge kusababisha mabishano na malumbano, akidai Bunge la Tanzania analoliongoza ni miongoni mwa mabunge tulivu duniani.

Aidha, aliongeza kusema kwa kuwa anafahamu vyema kanuni za Bunge lake, lakini analazimika kutumia busara kuliendesha huku akisisitiza kuwa, kama akiamua kutumia sheria, baadhi ya wabunge wataondolewa kwa kubebwa na polisi.


Makinda aliyasema hayo jana wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wakati anazungumza na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo alipowasili wilayani humo kwa ajili ya kuendesha harambee ya uchangiaji wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Theresa.


Alisema yupo wilayani humo kwa mwaliko wa shule hiyo ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki, lakini pia lengo la kuchangia upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kike lilimgusa zaidi na kukubali mwaliko huo.


Spika Makinda alisema, Bunge la Tanzania ni tulivu mno ikilinganishwa na mabunge mengine na kuongeza kuwa malumbano yanayotokea sasa yanasababishwa na baadhi ya wabunge kutoelewa kanuni ipasavyo.


"Waheshimiwa madiwani mimi sina neno na hayo yanayotokea ndani ya Bunge, lakini hata hivyo huwa natumia busara kuliendesha lile Bunge…wakati mwingine nikiamua kutumia sheria, baadhi ya wabunge wataondolewa pale kwa kubebwa na polisi," alisema.


Aidha, Makinda alisema yeye amekuwa ndani ya Bunge kwa takribani miaka 36 hivyo anafahamu vyema kanuni, lakini baadhi ya wabunge hufanya makusudi kusababisha malumbano ili yeye achukue sheria ambazo wakati mwingine zitasababisha vurugu.


"Lipo jambo wanataka nilifanye kisha zitokee vurugu za kudumu…mimi najua nini wanataka, nitaendelea kuwaelimisha kanuni na taratibu za vikao vya Bunge," alisema.


Hata hivyo Spika Makinda alielezea jinsi anavyokerwa na baadhi ya wasomi ambao huwapotosha wananchi kuhusu Muswada wa kuundwa kwa tume itakayoratibu mchakato wa wananchi kutoa maoni kuhusu Katiba mpya.


Alisema wasomi hao ambao wamesoma robo ya elimu inayohitajika, wamelenga kufanya upotoshwaji ili wananchi waamini kwamba Serikali imeandaa Muswada wa Katiba mpya jambo ambalo halikuwa na ukweli wa aina yoyote.


Alisema Muswada ambao ulisababisha baadhi ya wasomi kuzomea bila kujua nini kimeandikwa, ulikusudia kupata maoni ya wananchi juu upatikanaji wa tume hiyo kulingana na mapendekezo ya Rais Jakaya Kikwete.


"Baadhi ya wasomi wetu wamepata elimu robo robo, wameshindwa kuelewa Muswada unataka nini….hawa ni watu wa kuelimisha wananchi kweli, wengine wanazomea kiholela tu bila kuusoma vyema," alisema.


Alisema Muswada huo uliwasilishwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge, lakini kabla haujasomwa mara ya pili wananchi walipata fursa ya kutoa maoni katika vituo vya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar, lakini kuliibuka vurugu zilizosababisha kurejeshwa serikalini.


Hata hivyo alisema Kamati za Bunge zilizokuwa zikiratibu maoni hayo zilipata maoni mengi ambayo yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha Taifa linapata utaratibu ambao utasaidia upatikanaji wa Katiba mpya.

 
Tumechoka kuchakachuliwa
ban.maswali.jpg

Ansbert Ngurumo

NIMECHUNGUZA na kugundua kwamba serikali bado inafanya njama kuhujumu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya. Haitaki kujifunza. Inang’ang’ania uchakachuaji wa mchakato.

Imejiingiza katika harakati chafu za kutumia vituo kadhaa vya televisheni kutetea udhaifu wa muswada wa mabadiliko ya katiba ambao umepigiwa kelele, umepingwa na hatimaye kunyofolewa bungeni.


Serikali ina hasira. Na sasa inafanya njama za kulipiza kisasi kwa mbwembwe.

Kabla ya kukataliwa na wananchi, muswada huo uliokuwa umewasilishwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge Dodoma kwa Hati ya Dharura, uligundulika kuwa na kasoro nyingi za msingi. Wananchi wakaukataa, serikali ikalazimika kuuondoa ili iufanyie marekebisho na kuuwasilisha tena bungeni kwenye kikao cha Bunge cha Juni mwaka huu.

Lakini sasa serikali hiyo hiyo imejiingiza katika kazi chafu ya kumwaga na kusambaza kile kile kilichokataliwa na wananchi, kwa nia ya kuwaghilibu, kama njia ya kupuuza mapendekezo ya msingi ya wananchi.


Kama ambavyo ilitumia vyombo hivyo vya habari kuhadaa wananchi katika mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa Arusha kati ya CHADEMA na CCM, ndivyo inavyofanya sasa kuhusu muswada huu, baada ya kuaibishwa bungeni.


Kuna vielelezo viwili vya haraka haraka. Cha kwanza ni kauli ya Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Sinde Warioba, aliyenukuliwa na gazeti moja akisema: “hakukuwa na haja ya kupeleka Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011 kwa wananchi kwa kuwa wabunge ni wawakilishi wao.”


Hii ni kauli ya kushangaza na isiyotarajiwa kutoka kwa mwanasheria wa viwango vyake, maana mzee Warioba aliongeza kuwa wanaokataa muswada huu hawalitakii mema taifa hili.


Nataka kushawishika kwamba alikuwa hajausoma muswada wenyewe. Kama aliusoma, halafu akaibuka na kauli hii, naomba nikiri kwamba mzee Warioba amezeeka, amechoka. Aachwe apumzike!


Alisema: “Hivi naomba mjihoji kwanza, hasa nyie waandishi wa habari, ni mara ya kwanza kuwa na ‘bill (muswada)’ nchini? Kwa nini huu uwe mgumu, kwa nini wananchi ndio waamue wakati Bunge lipo kwa ajili yao? Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, ni muswada gani wa Katiba ulipelekwa kwa wananchi hivi?”

Mzee Warioba amegeuka mateka wa historia. Hataki kuitumia kujifunza mbinu mpya. Anataka kuendelee kunakili makosa ya kihistoria yaliyotebdwa huko nyuma. Hajasiki vema kauli ya wananchi. Wamesema "hatutaki.” Bahati nzuri, serikali imesikia, na imeng’amua hilo. Ndiyo maana imeuondoa muswada bungeni, ingawa kwa shingo upande.


"Shingo upande” hiyo ndiyo inamfanya Waziri wa Sheria Celina Kombani azungukie vituo kadhaa vya televisheni kila asubuhi, kuomba vipindi vya kusemea yale ambayo wananchi wameshamwambia hawayataki.


Na hiki ndicho kielelezo cha pili. Kombani anang’ang’ania kauli ya ile ile ya muswada uliokataliwa.

Baada ya kumsikiliza zaidi ya mara mbili, nimehisi kwamba kitu pekee anachojaribu kutetea ni mamlaka ya rais katika kusimamia mchakato huo kwa jinsi walivyoona wao. Na kwa bahati mbaya, Kombani anang’ang’ania kujadili hoja ya rais kuunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi.

Kinachowashinda Warioba na Kombani ni uelewa wa kawaida kwamba wananchi wanakerwa na usimamizi na uendeshaji wa mchakato.


Wananchi hawasemi rais asihusike kuunda tume, bali asipewe kauli ya mwisho. Wanataka kauli ya mwisho iwe ya wananchi wenyewe kupitia kura ya maoni.


Lakini kabla lhawajfika kwenye hatua hiyo, wanataka waridhike kwamba mchakato utakaowafikisha huko unazingatia maoni na matakwa yao. Wanataka mchakato unaojali hofu zao na matumaini yao.


Wanapinga kuunda katiba mpya kwa staili ile ile iliyounda katiba za zamani zinazolalamikiwa. Hawaombi serikali iwahusishe, bali wanadai haki yao ya kuandika katiba mpya inayotokana na utashi wao. Warioba na Kombani hawalielewi hili?


Wananchi wanataka mamlaka ya rais kuunda tume yasitokane na hiari yake binafsi, kama ambavyo muswada huu unadokeza. Wanataka muswada uzae sheria ya kumlazimisha na kumwekea misingi na vigezo vya kuunda tume hiyo.


Kwa jinsi kifungu cha tano cha sehemu ya pili ya muswada, kinavyosema, rais halazimiki kushauriana na mtu yeyote anapounda tume hiyo.


Walichotuletea kina Kombani kwenye muswada ni kile kile cha huko tulikotoka. Na huko tulikotoka, anakosifia Mzee Warioba, ndiko kumezaa katiba za mwaka 1961, 1962, 1964, 1965 na 1977. hizi ndizo tunazolalamikia, na huko siko tunakotaka kwenda. Warioba na Kombani hawalitambui hilo?


Nakubalina na hoja sahihi za Celina Kombani katika kujadili kifungu cha 9(2) kinachozungumzia tunu za kitaifa ambazo tunapaswa kuzienzi.


Zilizotajwa ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar; nguzo tatu uza dola (utendaji, mahakama na bunge); urais; Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; Umoja wa kitaifa; uchaguzi wa kidemokraisa wa mara kwa mara; kukuza utu na heshima ya mwanadamu, na utawala wa sheria; serikali kutoshikamana na dini; na uhuru wa mahakama.


Wapo waliotafsiri kwamba kifungu hicho kinatuzuia kuyajadili masuala hayo. Lakini baadhi ya wataalamu wa sheria – na sasa nimemsikia Kombali akizungumza lugha kama yao – wanasema mambo haya yanajadilika, isipokuwa wanaoyajadili hawaruhusiwi kuyavunja.


Hapo napo panahojika. Maana sheria yenyewe ya kuandikakatiba ndo inaandaliwa. Bado hatujakubaliana mambo hayo ya msingi. Serikali imejuaje kwamba hayo ndiyo tutakayotaka kuenzi,na hakuna mengine? Na imejuaje kwamba tutaafikiana na serikali juu ya mfumo wa kuyaenzi?


Naamini sehemu ya utata huu wa tafsiri imetokana na lugha iliyotumika kuandaa muswada - Kiingereza. Hakieleweki kwa kila mtu kwa kiwango kile kile. Tukumbuke pia imetumika lugha ya kisheria ambayo haieleweki kwa kila mtu.

Vile vile, muundo wa maneno yalitoyumika haukuondoa mwanya wa utata wa tafsiri.

Lakini serikali ilikurupuka kuweka hitimisho kabla ya mchakato na mjadala kuanza.

Serikali iache watu wajadili hoja kutoka pande zote. Kwa mfano, kama yupo anayedhani kwamba Muungano si muhimu, ajenge hoja. Kama atakuwa na hoja za kutushawishi sisi tunaotaka Muungano usivunjwe, tutamsikiliza. Kama hana hoja ya kutushawishi tutampuuza.

Lakini kuwazuia watu kujadili masuala nyeti kama haya, ni hatua ya kupandikiza mbegu mbaya ya ulalamishi na uchonganishi, ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi huko mbele ya safari. Mchakato huu una lengo kuu moja: kuwawezesha wananchi kuandika katiba yao.


Tume itakayoundwa itaratibu maoni ya wananchi – mazuri na mabaya. Itapima na kufanya uchambuzi baada ya wananchi kutoa maoni yao. Itayafanyia uchambuzi na kuyachuja kwa vipaumbele.


Tume ndiyo inapaswa kuchambua, lakini muswada huu, kwenye kifungu cha 16(3), unampa rais mamlaka ya kupokea ripoti ya tume na kuamua lipi liingizwe na lipi likataliwe.


Kwa maana hiyo, rais anapewa mamlaka ya kukataa, kupindisha au kubadilisha maoni ya wananchi. Rais amepewa uhuru wa kuamua lipi liende, lipi libaki. Hiki ndicho wananchi wanakataa. Warioba na Kombani wanashindwa kuelewa hata hili?

Kifungu cha 13 (2) kinampa tena rais mamlaka ya kuteua katibu wa tume. Maana yake ni kwamba katibu huyo atawajibika kwa rais aliyemtuma. Huko nyuma, tumejaribu mfumo huu katika tume zote zilizowahi kuwapo, lakini tumeishia kunung’unika.

Tusisahau kwamba mamlaka haya ya rais, na uteuzi wa aina hii, ndiyo sababu ya serikali kugoma kurekebisha au kufuta sheria mbaya zaidi ya 40 zilizoainishwa kwenye Tume ya Nyalali miaka 19 iliyopita. Badala yake, hata sasa zinatungwa nyingine mbaya kama zile, au zaidi ya zile.


Uteuzi huo na mamlaka hayo ndiyo sababu za mapendekezo ya Tume ya warioba kushindwa kutekelezwa. Mzee Warioba mwenyewe, mara kadhaa, aliilalamikia serikali ya Rais Mkapa kwa kupuuza ushauri wa Tume yake.


Mtindo huo ndiyo uliosababisha yalimpata Jaji Robert Kisanga katika Tume ya White Paper. Wananchi wamejifunza kutokana na makosa hayo ya kihistoria. Hawataki turejee huko, maana tume zinazowajibika kwa rais hazizai matunda yaliyotarajiwa.


Wanakataa kujifunga minyororo kwa kutegemea maoni, uzoefu na hekima binafsi ya rais. Wananchi waliokwishang’atwa na ‘nyoka’ huko nyuma, wana haki ya kuogopa hata mjusi. Warioba na Kombani hawalioni hilo?


Kuna kituko kingine. Kifungu cha 21(1) kinampa rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba. Hii ni dhambi ambayo tumekuwa tunaitenda huko nyuma. Wananchi wanasema hatupaswi kurudi huko. Wanataka Bunge la katiba lichaguliwe na wananchi wote kwa kura, kama tunavyofanya wakati wa uchaguzi mkuu. Na liwe kwa ajili hiyo tu. Likishamaliza kazi yake linakufa!


Kama serikali inaona ni muhimu kupiga kura kwenye uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais wanaodumu kwa miaka mitano tu, kwanini inashindwa kutambua kwamba tuna haki kubwa zaidi kupiga kura kuchagua wajumbe wa Bunge la Katiba, ambayo ni mwongozo na nguzo ya taifa?


Kwanini Warioba na Kombani wanaendekeza mazoea ya huko tulikotoka, ambako rais aliligeuza bunge lililokuwapo kuwa Bunge la katiba? Mchakato wa wakati ule, kama ulivyokuwa wa Zanzibar mwaka jana, ni mchakato-dola, unaotekeleza matakwa ya watawala. Kwanini Warioba na Kombani hawatambui kwamba wananchi wanataka mchakato-raia wa kupata katiba mpya?


Ajabu nyigine. Katika sehemu ya nne, kifungu 28(2) kinazuia wadau wa mchakato kufanya kampeni ya kuhamasisha wananchi kupiga kura ya maoni ya kuunga mkono au kukataa muswada.


Badala yake, muswada unataka tume ya uchaguzi ndiyo ifanye kampeni hiyo. Sasa kama tume inayosimamia uchaguzi, itafanyaje kampeni huku yenyewe ndiyo mwamuzi? Warioba na Kombani hawalioni hilo?


Niliwahi kudokeza huko nyuma. Nitarudia hapa. Kiinimacho kilichofanyika Zanzibar mwaka jana kilishindwa kuzaa katiba ya wananchi. Ya Zanzibar, kwa mtindo ulioileta, ni katiba ya watawala.


Mchakato uliotumika Zanzibar ni sawa na huu unaopendekezwa na serikali sasa katika katiba ya Muungano. Ndiyo maana hata kura ya maoni ilipopigwa Zanzibar, wanasiasa na wadau wengine walizuiwa kufanya kampeni, bali rais aliye madarakani alihamasisha watu wapige kura ya ”ndiyo.”

Kwa hiyo, ilikuwa kampeni ya upande mmoja. Watawala walikuwa wanahamasisha wananchi wapitishe ”kitu cha wakubwa.” Matokeo ya mchakato wa aina hii hauwezi kuzaa katiba ya wananchi.


Na hiki ndicho wananchi wanachokataa. Wanataka katiba yao, iliyoandaliwa katika mchakato usiofanana na wowote katika ile tuliyowahi kuwa nayo. Warioba na Kombani hawalielewi hili?


Nchini Kenya, wananchi, kwa mfano, wananchi walidai katiba mpya tangu mwaka 1964 lakini, kama ilivyo kwetu, hawakupitia mchakato rahisi, na iliwachukua muda mrefu.


Harakati zenye mashiko juu ya katiba mpya zilianza katika siku za mwisho wa madaraka ya KANU (dada yake CCM katika harakati za kupigania uhuru), mwaka 2002.


Kati ya 2003 na 2005, Kenya imekuwa na mchakato uliozaa miswada mitatu – Muswada wa Ghai, Muswada wa Bomas na Muswada wa Wako.


Katika yote, muswada wa Bomas ndiyo ulikuwa unawakilisha maoni ya wananchi. Lakini Rais Mwai Kibaki aliwageuka wananchi, akatumia mwanya wa vifungu vinavyofanana na vya muswada wetu nilivyotaja hapo juu na vingine, kupuuza maoni ya umma.


Akamtumia waziri wake wa sheria, Moses Wako, kupitia upya maoni ya wananchi (muswada wa Bomas) ili kutengeneza muswada unaowafaa wakubwa uliojulikana baadaye kama Muswada wa Wako.


Bahati nzuri, Wakenya walibaini njama za Rais Kibaki. Wadau wakagawanyika. Serikali ikameguka. Walipofanya kampeni na kupiga kura ya maoni, wananchi wakaibwaga serikali. Muswada wa rais ukakwama!


Inamshangaza na kumsikitisha sana mzee Warioba kuona serikali inasitisha muswada mbaya wa aina hii. Anashangaa kuona wananchi wanahojiwa katika suala linalogusa uhai wa maisha yao.


Anasikitika kuona wananchi wamekuwa na uwezo wa kuona kasoro zote walizoona, ,ambazo serikali haikuziona (hata hivyo ndiyo iliyoziasisi). Anashangazwa na wasiwasi wa wananchi juu ya haraka ya serikali kupitisha muswada mchafu kwa hati ya dharura.


Hajajua wananchi wamepata wapi nguvu hii. Hajajua kuwa wananchi wamechoka kuishi na kuongozwa kwa mfumo wa kale. Haelewi kwanini wananchi wenye mtazamo mpya hawataki mawazo mapya, na wangependa mchakato mpya. Tumsaideje?


Ndiyo, nakubaliana naye. Hii si mara ya kwanza kwa serikali kuleta muswada. Kwa hiyo? Tutumie mbinu za kale kupata katiba mpya?


Ndiyo, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi. Lakini ni mara ngapi (naye ameshuhudia) Bunge hili hili likishindwa kuwakilisha wananchi?


Mara ngapi Bunge hili limetunga sheria mbovu? Mara ngapi limetumika kutia mihuri miswada michafu ya serikali, kupuuza maoni ya wananchi na kukumbatia maoni ya chama chenye wabunge wengi? Mara ngapi limetumika kama kamati ya chama?


Ndiyo, hakuna muswada wa katiba uliowahi kupelekwa kwa wananchi. Ndiyo maana tumeishia kuwa na katiba yenye viraka. Na ndiyo maana wananchi wameendelea kudai katiba mpya. Wananchi wamechoka kuchakachuliwa! Warioba na Kombani hawana uwezo wa kuliona hili?
 
Mchungaji Lusekelo na harakati za kupigania Katiba mpya
ban.blank.jpg

Betty Kangonga

MJADALA wa katiba unaonekana kuteka akili na fahamu za Watanzania wote hakuna ambaye azungumzii suala hili, ingawa kuna wengi wanaozungumza neno katiba lakini ndani ya mioyo yao hawana ufahamu juu ya kitabu hicho.

Walio wengi wanataka mabadiliko hayo kutokana na kuona baadhi ya sheria na utaratibu uliowekwa katika katiba ya sasa kuwa na mapungufu mengi ambayo hayaendani na hali ya sasa.


Kila kundi katika jamii limekuwa likihakikisha linapiga kelele na kushiriki kikamilifu katika kuchangia juu ya kuanzishwa kwa katiba mpya. Kati ya kundi lililoonekana kuhamasishana na kuchangamkia mjadala huo ni la viongozi wa dini wa madhehebu ya kikristo.


Ni mara chache kukuta viongozi wa hao hasa wale wanaojiita wa kiroho kushiriki katika michakato ya kisiasa lakini hali inaonyesha kuwa kumekuwa na kuhamshana na kupeana taarifa za kuhitajika kuingiza maoni yao katika mjadala wa katiba.


Hivi karibuni wachungaji wa makanisa ya kipentekoste takribani 100 walikutana katika hafla ya chakula cha usiku ambapo inaonyesha kuwa ni nadra sana kukutana kwani kwa taarifa zilizokuwepo kusanyiko kama hilo liliwahi kutokea takribani miaka mitano iliyopita.


Hivyo hali katika ukumbi wa peack cock hotel iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam ilipofanyika hafla hiyo ilionekana tofauti kwani kila mchungaji aliyehudhuria alionekana kustaajabu kumu
ona mwenzake kwa vile hawajaonana siku nyingi ingawa wapo katika jiji moja.


Wengi waliopata nafasi ya kuzungumza walisema kuwa mara nyingi huonana kupitia vipindi vyao mbalimbali wanavyovirusha katika televisheni za hapa nchini.


Akitoa neno kwa wachungaji hao, mchungaji Anthony Lusekelo wa Kanisa la Ubungo Kibangu anasema ubinafsi ndiyo chanzo kikubwa kinachowafarakanisha wachungaji hasa fedha za wafadhili (wazungu) ni tatizo linalowagawanya watumishi hao.


Anasema jambo linalohitajika kufanywa na wachungaji hao kwa sasa ni kujenga misingi mizuri ili kuwa na umoja imara.


Mchungaji Lusekelo anasema kwa sasa taifa linahitaji wachungaji kutokana na kuwepo kwa mabadiliko muamko wa vijana ni mkubwa ukilinganisha na miaka ya utawala wa awamu zilizopita.


“Ukiangali upepo wa katiba ni mkubwa watu wameamka hivyo wachungaji nasi lazima tuende na upepo huo maana tukikaa kimya utulivu unaweza kuvurugika,” anasema.


“Sasa hivi ni tofauti na kipindi cha utawala wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akili za vijana zinatembea kama saa….vijana wameamka upepo huo ni mkubwa huku wasomi nao wameongezeka hivyo kila mchungaji asimame katika nafasi yake kuliombea Taifa la sivyo hali hiyo ikiachwa inaweza kuhatarisha amani,” anasisitiza

Anaendelea kusema kuwa ili kuondokana na uonevu unaofanywa na serikali dhidi yao kuna haja ya kuhamasisha waumini kushiriki katika mjadala wa katiba mpya ili kuondoa sheria mbovu iliyoundwa na serikali ya kuyataka madhehebu ya dini kupeleka taarifa za mapato na matumizi ya fedha zao.


Mchungaji huyo anasema bila kuwa na sauti za pamoja serikali itaendelea kuwafuatilia katika suala hilo wakati hawana msaada wa fedha wanazopata kutoka serikalini.


“Kuna sheria ambazo ni za uonevu , ni lazima tuhakikishe tunasimama kwa pamoja haiwezekani serikali hiitaji kupewa taarifa zetu za mapato na matumizi wakati hawatupi fedha …mambo hayo yanapaswa kufanywa na vyama vya siasa ambao wanapata ruzuku,” anafafanua.


Anasema mjadala wa katiba lazima kila mchungaji ahakikishe anauchangamkia kwani kuna mambo mengi yanahitaji mabadiliko ikiwemo kupigia kelele suala la tume huru bila kuona woga.


Anafafanua kuwa katika mchakato huo wa katiba wahakikishe wanapigania kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi isiyofungana na chama chochote cha siasa.


Anasema haiwezekani rais wa nchi awe ndiye mgombea katika uchaguzi halafu akashiriki kuteua viongozi ndani ya tume ya uchaguzi hatua ambayo haitoi haki kwa wagombea wengine.


“Hata mara moja haiingii akilini rais akawa ndiye mchezaji halafu muamuzi tukategemea matokeo yakawa ya hayana upendeleo inamaana kuwa Tume ya Uchaguzi imechaguliwa na rais naye anagombea tutawezaje kupata haki hili tusilikubali?” anasema Lusekelo.


Anaeleza ni lazima waumini wahakikishe wanapigania jambo hilo na kuingizwa katika katiba mpya ili hata ikitokea rais ameshindwa kuwajibika basi anaweza kuondolewa hata kabla ya miaka 5 kumalizika.


Mchungaji Lusekelo anasema ni muhimu wachungaji wakaliangalia hilo ili kujenga nchi yenye amani kwa kuwa ndiyo wanaotegemewa katika taifa.


Anasisitiza kuwa wachungaji kuhakikisha wanaliombea Bunge maana kwa hali ilivyo sasa linatia huruma na limepoteza muelekeo hasa ikizingatiwa ndipo panapojadiliwa masuala ya msingi ya nchi.


Anasema serikali inapaswa kuacha kubagua viongozi wa dini ambapo kuna wakati mwingine, wengine huonekana bora zaidi huku wote wakifanya kazi moja ya kulijenga taifa.


Kwa upande wake Askofu Mgullu Kilimba wa Kanisa la Christian Mission anasema kuwa wachungaji watumie fursa ya mjadala katiba kushiriki kikamilifu ili kupata Katiba inayokubalika na Watanzania.


Anasema sambamba na hilo wahakikishe wanaiombea nchi ili mchakato huo uende kwa amani na utulivu bila kuangalia itikadi za vyama vya siasa kwa vile katiba itakayopatikana itatumiwa na Watanzania wote.


Naye Dk. Vernon Fernandes wa Kanisa la huduma ya Agape anasema kuwa wakati akiwa katika maombi alipata neno la unabii kwa mwaka 2011 kuwa ni mwaka wa kuwa na umoja na wachungaji kuungana kuwa pamoja.


Anasema namba moja moja ni nadra kutokea na pindi zinapotokea lazima Mungu anataka kufanya kitu, hivyo jambo hilo limejidhirisha baada ya kualikwa katika hafla hiyo.


Hafla hiyo ilianza majira ya saa 1 usiku mei 3, ilipambwa na nyimbo mbalimbali za dini huku wachungaji wakiamka na kugongeshana glasi zao kuonyesha hali ya kukubali kuwa kitu kimoja.


Mshereheshaji Haris Kapiga ambaye ni mtangazaji wa Radio Clouds alionekana kuimudu vyema kazi hiyo hata pale alipoombwa na Dk Fernandes kumsaidia kutafsiri lugha ya Kiingereza aliyotumia hakuyumba.


Pamoja na yote shampeni zisizo na kilevi zilifunguliwa, na kila mchungaji aliyehitaji alipatiwa sambamba na kuandaliwa kwa kila aina ya supu, chakula kizuri na matunda ambapo majira ya saa 3 usiku hafla hiyo ilimalizika.

Huku Mchungaji Lusekelo akiahidi kuwakutanisha wachungaji hao kila baada ya mwaka mmoja.
 
[h=3]Mashoga Dar wataka kutambuliwa kikatiba[/h]
Stella Aron na Mohamed Hamad

SERIKALI imeombwa kuangalia kwa upana suala la mchakato wa uandaaji wa katiba mpya kwa kuweka kifungu kitakachowasaidia mashoga kuondokana na
adha na kero ya kunyanyapaliwa.

Ombi hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Bw. Abdul Zungu ambaye ni shoga na mwanaharakati katika tamasha la jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

Alisema kuwa kutokana na hali waliyonayo asilimia watu wengi katika jamii wamekuwa wakiwatenga na kuwanyanyapaa na kusababisha kuishi
kwa hofu na hata kutishiwa kuuawa kwa silaha.

Alisema pia wapo baadhi ya mashoga waliopoteza maisha kutokana na kuuawa na wanapofuatilia huwa kesi zao hazitiliwi maanani kutokana na kukosa utetezi.

"Tuna haja ya sisi kupata mwakilishi katika ngazi za maamuzi na ndio maana tunataka katiba yenye kututambua kama sehemu ya jamii inayopaswa kulindwa na kupata huduma za kibinadamu, " alisema Abdul.

Bw. Zungu alisema wanashangazwa na jamii kuwatenga na kuwanyima
kuwapa huduma muhimu kwa tuhuma kuwa vitendo wanavyofanya havimpendezi Mungu.

"Tunaiomba Serikali iangalie upya kwa kuweka kifungu ambacho
kitatulinda kwani kutokana na hali yetu tumekuwa tukikumbana na
kero mbalimbali ikiwemo ya kutengwa na jamii, " alisema.

Mshiriki huyo alisema kuwa licha ya umoja wao kuwa na sifa mbalimbali lakini wanapofanya maombi ya kazi katika ofisi mbalimbali wamekuwa wakinyimwa bila ya sababu.

Alidai kuwa si kwamba hawana uwezo wa kufanya kazi yoyote ya kuwapatia maslahi bali kinachofanyika ni kukosa nafasi hizo na kujikuta hawana kazi ya kufanya na badala yake huendeleza
ushoga ili kupata kipato cha kuwawezesha kuishi.

"Kama Mungu angekua hatupendi basi hata leo sisi tusingeweza kuishi hapa duniani nanyi hivyo hakuna sababu ya kututenga kuishi nanyi. Haya ni matwakwa yake," alisema.

Kwa upande wa suala la afya alisema wamekuwa wakinyanyapaliwa hasa pale
wapohitaji huduma hizo na wakati mwingine huduma hizo huzipata
kwa ubabe kwa baadhi ya madaktari ama kutopata kabisa.

Alisema ni vyema Serikali ikawatambua mahali walipo ili nao waweze kuchangia katika mapambano ya kuunda katiba mpya ambayo itajibu mahitaji yao.

"Kama katiba haitatutambua hakuna mtu ambaye anaweza akasimama kidete kututetea na badala yake ushoga utaendelea kila kukicha huku makundi yasiyokuwa na maadili yakiibuka ndani ya jamii," alisema.

Alisema mbali ya kundi lao ambalo linaonekana kutengwa pia kuna makundi mengi ambayo Serikali imeshindwa kuyatambua na kusema katiba nzuri ni ile inayogusa makundi yote ndani ya nchi yao.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Ananilea Nkya alisema njia pekee ya kujibu matatizo ya wananchi ni kupatikana kwa katiba inayotokana na
matatizo ya wananchi wenyewe hivyo hakuna sababu ya kuanza kujadili idadi ya kurasa wakati matatizo hayajainishwa.

"Wakati mwingine utasikia viongozi wa Serikali wakikosoa jitihada za wanaharakati wakidai kuwa wanaleta mlolongo wa mambo mengi ni katiba gani tutakayoandika yenye kuingiza mambo yote hayo?, " alisema

Hata hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya mashoga katika tamasha hilo na kuwa kivutio kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria ambao hawajapata kuwaona 'laivu' huku wengine baadhi ya wakiangua kilio na wengine kicheko.
 
haki za binadamu kwa mashoga...............................May the Almighty GOD intervenes just for me.......................not in my lifetime, at least............
 
[h=4]13 Maoni:[/h]
blank.gif

Anonymous said... Dduh huu ni mtihani kweli, sasa tuko katika Ulimwengu mwingine na hizi ndio dalili za KIYAMA!!!Hakuna dini wala mila zinazoruhusu hili jambo lakini limeshaingia ktk jamii, na haliepukiki limeshashamiri na kuota mizizi.Wazazi na jamii tuwe makini na vizazi vyetu tuhakikishe tunawapa mafunzo na maadili mema tusije tukaingia ktk mmomonyoko huu!!
September 15, 2011 10:32 PM
blank.gif

Anonymous said... HUU NI UOVU MKUBWA NA NI CHUKIZO KUBWA MBELE ZA MUNGU. MSITAKE KUIGEUZA TANZANIA KUWA SODOMA HATUTAKI LAANA KWENYE NCHI YETU. TUONDOLEENI BALAA HAPA. TENA ZINATAKIWA ZITUNGWE SHERIA KALI ZA KUWADHIBITI
September 15, 2011 11:13 PM
blank.gif

Anonymous said... KATU HATUWEZI KUKUBALI TANZANIA IWE SODOMA. RAIS, WABUNGE NA WADAU WOTE KATIKA KUINDAA KATIBA MPYA WATAKUWA PUNGUWANI IWAPO WATAKUBALI KUFANYA UOVU HUU. MUNGU AWALAANI. PELEKENI USHENZI WENU KWINGINE SI TANZANIA.
September 15, 2011 11:30 PM
blank.gif

Anonymous said... DHAMBI NI DHAMBI NA HAKUNA DHAMBI KUBWA WALA NDOGO WAPEWE HAKI YAO KUNA WATU WANAZALIWA WAKIWA NA HISIA HIZO MOJA KWA MOJA TUTAWAPELEKA WAPI WAKATI KADRI SIKU ZINAVYOZIDI KWENDA NDO WANAZIDI KUONGEZEKA WENZETU AFRIKA YA KUSINI WAMESHAPIGA HATUA
September 15, 2011 11:59 PM
blank.gif

Anonymous said... unajua tumezoea kuhukumu tu,lakini suala la ushoga ni zito sana,hizo ni hisia ambazo mtu anazaliwa nazo kabisa,japokuwa kuna wengine wamejifunza,mimi siongelei hao wanaojifunza,kuna watu kabisa wana hisia hizo tangu wakiwa wadogo kabisa,kabla hata hawajajua ushoga ni nini au mapenzi ni nini, na kuhusu huyo mchangiaji aliyechangia kuhusu laana KAMA LAANA MUNGU ALISHA ILAANI TANZANIA,KWA MAUAJI YA MAALBINO,UFISADI,UJAMBAZI,WIZI NA KILA AINA YA UCHAFU,TUSIONE TU KUWA USHOGA NDIO DHAMBI KUBWA,KUNA MADHAMBI MENGI TU WANAYOFANYA WATANZANIA AMBAYO YANASTAHILI LAANA TOKA KWA MUNGU
September 16, 2011 12:13 AM
blank.gif

Anonymous said... Ningemuona huyu Zungu haki ya Mungu ningemuua kwa mikono yangu miwili. Kufirwa afirwe yeye na aibu yake atuletee sisi ili kuonyesha watoto wetu au vijana wetu ujinga na upumbavu wake, Mbwa huyu, hivi risasi ziko wapi mimi nimmalizie laana mkubwa huyu. Anataka kuwafundisha nini watotowetu wa kiume, mbwa jike yeye, mtoeni hapa nchini, Mungu wangu mimi nikimuona nitamuua. Najuta, ningekuwa Nesi ningemchoma sindano ya sumu ili afe, Kenge huyu. Ana laana toka kwao, mtubisheni huyu shetani wa miguu saba.Aombewe fisi huyu.
September 16, 2011 1:13 AM
blank.gif

Karama said... Nawaomba wananchi kote nchini tumuwinde huyu shoga na amwagiwe acid (tindikali) ya uso iwe ni fundisho kwa wengine.
September 16, 2011 2:08 AM
blank.gif

Anonymous said... wapendwa ushaga ni kitu kibaya katika jamii ila kama alivyosema mchangiaji moja hapo juu kuwa ni hisia za mtu anakuwa nazo tangu utotoni japo wapo wanaoiga na kuanza kufanya hivyo ,hiyo ni kweli kabisa.napenda tu niwashauri wachangiaji wenzangu kuwa tusiwahukumu wala kuwlaani ila tukiwafahamu tujaribu kuwashauri wapo wanaweza acha.haya mambo yapo ulimwenguni kote nasema hivyo mimi nipo hapa ufaransa yaani mashoga wapo wazi sana na wana haki zao wapo wanakubali kuacha tabia hii wakipata washauri wazuri.Hivyo tuwaombee na tuwapokee wanapohitaji kushauriwa pengine pia ni kukata tamaa wanapoona jamii inawatenga.tusiwachoke bali tuwasaidie maana ni ndugu zetu.huu ndio ushauri wangu.asanteni.
September 16, 2011 2:19 AM
blank.gif

Anonymous said... mimi farida
nasema kwakweli dunia imefika mwisho kwa hiyo na wanaume wadhihirishwe kufirwa aaaaaah tena m/mungu awapige laana wawe vipofu maisha yao yote kila anaye taka kufirwa hata wanawake wakiwemo wanaofirwa wapigwe laaana astakafirullah laadhim qiama kimeingia
September 16, 2011 5:03 AM
blank.gif

Anonymous said... Mwanaume anayeona ana hisia za kufirwa akae nazo hisia zake hukohuko mafichoni. Asijaribu kutuletea laana mbaya kwenye nchi kwa kudai katiba ihalalishe mambo ambayo ni machukizo kwa Mwenyezi.
September 16, 2011 8:01 AM
blank.gif

Anonymous said... Ni kweli kabisa wasituletee mafano yao ya ufaransa na hata marekani.Hawa wanao tetea hebu tuwaulize hivi wakisikia kijana wao anafanya matende hayo watajisikiaje?,alafu unakaa nae pamoja mezani mnakula chakula alafu aanze kukuelaza eti basha wake alimhuzunisha sana jana sinaunaweza ukamrukia na kumuua mara moja.Shenzi kabisa we Zungu inabidi tukutafute tukufanyishie usiendelee kuharibu jamii.
September 16, 2011 2:03 PM
blank.gif

Anonymous said... we unaejidai kuwapondea sana,wewe ni madhambi mangapi unayofanya yanayomuudhi MUNGU? je,una uhakika kuwa kila unachokifanya kinamfurahisha Mungu?au unajiona una haki zaidi kuliko wao? au ni msafi zaidi kuliko wao? watu wote ni sawa mbele ya Mungu uwe shoga au usiwe shoga
September 17, 2011 12:39 AM
blank.gif

Mtanzania Halisi said... TANZANIA TUNAKWENDA PABAYA MNO ! NCHI SASA IMEGAWANYIKA KWA KUFUATA MAKUNDI YA KIJAMII. UTASIKIA NIMENYIMWA KAZI KWA SABABU MIMI NI MKRISTO, AU SIJATENDEWA HILI KWA KUWA MIMI NI MWISLAM ! ETI SASA WANATAKA WAPEWE KAZI KWA KUWA NI MASHOGA. BALAA HII
September 17, 2011 12:52 AM

[h=4]Post a Comment[/h]
 
Watanzania wenzangu na hasa wana JF sasa hii ni hatari. Hebu tuweke itikadi zetu pembeni na tuzame katika hili hivi kweli tunahitaji katiba inayowatambua mashoga kwa madhumuni na visingizio vya haki za binadamu. katiba ambayo baadhi ya wananchi akiwemo kiongozi wa nchi wanapendekeza katiba ya Tanzania isiyo na dini. Hivi tunajipenda kweli na kuipenda nchi yetu. Hivi ni kweli tutakuwa na katiba inayowataja mashoga halafu tukahoji matendo ya zinaa. kwanza hao walioandaa na kutoa fursa ya mawazo hayo wanastahili toba maalumu wafunge maana jehanamu ipo mwenye masikio na asikie
 
Back
Top Bottom