Mkutano wa Lissu waahirishwa Ukerewe, figisu zatajwa

Mkutano wa Lissu waahirishwa Ukerewe, figisu zatajwa

omugabire

Senior Member
Joined
Jun 17, 2019
Posts
128
Reaction score
174
Leo jumamosi 26.9.2020, mgombea Urais kupitia CHADEMA, mhe. Tundu Lissu alitarajia kufanya mkutano mkubwa jimbo la ukerewe kwenye viwanja vya stendi mpya mjini nansio.

Umati mkubwa wa watu ulijotokeza kwenye viwanja hivyo kumlaki na kusikiliza sera zake ambapo kwa mujibu wa ratiba ulikuwa ufanyike saa tatu asubuhi.

Mpaka saa sita mchana, mgombea huyo wa kiti cha Urais alikuwa bado hajafika jimboni ukerewe akitokea wilayani bunda. Ikumbukwe baada ya kuchelewa kufika asubuhi ilitarajiwa atafika saa sita na nusu mchana.

ilipotimu mishale ya saa saba na nusu mchana akizungumza na umati mkubwa wa watu uliojitokeza, mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, ndg. Sijaona james karoli alieleza sababu za kuhairisha mkutano huo huku sababu ikitajwa kuwa ni figisu kwenye kivuko cha ferry kati ya bunda na ukerewe.

"Ndugu zangu wana ukerewe, mheshimiwa Rais mtarajiwa hatofika kwenye mkutano huu kutokana na ferry kuamriwa kuondoka kabla ya muda na walipofika ng'ambo waligoma kumuijia" aliongeza.

baada ya kueleza sababu hizo za kuhairisha mkutano, mbunge huyo amewasihi wananchi waliojitokeza kutawanyika huku mkutano huo ukisogezwa mbele.

"makamanda leo mkutano hutofanyika badala yake mheshimiwa Rais mtarajiwa amehaidi kufanya mikutano mitatu mikubwa katika jimbo letu siku ya tarehe 7 na atatumia usafiri wa ndege(chopa) badala ya ferry hivyo nawasihi mtawanyike kwa amani" alimaliza.
 
Mtu mzima akienda kunya porini kijijini husingizia anaenda porini kuangalia mitego yake kama kuna mnyama kanasa

Lisu anaumwa tena sana kapewa ED

La kusingizia Ferry ni uongo
 
Bora apande ndege kuliko hivyo vivuko. Ni hatari kwa usalama wa mh Rais mteule. Wanweza kuzamisha kivuko ili afe ziwani ht km watakufa raia wengine
 
Viongozi wa dini wa Tanzania Sina maneno yanayotosha kuelezea chuki yangu dhidi yenu nampenda sana shetani kuliko viongozi wa dini wabtanzania. Except mwingira shekhbponda mwamakula na BAGONZA kutia ndani shoo.
 
Bora apande ndege kuliko hivyo vivuko. Ni hatari kwa usalama wa mh Rais mteule. Wanweza kuzamisha kivuko ili afe ziwani ht km watakufa raia wengine
Anaumwa ana ED ndege za kukodi mwanza ziko kibao angeagizia taarifa ni kuwa anaumwa yuko hoi
 
Back
Top Bottom