Leo jumamosi 26.9.2020, mgombea Urais kupitia CHADEMA, mhe. Tundu Lissu alitarajia kufanya mkutano mkubwa jimbo la ukerewe kwenye viwanja vya stendi mpya mjini nansio.
Umati mkubwa wa watu ulijotokeza kwenye viwanja hivyo kumlaki na kusikiliza sera zake ambapo kwa mujibu wa ratiba ulikuwa ufanyike saa tatu asubuhi.
Mpaka saa sita mchana, mgombea huyo wa kiti cha Urais alikuwa bado hajafika jimboni ukerewe akitokea wilayani bunda. Ikumbukwe baada ya kuchelewa kufika asubuhi ilitarajiwa atafika saa sita na nusu mchana.
ilipotimu mishale ya saa saba na nusu mchana akizungumza na umati mkubwa wa watu uliojitokeza, mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, ndg. Sijaona james karoli alieleza sababu za kuhairisha mkutano huo huku sababu ikitajwa kuwa ni figisu kwenye kivuko cha ferry kati ya bunda na ukerewe.
"Ndugu zangu wana ukerewe, mheshimiwa Rais mtarajiwa hatofika kwenye mkutano huu kutokana na ferry kuamriwa kuondoka kabla ya muda na walipofika ng'ambo waligoma kumuijia" aliongeza.
baada ya kueleza sababu hizo za kuhairisha mkutano, mbunge huyo amewasihi wananchi waliojitokeza kutawanyika huku mkutano huo ukisogezwa mbele.
"makamanda leo mkutano hutofanyika badala yake mheshimiwa Rais mtarajiwa amehaidi kufanya mikutano mitatu mikubwa katika jimbo letu siku ya tarehe 7 na atatumia usafiri wa ndege(chopa) badala ya ferry hivyo nawasihi mtawanyike kwa amani" alimaliza.