Mkutano wa SADC na EAC waazimia kuondoa vikosi vya kigeni visivyoalikwa katika ardhi ya DRC

Haya ni maigizo katika hali zote hawa wala hawana uamuzi wowote katika Vita hii...Wanaoamua Vita hii wako wanakunywa kahawa Dubai na Ulaya huko ....
Kuna Shida gani kuwatambua hao wanyamurenge??? Kuna shida gani kumwambia Kagame aache kuiba DRC???
 
Mimi sijaona chochote cha maana zaido ya unafiki na kuogopana. Hapo hamna azimio la maana la kisitisha mapigano na kurudisha amani. sijaona Rwanda ikikemewa wala M23 wakiamrishwa kuondoka wala DRC Governent wakipewa maelekezo yoyote ya kuwatambua na kuwapa uraia Banyamulenge ambao ni raia asilia wa Congo tangu karne ya 18
 
Wamepoteza muda hamna walilofanikiwa.
Nilijua wangekuja na maagizo haya
kuwa M23 wapewe siku 7 wawe awapo Congo baada ya apo majeshi full scale ya Nchi wanachama yaingie Congo mashariki haraka sana kuwaondoa.
 
S
Haya ni maigizo katika hali zote hawa wala hawana uamuzi wowote katika Vita hii...Wanaoamua Vita hii wako wanakunywa kahawa Dubai na Ulaya huko ...
Kumbuka unapojadili migogoro ya nchi nyingine unatakiwa kutumia Diplomasia ya hali ya juu.
 
Nani wa kumkemea Rwanda pale unavyoona?
 
haya maazimio ni ushindi mkubwa kwa wanyamulenge na PK maana sasa ni rasmi sasa hao wanyamulenge ni wana DRC halali ndomaana wamepata mwaliko wa kuyajenga na serikali ya DRC. apa naona Kivu republic imeshazaliwa rasmi.
 
Hao Banyamulengw wasipopewa uraia na haki zao za msingi hawawezi kukubali.

Ingawa inawezekana Kagame kaongeza Banyamulenge, lakini tujiulize kama ndiyo wewe Banyamulenge ambapo kizazi chako kilikuwepo hapo tangu Berlin conference 1884 unahisi ufanyaje unapoambiwa urudi Rwanda na ile hali huko Rwanda hupajui!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…