Kiswahili kilipitishwa na AU kama lugha ya mawasiliano, lakini mwisho nimeona DONE kwa lugha zingine pasipo kiswahili tatizo nini?
Pili sijapenda walivyoa mua, wamefunika kombe mwanaharamu apite. Mbona sikuona Muwakilishi wa M23 au ndio Kagame na Museveni?
Mipaka ya Kongo iheshimike, Kivu na Goma ni sehemu ya DRC siyo uwanja wa vita, M23 wakubali kuishi DRC kwa masharti ya DRC siyo masharti yao.
Kuwaacha M23 bila kuwaonya nikama wameogopwa, au taarifa ilipunguza maongezi yaliyokuwepo?
Anyway tusubiri mengine labda hii ilikuwa supu ya kupasha matumbo, tusubili nyama.