Ok sasa hayo majeshi ya SADC yanafanya nini huko Mashariki mwa DRC?Serikali ya DRC imeshindwa KUWANYANG'ANYA silaha na KUWAPIGA M 23....
Majeshi ya nchi za kigeni yatapiganaje na raia wa kikongomani wenye silaha(M 23)?!!!
Mi nilidhani sababu kuu ni ku prempty mapigano?
Yapo majeshi na vita vinapiganwa hiyo amani gani sasa wanalinda, au wanachukua posho tu hayo mengine tutajijua wenyewe?
Ikiwa ahayana kazi kuna sababu gani wa Majeshi hayo kujirundika huko, ikiwa mapigano yapo na wananchi wanauwawa kwa maelfu?
Au kulinda amani kukoje?
Hawa nchi za SADC haswa ndio wanapaswa kuzuia na kuingilia kati wakiacha hivyo, sioni maana ya wao kukutana bila kuwa na maamuzi?