Mkutano wa SADC na EAC waazimia kuondoa vikosi vya kigeni visivyoalikwa katika ardhi ya DRC

My take

M23 ambae ndie aliekiwasha, katajwa mara moja tu kwenye hiyo comminique.

Itashika hii?

Nimependa uondoaji majeshi ya wageni, cha kushangaza wameogopa kuwataja?
 
Haya ni maigizo katika hali zote hawa wala hawana uamuzi wowote katika Vita hii...Wanaoamua Vita hii wako wanakunywa kahawa Dubai na Ulaya huko ....
Kuna Shida gani kuwatambua hao wanyamurenge??? Kuna shida gani kumwambia Kagame aache kuiba DRC???
M23 katajwa mara moja tu, watakubali kudogoshwa wakati wao ndio waanzilishi.

Ile bwana banamuita Mfilisi atakubali hilo🤣🤣🤣🤣😅

Kazi kweli.

Hii ina reinforce ulichokisema (wanabweka tu?)
Kuna shida gani ya kuwatambua ama kuwaanika hao "wageni"?
 
My take

M23 ambae ndie aliekiwasha, katajwa mara moja tu kwenye hiyo comminique.

Itashika hii?

Nimependa uondoaji majeshi ya wageni, cha kushangaza wameogopa kuwataja?
Nadhani ni hekima ya kidiplomasia....baadhi ya majeshi hayo wakuu wake wako mezani....ni lazima HEKIMA NA BUSARA kutawala
 
Kama hayo ndio maazimio basi, huo ulikuwa ni mkutano wa wapumbavu, waliokutana kipumbavu ili kuja na maazimio ya kipumbavu.
Tulia ww . Ungefanya nn na lugha yako haijastaharabika. ZANZIBAR ASP ni Wastaa Arabu bana
 
Sawa.....

Uhusiano mbovu wa hao M 23 na serikali ya DRC haujaanza hivi karibuni.....

Kabla ya SADC-EAC kuwaingiza mkutanoni mwao ,je serikali ya DRC ilianza lini kukaa katika meza ya kweli ya usuluhishi* na hao watu ?!!
Unaelewa maana ya usuluhishi?

Nafahamu haujaanza jana huo mgogoro, lakini kila chenye mwanzo huwa kina mwisho, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Hao ni mahasimu wasiopendana wala hawataki kufahamiana au kushirikiana, hivyo wanakuwepo mediators ambao wanafanya mikutano ya usuluhishi kama huu unaofanyika sasa.

Wangekuwa wanaweza kukaa meza moja na kuongea tusingefika hapa tulipo.

Huu mgogoro wao na kutokusikilizana na kueleweshana madai yao ni yapi ndiyo yametufikisha tulipo, hao watu wa M23 na DRC hawana maelewano ndio maana kunapiganwa vita, na ndio maana kuna majeshi ya kulinda amani, na ndio maana sasa wanaanza kutengeneza platform ya kuelekea kwenye suluhu ya mgogoro.
 
Nadhani ni hekima ya kidiplomasia....baadhi ya majeshi hayo wakuu wake wako mezani....ni lazima HEKIMA NA BUSARA kutawala
Hii heshima ya Kidplomasia ya Upande mmoja tu siaaki. Ukiwasikia hao wakulu huko nje na Lugha hiyo hiyo ya Kidiplomasia, hawamumunyi.

nadhani Trampu ataounguruma hv karibuni. Wapo matajiri wenye interest zao huko, nadhani pia kwa lugha ya kidiplomasia😁 atasema awalete Mercenaries wamalize mchezo huko. Muda utaongea
 
Haya ni maigizo katika hali zote hawa wala hawana uamuzi wowote katika Vita hii...Wanaoamua Vita hii wako wanakunywa kahawa Dubai na Ulaya huko ....
Kuna Shida gani kuwatambua hao wanyamurenge??? Kuna shida gani kumwambia Kagame aache kuiba DRC???
Tulia mdogo wangu, kula mtori nyama zipo chini. RWANDA wakidharahu hayo maazimio, kitakaxhowakuta Mungu anajua.
 
Unaelewa maana ya usuluhishi?

Nafahamu haujaanza jana huo mgogoro, lakini kila chenye mwanzo huwa kina mwisho, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Hao ni mahasimu wasiopendana wala hawataki kufahamiana au kushirikiana, hivyo wanakuwepo mediators ambao wanafanya mikutano ya usuluhishi kama huu unaofanyika sasa.

Wangekuwa wanaweza kukaa meza moja na kuongea tusingefika hapa tulipo.

Huu mgogoro wao na kutokusikilizana na kueleweshana madai yao ni yapi ndiyo yametufikisha tulipo, hao watu wa M23 na DRC hawana maelewano ndio maana kunapiganwa vita, na ndio maana kuna majeshi ya kulinda amani, na ndio maana sasa wanaanza kutengeneza platform ya kuelekea kwenye suluhu ya mgogoro.
....wanaanza kutengeneza platform ya kuelekea kwenye usuluhishi.....

Kikao cha SADC-EAC hakikuwa cha USULUHISHI mkuu wangu.....

Yametolewa maazimio mengi ambayo yanaanza kutekelezwa kwa KIKAO cha "chiefs of staff of armed forces" ndani ya siku 5.....ndani ya siku 30 watakaa mawaziri wa SADC-EAC....

Tshisekedi na serikali yake watumie njia za kisiasa na kidiplomasia na hao M 23....

#Tanzania Kwanza!
 
Yaani Kagame kawapiga kijeshi, kawafuata Dar kawapiga kidiplomasia, atakuwa sasa hivi anacheeka
baambie.
kuna sehemu nimesema Huyo hata akizomewa na fisi huwa anacheka kicheko cha fisi😂😂😂😂 Jamaa ni mgumu sana👉💥

Wenye mahandaki/migodi yao ya kuchimba dhahabu na rare earth ndio wanaocheka.
 
Tulia mdogo wangu, kula mtori nyama zipo chini. RWANDA wakidharahu hayo maazimio, kitakaxhowakuta Mungu anajua.
Jahazi moja hili....

Kwanini unawalaumu tu Rwanda....

Huuoni mzigo mzito alionao Tshisekedi ?!!

1)Awanyang'anye silaha nzito FDRL....waishi kiraia(kuna kuomba uraia).
2)Akae mezani na M 23 na kuchora "roadmap plan" ya kisiasa na kidiplomasia nao...

Hilo ni ZIGO haswaa...

#Chifu Hangaya tena 2025!
 
....wanaanza kutengeneza platform ya kuelekea kwenye usuluhishi.....

Kikao cha SADC-EAC hakikuwa cha USULUHISHI mkuu wangu.....

Yametolewa maazimio mengi ambayo yanaanza kutekelezwa kwa KIKAO cha "chiefs of staff of armed forces" ndani ya siku 5.....ndani ya siku 30 watakaa mawaziri wa SADC-EAC....

Tshisekedi na serikali yake watumie njia za kisiasa na kidiplomasia na hao M 23....

#Tanzania Kwanza!
Ok sawa sikuwa na taarifa kwamba siyo kikao cha usuluhishi, kama Mkuu wa majeshi aanaanza kutekeleza ni sawa pia kwasababu kisichotakiwa ni mapigano na watu wasio na hatia kuendelea kuuwawa.

Njia za kisiasa haziwezi kuleta muafaka kwa watu wanaopigana miaka yote hiyo. Wao wanataka kujitenga na DRC, na hivyo wanataka eneo la kuitwa nchi.

Ni ama wapigwe wanyang'anywe silaha au wapewe wanachotaka yaishe.
 
Serikali ya DRC imeshindwa KUWANYANG'ANYA silaha na KUWAPIGA M 23....

Majeshi ya nchi za kigeni yatapiganaje na raia wa kikongomani wenye silaha(M 23)?!!!
 
Back
Top Bottom