Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu anatarajiwa kuongea na waandishi wa habari muda wote kuanzia sasa.
Fuatilia updates kadiri zitakavyojitokeza.
- Wakati anazungumza na waandishi wa habari Tundu Lissu amedokeza kuwa kutokana na yale yanayoendelea kwenye Uchaguzi ni vyema CHADEMA wakarudi nyuma na kujipanga upya
Mimi napenda kuamini tunaimba wimbo mmoja, kama hatuimbi wimbo mmoja basi tutakuwa na hali mbaya sana. Kama hatuwezi kukubaliana kwamba Samia anahitaji kukabiliwa kwa pamoja na kauli moja na sisi wote, kama kuna wanaofikiria wataenda mafichoni kukutana na Samia na kuteta, tutakuwa na hali mbaya sana, mimi naogopa.
- Aidha Tundu Lissu alisema katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu 2024 kikubwaa CHADEMA watapigania wagombea waliobaki tu lakini huu kifupi umekwisha kwani udanganyifu umekuwa mkubwa.
- Aidha alisema kuwa CHADEMA kwa sasa kijikite zaidi katika kugombea Katiba mpya, Tume uhuru, Demokrasia, na Haki.
- Pia alidokeza kuwa wagombea wengi wa CHADEMA waliwekewa mapingamizi hata kabla ya majina yao kubandikwa
Singida tulisimamisha wagombea takriban 1225, wamepigwa mpaka tuliobaki nao nafikiri hawafiki 500 zaidi ya nusu wameondolewa pamoja na kwamba kanuni zinasema mapingamizi yataamuliwa ndani ya siku mbili tokea mapingamizi hayo yapokelewe.
Mapingamizi yalitakiwa yapokelewe tarehe 9 na tarehe 10 Novemba. Mapingamizi mengi yameletwa tarehe 8, kwa mujibu wa kanuni, tarehe 8 ilikuwa siku ya kuteua wagombea tu.