Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Kiukweli hao viongozi watakuwa ni wapumbavu sana!
Naona sindano imepenya kwenye makalio tulia Sasa dawa ikuingie bwashe..

Siasa zinawafanya kuwa vipofu na wajinga Sana.
 
Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi, hakuna hata mmoja aliyetokea hadharani kukemea jambo hilo hata angalao kulia pamoja naye.
Maiti zilipokuwa zinaokotwa kule ufukweni, hakuna hata mmoja aliyejitokeza kuhoji watawala watoe maelezo kuwa zilifijaje hapo, licha ya kitendawili kuwa ni za nani. Maiti zilizookotwa mto Ruvu sikuwasikia wakihoji. Mauaji ya Aquilina sikuwasikia. Kwamba Ben Saanane yuko wapi, Azori Gwanda , Simon Kanguye sikuwasikia hata viongozi wa madhehebu yao wakihoji. Amani wanayoiomba ni ipi? Nadhani wangeliomba kuwa haki itamalaki zoezi lote la uchaguzi. Nadhani wangelitubia dhambi ya rushwa iliyotamalaki katika zoezi la awali la watia nia, na kukukemea lisiwepo wakati wa uchaguzi. Nadhani wangekemea kauli kama zile za kutumia vyombo vya dola ili kubaki madarakani n.k. Hawa sio wa kweli wala wa haki wala sio wapenda amani ya kinaukweli. Yarabi tunusuru.
Swala la tund lissu kupigwa risasi na hao wengine Sijui kupotea Niya kiintelijensia zaidi Huwezi ukatoka tu ukaanza kupayuka bila ushahidi wa kutosha Ila Mambo aliyofanya Mh. Rais yanaonekana kwa macho kiasi kwamba hata mtoto wako anaweza kukusimulia vizuri kabisa na akakuelewesha.

Ikumbukwe; mpaka leo pamoja na Lissu kujikuta anajua Mambo mengi na Sheria kibao bado hata yeye hajui namna ya kutetea kesi yake na ya wale wenzake waliopotea alichobakiza nikusema watu wasiojulikana na kulialia online tu Basi.
 
Upepo utakapoanza kubadilika watabadili gea angani. hizo ni bendera bwana.
 
Naomba kuuliza,dhehebu langu RC nao Walikuwepo?nataka Nijue ili nichukue hatua stahiki
 
Swala la tund lissu kupigwa risasi na hao wengine Sijui kupotea Niya kiintelijensia zaidi Huwezi ukatoka tu ukaanza kupayuka bila ushahidi wa kutosha Ila Mambo aliyofanya Mh. Rais yanaonekana kwa macho kiasi kwamba hata mtoto wako anaweza kukusimulia vizuri kabisa na akakuelewesha.

Ikumbukwe; mpaka leo pamoja na Lissu kujikuta anajua Mambo mengi na Sheria kibao bado hata yeye hajui namna ya kutetea kesi yake na ya wale wenzake waliopotea alichobakiza nikusema watu wasiojulikana na kulialia online tu Basi.
Viongozi wa dini ni vinywa vya binadamu wanyonge wanaoonewa na mfumo wowote. Kazi yaoni kuhoji na kukemea watawala wanapoonea watu wengine iwe kwa kutumia diplomasia au kutumia neno la kinabii au njia nyingine yoyote. Watu wanatekwa na kuumizwa na binadamu wajiitao watu wasiojulikana na viongozi wa dini wapo kimya eti tukubali kuwa ni suala la kiintelijensia hivyo wakae kimya. Mie sisemi wafanye uchunguzi. Ila Wawahoji wenye dhamana ya ulinzi wa watu na mali zao. Wawaulize kuwa kulikoni watu wanapotezwa? Kulikoni maiti zinaokotwa zikiwa zimeharibika? Kulikoni lipo kundi jipya llinaloitwa watu wasiojulikana katika jamii yetu?Watake majibu kutoka kwa wasimamizi wa hizo intelijensia kwa niaba ya waumini wao! Nani anatakiwa kuwahoji watawala mambo hayo kama sio viongozi wa dini? MO katekwa halafu kaachiwa na watu wasiojulikana. Roma Mkatoliki katekwa na watu wasiojulikana na akapatikana. Lisu kapigwa risasi na hao. Na hao waliotoweka hawajapatikana wakiwa hai au maiti zao. Haiyumkiniki kuwa hao ni kati ya maiti zilizookotwa mto Ruvu au fukweni? Viongozi wa dini wanao wajibu kwa niaba ya dini zao kuwahoji watawala. Ndio maana tunawashangaa kwa haya wafanyayo sasa.

Sent from my SM-T535 using JamiiForums mobile app
 
You have see the future.
Ndio maana ulaya na Marekani vijana hawana muda na mambo ya dini halafu huwa tunawaona wamepotoka, kumbe wako sahihi [emoji817][emoji817]

Kwa ujinga huu makanisa ni lazima yakose watu ndani ya miaka michache tu mbele.
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu, wao kama wanadamu wanayo haki ya kupenda chama chochote cha siasa lakini kwa hadhi waliyoibeba kwenye jamii hawakupaswa kufanya hivi. Chama tawala kuna sehemu kinaonea baadhi ya watu (HII SIYO SIASA NI UKWELI WA WAZI KABISA) , kuna upendeleo mkubwa wa usambazaji wa huduma za jamii mfano huo umeme alioisemea Mh Waziri Mkuu, unatolewa kwa upendeleo mkubwa sana, vijiji hivyo vina umeme ila wananchi walengwa hawana umeme, maji yanawekwa sehemu kulingana na mlengo wa siasa ulipo kwenye jamaii husika, hospital, stendi nk Kibaya zaidi kuna sehemu wana mlengo wa chama tawala lakini na wao hawana huduma za kijamii. Haya yote viongozi wa Dini wanayajua maana wateja wao ndiyo wahanga. Hawana uwezo wa kutenda usawa, wanaogopa viongozi wa kisiasa mfn mzuri ni Kakobe, mwanzoni alimpinga sana Magufuli lakini walipo mkabili akaaunga mkono juhudi. Mtu yeyote ambaye yuko kinyume na serikali lazima aonekane mbaya na viongozi wetu wa dini wanafumba macho. Nawahurumia sana waumini ambao wanaamini hawa viongoz wa DINISIASA. Hawawezi jifunza juu ya makosa yaliyofanywa na kanisa Katoliki huko Rwanda mwaka 1994 !. Wanasisitiza amani lakini hawasemeo Haki? Tangu lini amani ikawepo pasipo kuwa na Haki? Wakushukuriwa ni Watanzania na siyo serikali, Watanzania wamekuwa wavumilivu wa kipekee sana hata serikali inapaswa kuwashukuru, hata Kenya tu najua hakuna uvumilivu wa kiasi cha Watanzani. Kama isingekuwa ni Uvumilivu wa Watanzania naamini miaka ya hivi karibun tungekuwa na sura nyingine kwenye uso wa Dunia
 
Mkuu ndiyo sababu Watanzania wengi wanaojitambua hawaoni umuhimu tena kwenda misikitini na makanisani kuwasikiliza hawa wanafiki AKA Viongozi FAKE wa dini.

Ukweli viongozi wa dini wamefanya jambo la hovyo sana . Kwanza hawakupaswa kuwa hivyo
 
Kama utaamua kutumia akili na kuacha hisia za uoga, kusujudu na kuabudu binadamu basi utagundua DINI ya kweli huwezi kuipata kwenye NYUMBA ZA IBADA katika karne hii ya 21.

Ni kwasabau DINI zetu zimeingiliwa na Tamaa, chuki, unafiki, ulafi na uongo wa hali ya juu na tunatumia nyumba za ibada kuficha dhambi Hizi. Viongozi wa dini leo hii wanatukana hadharani wapate nafasi za kisiasa, wanachochea chuki na badala ya kuunganisha watu wao ndio chanzo cha matabaka na mgawanyo.

Hakuna Dini nzuri kama kuhubiri na kuishi UPENDO, kusaidia WAHITAJI na kuwasamahe wale wote waliotukusea. Hizi ni bidhaa adimu kwenye dini za leo ambazo viongozi Wamekuwa MABALOZI wanasiasa.

Inasikitisha kuambiwa Watu hawa wanaliombea taifa amani, taifa ambalo linapandikizwa chuki na visasi vinavyopewa baraka na viongozi hao hao wa dini.

Hawa viongozi wa dini ni wa kupingwa vikali na wanasiasa wa vyama vyote sio CCM, CHADEMA,ACT n.k
😁😁
 
Kweli siasa SI HASA. Kuna viongozi wa dini na waumini wanaowaongoza ambao wana ufuasi wa kisiasa tofauti lakini viongozi wanaonesha wanaegemea wapi hata kama jambo(event) lipo kiserikali? Mafungu ya 10 yataendelea kutolewa na wale wengine hata kama ni jambo la kiimani?
Hutaki Serikali iseme mazuri yake?
 
Shenz type Waziri mkuu kenya Hadi kibanda cha kuku ukiwa nayo unawekewa umeme huku kwetu full vurugu
 
Amani ni tunda la haki.
Hakuna hata mmoja aliyetaja neno HAKI?
 
Naimbeni mnijuze kamà Askofu wa moravian yuko hapo niongeze miaka ya kutokwenda kanisani kwa sasa nina miaka 5 kama yupo humo niongeze mengine kama MUNGU WETU atanijalia miaka mingine
 
Kwa mara ya kwanza dini inatumika mwaka huu kuipatia CCM madaraka..

Kuna kitu cha ajabu kitatokea..

Watch this space
Mungu ana jambo lake hapo October 28, Acha wajaeee wote Kwa JPM, kama ulivyokuwa kipindi cha vita Kati ya wanaisraeli vs washami, wakoma kumi tuu kishindo Chao kiliwakimbiza jeshi la washami ndivyo itavyokuwa!

Hii vita Daudi (lissu) vs Goliath (meko)
 
Mungu ana jambo lake hapo October 28, Acha wajaeee wote Kwa JPM, kama ulivyokuwa kipindi cha vita Kati ya wanaisraeli vs washami, wakoma kumi tuu kishindo Chao kiliwakimbiza jeshi la washami ndivyo itavyokuwa!

Hii vita Daudi (lissu) vs Goliath (meko)
Ni wenye ukoma wanne tu mkuu, siyo kumi.
 
Back
Top Bottom