Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Mimi ni muumini kweli ila sikuwahi kuwa hata na mazoea na viongozi wa dini yangu. Kwangu mimi sihitaji kuongozwa kwakuwa najua kusoma yaliyoteremshwa na Mungu ninayemuamini.
Kwangu mimi mtu wa kumheshimu ni mwalimu wangu ambaye sio kiongozi ila wengi ni washikaji zangu tu.
Siwezi kuongozwa na kundi la watu kama Bakwata, aisee hata unishikie kisu siwezi kuitambua Bakwata hata Rais aniambie nitamke hadharani nitambishia hadharani kabisa.
Nawaonea huruma sana wanaohangaika na watu wanaitwa viongozi wa dini, wewe kama muumini nenda zako kaswali achana na hawa watu, wakikuzuia kuswali kwenye majengo yao piga swala nyumbani kwako Mungu yupo kila kona. Wakitishia kususa maziko furahia kabisa washikaji watakuja kukuzika kwani Mungu hana habari na mahubiri yao kwenye mazishi yako kikubwa matendo yako tu.
 
Karibu.

Mkutano uko mubashara kupitia Channel ten kutoka ukumbi wa JNICC na mgeni rasmi ni waziri mkuu mh Majaliwa.

Up dates;

Kwa sasa mh Majaliwa anahutubia na anajaribu kuelezea kwa kirefu mafanikio ya serikali ya awamu ya 5

Waziri mkuu anawashukuru viongozi wa dini kwa dua zao zilipelekea nzige wa hatari kuishia mpakani kwa nchi jirani na wasiingie kwetu kadhalika Corona ikatoweka.
Sijatazama huo mkutano ila naomba unijulishe kama viongozi wangu wa kanisa langu takatifu ninalolipenda sana la KKKT iwapo nao wamehudhurua
 
Ningewaona wazee hawa wa maana kama wangekuwa na uthubutu wa kumwambia Mkuu mapungufu katika utawala wake!! Na yakasemwa kwa umma. Umma upate mazuri na mabaya yake ya awamu hii!! Ili mabaya yarekebishwe!!

Sasa kama unaalikwa ili kuwezesha justification (kutakatisha mapungufu) kama tunavyoona basi hili ni tatizo.

Viongozi wenzako wa dini wako ndani mwaka wa sita..hata kuuliza tu huwezi Je kuna umuhimu wa mkutano!
 
Hili swali nimemuuliza huyo kada John Ila kanijibu kwa hasira sijui kwa nini?
Bwashee siyo kwa hasira ila mkutano wa viongozi wa dini haukamiliki bila uwepo wa mafiga matatu TEC, CCT na Bakwata nadhani sasa umenielewa.

Hao wengine ni wanogeshaji tu sawa na kachumbari kwenye pilau ambapo pilau ni utatu wa mchele, nyama na mafuta!
 
Kweli siasa SI HASA. Kuna viongozi wa dini na waumini wanaowaongoza ambao wana ufuasi wa kisiasa tofauti lakini viongozi wanaonesha wanaegemea wapi hata kama jambo(event) lipo kiserikali? Mafungu ya 10 yataendelea kutolewa na wale wengine hata kama ni jambo la kiimani?
Hawa ni wachuuzi wa dini
 
Asante kwa taarifa. Nishajua cha kufanya kwenye bahasha zangu za Ahadi, Jengo na Uwakili. Fungu la kumi nilishamalizana nao bado hizo zingine
Bwashee usichanganye mambo ya dini na uzima wa milele.....hivi ni vitu viwili tofauti.

Endelea kumtolea Mungu sadaka yako!
 
Huu unaweza kuwa ni usaliti mkubwa wa viongozi wetu wa dini... wanawasaliti watanzania kwa watawala .

Yesu Kristo pia alishitakiwa na MAKUHANI (wakuu wa dini).. Akashitakiwa kwa kosa la uchochezi... akasuruniwa zamani zile za utawala wa warumi, chanzo walikiwa wakuu wa dini wakala njama kwamba ni lazima Yesu asurubiwe!!

Watu wa dini hata kwenye maandiko matakatifu si watu wa kuamni amini..!!
 
Bwashee usichanganye mambo ya dini na uzima wa milele.....hivi ni vitu viwili tofauti.

Endelea kumtolea Mungu sadaka yako!
Yaani natoa sadaka ambazo wao wanatumia kuweka mafuta kwenye magari yao na kuwafikisha huko kwenye mkutano!
Natoa sadaka ambazo wao wanalipwa mshahara.
Natoa sadaka ambazo zinanunulia hayo magari ya kuwafikisha kwenye hiyo mikutano.
Sichamganyi dini na siasa bali ninajua cha kufanya kwenye bahasha yangu ya ahadi,uwakili na jengo
 
Mpumbavu ni wewe unayeyauonea haya ukweli wa mambo, Mazuri yakifanywa na yeyote hata ni Chama kipya kitakachoingia madarakani, ifike mahali Kwanza tuyapende yanayofanywa na kusimamiwa vizuri na viongozi wetu na kutoka kila pahala, yakifanywa na mpinzani tuyakubali na kujivunia pia

Tujivunge Kwa lipi kuyaongelea haya mapinduzi makubwa kabisa yaliyofanyika Chini ya usimamizi wa Raisi wetu? Tujivunge kuipenda nchi yetu na vitu vinavyofanyika Kwa sababu Tu kafanya mtu asiyependwa na wapinzani siyo,

Huo ndio upumbavu sasa, tutayapenda na kujivunia yote atakayokuja kuyafanya mh Lisu Pindi Mungu atakapoona vema awe Raisi wetu

Acha Ujinga kuandika Ujinga
Kiongozi wa nchi ambaye walio na mtizamo tofauti na wake kisiasa wanaadhibiwa halafu viongozi wa dini wanapongeza eti mazuri aliyofanya, hao viongozi wa dini ni wapumbavu!
 
Yaani natoa sadaka ambazo wao wanatumia kuweka mafuta kwenye magari yao na kuwafikisha huko kwenye mkutano!
Natoa sadaka ambazo wao wanalipwa mshahara.
Natoa sadaka ambazo zinanunulia hayo magari ya kuwafikisha kwenye hiyo mikutano.
Sichamganyi dini na siasa bali ninajua cha kufanya kwenye bahasha yangu ya ahadi,uwakili na jengo
Una uhakika gani kama wamefika ukumbini kwa kutumia petrol ya Kanisa?

Kutoa sadaka ni tendo la kiimani zaidi!
 
Una uhakika gani kama wamefika ukumbini kwa kutumia petrol ya Kanisa?

Kutoa sadaka ni tendo la kiimani zaidi!
Kama hawakutumia sadaka kwenda hapo kwa nini basi wanajitambulisha au wanawakilisha viongozi wa kidini. Wangeenda basi kama raia wengine tukawaelewa!!
 
Kiongozi wa nchi ambaye walio na mtizamo tofauti na wake kisiasa wanaadhibiwa halafu viongozi wa dini wanapongeza eti mazuri aliyofanya, hao viongozi wa dini ni wapumbavu!
Sisi kama Taifa, hatuwezi kujivunga kusema kila ambacho kiongozi wetu yeyote Yule kasimamia vizuri Kodi zetu na akafanya vitu vizuri vyenye manufaa kwetu kama Taifa, eti kisa ni wa CCM itakuwa vibaya machoni Kwa wapinzani, eti Kwa sababu kafanya kiongozi Kutokea ACT, CCM wakasirike wanapoona tukiongea mazuri aliyoyafanya Kwa nchi yetu

Huwezi kuzuia hayo Kwa mandiko yako mkuu

Acha wakutane na wapongeze Kwa kuwa hakuna dhambi hata kidogo, na wewe si chochote kwao, utanuna na utaumia bule
 
Ungebadilisha kichwa cha habari kisomeke,mutano wa watoza ushuru na matapeli kupitia kivuli cha dini
 
Back
Top Bottom