Nadhani wewe ni mdogo kiumri na haujui mazingira yaliyopelekea mazingira magumu ya kiuchumi, skiliza: Kilichoharibu uchumi wa Tanzania ni vita vya kagera. Vita vya kagera vilitokea mwaka 1978 na vikaisha kabisa mwaka 1980! Kabla ya vita hivyo uchumi wa nchi yetu ulikuwa mzuri sana, tulikuwa na viwanda vingi sana. Dola moja ya marekani ilikuwa sawa na sh 8 za Tanzania. Tulikuwa na shilingi yenye nguvu sana. Vitu vingi vilikuwa vinanunuliwa kwa senti yaani pungufu ya shilingi moja. Vile vita vilitugharimu sana. Baada ya vita ikatangazwa miezi 18 ya kufunga mikanda. Lakini pia mwanzoni mwa miaka ya 80 kulitkkea ukame mkubwa sana na kukawa na njaa kali. Hiyo pia ikasababisha mambo kuwa magumu. Kipindi hicho ndio kilikuwa kigumu kwa kukosa bidhaa muhimu na Taifa liliishiwa kabisa pesa za kigeni.
Vinginevyo Tanzania ilikuwa inaheshimika sana duniani na haikuweza kuyumbishwa hata kidogo. Awamu iliyopita ilijitahidi sana kurejesha heshima hiyo.