Mkuu wa Kikundi cha Wagner Yevgeny Prigozhin, ametoa maoni yake juu ya mzizi wa matatizo nchini Niger

Mkuu wa Kikundi cha Wagner Yevgeny Prigozhin, ametoa maoni yake juu ya mzizi wa matatizo nchini Niger

Sasa zikitoka kwa Mfaransa, then Mrusi nae ataenda kunyonya?. Au wanataka kubadili Mkoloni? Vipi Mali,na Bukina Faso nazo hari zao kiuchumi si pia mbaya boss. Tukitaka kuendelea tusishawishiwe na Urusi, US, France au China bali tuwe sisi na Tekinolojia yetu tu.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
Ukisoma hiyo taarifa imesema ufaransa inauza kilo ya uranium kwa Dola 259+ lakini Niger inapata Dola 11 tu,prigozin anasema inawezekana kuwa na muwekezaji atayetoa 50/50,so Kama urusi atatoa zaidi kwa nini asipewe!?
 
"Nitajibu ni nini msingi wa mabadiliko ya mamlaka nchini Niger. Msingi(tatizo) ni uchumi. Population ya watu wa Niger imekuwa katika umaskini kwa muda mrefu.

Kwa mfano, kampuni ya Ufaransa iliyochimba uranium iliiuza sokoni kwa $218, huku ikilipa Niger $11 pekee . Unaweza kufanya kazi na wawekezaji kwa msingi wa 50-50 au 30-70 (%), lakini haiwezekani kuwarudishia wazawa wa nchi, ambao walizaliwa katika nchi hii, wanaoishi katika nchi hii, na wanaotarajia hilo. maliasili za nchi hii ni zao, na kwa mujibu wa Katiba, ni mali yao, ni 5% tu ya utajiri unaopokea.

Ili kuficha uhalifu huu wa kiuchumi, nchi ilikuwa imejaa idadi kubwa ya magaidi. Idadi hii kubwa ya magaidi, kinadharia, ingepaswa kudhibitiwa na idadi kubwa ya wanajeshi tofauti, wanaofadhiliwa na UN, Umoja wa Ulaya, Wamarekani, Waingereza, na wengine. Kwa sababu hiyo, wakazi wa Niger, ambao walipaswa kuwa huru na wenye furaha kutokana na fursa za kiuchumi nchini mwao, waliporwa, na ili kuwanyamazisha, waliwekwa katika hofu kwa miongo kadhaa.

Kuonyesha kwamba wezi na waporaji hawa wanahitajika katika eneo la jimbo, namaanisha nchi za Magharibi kama Ufaransa, USA, na kadhalika, umati wa askari walipelekwa huko ambao hawakufanya chochote isipokuwa kupokea bajeti kubwa ambazo pia zilifujwa katika ngazi mbalimbali. Ndio maana mabadiliko nchini Niger yalikuwa ya lazima.

Nguvu iliyokuwa katika muungano na Bazoum (rais aliyeondolewa madarakani) na wafuasi wake, ilifunika tu, kuruhusu muungano wa watu waliopora taifa kuwepo katika eneo la Niger. Ni hayo tu. Kwa hivyo, haya ni mapambano ya ukombozi, harakati za ukombozi wa uhuru wa nchi hii, na Mungu awape mafanikio."

=======================
Mabeberu yamezoea kupora sana maliasili za wanyonge, sasa yamenyang'anywa kwa nguvu kitoweo mdomoni. Ndio maana yanabwekabweka sasa.
 
Vipi ushawai kutengeneza chochote apo nyumbani kwako ambacho tunaweza kulitumia kwa kujitegemea? Au unatumia Tekinolojia ya China, EU, US na Urusi kunitukana. Naamaanisha una Tekinolojia hapo ya Kibantu? Kama unayo una haki ya kunitukana.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
Kama hatuna ndo tusherehekee kutawaliwa.Kumbuka humu hatujawahi kutawala.Fikiri kiakili, mfano kila eneo atawalalo mfaransa likichukuliwa daima.Ataweza kuwa na nguvu alizonazo kiuchumi kwa miaka 50 ijayo?
 
I was just reading this on the current edition of The New Yorker.

hivi kiranga,
wewe hufuatilia vita vya ukraine na urusi?
una maoni gani? Je anachofanya urusi ni sahihi.
 
Mapinduzi ya kijeshi NDIO suluhu la upumbavu wa Waafrika wengi hasa Yale mavyama yanayojiona ya milele
Wakina Mwigulu hawa wanaiba tu hela na kutuongezea kodi, sasa mijitu kama hii ikipinduliwa utasikitika kwa lipi, labda uwe mjinga na mpumbavu.
 
hivi kiranga,
wewe hufuatilia vita vya ukraine na urusi?
una maoni gani? Je anachofanya urusi ni sahihi.
Hii vita haina justification ya maana, hata Yevgeny Prigozhin mwenyewe alishasema.

Ni zile vita za "leo nasikia nyege za kumpiga mtu, niko bored, natafuta medali za ushujaa wa vita, ngoja nitafute kibonde wangu wa karibu nimpige nifurahishe watu wangu na kuwasahaulisha matatizo yao mengine"
 
Mhhh. Ufaransa ana ardhi nyingi anazomiliki( France Territories) kama ardhi yake au nchi yake nje ya Ufaransa, kuliko hizo African francocone au nchi zilizo huru kisiasa lakini zinaitegemea Ufaransa. Ufaransa haiwezi kufirisika kwa sababu ya Hizo nchi za Africa ila hizo nchi za Africa zitateseka kwa kumkosa Ufaransa. Africa haijiwezi na Watu wake ni watu wa Lawama. Hizo chini ni ardhi za Ufaransa inazomiliki katika bahari ya Hindi, Pacifiki na Attlantic, je Senegal au Ivory coast akimkataa Mfaransa, Mfaransa atafirisika?.View attachment 2707833

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
Hivo visiwa kama St. Martin and the like havina rasimali ya kutosha kama zilizopo afrika.
 
Mapinduzi ya kijeshi NDIO suluhu la upumbavu wa Waafrika wengi hasa Yale mavyama yanayojiona ya milele

Kabisa rushwa na uporaji wa rasilimali za nchi kwa mgongo wa demokrasia huku wananchi wakiumizwa haikubaliki lazima viongozi wajinga wafurushwe ili kunusuru rasilimali kwa manufaa ya vizazi vijavyo
 
"Without Africa, France will slide down into the rank of a third [world] power."

—Former French President Jacques Chirac, March 2008
Hili limejionesha hata kwenye mpira
 
Hii vita haina justification ya maana, hata Yevgeny Prigozhin mwenyewe alishasema.

Ni zile vita za "leo nasikia nyege za kumpiga mtu, niko bored, natafuta medali za ushujaa wa vita, ngoja nitafute kibonde wangu wa karibu nimpige nifurahishe watu wangu na kuwasahaulisha matatizo yao mengine"

umeifuatilia historia yake ilipoanzia?
huoni kama warusi walichokozwa?
au hauifuatilii kabisa, kwa sababu sijawahi ona maoni yako kuihusu ?
 
umeifuatilia historia yake ilipoanzia?
huoni kama warusi walichokozwa?
au hauifuatilii kabisa, kwa sababu sijawahi ona maoni yako kuihusu ?
Hili sakata maongezi yake yamekaa kishabiki zaidi na watu washaamua pande wanazotaka ku support kwa sababu ya nostalgia.

Sijaona mtu anayetafuta facts, anayeangalia evidence, kwa hivyo sikutaka kuingia jatika mizozo ya ligi za Simba na Yanga.

Warusi wakichokozwa lini, wapi? Chanzo cha mzozo ni nini? Madai ya Yevgeny Prigozhin kuhusu chanzo cha vita umeyasikia? Unayakubali au unayajibu vipi?
 
warusi walitaka hakikisho la ukraine kutojiunga na nato, west wakagoma.

Kama ujuavyo ukraine imepakana na urusi na nato specifically US huweka silaha zake na majeshi katika nchi wanachama hivyo wangekuwa wamemsogelea sana urusi kama ukraine angekuwa member.

Huoni kama urusi alikuwa sahihi kujihami haraka kabla ukraine na nato hawajatimiza hilo?
 
Kwanza kwa nini Warusi wawapangie Ukraine wajiunge wapi na wasijiunge wapi wakati Ukraine ni nchi huru?
 
Kuna baadhi zinazo, kuna nchi inaitwa French Guiyana ipo Bara la America Kusini imepakana na Brazil, Suriname, na Venezuela ni kubwa pia. Nchi za Ulaya sio kubwa kama Tanzania vile au Congo, lakini zina misuri ya Tekinolojia, Rasilimali watu ilioelimika na kujitambua, na Mpangilio bora wa Uchumi, ndio Maana wanazitawala kifikra nchi za Africa. Tatizo la Africa ni viongozi wake toka Uhuru walikosa kabisa utashi wa misimamo ya usawa, badala yake wakawekeza kwenye Umimi. Africa hivi leo (Tanzania) viongozi wamelisi haiba ya CCM kwanza, wengine watatuchelewesha, kiufupi mpaka Yesu anarudi Africa itakua hivihivi.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
Mkuu,

Uafrika hasa utanzania ni laana.
 
Kwanza kwa nini Warusi wawapangie Ukraine wajiunge wapi na wasijiunge wapi wakati Ukraine ni nchi huru?

unadhani mexico pale akitaka kuungana kijeshi na urusi,marekani atakubali?
unaufahamu mgogolo wa cuba 1961?
 
unadhani mexico pale akitaka kuungana kijeshi na urusi,marekani atakubali?
unaufahamu mgogolo wa cuba 1961?
Kwani mimi wapi nilisema nakubaliana na Wamarekani kuhusu Cuban Missile Crisis?

Cuba na Ukraine zote ni nchi huru na zina haki ya kuamua z8nafanya nini.

Ukiingilia haki hiyo unafanya ubeberu.
 
Kwani mimi wapi nilisema nakubaliana na Wamarekani kuhusu Cuban Missile Crisis?

Cuba na Ukraine zote ni nchi huru na zina haki ya kuamua z8nafanya nini.

Ukiingilia haki hiyo unafanya ubeberu.

ni kweli ni nchi huru lakini kama urafiki wa jirani yangu unatishia usalama wangu basi huyo jirani atafyekwa hakika.

kama ambavyo marekani ange react kwa mexico kama ingeweka uhusiano wa kijeshi na urusi, ndivyo ambavyo urusi ana react pale ukraine inapotaka kujiunga na NATO.
 
Unaji contradict. Halafu unaleta mfano mwingine kwa namna ya "two wrongs make a right".

Two wrongs do not make a right.
 
umeifuatilia historia yake ilipoanzia?
huoni kama warusi walichokozwa?
au hauifuatilii kabisa, kwa sababu sijawahi ona maoni yako kuihusu ?
Unajichosha tu.... Sasa Kwa Majibu anayotoa unataka kumuelewesha nini .....
 
Back
Top Bottom