Mkuu wa kituo Mabwepande huyo Mama uliyemuweka ndani kisa mchango wa ulinzi shirikishi Tsh. 15,000 kwa mwezi, ipo siku utalipa

Status
Not open for further replies.
Wenginec1000, 2000, 3000 mpaka wachache sana elfu 5. Wanaolipa 5000 labda wako na nyumba chache ktk mtaa. Mitaa ya huko ina nyumba nyingi hazipungui 500 kwa bei hiyo wanapigwa.
 
Toa hela ya Ulinzi acha Majungu. Huyo mama yako anawatukana walinzi na kuwavunja Moyo wasilinde mtaa .Mchango huo mlikubaliana wenyewe na serikali yenu ya Mtaa tena mliambiwa asiyeweza kutoa pesa ajitolee kulinda maana jukumu la ulinzi wa taifa ni la kila Raia sasa huyo Mama yako anakiuka makubaliano ya Mtaa wote mbaya zaidi anawatakana Walinzi wa Mtaa .

Kichekesho zaidi kuwa kukataa kushiriki ulinzi ni Makosa ya jiji ukikamatwa unapelekwa mahakama ya jiji sasa kama yupo Polisi tokea akamatwe maana yake ametenda na kosa la jinai.

Wasiolipa michango ya sungusungu wapo wengi tu kwenye Mtaa wenu shida lakini hawajakamatwa ila kwa huyo Mama yenu kuna tatizo zaidi ya hilo Msimsingizie Mkuu wa Kituo Mabwepande kwa tuhuma za Uongo.

LIPA HELA YA ULINZI ACHA MBEEMBWE MTAA WENU WATU WALIKUWA WANAKABWA MPAKA MCHANA LAKINI TOKEA KUUNZA SUNGUSUNGU HATA USIKU HUKABWI. KUMBUKA JUKUMU LA ULINZI NI LA KILA RAIA SOMA KATIBA YA TANZANIA IBARA YA 27 NA 28
 
Mkuu huo ndo ukweli tsh.15000/= kwa mwezi na anayezichangisha ni mjumbe wa Chama Cha mapinduzi naskia aliwahi alitumbuliwa kwakuwa na vyeti feki
 
Mkuu wewe mtaa wako unalipa tsh. Ngapi. Mkuu hiyo ibara inasema watu wachangie fedha ya ulinzi kila mwezi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…