Mkuu wa Majeshi Afrika Kusini amjibu Rais Kagame

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Afrika Kusini (SANDF), Jenerali Rudzani Maphwanya, amejibu kauli ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuhusu mchango wa vikosi vya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), akisisitiza kuwa jeshi la kikanda limeisababishia hasara kubwa M23 katika mapambano ya hivi karibuni.

Jenerali Maphwanya amesema kuwa Kikosi cha Kulinda Amani cha Kikanda nchini DRC (SAMIDRC), kinachojumuisha vikosi vya jeshi kutoka Afrika Kusini, Malawi, na Tanzania, kimefanikiwa kuwadhibiti waasi wa M23, ambao wamekuwa wakisababisha machafuko mashariki mwa nchi hiyo.

SOMA: Jeshi la Afrika Kusini pamoja na FARDC limefanikiwa kuwadhibiti M23 kuelekea GOMA

Katika taarifa yake leo, Maphwanya alieleza kuwa waasi wa M23 wanadaiwa kupata mafunzo na kuungwa mkono na Serikali ya Rwanda, ambayo ni jirani wa DRC.

"Tishio kuu katika eneo hili linatokana na kundi la waasi ambalo linadaiwa kuwa na silaha, kuungwa mkono, kufunzwa, na kusaidiwa na Jeshi la Ulinzi la Rwanda.

Katika majibizano ya hivi karibuni, vikosi vyetu vya SAMIDRC vilifanikiwa kupambana na M23 na kuwazuia kutekeleza malengo yao ya kusonga mbele hadi Goma," alisema Maphwanya.

PIA SOMA
- Kagame: Rwanda is ready for a confrontation with South Africa if necessary!
 
1738251577073.png
 
Nchi tatu zinashindwa na kikosi cha wanamgambo?

Hii si aibu?
 
Sasa hapo sijajua ndio kawajibu nini.

Uharibifu anaousemea upo kiujumlajumla sana bila kuspecify ni upi, kama vile labda tumeangusha ndege kadhaa,tumeharibu vifaru kadhaa,tumeua waasi kadhaa,n.k.ndio vitu nilivyotegemea kuvisikia.

Hapo kapiga siasa tu na huenda wanapokea kichapo haswaa
 
Back
Top Bottom