Mkuu wa Majeshi lazima atoke Jeshi la Kujenga Taifa?

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Nimekuwa nikisumbuliwa muda mrefu na swali hili Hivi huyu mkuu wa majeshi ya ulizi tanzania Aden Mwamunyange si alikuwa JKT?

Ssa swali langu ni kwamba ilikuwaje achaguliwe kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania na kwanini siku moja mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania asitoke jeshi la polisi au magereza?

Na tunaposema mkuu wa majeshi tunamaana kwamba ni mkuu wa majeshi yote yaani mgambo,magereza,polisi,JKT,JWTZ,TAKUKURU n,k.pia kuna tofauti gani kati ya Amirijeshi mkuu na mkuu wa majeshi?

Yaani mambo haya yananichanganya sana hasa hilo la mkuu wa majeshi ina maana rais anashauriwa kuteua mtu yeyote yule? Au ni lazima atoke JWTZ na JKT? Au hata jeshi la polisi, magereza, uhamiaji, KMKM nayo yana uwezo wa kutoa mkuu wa majeshi?

Na ukiangalia ndani ya gari la uhuru utakuta kuna Rais na mkuu wa majeshi tu yaani watu 2 tu kwanini asiongezeke IGP, Mkuu wa magereza,usalama wa taifa n,k!jamani naomba majibu kwa mada hii kwa yeyote anayefahamu maana maswali hayo najiuliza huu mwaka wa 6 sasa bado sijapata jibu labda hapa jamvini mnaweza kunisaidia swali hili!
 
pole kaka kwa kujiuliza muda mrefu hivyo. nadhani ni makosa kumuita mkuu wa majeshi, cheo hicho ni cha rais na neno amiri jeshi mkuu, lina maana ya "mkuu wa jeshi mkuu" kwani neno amiri lina maana ya mkuu. cheo cha mwamunyange kinapaswa kuwa mkuu wa JWTZ na sio mkuu wa majeshi kwani JWTZ ni jeshi moja. ila kutokana na majukumu ya kulinda mipaka ya nchi na kuhakikisha uhuru wa jamhuri, ndio maana unamuona mkuu wa JWTZ akiambatana na rais kwenye sherehe za uhuru na hata za muungano.

kwa kumalizia, mkuu wa JWTZ lazima atoke JWTZ na rais humteua baada ya kushauriana na makamanda waandamizi wa JWTZ. kwa hiyo JKT ni sehemu ya JWTZ ni kama idara tu ya JWTZ. sio mwamunyange pekee bali hata shimbo alikuwa mkuu wa JKT kabla hajawa mnadhimu mkuu wa JWTZ. so ichukulie JKT kama idara mojawap ya JWTZ to make life easier. thanx kwa kunisoma
 
nashukuru sana nimekupata kaka kwa hiyo hakuna uhusiano wowote kati ya jeshi la polisi na JWTZ maana kipindi cha sherehe mbalimbali huwa naona wanacheza Rigwaride pamoja na kutoa heshima kwa pamoja
 
Mkuu wa Jwtz automaticary yeye ndio senior wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, tatizo wabongo hata hiyo katiba mbovu tuliyonayo hamtaki kuisoma, kila siku hapa jamvini huwa inaletwa kwenye soft sheet ili muisome na muone mapungufu yake lakini hamtaki, mfano hai leo asubuhi east african radio walikuwa wanapotosha watu eti katiba imeandikwa kwa kiingereza ndio maana watu wengi hawaijuwi! uongo mtupu katiba imeandikwa kwa kiswahili safi kabisa, isearch humu humu jamvini utaipata
 
hapo penye bold nimepapenda. kweye gwaride huwa wankusudia kutoa kiapo cha utii na hesjhima zao kwa amiri jeshi mkuu ambaye ndiye commanda in chief wa majeshi yote, hapo ndipo majeshi yote yanapohusika kila jeshi kivyake. ni katika kuonyesha uniformity ndio maana wanafanya mazoezi kwa pamoja laini wakati wa kumatch, kla jeshi linatengeneza gadi zake, hawachanganyiki kuonyesha kuwa ni majeshi tofauti. enzi za mwalimu aliwahi kuwa na ADC kutoka polisi . kwa hiyo kwa suala la nani awe AD linaweza kutoka katika majeshi mengine, ila nadhani wanaona kama ujiko fulani hivi kumchukua toka JWTZ
 
Mkuu wa Jwtz automaticary yeye ndio senior wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, tatizo wabongo hata hiyo katiba mbovu tuliyonayo hamtaki kuisoma, kila siku hapa jamvini huwa inaletwa kwenye soft sheet ili muisome na muone mapungufu yake lakini hamtaki, mfano hai leo asubuhi east african radio walikuwa wanapotosha watu eti katiba imeandikwa kwa kiingereza ndio maana watu wengi hawaijuwi! uongo mtupu katiba imeandikwa kwa kiswahili safi kabisa, isearch humu humu jamvini utaipata

tumegee kidogo mkuu ibara inayohusika na wenzio tufungue macho. thanx
 
pole kaka kwa kujiuliza muda mrefu hivyo. nadhani ni makosa kumuita mkuu wa majeshi, cheo hicho ni cha rais na neno amiri jeshi mkuu, lina maana ya "mkuu wa jeshi mkuu" kwani neno amiri lina maana ya mkuu. cheo cha mwamunyange kinapaswa kuwa mkuu wa JWTZ na sio mkuu wa majeshi kwani JWTZ ni jeshi moja. ila kutokana na majukumu ya kulinda mipaka ya nchi na kuhakikisha uhuru wa jamhuri, ndio maana unamuona mkuu wa JWTZ akiambatana na rais kwenye sherehe za uhuru na hata za muungano.

kwa kumalizia, mkuu wa JWTZ lazima atoke JWTZ na rais humteua baada ya kushauriana na makamanda waandamizi wa JWTZ. kwa hiyo JKT ni sehemu ya JWTZ ni kama idara tu ya JWTZ. sio mwamunyange pekee bali hata shimbo alikuwa mkuu wa JKT kabla hajawa mnadhimu mkuu wa JWTZ. so ichukulie JKT kama idara mojawap ya JWTZ to make life easier. thanx kwa kunisoma

Amir ni neno la kiarabu lenye maana kamanda mkuu au Jemedari Mkuu wa wakuu, hivyo Rais anakuwa Mkuu wa Wakuu wa Majeshi, haihitajiki kuwa na Mkuu mwengine wa Majeshi...
 
pole kaka kwa kujiuliza muda mrefu hivyo. nadhani ni makosa kumuita mkuu wa majeshi, cheo hicho ni cha rais na neno amiri jeshi mkuu, lina maana ya "mkuu wa jeshi mkuu" kwani neno amiri lina maana ya mkuu. cheo cha mwamunyange kinapaswa kuwa mkuu wa JWTZ na sio mkuu wa majeshi kwani JWTZ ni jeshi moja. ila kutokana na majukumu ya kulinda mipaka ya nchi na kuhakikisha uhuru wa jamhuri, ndio maana unamuona mkuu wa JWTZ akiambatana na rais kwenye sherehe za uhuru na hata za muungano.

kwa kumalizia, mkuu wa JWTZ lazima atoke JWTZ na rais humteua baada ya kushauriana na makamanda waandamizi wa JWTZ. kwa hiyo JKT ni sehemu ya JWTZ ni kama idara tu ya JWTZ. sio mwamunyange pekee bali hata shimbo alikuwa mkuu wa JKT kabla hajawa mnadhimu mkuu wa JWTZ. so ichukulie JKT kama idara mojawap ya JWTZ to make life easier. thanx kwa kunisoma

Asante kwa Maelezo yako mazuri Miss Judith. Kwa muundo wa jeshi letu ulivyo, unafikiri JKT inafanya kazi zile zile za main stream ya JWTZ? Well, kwangu mimi binafsi sioni tatizo kama mkuu wa majeshi atatokea popote hata polisi. Historia inaonyesha kuwa Marekani wakati Gemn. Colin Powel alipoteuliwa kuwa kiongozi wa joint of staff yalizuka maneno mengi sana maana hakuwa katika kazi mama za jeshi karibu katika career yake yote. Alikuwa kisiasa zaidi kuliko kijeshi na bado akawa mkuu wa majeshi.
 
..Mwamunyange na Shimbo walikuwa JWTZ, baadaye[as major generals] ndiyo wakapelekwa kuongoza JKT.

..JKT ni sehemu ya JWTZ. wote wanapata mafunzo ya kijeshi na utawala ya aina moja. kwa msingi huo ukiwa Capt wa JKT na JWTZ wote ni sawa wanachotofautiana ni utaalamu na majukumu ya kila siku.
 
nashukuru sana nimekupata kaka kwa hiyo hakuna uhusiano wowote kati ya jeshi la polisi na JWTZ maana kipindi cha sherehe mbalimbali huwa naona wanacheza Rigwaride pamoja na kutoa heshima kwa pamoja
Na kipindi inapotokea vita ina maana jeshi la polisi,mgambo na magereza nao huwa wanaenda kushiriki?pia nakumbuka ile vita ya mwaka 1978 ya Idd amin yaani Tanzania na Uganda nilikuwa naona Raia wanachukuliwa kwenda kupigana sasa hawa huko walikuwa wanasimama kama wanajeshi au kama nani maana makundi wa watu toka mikoa mbalimbali walienda kupigana vita vile pia na sasa ikitokea vita watabebwa hivyohivyo?na ukikataa kwenda inakuweje utalazimishwa?
 
sorry miss judith kwa kukuita kaka sikuangalia vizuri kumbe ni jinsia ke
 
Na kipindi inapotokea vita ina maana jeshi la polisi,mgambo na magereza nao huwa wanaenda kushiriki?pia nakumbuka ile vita ya mwaka 1978 ya Idd amin yaani Tanzania na Uganda nilikuwa naona Raia wanachukuliwa kwenda kupigana sasa hawa huko walikuwa wanasimama kama wanajeshi au kama nani maana makundi wa watu toka mikoa mbalimbali walienda kupigana vita vile pia na sasa ikitokea vita watabebwa hivyohivyo?na ukikataa kwenda inakuweje utalazimishwa?

mkuu mgambo ndo walitangulizwa mbele kama chambo unajua 2likuwa a2na vifaa vya kisasa kutambua adui yupo upande gani so mnawatanguliza mgambo nyie mnabaki mbali wakishambuliwa mnajua wapo mwelekeo gani
 
kumbe tulipoteza watu wengi sana kama kipimio cha kujua adui yupo wapi ilikuwa ni mgambo
 
Nimekuwa nikisumbuliwa muda mrefu na swali hili Hivi huyu mkuu wa majeshi ya ulizi tanzania Aden Mwamunyange si alikuwa JKT?sasa swali langu ni kwamba ilikuwaje achaguliwe kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania na kwanini siku moja mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania asitoke jeshi la polisi au magereza?na tunaposema mkuu wa majeshi tunamaana kwamba ni mkuu wa majeshi yote yaani mgambo,magereza,polisi,JKT,JWTZ,TAKUKURU n,k.pia kuna tofauti gani kati ya Amirijeshi mkuu na mkuu wa majeshi?yaani mambo haya yananichanganya sana hasa hilo la mkuu wa majeshi ina maana rais anashauriwa kuteua mtu yeyote yule?au ni lazima atoke JWTZ na JKT?au hata jeshi la polisi,magereza,uhamiaji,KMKM nayo yana uwezo wa kutoa mkuu wa majeshi?na ukiangalia ndani ya gari la uhuru utakuta kuna Rais na mkuu wa majeshi tu yaani watu 2 tu kwanini asiongezeke IGP,Mkuu wa magereza,usalama wa taifa n,k!jamani naomba majibu kwa mada hii kwa yeyote anayefahamu maana maswali hayo najiuliza huu mwaka wa 6 sasa bado sijapata jibu labda hapa jamvini mnaweza kunisaidia swali hili!
Una umri gani? ....................... Tatizo lako hukuwahi kupitia JKT, daah miaka sita hiki kitu kinakusumbua ?! una kazi ya kufanya?
 
Back
Top Bottom