kuweka rekodi sawa, mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama lazima atoke JW kwa kuwa ndio senior na tunaposema majeshi tunazungumzia jeshi la anga, jeshi la maji, jeshi la nchi kavu, na jeshi la kujenga taifa. Wakati wa magwaride yote ya kitaifa hayo majeshi ndio hutangulia mbele ikiongozwa na jeshi la nchi kavu, polisi na wenzake hufunga tela. anapokuja raisi wa nchi nyingine gwaride linahusu JW peke yao na siku rais anaagwa gwaride linahusu JW peke yao, gwaride la muungano au la uhuru huongozwa na kamanda toka JW mind you kwamba hata hizo guard zina wakuu wao ambao wanachukua amri kutoka kwa mkuu wa parade ambaye anakuwa na cheo cha luteni kanali . Raisi huingia na mkuu wa majeshi uwanjani kwa kuwa naye ni raisi asiyeonekana akitaka kumwondoa rais madarakini hufanikiwa kwakuwa silaha zote kuu zipo chini yake kupitia anga, ardhi na maji. polisi hawezi kuwa ADC wa rais hata siku moja utaratibu lazima atoke JW na awe senior officer yaani anzie cheo cha major na asizidi cheo cha kanali.