Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimekuwa nikisumbuliwa muda mrefu na swali hili Hivi huyu mkuu wa majeshi ya ulizi tanzania Aden Mwamunyange si alikuwa JKT?
Ssa swali langu ni kwamba ilikuwaje achaguliwe kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania na kwanini siku moja mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania asitoke jeshi la polisi au magereza?
Na tunaposema mkuu wa majeshi tunamaana kwamba ni mkuu wa majeshi yote yaani mgambo,magereza,polisi,JKT,JWTZ,TAKUKURU n,k.pia kuna tofauti gani kati ya Amirijeshi mkuu na mkuu wa majeshi?
Yaani mambo haya yananichanganya sana hasa hilo la mkuu wa majeshi ina maana rais anashauriwa kuteua mtu yeyote yule? Au ni lazima atoke JWTZ na JKT? Au hata jeshi la polisi, magereza, uhamiaji, KMKM nayo yana uwezo wa kutoa mkuu wa majeshi?
Na ukiangalia ndani ya gari la uhuru utakuta kuna Rais na mkuu wa majeshi tu yaani watu 2 tu kwanini asiongezeke IGP, Mkuu wa magereza,usalama wa taifa n,k!jamani naomba majibu kwa mada hii kwa yeyote anayefahamu maana maswali hayo najiuliza huu mwaka wa 6 sasa bado sijapata jibu labda hapa jamvini mnaweza kunisaidia swali hili!
pole kaka kwa kujiuliza muda mrefu hivyo. nadhani ni makosa kumuita mkuu wa majeshi, cheo hicho ni cha rais na neno amiri jeshi mkuu, lina maana ya "mkuu wa jeshi mkuu" kwani neno amiri lina maana ya mkuu. cheo cha mwamunyange kinapaswa kuwa mkuu wa JWTZ na sio mkuu wa majeshi kwani JWTZ ni jeshi moja. ila kutokana na majukumu ya kulinda mipaka ya nchi na kuhakikisha uhuru wa jamhuri, ndio maana unamuona mkuu wa JWTZ akiambatana na rais kwenye sherehe za uhuru na hata za muungano.
kwa kumalizia, mkuu wa JWTZ lazima atoke JWTZ na rais humteua baada ya kushauriana na makamanda waandamizi wa JWTZ. kwa hiyo JKT ni sehemu ya JWTZ ni kama idara tu ya JWTZ. sio mwamunyange pekee bali hata shimbo alikuwa mkuu wa JKT kabla hajawa mnadhimu mkuu wa JWTZ. so ichukulie JKT kama idara mojawap ya JWTZ to make life easier. thanx kwa kunisoma
JKT ni wing ya JWTZ; maafisa wote wa JKT (NCOs na COs) ni maafisa wa JWTZ. Tofauti iliyopo ni kuwa askariwa JKT ni askari-raia wanaosimamiwa na JWTZ, wakati askari wa JWTZ ni askari walioapishwa.
Judith amebugi man!nashukuru sana nimekupata kaka kwa hiyo hakuna uhusiano wowote kati ya jeshi la polisi na JWTZ maana kipindi cha sherehe mbalimbali huwa naona wanacheza Rigwaride pamoja na kutoa heshima kwa pamoja
Kwa kuongezea Mkuu wa Majeshi, IGP, Mkuu wa Magereza Hawa wote lazima wawe TISS ....
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
JKT ni wing ya JWTZ; maafisa wote wa JKT (NCOs na COs) ni maafisa wa JWTZ. Tofauti iliyopo ni kuwa askariwa JKT ni askari-raia wanaosimamiwa na JWTZ, wakati askari wa JWTZ ni askari walioapishwa.
Acha uongo, kama hujui usipotoshe jamii, kumbuka huku jamvini huenda hata Mwamnyange akawa member so usipende kupotosha. JKT na JW wana kiapo sawa, tofauti yao tena hapa nasisitiza ni ndogo mno tena ni kimajukumu tu. linapokuja suala la core activities wote wako sawa kimajukumu.
Kilimasera;Nimekuwa nikisumbuliwa muda mrefu na swali hili Hivi huyu mkuu wa majeshi ya ulizi tanzania Aden Mwamunyange si alikuwa JKT?
Ssa swali langu ni kwamba ilikuwaje achaguliwe kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania na kwanini siku moja mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania asitoke jeshi la polisi au magereza?
Na tunaposema mkuu wa majeshi tunamaana kwamba ni mkuu wa majeshi yote yaani mgambo,magereza,polisi,JKT,JWTZ,TAKUKURU n,k.pia kuna tofauti gani kati ya Amirijeshi mkuu na mkuu wa majeshi?
Yaani mambo haya yananichanganya sana hasa hilo la mkuu wa majeshi ina maana rais anashauriwa kuteua mtu yeyote yule? Au ni lazima atoke JWTZ na JKT? Au hata jeshi la polisi, magereza, uhamiaji, KMKM nayo yana uwezo wa kutoa mkuu wa majeshi?
Na ukiangalia ndani ya gari la uhuru utakuta kuna Rais na mkuu wa majeshi tu yaani watu 2 tu kwanini asiongezeke IGP, Mkuu wa magereza,usalama wa taifa n,k!jamani naomba majibu kwa mada hii kwa yeyote anayefahamu maana maswali hayo najiuliza huu mwaka wa 6 sasa bado sijapata jibu labda hapa jamvini mnaweza kunisaidia swali hili!
Kichuguu MBONA UNAZIDI KUDANGANYA?Wanaopenda kuonyesha vidole kuwa wenzao ni waongo, kwa kawaida huwa ndio waongo; ungekuwa umeonyesha kiwango kikubwa kwa kupinga hoja yangu bila kuniita mwongo. Hata hivyo nitakupa elimu fupi, na isipokutosha niambie nifafanue zaidi.
Ukisoma sheria ya JKT na sheria ya JWTZ utafahamu kuwa jeshi la kujenga taiofa ni kama jina lake lilivyo; "Kujenga Taifa," wakati jeshi la wanachi ni jeshi la ulinzi wa mipaka ya Tanzania. Kwa hiyo askari wa JKT "hawalazimiki" kupigana vita wakati askari wa JWTZ wanalazimika. Askari wa JKT hawezi kushitakiwa court martial wakati yule wa JWTZ anaweza kushitakiwa huko.
Nadhani wewe kinachokuahadaa ni wale maafisa wanaoendesha JKT ambao ni maafisa wa JWTZ; hakuna afisa wa JKT. Askari wa JKT ni kama vile wale wabunge waliokuwa wamekwenda kupigwa msasa hivi majuzi, na vijana wanaoweza kujiunga na jeshi hilo kwa kujitolea; hawa wanitwa Servicemen," ingawa sina uhakika pia kama kuna "Servicewomen," na kwa muda mrefu namba zao za jeshi zimekuwa zinaanza na SM (Serviceman). Hawa siyo waajiriwa wa serikali ya Tanzania. Askari wa JWTZ ambao kufupi wanajulikana kama wapiganaji, ni waajiriwa wa serikali ya Tanzania, na namba zao kwa muda mrefu zilikuwa zinaanza na MU (mlinzi wa umma.)
Tambua tena kuwa mafunzo yote ya JKT yanaendeshwa na JWTZ; ndiyo maana askari wote wanaoendesha mafunzo ya JKT kuanzia ngazi ya private mpaka Major General ni waajiriwa wa JWTZ. Maafisa wa JWTZ wanaonedesha JKT siyo askari wa JKT. Zamani kidogo wakati bado kuna jeshi la Mgambo, mambo yalikuwa hivyo hivyo; kuwa shughuli zote za kuendesha jeshi hilo zilikuwa chini ya JWTZ ingawa wanamgambo hawakuwa askari wa JWTZ, na wale askari waliokuwa wakiendesha mafunzo ya mgambo hawakuwa askari wa mgambo.
Nadhani mpaka hapo utakuwa umeelewa tofauti baina ya (a) askari wa JKT, (b) askari wa JWTZ, na (c) askari wa JWTZ wanaonedsha JKT.
Kichuguu MBONA UNAZIDI KUDANGANYA?
ACHA UONGO HII STORY UNGEIACHA KWANI TULISHAIZUNGUMZIA HUMUHUMU JF NA ASKARI WOTE NI SAWA WAMAPIGANA VITA NA WAPO WALIOENDA DARFUR WAKIWEMO POLISI
Vita vya Uganda mpaka Mgambo walikuwepo bega kwa bega na JKT na askari wa akiba (Sisi Raia tuliopitia JKT tukapewa mafunzo hayo) na walikuwa zaidi kwenye Vikosi vya Infantry (Askari wa Miguu) vinavyokuwa mstari wa mbele nyuma ya vifaru na magari ya deraya
Hapo kwenye RED unapodai askari wa JKT halazimiki kupigana Vita ni kichekesho kwani inaonesha wengi wa Raia humu Nchini tukivamiwa na Manduli hasa haya yanayonyemelea nchi yetu kutoka maziwa makuu mtajificha Uvunguni mwa vitanda mama zetu na kina dada wakibakwa. (Raia wote ni Askari na mnatakiwa muende mstari wa mbele mkiongozwa na JKT ya kina Zitto na Halima Mdee)
Kwas kifupi tu JKT ni Askari wa kawaida wa JWTZ na anashtakiwa katika Court Marshal na hakimu wake ni CO wa kikosi na kufungwa Uraiani au kuachishwa Jeshi kilimasera labda kwa kuongeza Mwamunyange navyofahamu ni kweli alitoka TPDF akaenda JKT na wakati wa Utawala wa Mkapa wakati huo Mkuuwa Majeshi alikuwa Waitara na Msaidizi Gau sasa wakastaafu wote ndipo akarudishwa Mwamunyange TPDF kutokana na Rank, alipoingia JK wa awamu ya Nne akamteua kuwa CDF
WAKATI VITA IKIPIGANWA mapigano yote yanawasilishwa kwa Chief of Defence (Mkuu wa Majeshi) naye anayawasilisha kwa Commanding ni Chief ambaye ndiye Kiongozi wa nchi (Rais) Hii thread ipo humu nitakuwasilishia
Nimekuwa nikisumbuliwa muda mrefu na swali hili Hivi huyu mkuu wa majeshi ya ulizi tanzania Aden Mwamunyange si alikuwa JKT?
Ssa swali langu ni kwamba ilikuwaje achaguliwe kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania na kwanini siku moja mkuu wa majeshi ya ulinzi tanzania asitoke jeshi la polisi au magereza?
Na tunaposema mkuu wa majeshi tunamaana kwamba ni mkuu wa majeshi yote yaani mgambo,magereza,polisi,JKT,JWTZ,TAKUKURU n,k.pia kuna tofauti gani kati ya Amirijeshi mkuu na mkuu wa majeshi?
Yaani mambo haya yananichanganya sana hasa hilo la mkuu wa majeshi ina maana rais anashauriwa kuteua mtu yeyote yule? Au ni lazima atoke JWTZ na JKT? Au hata jeshi la polisi, magereza, uhamiaji, KMKM nayo yana uwezo wa kutoa mkuu wa majeshi?
Na ukiangalia ndani ya gari la uhuru utakuta kuna Rais na mkuu wa majeshi tu yaani watu 2 tu kwanini asiongezeke IGP, Mkuu wa magereza,usalama wa taifa n,k!jamani naomba majibu kwa mada hii kwa yeyote anayefahamu maana maswali hayo najiuliza huu mwaka wa 6 sasa bado sijapata jibu labda hapa jamvini mnaweza kunisaidia swali hili!
samahani Kichuguu labda nimetoka nje au tuko sawa lakini kwa ninavyojua JWTZ (TPDF) ndilo hubeba JKT (National Service)Ukijua tofauti hzio ndipo utagundua kwa nini nyota za maafisa wa JKT zina maandishi ya JWTZ na wala siyo JKT. Vile vile uniform za maafisa wote wa wanaonedsha JKT zina nembo ya JWTZ wala siyo ya JWTZ. Askari wa JKT anapomaliza mafunzo yake huko JKT hupewa cheti chenye na nembo ya JKT siyo ya JWTZ.
Unaweza kueleza ni kwa nini iwapo JKT ni jeshi kama JWTZ kwa nini maafisa wake wasitumie nembo yao kama vile ilivyo majeshi mengine ya polisi na magereza, badala yake wanatumia nembo ya JWTZ na kuiacha ile ya JKT.
Kuhusu polisi na magereza kwenda vitani, hiyo ni sehemu ya majukumu yao wakati wakitakiwa kufanya hivyo na amiri jeshi mkuu.