Mwandwanga
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 3,059
- 1,572
Wanaopenda kuonyesha vidole kuwa wenzao ni waongo, kwa kawaida huwa ndio waongo; ungekuwa umeonyesha kiwango kikubwa kwa kupinga hoja yangu bila kuniita mwongo. Hata hivyo nitakupa elimu fupi, na isipokutosha niambie nifafanue zaidi.
Ukisoma sheria ya JKT na sheria ya JWTZ utafahamu kuwa jeshi la kujenga taiofa ni kama jina lake lilivyo; "Kujenga Taifa," wakati jeshi la wanachi ni jeshi la ulinzi wa mipaka ya Tanzania. Kwa hiyo askari wa JKT "hawalazimiki" kupigana vita wakati askari wa JWTZ wanalazimika. Askari wa JKT hawezi kushitakiwa court martial wakati yule wa JWTZ anaweza kushitakiwa huko.
Nadhani wewe kinachokuahadaa ni wale maafisa wanaoendesha JKT ambao ni maafisa wa JWTZ; hakuna afisa wa JKT. Askari wa JKT ni kama vile wale wabunge waliokuwa wamekwenda kupigwa msasa hivi majuzi, na vijana wanaoweza kujiunga na jeshi hilo kwa kujitolea; hawa wanitwa Servicemen," ingawa sina uhakika pia kama kuna "Servicewomen," na kwa muda mrefu namba zao za jeshi zimekuwa zinaanza na SM (Serviceman). Hawa siyo waajiriwa wa serikali ya Tanzania. Askari wa JWTZ ambao kufupi wanajulikana kama wapiganaji, ni waajiriwa wa serikali ya Tanzania, na namba zao kwa muda mrefu zilikuwa zinaanza na MU (mlinzi wa umma.)
Tambua tena kuwa mafunzo yote ya JKT yanaendeshwa na JWTZ; ndiyo maana askari wote wanaoendesha mafunzo ya JKT kuanzia ngazi ya private mpaka Major General ni waajiriwa wa JWTZ. Maafisa wa JWTZ wanaonedesha JKT siyo askari wa JKT. Zamani kidogo wakati bado kuna jeshi la Mgambo, mambo yalikuwa hivyo hivyo; kuwa shughuli zote za kuendesha jeshi hilo zilikuwa chini ya JWTZ ingawa wanamgambo hawakuwa askari wa JWTZ, na wale askari waliokuwa wakiendesha mafunzo ya mgambo hawakuwa askari wa mgambo.
Nadhani mpaka hapo utakuwa umeelewa tofauti baina ya (a) askari wa JKT, (b) askari wa JWTZ, na (c) askari wa JWTZ wanaonedsha JKT.
KIAPO NI KILE KILE,tofauti penye jw unaweka Jkt na pia mafunzo ya vijana Jkt yanaweza tolewa na Volunteer leaders,hawa ni askari wa jkt waliopata course ya instructors. Na kuhusu kushitakiwa ukibainika ulipitia Jkt na upo ndani ya mkataba na Jkt unashtakiwa Kijeshi.
kuhusu vita kuna vigezo vya kumpeleka askari kule mojawapo ni kuwa lazima askari huyo awe amepiga kozi ya Level 1,nje ya hapo haendi, kumbuka kuna privates wa Jeshi hawajapiga hiyo course! na juu ya askari wa jkt kwenda vitani inawezekana kabsa kama atakidhi viwango tajwa hapo juu.