Mkuu wa Majeshi lazima atoke Jeshi la Kujenga Taifa?


KIAPO NI KILE KILE,tofauti penye jw unaweka Jkt na pia mafunzo ya vijana Jkt yanaweza tolewa na Volunteer leaders,hawa ni askari wa jkt waliopata course ya instructors. Na kuhusu kushitakiwa ukibainika ulipitia Jkt na upo ndani ya mkataba na Jkt unashtakiwa Kijeshi.
kuhusu vita kuna vigezo vya kumpeleka askari kule mojawapo ni kuwa lazima askari huyo awe amepiga kozi ya Level 1,nje ya hapo haendi, kumbuka kuna privates wa Jeshi hawajapiga hiyo course! na juu ya askari wa jkt kwenda vitani inawezekana kabsa kama atakidhi viwango tajwa hapo juu.
 

Huyu jamaa sijui yukoje! Asante kwa kumpa darasa.
 
ipi tofauti ya Kamandi, Brigedi na Kikosi.

Kwa ufupi,Jw wana kamandi ya Jeshi la anga, Ardhini,Majini..
Askari wa Ardhini ndani yake kuna Jkt,Mizinga,komandoo(Comando wapo kamandi zote). Brigedi hapa wamegawanya Vikosi vya jeshi kikanda mfano kunaweza kuwepo na brigedi ya kusini,kaskazini nk.......Wanakuja
Karibu Jkt.
 

ahsante mkuu
 
Tanzania tuna komand 4, nazo ni komand ya ardhi(infantria), anga (air force) , maji (navy) na jkt. Swala linakuja ni kwamba jkt ni jeshi la vijana huku walimu wao wakiwa ni tpdf. So kinachotokea ili wewe wa tpdf uje kufundisha jkt inabidi uende kozi na hapo unakuwa upo komand ya jkt. Hata viongozi wa jkt wao ni tpdf !. Mkuu wa majeshi ni lazima atoke tpdf/jkt. Cause hauwezi kufananisha mtu aliyepita tpdf na yule aliyepita polisi/mageleza, hizo ni different aspect !. Na hata kwenye system za majeshi ya hapa bongo tpdf ndio masenior wa majeshi yote.
 

wakuu, nisaidieni kunijuza kuhusu cheo cha Brigedia General, ni sahihi kutamkwa hivo? kwa nini sio Brigedia? nilivo kuwa nafahamu mimi vyeo vya jeshi kuanzia Meja, Lt Kanali, Kanali, Brigedia, Meja General, Lt General na General. Hapa ktk vyeo hivi kuanzia Meja nembo ya ngao ya adamu na eva ipo kote? so please anaye jua naomba anijuze.
 

Brigadier na brigadier general ni kitu kile kile ila jina limebadilika kutokana na umoja wa commonwealth

Rank insignia za jwtz zipo hapo chini kwenye hiyo liink

Tanzania Peoples’ Defence Force - Land Forces / Jeshi la Wananchi la Tanzania - JWTZ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…