Mkuu wa majeshi wa Uganda, Gen. Muhoozi Kainerugaba, anapanda mbegu gani kisiasa na anatoa ujumbe gani kwa demokrasia ya Afrika Mashariki?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
C&P
Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ametangaza rasmi kuwa hatagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2026, isipokuwa ataelekeza nguvu zake jeshini huku akimuunga mkono baba yake, Rais Yoweri Museveni, ambaye anatarajiwa kugombea tena urais mwaka huo.

Kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa X, Muhoozi ameeeleza kuwa Mungu alimwelekeza aelekeze nguvu zake kwenye jeshi ili kuwalinda raia wa Uganda.

"Ningependa kutangaza kuwa sitakuwa kwenye karatasi ya kura mwaka wa 2026. Mwenyezi Mungu aliniambia nijikite kwanza kwenye Jeshi lake. Kwa hivyo, namuunga mkono kabisa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao", ameeleza Gen. Muhoozi.

Katika taarifa yake, Muhoozi ameonekana kuweka wazi kuwa ataendelea kutumikia kama Mkuu wa Majeshi akisema kuwa hakuna kitu kitakatifu zaidi hapa duniani kuliko Jeshi la wananchi wa Uganda (UPDF).

"Kwa hiyo, siwezi kufikiria heshima kubwa zaidi kuliko kuwa sehemu ya UPDF. Ni ardhi takatifu!! Mungu ibariki UPDF takatifu na Uganda yenye baraka milele”, alisema Muhoozi.

Rais Yoweri Museveni (80) ambaye anatarajiwa kugombea tena urais mwaka 2026, alichaguliwa tena kwa muhula wa sita mwaka 2021, baada ya kuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Licha ya tangazo hili, haijulikani kwa nini Muhoozi alibadili uamuzi wake wa kugombea urais, jambo ambalo limewashangaza mashabiki wake wengi waliokuwa tayari kuanza kampeni za kumuunga mkono.

Mwaka 2023, Muhoozi alitangaza nia yake ya kugombea urais mwaka 2026 akisisitiza kuwa ni wakati wa kizazi kipya kuchukua hatamu za uongozi kwa kuwapumzisha wazee.

"Kwa jina la Yesu Kristo Mungu wangu, kwa jina la vijana wote wa Uganda na dunia, na kwa jina la mapinduzi yetu makubwa, nitasimama kugombea urais mwaka 2026”, ameandika Muhoozi.

Uchaguzi wa mwaka 2026 unatarajiwa kuvutia wagombea mashuhuri kama mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, na Dk. Kizza Besigye, hata hivyo kauli nyingine ya Muhoozi huenda ikabadili mwelekeo wa siasa za Uganda.

Amesema kuwa kamwe vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Uganda havitaruhusu raia kushika madaraka ya Urais pindi baba yake atakapoamua kutokugombea.

"Hakuna raia atakayeongoza Uganda baada ya Rais Museveni. Vikosi vya usalama havitaruhusu hilo. Kiongozi ajaye atakuwa mwanajeshi au polisi", Gen Muhozi Kainerugaba aliandika hivyo kwenye ukrasa wake wa X , hapo majuzi.

Je, kwamba utawala wa kiraia ni ndoto ya mchana Uganda?

Au anahamasisha ujasiri kwa vijana majeshini kujiandaa kuchukua hatamu za uongozi wa kisiasa kwa muda muafaka, au ni maandalizi ya mapinduzi ya kidemokrasia Africa mashariki?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Ukishaona nchi, mtoto wa Rais anateuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi, hili taifa ni mali ya familia; unapoteza muda kuongelea demokrasia hapo
Je,
Ni dictator Gen.Idd Amini wa aina mpya anakuja kuvuruga utawala wa kiraia na demokrasia uganda, kuisambaratisha East Africa kwa namna ya tofauti?🐒
 
C&P
Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ametangaza rasmi kuwa hatagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2026, isipokuwa ataelekeza nguvu zake jeshini huku akimuunga mkono baba yake, Rais Yoweri Museveni, ambaye anatarajiwa kugombea tena urais mwaka huo.

Kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa X, Muhoozi ameeeleza kuwa Mungu alimwelekeza aelekeze nguvu zake kwenye jeshi ili kuwalinda raia wa Uganda.

"Ningependa kutangaza kuwa sitakuwa kwenye karatasi ya kura mwaka wa 2026. Mwenyezi Mungu aliniambia nijikite kwanza kwenye Jeshi lake. Kwa hivyo, namuunga mkono kabisa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao", ameeleza Gen. Muhoozi.

Katika taarifa yake, Muhoozi ameonekana kuweka wazi kuwa ataendelea kutumikia kama Mkuu wa Majeshi akisema kuwa hakuna kitu kitakatifu zaidi hapa duniani kuliko Jeshi la wananchi wa Uganda (UPDF).

"Kwa hiyo, siwezi kufikiria heshima kubwa zaidi kuliko kuwa sehemu ya UPDF. Ni ardhi takatifu!! Mungu ibariki UPDF takatifu na Uganda yenye baraka milele”, alisema Muhoozi.

Rais Yoweri Museveni (80) ambaye anatarajiwa kugombea tena urais mwaka 2026, alichaguliwa tena kwa muhula wa sita mwaka 2021, baada ya kuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Licha ya tangazo hili, haijulikani kwa nini Muhoozi alibadili uamuzi wake wa kugombea urais, jambo ambalo limewashangaza mashabiki wake wengi waliokuwa tayari kuanza kampeni za kumuunga mkono.

Mwaka 2023, Muhoozi alitangaza nia yake ya kugombea urais mwaka 2026 akisisitiza kuwa ni wakati wa kizazi kipya kuchukua hatamu za uongozi kwa kuwapumzisha wazee.

"Kwa jina la Yesu Kristo Mungu wangu, kwa jina la vijana wote wa Uganda na dunia, na kwa jina la mapinduzi yetu makubwa, nitasimama kugombea urais mwaka 2026”, ameandika Muhoozi.

Uchaguzi wa mwaka 2026 unatarajiwa kuvutia wagombea mashuhuri kama mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, na Dk. Kizza Besigye, hata hivyo kauli nyingine ya Muhoozi huenda ikabadili mwelekeo wa siasa za Uganda.

Amesema kuwa kamwe vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Uganda havitaruhusu raia kushika madaraka ya Urais pindi baba yake atakapoamua kutokugombea.

"Hakuna raia atakayeongoza Uganda baada ya Rais Museveni. Vikosi vya usalama havitaruhusu hilo. Kiongozi ajaye atakuwa mwanajeshi au polisi", Gen Muhozi Kainerugaba aliandika hivyo kwenye ukrasa wake wa X , hapo majuzi.

Je, kwamba utawala wa kiraia ni ndoto ya mchana Uganda?

Au anahamasisha ujasiri kwa vijana majeshini kujiandaa kuchukua hatamu za uongozi wa kisiasa kwa muda muafaka, au ni maandalizi ya mapinduzi ya kidemokrasia Africa mashariki?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
ukiona mambo kama hayo yanatokea na raia wapo kimya ujue hakuna mbada wake kungekuwa na mbadala wake raia wangeshafanya maamuzi magumu
 
KIla wanapotaja UPDF bila shaka akili zao zinajua kuwa bila TPDF wasingekuepo zaid zaid kangekua ni kakikundi tu ka wahun wahun kama Burundi
kwahivyo updf ndio kila kitu uganda, right?
nini hasa tishio hadi utawala wa kiraia uogopwe kiasi hicho?🐒
 
Huyo ndiye rais ajaye

Ova
ndiyo,
ni sawa. Lakini kuna haja ya vitisho na kujiapiza kwamba hakuna raia au polisi ataingoza Uganda?

huko si kuwaamsha sasa ili wajitokeze kijeshi kutoka humo humo ndani anapopadharau?🐒

huko si kuamsha hasira, tamaa na ubabe ndani ya Majeshi ya Uganda?
Wapo generals wenye sifa na uwezo dhidi yake huenda wamejiskia vibaya sana 🐒
 
UPDF ni kama CCM tu hapa bongoland…..
Wanakupa zawadi ya luninga alafu wanakutoboa macho,,,,
Demokrasia my foot….😎
unapotosha gentleman, tena wazi wazi tu 🐒
 
Back
Top Bottom