Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi awasamehe waliofukuzwa JKT, watakiwa kurudi jeshini

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi awasamehe waliofukuzwa JKT, watakiwa kurudi jeshini

Wana uhakika wa kuwapa ajira walizokua wanataka au wanawarudisha kumalizia mkataba wa kujitolea then warudi home?
 
Wana uhakika wa kuwapa ajira walizokua wanataka au wanawarudisha kumalizia mkataba wa kujitolea then warudi home?
Hizi ndio hoja watu wanatakiwa wajiulize. Anaweza kuwasamehe na wanasota tena miaka minne bila ajira wakati uko mtaani walikuwa washaanza kujipanga. Kilichowafanya wagome ni kuambiwa warudi nyumbani, sio kwamba walikaa muda mrefu bila kuajiriwa.

Marekani ilifukuza baadhi ya wanajeshi waliogoma kuchanjwa wakati raia wa kawaida hawalazimishwi. Jeshi lina taratibu zake sio siasa
 
Labda ni kwa ajili ya vita; Russia-Ukraine war,vita Cabo Delgado,ndio maana maamuzi mengine yanakuwa revisited, reconsidered, discarded.
 
Hakuna cha kanuni bana...

Sasa kama Amiri Jeshi mkuu alitoa ahadi (ambayo ni amri) kuwa waajiriwe permanent kwanini jeshi likakiuka maagizo?
Ni kweli walistahili ajira lakini aliyewaahidi tayari alishaonja mauti na pia taritibu za kudai haki jeshini haziruhusu migomo wala maandamano mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo ametoa msamaha kwa vijana 853 kati ya 854 (mmoja alifariki) waliofukuzwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Aprili 2021 kwa makosa ya kinidhamu.

Jenerali Mabeyo ameagiza vijana hao warejeshwe katika kambi za JKT tayari kuanza mafunzo.

"Vijana wa JKT 853 waliosamehewa wapokelewe ifikapo March 12, 2022 na watakapokelewa katika Kambi moja tu, kambi namba 841 ya JKT ipo Mafinga Iringa.

"Katika msafara wa mamba na kenge watajipenyeza, niwaombe Vijana ambao hawahusiki na msamaha huu wasijipenyeze, Vijana hawa 853 orodha yao yote imeandaliwa na tumefanya utafiti mpaka kwenye ngazi zao za Familia, hata makundi yao ya damu kwa kila mmoja limeorodheshwa kwa hiyo udanganyifu hautojitokeza utapimwa kwa jina picha na damu yako," amesema Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ).

Pia, soma:

1). JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi
ningepewa mamlaka haki ile system ya watumishi kupelekwa jeshini kwanza ningerudishaa...jeshi tuu ndo mahala nidhamu na maadili huzingatiwa kwa asilimia zote...one up kwa Mkuu Mabeyo!
 
Maamuzi yote iwe ya DPP au CDF yamefanywa baada ya Rais kukubali bila hivyo kisingefanyika chochote kati ya hayo matukio mawili.
 
Safi sana CDF Mabeyo haiwezekani asamehewe gaidi mbowe alafu vijana wazalendo wa JKT waliojenga ukuta wa Mererani na Ikulu ya Dodoma waachwe wakiteseka mitaani
Dikteta Magufuli alikuwa mnyama sana! Baada ya kuwatumikisha watoto wa wenzake bila malipo akaamua kuwatimua. Bila shaka maovu yote aliyotenda mnyama Magufuli yatarekebishwa!
 
Ni kweli walistahili ajira lakini aliyewaahidi tayari alishaonja mauti na pia taritibu za kudai haki jeshini haziruhusu migomo wala maandamano mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo bro ... Mfano mpo jeshini na mnaona (mnadai) haki yenu mnaona mnadhululiwa/haitimizwi vile kiuhalali huwa Kuna njia gani?
Mnakula buyu haki inapotea mnashuhudia?
 
Eti ajibu mapigo 😂😂😂😂
Hao vijana wanakwenda Mafinga kula kozi, hilo linafanyika kwa idhini ya mwajiri mkuu, ambaye ni Rais.

Au amejibu mapigo ya DPP?
 
Naona Jeshi la Waaasi miaka 20 mbele, tusilete Siasa kwenye Ulinzi na Usalama wa Taifa letu. Unarudisha Jeshini Askari waaasi wa Kiapo cha Kijeshi.. africa is shithole, nitakuwa wa mwisho kuelewa hii logic
hiv unajua hata kilichotokea?
 
Dikteta Magufuli alikuwa mnyama sana! Baada ya kuwatumikisha watoto wa wenzake bila malipo akaamua kuwatimua. Bila shaka maovu yote aliyotenda mnyama Magufuli yatarekebishwa!
Hao vijana wametimuliwa April 2021 magufuli ameshafariki
Jitahidi kufatilia mambo kwanza kabla hujaanza kulaumu
 
hao wanaandaliwa kupewa permanent.waligoma na kutaka kuandamana wakishinikiza ajira ya moja kwa moja kama walivyohaidiwa na JPM pindi watakapomaliza ujenzi wa ikulu ya Chamwino na kujitolea kwenye miradi mingine ya maendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
Watasimulia watakachokikuta ile kambi ngumu sana
 
yaani aisee hii nchi sijui ilikuwa inapelekwa wapi na mwendazake, huwa nakaa nafikiria hata sielewi. maza ameingia vihela mtaani vimeanza kuonekana. mambo mengine aisee.
 
Kwani Mererani ndo nini?
Waliopigana Uganda walirudishwa uraiani, sasa itakuwa hao?
Una umri gani kijana?.

Vijana waliopigana vita kule Uganda wakikuwepo raia, mgambo na majeshi yetu, baada ya vita kuna raia hata mganbo ambao wengine ndiyo wanastaafu na wengine walistaafu mwaka jana kutoka kwenye ajira jeshi la polisi au JW na hapo kabla hawakuwa waajiliwa.
 
Safi sana CDF Mabeyo haiwezekani asamehewe gaidi mbowe alafu vijana wazalendo wa JKT waliojenga ukuta wa Mererani na Ikulu ya Dodoma waachwe wakiteseka mitaani
Utaumia na kuteseka Sana kipindi hiki!
Poleni chawa mnaoinyonya maiti mkidhani mtasurvive! It's too late to catch the train!
 
Back
Top Bottom