TANZIA Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (KDF) Jenerali Francis Ogolla afariki katika ajali ya Helikopta ya Jeshi

Taifa. Afrika imebaini kuwa helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) iliyokuwa imembeba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Francis Ogolla iliyoanguka Alhamisi ilikuwa ikitoka kwenye misheni ya amani katika Kaunti ya Pokot Magharibi.

Chopa hiyo ilianguka katika eneo la Sindar kwenye mpaka wa kaunti za Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet, na kuua watano.

Watu wanane waliokuwa helikopta hiyo walikuwa wametoka katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Cheptuel katika Eneo Bunge la Sigor, Kaunti ya Pokot Magharibi, ambapo KDF inajenga upya shule zilizoathiriwa na ujambazi.
 
Mbinu za kimedani!
 
Hebu mwenye history ya namna huyu Mkuu wa Majeshi alivyopanda cheo atuwekee humu. Nahisi alipata kama shukrani kutoka kwa William Rutto kwa mambo aliyomsaidia wakati wa uchaguzi
 
Hebu mwenye history ya namna huyu Mkuu wa Majeshi alivyopanda cheo atuwekee humu. Nahisi alipata kama shukrani kutoka kwa William Rutto kwa mambo aliyomsaidia wakati wa uchaguzi
Inadaiwa, na Ruto amewahi kusema, Ogolla ni mmoja ya watu ambao walitaka asiwe Rais wa Kenya. Anadai alitumwa kumzuia mwenyekiti wa tume ya uchaguzi asimtangaze Ruto kama mshindi.

Licha ya hayo yote, Ruto baada ya kuwa rais aliamua kumteua kwakuwa aliamini ni mtu makini na mwenye sifa zote za kuwa CDF.

Sasa hatujui kama alipewa mafuta mengi ili anenepe au ili apate presha na afe mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…