Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha; tunakuomba uingilie mgogoro ulioko kati ya Jiji la Arusha na shule ya msingi Arusha (Arusha School) iliyoko mkabala na Tanesco Arusha!
Sisi wazazi tunalipa ada Ili watoto wapate huduma mbalimbali za kimasomo, chai asubuhi, chakula cha mchana na chakula cha Jioni Kwa wale wa bweni!
Chakushangaza Mkurugenzi wa Jiji Kwa kushirikiana na madiwani kadhaa wamekuwa wakishinikiza kuwa shule itoe gawio la milioni 100 Kila mwaka kwenda Jiji. Matokeo yake watoto wetu hawapati huduma za kuridhisha na hawashibi chakula kutokana upungufu wa Hela.
Ofisi za walimu hazina samani za kutosha, meza hata vitu havitoshi Kwa walimu lakini wao wanalazimisha gawio! Je Kuna biashara Gani hapo shuleni Wadai gawio wakati ni ada za wazazi?
Tunakuomba utusaidie warudishe na walizochukua miaka iliyopita. Hata anayewapa chakula wanafunzi (caterer) hajalipwa muda mrefu sana. Je shule ya serikali inaweza kufanyiwa huu uhuni na Mkurugenzi ambaye anadai ndio mmiliki wa hii shule?
Tunaomba msaada wako huu uhuni na wizi uishe Kwa kuwa Jiji Lina vyanzo vingi sana vya mapato!
Asante.
Mzazi, Arusha Primary School (Arusha School).