Chifu Rocket Mwashinga naye akazia viongozi waungwe mkono mkataba wa bandari
Viongozi wetu wanaofanya kazi wasikashifiwe awaomba machifu wenzie wote wa hapahapa Mbeya wasikubaliane na hilo
Hapahapa mjini Mbeya vijana wetu wanadiriki hata kufungua kesi ya kihistoria ya katiba kuipinga serikali kwa kazi ya bandari, hivi wanaMbeya tutaeleweka kweli ?! anahoji Chifu Rocket Mwashinga
Chifu anasimulia uzoefu wake pale bandarini Dar es Salaam pana wizi mkubwa, nimefanya kazi pale miaka 8 bandarini Dar es Salaam niliona hata kitu kikubwa kama container eti linapotea kama vile ni kitu cha kubeba mkononi kimepita getini bila kuonekana !
Sisi wanaMbeya, viongozi wa mkoa na wilaya pia wa chama tutaeleweka vipi ikiwa serikali ambayo ndiyo rais mwenyewe anashitakiwa hapa hapa mahakamani mjini Mbeya anahoji Chifu Rocket.
Anaongeza na kuonesha hofu kuwa hatua hiyo inaweza kukwamisha serikali kuleta maendeleo yaliyoanza kufanyika hapa Mbeya anahitimisha hotuba yake kiongozi huyo wa kijadi.
Ikumbukwe kuwa sasa machifu ushawishi wao umeongezeka baada ya machifu wote wa kijadi Tanzania kuwa karibu na serikali kupitia makongamano ya kitaifa ya machifu wa jadi ambayo hufanyika kila mwaka.
Hivi karibuni mheshimiwa rais Samia Hassan alisimikwa kuwa Chifu wa Machifu wote na kupewa jina rasmi la kijadi na UMT Umoja wa Machifu Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisimikwa kuwa Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa Chifu Hangaya katika hafla ya kilele cha Tamasha la Utamaduni, lililofanyika leo kwenye viwanja vya Redcross, Kisesa jijini Mwanza