Mkuu wa Mkoa Mbeya na Spika Tulia wawaomba Machifu wawaloge wanaopinga Mkataba wa Bandari

Mkuu wa Mkoa Mbeya na Spika Tulia wawaomba Machifu wawaloge wanaopinga Mkataba wa Bandari

🤣🤣🤣Sasa hapa mbeya na rukwa tumekubaliana Kati ya mwabukusi,tulia,nshala,pengo ,mizengo pinda,mzee wa upako na tulia 🙏baada ya ulozi mmoja aondoke,na tambiko limefanyika pale nakonde,penye jiwe la mpaka🙏🙏🙏
 
Masache Kasaka - Wananchi Tuiamini serikali yetu ya CCM katika mkataba wa bandari

 
19 July 2023
Mbeya, Tanzania

China wa China awavaa vikali CCM kuhusu mkataba wa bandari, awabana Tulia na Silinde warudi tena jukwaani Mbeya na mkataba mkononi


Wana Mbeya wana maswali mengi ya kuwahoji wabunge wote wa CCM Mbeya kuhusu mkataba....

WanaMbeya wanasema bandari ni mali yao pia urithi wa vizazi vijavyo haiwezekani kuuzwa kimya kimya.... maoni ya wananchi kupuzwa na CCM hayakubaliki ..

Pia Joseph Mwasote ‘China wa China’ amewakumbusha kuwa kesho kesi ya wananchi ipo mahakama kuu.
Source : Big Star TV
 
Mkuu wa Mkoa Mbeya na Spika TULIA Wawaomba MACHIFU WAWALOGE wanaopinga MKATABA WA BANDARI😂🤣



Mkuu wa mkoa akiongea zilisikika sauti za wanaCCM wakidai walogwe wale wanaopinga mkataba na ikabidi mkuu wa mkoa akubali rai ya wanaCCM kuwa wanaopinga basi machifu wafanye yao kama wanaCCM walivyodai

Huyu bwana moyo wake umebeba mambo mengi, ila naona achanganya mambo mengi kichwani kwa wakati mmoja

Anasema mwanae aliuliwa , na yupo aliemtakia kwamba amemua kweli ili apate cheo , je kijana wake alikua nani ,? na alifanya nini mpaka kuuwawa, kifo chake kilitokea wapi?

Huyu namfaham kama mwimbaji wa nyimbo za injili, ( kikosi kazi) na kweli alikua mfuasi wa Mwendazake maana upo mpaka wimbo aliimba juu ya mwendazake you tube upo

Lakin anasema alifuata Tulia mara kadhaa kabla ya mwanae uwawa, ila bado anasisitiza na kulaum Sana Mkurugenzi wa Taifa , hii imekaa vipi ,

Mwenye kuelewa hili basi atutupie mnofu kidogo tujue
All in all anamachungu sana
 
watashidwa tu, hatuwezi kukubali watu wachache wauze maliasili ya Tanganyika kwa manufaa yao na familia zao.
 
Chifu Rocket Mwashinga naye akazia viongozi waungwe mkono mkataba wa bandari



Viongozi wetu wanaofanya kazi wasikashifiwe awaomba machifu wenzie wote wa hapahapa Mbeya wasikubaliane na hilo

Hapahapa mjini Mbeya vijana wetu wanadiriki hata kufungua kesi ya kihistoria ya katiba kuipinga serikali kwa kazi ya bandari, hivi wanaMbeya tutaeleweka kweli ?! anahoji Chifu Rocket Mwashinga


Chifu anasimulia uzoefu wake pale bandarini Dar es Salaam pana wizi mkubwa, nimefanya kazi pale miaka 8 bandarini Dar es Salaam niliona hata kitu kikubwa kama container eti linapotea kama vile ni kitu cha kubeba mkononi kimepita getini bila kuonekana !

Sisi wanaMbeya, viongozi wa mkoa na wilaya pia wa chama tutaeleweka vipi ikiwa serikali ambayo ndiyo rais mwenyewe anashitakiwa hapa hapa mahakamani mjini Mbeya anahoji Chifu Rocket.

Anaongeza na kuonesha hofu kuwa hatua hiyo inaweza kukwamisha serikali kuleta maendeleo yaliyoanza kufanyika hapa Mbeya anahitimisha hotuba yake kiongozi huyo wa kijadi.

Ikumbukwe kuwa sasa machifu ushawishi wao umeongezeka baada ya machifu wote wa kijadi Tanzania kuwa karibu na serikali kupitia makongamano ya kitaifa ya machifu wa jadi ambayo hufanyika kila mwaka.

Hivi karibuni mheshimiwa rais Samia Hassan alisimikwa kuwa Chifu wa Machifu wote na kupewa jina rasmi la kijadi na UMT Umoja wa Machifu Tanzania

View attachment 2689071
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisimikwa kuwa Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa Chifu Hangaya katika hafla ya kilele cha Tamasha la Utamaduni, lililofanyika leo kwenye viwanja vya Redcross, Kisesa jijini Mwanza

machifu wa mchongo.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Mungu awasamehe tu kwa kuwa hawajui watendalo. Kwa kifupi tu ni watu wa kuonewa huruma kwa sababu wapo dunia nyingine kabisa tofauti na dunia ya sasa ya teknolojia wao wapo zama za kati za mawe.

Na watanzania wakikubali kuendelea kuongozwa na viongozi wenye upeo kama mkuu wa mkoa wa Mbeya basi tutarajie mambo mengine ya hovyo zaidi ya haya tuayoyaona sasa.
 
20 July 2023
Mbeya, Tanzania

Mwabukusi - Tumeridhika Na Maamuzi ya Jopo la Majaji wa Mahakama Kuu Kuwa Kesi ya Mkataba wa Bandari Ni Jambo La Kusikilizwa Bila Kupoteza Muda

1689931392222.png
 
28 Julai 2023
Mbeya, Tanzania

Chifu Prince Mwaihojo Mwambipile - " Wezi Wote Wamehamia CCM



Chifu huyo maarufu aliyekuwa mwanachama wa CCM iliyokuwa TANU ya miiko ya Kusema Kweli Daima, Fitina Mwiki na haki kwa wote akumbuka mazuri ya TANU ambayo sasa yametelekezwa na CCM ya kisasa.

Chifu Chris Mwambipile akiomba chama kongwe dola cha CCM kuacha kutumia vyombo vya dola kama Polisi maana huko ni kutengeneza uhasama na watoto wao ambao wengine ni mapolisi kuwabugudhi watoto wengine ambao wanatetea bandari.

Kwani kwa mujibu wa uchifu ukiwa kiongozi wa jamii, watoto na vijana wote ni wanae chifu hivyo viongozi wa CCM ambao wanadhama ya uongozi wasiwasumbu vijana wote wa kiTanzania kwa kisa cha kupinga bandari kuuzwa.
 
Mkuu wa Mkoa Mbeya na Spika TULIA Wawaomba MACHIFU WAWALOGE wanaopinga MKATABA WA BANDARI😂🤣



Mkuu wa mkoa akiongea zilisikika sauti za wanaCCM wakidai walogwe wale wanaopinga mkataba na ikabidi mkuu wa mkoa akubali rai ya wanaCCM kuwa wanaopinga basi machifu wafanye yao kama wanaCCM walivyodai

Tunaomba hao Machifu wawaloge TARI na wote wanaotaka kunyanganya wananchi eneo lap.
 
Dr nshala lazima asikitike mwanafunzi wake huyo
Mtu akishakuwa mwanasiasa hofu ya Mungu inaisha na shetani anamtumia vizuri,ila mwisho wao hauwi mzuri kwa sababu ya laana na machozi ya watu. Nikiambiwa nimshauri mtu,siasa siyo carieer nzuri yenye mwisho mzuri.
 
Back
Top Bottom