July 2023
Mbeya, Tanzania
Spika Tulia naye atoa somo kuhusu treaties na agreements kwa wanaCCM Mbeya
Akiongea katika mkutano uliosheheni viongozi wa CCM kutoka pande zote za nchi akiwemo mzee Stephen Masato Wasira , Makongoro Nyerere, ma-MNEC wa CCM kama Jerry William Slaa, Richard Atufigwege
Kasesela, mh. prof. Kitila Mkumbo waziri wa Uwekezaji / Mipango, mh. injinia Maryprisca Mahundi naibu waziri maji, mh. David Silinde naibu waziri wa Utumishi na Utawala Bora na Mh. Atupele F. Mwakibete naibu waziri wa uchukuzi n.k
Spika wa Bunge Mh. Tulia asisitiza wale wote wanaopinga mkataba wa bandari 'wamevurugwa' ...
Mheshimiwa spika Tulia Ackson akiongea kwa hisia kali kuliko mbele ya mamia ya wanaCCM wa Mbeya waliojitokeza leo 15 July 2023 viwanja vya Luanda Nzovwe Mbeya kutetea alichoita makubaliano na nchi ya Dubai kuhusu bandari
CHONGOLO ATINGA MBEYA, KUWEKA BAYANA MAMBO YA BANDARI
Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Daniel Chongolo akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe jijini Mbeya, tayari kwa mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Uwanja wa Luanda, Jijini humo, ambapo pamoja na mambo mengine ataelezea usahihi wa makubaliano ya uendeshaji wa bandari.
Katibu mkuu wa CCM na ujumbe wake mzito wa viongozi wa chama na serikali, uwanja wa Ndege amelakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mikoa jirani pamoja na Spika wa Bunge, Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini.
Mkutano huo utahudhuriwa pia na baadhi ya wananchi kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa
Source : ccmchama.blogspot.com