Mkuu wa mkoa Paul Makonda, na sisi wakazi wa Mpigi Magoe tunaomba utukumbuke, barabara yetu ni mbaya haswa

Mkuu wa mkoa Paul Makonda, na sisi wakazi wa Mpigi Magoe tunaomba utukumbuke, barabara yetu ni mbaya haswa

Sio huko tuu kuna siku moja nilipita hii njia ya kimara matosa kuelekea goba barabara nne ni short cut nfupi ila kama sio gari kuwa nzima kidogo siku hiyo lingenilaza njiani
Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, kwanza nakupongeza kwa juhudi kubwa ulizonazo katika kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu kipenzi Dr. John Pombe Magufuli.

Leo naomba kuja kwako na ombi moja la barabara ya kutokea mbezi mwisho kupitia mbezi high school mpaka Mpigi Magoe. Barabara hii ni kati ya barabara zenye magari mengi katika jiji la Dar es Salaam lakini pia ikiwa na urefu wa takribani kilometer 11 toka mbezi hadi mpigi magoe.

Ukiangalia urefu wa barabara utaona ni jinsi gani wakazi wa huku tunavyopata shida. Wenye magari inafikia kipindi hawaweki magari yao barabarani hivyo kutufanya sisi wananchi wako kwenda makazini kwa mbinde sana. Lakini pia, vijana pale mbezi wametugeuza mitaji yao kwa kutuibia pale tunapokuwa tunagombania magari ya kwenda huko.

Tunakuomba mkuu wetu wa mkoa na sisi pia utuombee kwa Mheshimiwa rais ili atukumbuke kama walivyokumbukwa wananchi wa Goba na Madale. Kama kuna jambo wananchi wa huku wanajutia ni kuendekeza kuchagua watu wasioonekana kabisa kuwatetea wananchi. Lakini mwaka kesho Mungu akipenda wananchi wameahidi hawatafanya makosa kwa kuendelea kuchagua vibaya.

Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Mkuu wa mkoa utasoma hapa na utanipatia majibu.

Ni mimi mwananchi wako wa Dar es Salaam
 
Kaandike instagram mkuu kule ndiko anakopokea maagizo na kutoa maagizo.
 
Back
Top Bottom